CHADEMA yaendelea kuigalagaza CCM ktk chaguzi ndogo jimbo la Buchosa - Sengerema

Kweli CCM ilikufa rasmi 2010, maziko ni 2015. Wanapigwa mijini hadi vijijini na hakuna mtetezi.
MNARA UKIANZA KUPOROMOKA DAWA NI KUUKIMBIA ILI KUSALIMISHA MAISHA YAKO, UKIJARIBU KUUZUIA UTAKUANGUKIA NA KUKUUA.
Kujaribu kuinusuru CCM ni kujitakia kifo!
 
Sugu alimaliza kwa kusema "...Huu siyo upepo bali ni KIMBUNGA, kama hakita angusha nyumba basi lazima paa ling'oke.." Sasa tunashuhudia vijijini nyumba na paa za kisiasa zina ondoka, kimbunga hiki kitafika magogoni 2015 tena kikiwa na nguvu ya ajabu.
 
Tanzania bila ccm inawezekana.Wao waache wajilopokee na mawaziri wanaoteleza sera zao jangwani-jukwaani kwa mdomo.Waache tu mawaziri wazunguke TZ nzima kisha walipe allowances zinazotokana na kodi zetu.Sisi wengina hatuna hela za kusomba watu kwenye malori lakini tunazo akili za kufanya watu watusikilize na kutuelewa.R.I.P MAGAMBA
 
Tru, nimeshindwa kuamini kuna kijiji kimoja kipo mbinga ( mwisho wa barabara) kinaitwa kingole. Ni kijiji ambacho niliamini ni mtaji wa ccm kwani bado watu wake hawamaliza stage ya ujima. Wiki iliyopita alitembelea mshua wangu anaitwa a.k.a Mzee Zito. Sikuamini kusikia wameasi kijiji kizima wapo chadema. NiLIMUULIZA wanapataje uhamasishaji kwani mf gari huenda mara 1 kwa mwezi.simu hakuna, redio ni TBC tu. Wakasema hukusanyika kwa jamaa mmoja ambaye ana jenereta, TV, na dish kuangalia Taarifa za habari ITV,TEN, NK.

Kwa kweli wamehamasika
 
Safi sana vijijini wameamka na hawadanganyiki kwa pilau wala khanga za bure,
itafika kipindi Nape atavaa khanga zake mwenyewe,
Pongezi kwa watu wa Kalebezo.
 
Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeesssssssssssssssspoooooooooooooooweeeeeeeeeeer

raaaaaaaaaaaahhhhhhhhhhhhaaaaaaaaaa
 
Siku ukiwa hai, tambua kuwa Mungu ni mwema na mara zote husikiliza na kujibu sala za wanyonge wanaoonewa na CCM.
 
Vijiji vya Kalebezo na Magulukenda vyote viko kata ya Kalebezo jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema na ndipo CDM ikawagaraza mafisadi ktk uchaguzi ulifanyika hapo vijijini leo.

Viva Chama makini kwa wanainchi wake!

Natamani kujua kama vijiji hivyo vilikuwa chini ya CCM au CHM hapo kabla? Uchaguzi umefanyika kwa sababu gani? Tuletee na hizo pia.
 
Katika uchaguzi mdogo uliofanyika jana kuchagua wenyeviti wa serikali za vijiji vya Kalebezo na Magurugenda, kata ya Kalebezo, jimbo la Buchosa,chama cha Demokrasia na Maendele (CHADEMA) kimekichakaza vibaya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutwaa vijiji vyote viwili ambavyo awali vilikuwa vikishikliwa na CCM.

Katika kujiji cha Magurukenda mgombea wa CHADEMA bwana William Sweke alimshinda mgombea wa CCM kwa kupata kura 277 dhidi ya 259 za mpinzani wake. Na katika kijiji kikubwa na maarufu cha Kalebezo, mgombea wa CHADEMA bwana Paulo Shagembe alimbwaga vibaya mpinzani wake kwa kuapata kura 670 dhidi ya 533. Huu ni ushindi wa tatu mfululizi kwa CHADEMA katika chaguzi ndogo nne za vijiji zilizokwisha fanyika mpaka sasa.

Katika uchaguzi mwingine mdogo uliofanyika mwezi April mwaka huu katika kijiji cha Mwabasabi kata ya Nyehunge, CHADEMA waliibuka washindi pia kwa kutwaa kijiji kilichokuwa mikononi mwa CCM. Wimbi hili la ushindi kwa CHADEMA ni mwendelezo wa kimbunga cha mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayozidi kushika kasi katika jimbo la Buchosa.

Mabadiliko haya yalioanza tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo mgombea ubunge wa Chadema alishindwa kwa mazingira ya kutatanisha, yameanza kulikumba pia jimbo la Sengerema hasa baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa diwani wa kata ya Nyampurukano na kujindoa kabisa ndani ya CCM na kujiunga CHADEMA mapema mwaka huu. Hongera wana Kalebezo na Magurukenda, hongerea
wana Buchosa!

Chanzo: Ikwalala
 
Ningeliijua nchi iliyonyoofu nami ningeifuata; CCM, kufa mara mbili ni mpaka umewahi kufufuka. Vinginevyo kufa ni mara moja tu, Please RIP CCM.
 
Back
Top Bottom