CHADEMA yaibwaga CCM Arumeru Mashariki; CCM Yakubali kushindwa (Zaidi ya kura 6,000)

Tuna uhakika na tunavyotarajia kwa njia ya kusikia wanaotupa taarifa hzi ni wapenda mabadiliko wa kweli.God blesse Chadema and 2015 we can bring changes
 
Safi sana! Wana wa arumeru mmeonyesha ukomavu wa kukataa kuburuzwa na utawala wa kifalme na kisultani. Kwengine tufuate mwendo huo huo.
 
Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.

Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.

My Take:
Bila ya shaka Uongozi wa taifa wa CDM hauna sababu ya kujiuzulu kwa wakati huu! Upepo umevuma upande wao na mtumbwi unaelekea kwenye ushindi 2015:

Kama score board inasoma hivyo, hawa ITV wanafanya nini na haya matangazo yao ya LIVE? Bwana Kagenzi Trasease anasema matokeo bado! Kipi ni sahihi? Japo pamoja na unazi wa Masako kwa CCM bado kura zinaonekana ziko nyingi Chadema
 
Mbona sredi zote zinazohusu uchaguzi zinaunganishwa lakini hii ambayo ni tetesi tu inaachwa?
Huu ni udhalilishaji wa JF, hata kama ni MMM!
Uliaga unaenda kulala vipi tumbo linakuuma.
 
RFA sasa wanaripot ati kuna mchuano mkali na huyo mwanahabari wao yumo chumba cha kuesabia eti kamanda Nassari amesusia matokeo na ametoka nje hana time kabisa tunaomba taarifa.
 
Ritz alijiapiza kwamba CDM ikishinda Arumeru atatembea uchi kuanzia Ubungo mataa hadi Kimara Bungokwa. Sasa tunataka aje hapa JF atuambie ni lini atafanya hiyo safari ili tukamshuhudie. Ritz come back my friend. Hii ndio siasa, ulituahidi tunaomba utimize ahadi yako.

Rejao analala na viatu leo
 
Ritz alijiapiza kwamba CDM ikishinda Arumeru atatembea uchi kuanzia Ubungo mataa hadi Kimara Bungokwa. Sasa tunataka aje hapa JF atuambie ni lini atafanya hiyo safari ili tukamshuhudie. Ritz come back my friend. Hii ndio siasa, ulituahidi tunaomba utimize ahadi yako.

Atapotea hapa Jukwaani kwa mwezi mzima akiomboleza
 
Mkuu tunaomba walau turushie matokeo katika kata zote basi.halafu nashangaa sioni post za awali kuhusu uchaguzi nini kimetokea au ndo ccm wanamiliki hadi huku?
 
are you sure? au fools day maana siku yale imechanganyika na hiyo day watu sasa wanaitumia vibaya.

Hakuna cha all fools day au nini! Magamba chali, hata Rejao atakwambia! People's............!
 
Ushindi wa Arumeru ulionekana mapema mno. Ni kiburi tu cha CCM na watanzania wengine wasiotaka kuthubutu. CCM must go!
 
Back
Top Bottom