CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais

Watch TBC Live toka Bungeni!
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekubali yaishe, wanamtambua JK kama Rais, Wanampongeza!
Mbowe ameomba reconciliation for the sake of Umoja wa Kitaifa.

Big Up kwa Freeman Mbowe, sio siri mimi binafsi nilikuwa simuheshimu sana Mbowe nikimuona kama spoon fed leader.
Kuanzia sasa ni heshima mbele! Huo ndio uanamume, kukubali kushindwa na kukubali yaishe!

Mbowe amewashukuru wapiga kura kwa kura walizoipigia Chadema!.

Hiki Mbowe alichokifanya Bungeni, ndicho Dr. Slaa alichotakiwa kukifanya ile siku ya kutangazwa matokeo!

Nilisema that was a golden missed opportunity. Sasa Mbowe amerekebisha makosa ya Dr. Slaa. Chadema sasa inarudi juu!

Kuna posti niliwahi kuiposti kuwa Chadema hawajajipanga, nilishambuliwa piga ua. Sasa nasema Chadema imeanza kujipanga. Big up!.

Kwanza mlibanaaa... mwisho mmeachia... I'm glad I was damm right!

Chadema sasa tusonge mbele, hata mimi nikirudi uraiani, naweza kufikiria kujiunga Chadema, kuimarisha nguvu!

Asante sana Freeman Mbowe!.

Update 1: Angalizo!.
Kuna kitu kinaitwa expressly na impliedly!
Expressly ni kwa Mbowe kutangaza kwamba sasa Chadema inamtambua Rais!
Impliedly ni pale Mbowe alipompongeza rais, akamsifu, akamshukuru na bla bla bla nyingi za kusifu na kutukuza na kuonyesha spirit ya reconciliation.

mkubali msikubali, Chadema imemtambua Rais JK impliedly na wamekubali yaishe zaidi ya hapo ni ubishi tuu, vinginevyo Mbowe afanya Press Conference afafanue na kukazia kutomtambua JK!

Pasco.

attachment.php

Yah, hata mie nimemsikia, hongera mbowe kwa kutambua ukweli
 
Huyu Bwana mtoa mada atakuwa amenunuliwa ka Jenereta kadogo na JK na kuahidiwa kuwekew dizeli hadi mgao wa umeme utakapoisha! Naomba kuwasilisha!
 
Hii habari ndiyo imekwisha.............................

Halima, Halima, ZIMAAAAA..........

 
Last edited by a moderator:
Aombe radhi kwa sababu ya ufahamu wake? If he believes Mbowe amemtambua Rais, ataendelea kuamini hivyo. What's the point ya kuomba radhi kwa ajili ya kuridhisha watu tu.

Au ndo tunataka watu waaanze kuficha kueleza mawazo yao kwa kuwa hayaendi sambamba na kile wengi wanachokiamini?
You are very funny ati aendelee kuamini wakati wenye chama wenyewe hawamtambui mwisho unaonekana kituko sasa.
 
Nasikitika sana na uelewa wetu Watanzania....ile kutu ya CCM haitatoka kamwe kwenye mbongo za wengi wetu....yaani siwaelewi kabisa nyie mnaoshabikia kuwa Mbowe kajisalimisha...kwanza yeye kampongeza kwa jambo moja...kukubali kubadili katiba....nyiye mnajumuisha kuwa kamkubali urais wake....halafu wengine mnasema kamsifu badala ya kumpongeza...kunatofuti kati ya maneno hayo mawili.....hivi Mwalimu hakuwa anampongeza Malkia baada ya 1961?...na bila uchambuzi mnafurahia picha isiyohusiana na tukio lenyewe.
 
Ahaaaaaaaaaaaaa... nimemuelwa pasco...:doh:

YEYE KASEMA BRAKING NEWS, S:dance:ISI TUNADHANI NI BREAKING NEWS:boxing:
 
Huyu ni pasco tumjuaye au kuna mtu katumia id yake?

Upupu huu mkuu ni chini ya kiwango.


Off course ni yeye!! Hata mimi nimestuka. kama angekuwa ni Maggid nisingeshangaa lakini huyu ni Pasco!!! Mod huyu bwana inabidi awe demotted from JF premium member kama inawezekana kwa kutuwekea habari ya propaganda hapa jukwaani!!! Ingekuwa ni mawazo minafsi tungemuelewa lakini hii amereport habari live toka bungeni na kuongeza propaganda zake.
 
Kila mtu na ufahamu wake

Yeye kwa mujibu wa sequence za matokeo na maneno ya Mheshimiwa Mbowe ameona ni sawa na kumtambua tu.

Alichofanya hapa ni kutoa mawazo yake binafsi na kuelezea umati kwamba ndio fikra za Mbowe... (hii ndio definition nyingine ya kupotosha) Sisi wanajamvi tuna uelewa wa kutosha wa kuweza kudigest ni nini Mbowe alisema..., kwahiyo ambacho angefanya ni kuelezea ni nini Mbowe kasema alafu kwenye MY TAKE ndio akatwambia yeye binafsi anaona nini ndio tafsiri yake, am sorry hapa inabidi tuseme ukweli kwamba ndugu yetu ametoka kwenye line
 
WABUNGE wa Chadema jana walimtikisa waziri mkuu, Mizengo Pinda (pichani) katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo wakimtaka kueleza serikali ina tamko gani kuhusu mauaji yaliyotokea Januari 5 mkoani Arusha.

Kadhalika kikao cha tatu cha mkutano wa pili wa Bunge la kumi, jana kilishuhudia mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa mbunge wa kwanza katika bunge la kumi kuwekwa kikaangoni baada ya kupewa siku tano na Spika wa Bunge, Anne Makinda athibitishe madai yake kwamba Waziri Mkuu Pinda aliudanganya umma wa Watanzania wakati akijibu swali kuhusu vurugu za Arusha.

Hoja ya Mbowe
Msumari wa kwanza kwa Pinda, ulipigiliwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, baada ya kuuliza serikali inatoa tamko gani rasmi kuhusu tukio la mauaji ya watu watatu katika vurugu na maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na wahusika akiwamo IGP Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu.

Katika swali lake la nyongeza Mbowe alitaka kujua ni lini serikali itaunda tume ya kisheria kuchunguza tukio hilo kwa kupata maelezo kutoka pande zote husika tofauti na sasa ambapo taarifa zilizopo serikalini ni zile zinazotoka upande mmoja wa jeshi la polisi.

Majibu ya Pinda
Hata hivyo, akijibu kombora hilo, Pinda aliinyoshea kidole Chadema akisema kwa mujibu wa maelezo aliyopewa ilivunja makubaliano yake na polisi na kuandamana.

Pinda aliweka bayana kwamba, baada ya hali hiyo kilichotokea ni polisi kujaribu kuzuia maandamano hayo ya wanachama wa Chadema ambao tayari walikuwa wamehamasishwa na viongozi wao kwenda "kuwakomboa" wenzao waliokuwa wameshilikiwa kituo cha polisi mjini Arusha.

"Nakushukuru Mbowe kwa kuuliza swali hilo, serikali hii ni makini, ikiwa jambo limetokea usikimbilie kusema serikali,
serikali..., ni vizuri kuulizaa aliyesababisha...,'' alisema Pinda na kuongeza:

''Mlikiuka makubaliano na polisi, matamshi ya kwenye mkutano
hayakuwa ya chama chenye dhamira ya kujenga amani, mkawataka wafuasi waende kuwakomboa wenzao."

Katika kuondoa wingu na kuweka hadharani kila kitu, Pinda alisema pamoja na juhudi za polisi kuzuia maandamano
hayo, lakini yaliendelea hadi mita 50 kutoka kituo cha polisi,
nao hawakuwa njia nyingine kwa kuwa hawakujua nini kingewakuta kama waandamanaji wangevamia kituo cha
polisi.

"Police were left with no option' (hawakuwa na njia nyingine), ndipo watu watatu wakapoteza maisha. Kama Mbowe na Chadema mngeamua
kushirikiana na serikali haya yasingetokea," alisema Pinda.

Kuhusu kuunda tume ya wanasheria kuchunguza tukio hilo na kutoa alichokiita Mbowe ni ukweli na
kuchukua hatua, Pinda alisema uchunguzi unaweza kufanyika, lakini lazima serikali ijiridhishe kwanza ndipo hilo lifanyike.

"Ni sawa uchunguzi unaweza kufanyika, lakini lazima serikali ijiridhishe. Rai yangu tushirikiane, lazima muda wote
tujitahidi tujenge nchi ya amani na utulivu,'' alionya Pinda.

Uchaguzi wa Meya Arusha

Katika hatua nyingine, Pinda alisema taratibu zilizotumika kumpata Meya wa mji wa Arusha na Naibu wake ni sahihi.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalum Manyara, Martha Umbulla aliyetaka kujua pamoja na mambo mengine, msimamo wa serikali kuhusu Meya na Naibu Meya wa Arusha.

"Sasa niseme hivi, kwa hesabu za kawaida za mtoto wa darasa la kwanza, katika uchaguzi mwenzako ana madiwani
16 wewe una 14 utashindaje, baada ya hayo wakasema wakutane wazungumze, watazungumza nini?

Hili ni suala la kisheria; Mimi nilikuwa Tamisemi, utaratibu uliofuatwa katika
uchaguzi ule ni sahihi, Meya sahihi, Naibu Meya sahihi," alitoa msimamo Pinda.

Hata hivyo, alisema pamoja na kuwepo kwa taarifa za Naibu Meya huyo wa Arusha kujitoa, lakini serikali haijapata
barua rasmi kuhusu uamuzi huo.

Pinda pia alisema, wabunge waliotajwa kuwa chanzo cha mvutano, aliowataja kuwa ni Chatanda wa CCM na
Rebecca Mngodo wa Chadema ni halali.

Lema: Pinda amedanganya
Baada ya Pinda kumaliza maelezo yake hayo mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika kwa kusema "Mwongozo wa spika," akitumia kifungu cha 68.

Lema baada ya kuomba mwongozo wa spika na kuruhusiwa alihoji; "Hatua gani zinaweza kuchukuliwa kama waziri mkuu analidanganya Bunge na umma? Naona waziri mkuu amelidanganya taifa," alisema Lema bila ya kufafanua
alichodai kuwa ni uongo.

Hata hivyo, kauli hiyo ilimchefua spika Makinda ambaye aling'aka akisema; "Bunge letu lina adabu lazima hiyo ifuatwe, huwezi kusema hivyo ikaishia hivi hivi tu, kama unaona waziri mkuu amedanganya basi nenda kaandike alafu ulete, maelezo yako,".

Spika akionyesha kuchukizwa na kauli hiyo ya Lema, wakati akihitimisha kipindi hicho alimpa mbunge huyo wa Arusha mjini siku tano za kuwasilisha maelezo yake bungeni kuthibisha uongo wa waziri mkuu.

Makinda alisema iwapo mbunge huyo atashindwa kuwasilisha uthibitisho huo, atatakiwa kujirekebisha kwa kufuta kauli yake au kuomba radhi, adhabu atakayokabiliana nayo ni
kusimamishwa kuhudhuria vikao visivyozidi vitano vya bunge.

Alimtaka kuthibitisha madai hayo, lakini kwa wakati Spika akitangaza hayo Lema hakuwepo ndani ya ukumbi wa Bunge.

Hata hivyo, akizungumza na wanahabari baadaye nje ya ukumbi wa Bunge, Lema alisema : "Leo siwezi kuwathibitishia nisiharibu ushahidi, lakini nipo tayari kuthibitisha uongo huo wa waziri mkuu."

Alifafanua kwamba," Bunge limeniambia nithibitishe, nasema waziri mkuu amedanganya na nitathibitisha hilo
Februari 14 asubuhi, pia nitaongea nanyi (waandishi wa habari) na nitawapa uthibitisho."

Alipoulizwa haoni kwamba pengine waziri mkuu alipewa taarifa potofu na siyo kusema uongo, Lema alisema: "Sio kwamba amepewa taarifa potofu, hilo ni lake yeye kulisema, lakini nasema waziri mkuu ameudanganya umma na nitathibitisha Februari 14."

Spika Makinda alitoa agizo hilo kwa Lema, baada ya waziri mkuu kumalizia kujibu swali la mwisho lililoulizwa
na Hamad Rashid wa CUF, kuhusu hali ya chakula na tishio la kupanda bei ya mafuta nchini.

Madiwani Chadema kama wabunge wao
Mwandishi, Moses Mashalla anaripoti kuwa sakata la uchaguzi wa umeya mkoani Arusha limeendelea kukufukuta kufuatia madiwani wa Chadema kususia kikao cha kwanza cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Arusha kwa kutoka nje ya ukumbi, kwa madai kwamba hawamtambui meya wa manispaa ya hiyo, Gaudence Lyimo.

Hatua ya madiwani hao imekuja saa 48 tangu wabunge wa Chadema watoke nje ya bunge ikiwa ni hatua ya kupinga hatua ya kufanyiwa tafsiri maneno ‘Kambi rasmi ya upinzani bungeni', katika kanuni za bunge toleo la mwaka 2007.

Hatua ya madiwani hao wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wakati kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kikiendelea kilijitokeza jana majira ya saa 8:30 mchana wakati ajenda ya kuteua kamati za kudumu za manispaa ya Arusha ikitaka kuanza.

Kabla ya madiwani hao kutoka nje kulikuwa na mvutano na malumbano ndani ya kikao hicho baina ya madiwani wa Chadema na CCM hali iliyomlazimisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Estomihi Chang'a kutoka nje ya ukumbi ili kupisha kikao kisicho rasmi cha muafaka baina ya pande hizo, huku mkuu wa wilaya ya Arusha akihudhuria kikao hicho.

Madiwani hao wa Chadema wakiongozwa na kiongozi wao,ambaye ni diwani wa kata ya Elerai, John Bayo walitoka nje na kuwaacha madwiani wa CCM wakiwemo watumishi wakiendelea na kikao.

Akizungumza mara baada ya kutoka nje, Bayo alisema walichukua hatua hiyo baada ya kufikia maafikiano na uongozi wa chama chao ngazi ya taifa ya kuwa hawamtambui meya wa manispaa ya Arusha.

"Sisi hatumtambui meya wa Arusha kwasababu alipatikana kwa njia za zisizo halali, hivyo tumetoka nje ya ukumbi kwa maafikiano ya madiwani wetu na uongozi wa taifa kuwa hatuwezi kushiriki kikao cha utekelezaji na mtu ambaye hatumtabui,"alisema Bayo.

Bayo alisema wao walipokea taarifa za kikao hicho cha madiwani ambapo ajenda walizoambiwa kuwa ni pamoja ana kufungua kikao, kuunda kamati za kudumu za manispaa ya Arusha na kuunda ratiba ya vikao vya manispaa kwa mwaka mzima.

Alisema walipofika katika ukumbi huo waliomba watumishi wa manispaa hiyo watoke nje ili waweze kujadili muafaka wa masuala mbalimbali baina yao na madiwani wa CCM na ndipo walipokubaliana na kisha kuzungumzia masuala mbalimbali walioafikiana baina ya pande zote mbili.

Alidai kuwa mojawapo ya masuala ambayo walikubaliana na madiwani wa CCM ni pamoja na kuitaka serikali izikutanishe pande mbili zinazopingana ili ziweze kujadili hali ya mvutano uliopo na kutafuta suluhu.

Hatahivyo, alisitiza kuwa mara baada ya kikao hicho walikubaliana pia kutafuta muafaka wa suluhu la utata wa umeya wa Arusha lakini baadhi ya madiwani wa CCM walipinga na kudai kuwa waendelee na ajenda zilizopo na suala hilo litafuata baadaye kitendo ambacho hawakukiafiki.

Bayo alisema mbali na kulalamikia uchaguzi wa umeya pia walikuwa na wasiwasi na baadhi ya uundwaji wa kamati za kudumu za manispaa hiyo, kufuatia majina ya madiwani wa Chadema kuwekwa katika orodha katika baadhi ya kamati ihali hawakuomba kamati hizo.

Kwa upande wake Meya Lyimo alisema wanashangazwa na hatua ya madiwani wa Chadema kutoka nje ya kikao hicho kwa madai ya kutotambua nafasi yake.

Lyimo, alidai kuwa pamoja na madiwani hao kususia kikao, wao waliendelea na uundaji wa kamati za kudumu za manispaa ya Arusha kama kawaida bila kuwashirikisha madiwani wa Chadema kwa kuwa hawakuwepo na wataendelea kuchapa kazi za kuwatumikia wananchi.

"Sisi hatukuwafukuza kwenye kikao lakini tumechagua kamati bila wao kuwepo kwa sababu hawakuwepo pia lakini tulitaka hata wao waongoze baadhi ya kamati," alisema Lyimo.


CHANZO: MWANANCHI
 
Nadhani kuna mtu anacheza na ID ya Pasco !!!!! Kama ni real pasco naomba uombe radhi kwa udanganyifu huu.
 
Jemedari Dr. Slaa alikuwa muungwana sana baada ya kuchakachuliwa kura za uraisi. Alitulia. Peoples power tulikuwa tunasubiri Jemedari apulize kipenga, watu waingie mtaani kama Tunisia na Misri. Bahati yao. Warudie tena kuchakachua kura zetu 2015 waone kama nchi itakalika
 
Jemedari Dr. Slaa alikuwa muungwana sana baada ya kuchakachuliwa kura za uraisi. Alitulia. Peoples power tulikuwa tunasubiri Jemedari apulize kipenga, watu waingie mtaani kama Tunisia na Misri. Bahati yao. Warudie tena kuchakachua kura zetu 2015 waone kama nchi itakalika

Ki ukweli Bunge limeniboa hasa..Yaani kipindi cha maswali kikiisha sijisikii tena kusikiliza mipasho na vijembe vyao.Jumatatu ifike haraka tumalize kuchangia hii hotuba ya Rais inayotupa nafasi ya kuogeleoa popte unapotaka.


Sasa nashindwa kuelewa ikiwa Regia mwenyewe amamkubali Rais sasa uzushi wa Pasco ni nini? anyway siasa ngumu ngoja nirudi kijijini nikalime.
 
Kama ametoa pongezi hizo directly kwa rais kwa kufanya maamuzi yanayotokana ama kufanywa na institution ya urais,then ameitambua institution hiyo hence kumtambua rais.Kama angekuwa specific na kusema wanampongeza kama mwenyekiti wa ccm,then ingeweza kuleta utofauti.
Pasco:Kwenye post yako ya mwanzo umeandika mengi kutokana na hisia ama mtazamamo wako lakini hujaweka mengi yaliyosemwa na mwenyekiti wa cdm.Ni vyema ungeweka maneno aliyoyasema,hapo wala usingekuwa na haja ya kuongezea maneno yote hayo ambayo inaoneka kama umeongeza chumvi mingi.
 
Back
Top Bottom