CHADEMA yaisambaratisha CCM Ngorongoro

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimevunjavunja ngome ya CCM wilaya ya Ngorongoro ambapo wanachama 800 wa CCM walijitoa katika chama hicho na kujiunga na CDM.

Tukio hilo kubwa lilitokea juzi baada ya Mbunge wa Karatu Mchungaji Israel Natse kufanya mkutano mkubwa wa hadhara wilayani hapo na kutoa somo kubwa la uraia kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akikabidhi kadi mpya kwa wanachama hao Mchungaji Natse aliwataka wakazi hao kuwa mabalozi wa
CHADEMA katika maeneo ya vijijini wanakotoka na kuwaambia sasa hivi hakuna kulala mpaka CHADEMA itakapokamata dola mwaka 2015.

Baadhi ya wanachama wa
CHADEMA walimweleza Mchungaji Natse kuwa wamekuwa wakipata vitisho kutoka kwa viongozi wa serikali wilayani hapo wakilaaniwa kwa uamuzi wao wa kuipinga CCM.

Hata hivyo wanachama hao wameahidi kupambana mpaka tone la mwisho.

Source: Mwananchi Alhamisi Uk 16
 
habari njema sana hizi, ngoja aje Rejeo asema kuwa huu ni upepo tu utabita...
 
Magamba hayo lazima yavuke. Vijitu 800 katika wilaya ya watu millioni 4 ni kama ushuzi wa ngomani, upo lakini haunusiki.!
 
Magamba hayo yaliziama yavuke. Vijitu 800 katika wilaya ya watu millioni 4 ni kama ushuzi wa ngomani, upo lakini haunusiki.!

Mkuu una maneno machafu sana.Nisije nikakujibu ukanisababishia BAN kama ulivyomsababishia MOLEMO
 
Magamba hayo yaliziama yavuke. Vijitu 800 katika wilaya ya watu millioni 4 ni kama ushuzi wa ngomani, upo lakini haunusiki.!

kufikir kwako kuko mbali kweli ! Yaan wilaya inakuwa na watu million nne we moms! Mkoa je?
Hamnazo ni hamnazo Tu hata akijua kusoma!
 
Habari njema.
Hao viongozi wa serikali hawana mamlaka ya kuwachagulia wananchi vyama.
 
Magamba hayo yaliziama yavuke. Vijitu 800 katika wilaya ya watu millioni 4 ni kama ushuzi wa ngomani, upo lakini haunusiki.!

Hapo kwenye Bluu ni kama zile story za sizitaki mbichi hizi! Lakini pia hapo kwenye Red I can feel the pain in your heart! Unaongea kwa jazba Uongo wa wazi wazi wilaya ya watu milion nne? Give us a break Lier. sooo sad
 
hii ni nonstop movement, yaani Nape katibu mwenezi wa Chama anapigwa AC tu pale Rumumba na tumbo kuubwa hana wasiwasi na hii movement ya mabadiliko.. Dah
 
Je na hawa nao walikuwa wamepewa barua za kufukuzwa chamani Mh. Nape!
 
Back
Top Bottom