CHADEMA yaitaka UN kuibana serikali

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Na Edward Kinabo


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeuomba Umoja wa Mataifa (UN), kutoa tamko rasmi kuhusu matokeo ya Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja huo, kilichojadili hivi karibuni taarifa ya timu ya wataalamu iliyoiunda kufuatilia utekelezaji wa maazimio yake kuhusu vita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), likiwemo suala la usafirishaji wa silaha na utoroshaji wa dhahabu katika maeneo husika.
Tamko lililotolewa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama hicho, John Mnyika, ambaye alisema kuna haja kwa UN kutoa tamko rasmi, kwani taarifa zinazoendelea kusambaa kwa njia ya mtandao zinaonyesha kwamba tayari Baraza la Usalama limekaa Novemba 20, Novemba 25 na Desemba kupitia taarifa husika.
Alisema ni muhimu kwa UN kutoa tamko, hivi sasa kwa kuwa mwanzoni mwa mwezi Desemba, UN kupitia ofisi yake ya Tanzania ulieleza kwamba taarifa ya timu ya wataalamu haikuwa rasmi mpaka baada ya kujadiliwa na vikao hivyo.
Aliitaka UN izingatie kuwa mpaka sasa Wizara ya Mambo ya Nje haijawasiliana rasmi na wawakilishi wa wananchi (wabunge), vyama vya siasa na wadau wengine wa msingi kupata maoni yao kuhusu tuhuma zilizomo kwenye ripoti husika ili kutoa msimamo wa pamoja, hivyo ni muhimu kwa milango ya majadiliano kuhusu suala hili kuendelea kufunguliwa.
Wakati huo huo, mkurugenzi huyo ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kutoa kauli kuhusu hatua zilizofikiwa katika kumchunguza Bande Ndagundi na watu wengine wanaotajwa kwenye mtandao wa biashara ya silaha wanaoishi Tanzania.
 
Back
Top Bottom