CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

Issued exclusively through JF; press corps, feel free to use it in your stories tommorrow:



TAARIFA KWA UMMA

Taarifa inatolewa kwa umma na kwa vyombo vya habari kwamba Kamati Kuu ya CHADEMA inaendelea na kikao chake cha kawaida kilichoanza saa 5 asubuhi Dar es salaam katika Hoteli ya Keys Mbezi leo tarehe 2 Disemba na kikao hicho kitamalizika kesho tarehe 3 Disemba 2009.

Ajenda za kikao hicho ni: Yatokanayo na muktasari wa Kikao kilichopita; Hali ya Siasa Tanzania; Tathmini ya Uchaguzi wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji; Kupanga shughuli za kutekeleza Mpango Mkakati wa chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010; Kuthibitisha Makatibu wa Wilaya/Mikoa na sekretariati zao; Taarifa za Rufaa mbalimbali za uchaguzi wa ndani ya chama; Taarifa ya Zanzibar; Taarifa kuhusu Mfumo wa uanachama kwa njia ya kieletroniki (E-Membership); Taarifa ya Fedha; Uteuzi wa Bodi ya Wadhamini; Tarehe za mikutano ya Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.

Aidha tunasikitika kupokea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na mmoja wa waasisi wa CHADEMA Kanali (Mstaafu) Geofrey Marealle kilichotokea jana usiku. CHADEMA inatuma salamu za pole kwa familia ya marehemu na wanaCHADEMA wote duniani kutokana na msiba huo. Salamu za rambi rambi zitatolewa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe mara baada ya kutaarifiwa utaratibu mzima wa mazishi toka kwa familia ya marehemu.

Imetolewa tarehe 2 Disemba 2009 saa 11 jioni na Katibu Mkuu; Dr Wilbroad Slaa.

Asante kwa taarifa japo mida na kutolewa inaonekana kuwa mbele ya muda halisi! Sijajua umekopy na kupaste au kuna katumia jina la mnyika. Maana naona mambo ya 2010 na 2010!
 
Asante kwa taarifa japo mida na kutolewa inaonekana kuwa mbele ya muda halisi! Sijajua umekopy na kupaste au kuna katumia jina la mnyika. Maana naona mambo ya 2010 na 2010!

Wewe ndio utakuwa umeingia choo cha kike.
 
mnyika na chama chenu cha kibaguzi hamna jipya mtaonea watu mpaka lini.
 
Wewe ndio unahitajika kuwa mwangalifu sana, @Pdiddy alicomment thread hii tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka 2009.
Inawezekana sikukuu syndrome imenikamata lakini tarehe iliyotolewa si jana wala juzi na agenda haziendani.
Hata hivyo asante sana!
 
Back
Top Bottom