CHADEMA yajipanga kuchukua majimbo Shinyanga

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Mkoa wa Shinyanga limejipanga kuchukua majimbo yote ya mkoa huo na kuwa chini ya chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa baraza hilo jana mjini hapa na kuyataja majimbo watakayoyapa kipaumbele kuwa ni Bariadi Mashariki, Bariadi Magharibi, Kishapu na Solwa kwa kufungua matawi na kufanya mikutano ya mara kwa mara kwa wananchi wa maeneo hayo.
Alisema mpango huo utakuwa ni ‘Operesheni Kumekucha’ badala ya ‘Washa Taa’ ambayo inatumiwa katika mikoa mingine na kwamba watahakikisha wanazunguka mkoa mzima kwa lengo la kuzindua matawi katika majimbo yote kwa kuanzia majimbo sugu yaliyo ndani ya mkoa huo.
“Tumejipanga kuhakikisha majimbo yote ya Mkoa wa Shinyanga ambayo ni sugu yanakuwa mikononi mwa CHADEMA pamoja na kata na halmashauri zote zinashikiliwa na CHADEMA kama ilivyo katika maeneo mengine,” alisema.
Alisema hatua hiyo itasaidia vijana kufahamu haki zao kupitia chama hicho na kuwataka wajitokeze kwa wingi bila kujali elimu zao na kuepukana na matendo maovu ya uasherati na wizi ili kuondoa madoa machafu hapo baadaye wanapotaka kuwania uongozi. Katika hatua nyingine, wajumbe wa baraza hilo wametoa kilio chao kwa kutaka kuwa na kadi za uanachama za vijana zitakazowafanya watambulike katika jamii.
 
Twende kazi..................hakuna lisilowezekana kwa mungu
 
Msijipange kuchukua Majimbo bali jipangeni kurudisha majimbo kwa UMA,
Kwa upande wa CCM Ubunge ni issue binafsi ndio maana hawajishughulishi
kwa maslahi ya UMA.

Na nyie CHADEMA ni binadamu kama wao CCM, kuweni makini msije kuingia
kwenye matatizo kama haya.

Acheni kusema sisi CHADEMA, semeni sisi UMA.Mabosi wenu SLAA na MBOWE
wao husema wananchi ndio wenye Mali hii (Tanzania)
 
maneno safi kweli haya...sasa na nyinyi vijana wa huko shinyanga mugangamale msiwe kama wenzenu wa dar kutwa wako pale sinza kumekucha Golden hotel wanalewa na kupiga makelele tu hasa yule dada mwenyekiti sijui wa BAVICHA dar....ananikera ka nini
 
Back
Top Bottom