Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,269
- 675
MATOKEO ya uchaguzi wa udiwani wa kata ya Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar es Salaam yaliyomtangaza mgombea Uloleulole Athumani wa CHADEMA kuwa ni mshindi, yamebatilishwa na Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu.
Uamuzi huo umetolea leo Mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Genvitus Dudu katika kesi ya kupinga matokeo hayo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo.
Dudu katika uamuzi wake alisema amesikiliza mashahidi wa pande zote mbili, mahakama imeona mdaiwa katika fomu yakugombea nafasi hiyo, aliandika jina la Uloleulole Juma Athumani wakati kwenye hati ya kisheria lipo jina la Juma Uloleulole Athumani.Alisema mahakama hiyo imeona kwamba hao ni watu wawili, inakubaliana na Bulembo (mdai) kuwa kungekuwa na hati ya kiapo inayoonyesha mdaiwa alibadilisha jina lake.
Alisema kutokana na kukosekana na hati hiyo, inatosha kumvua mdaiwa nafasi aliyokuwa nayo na pia katika hati ya kisheria anayotakiwa kutia saini mbele ya hakimu, mdaiwa imeweza kuleta mashaka kwa kuwa ina tarehe mbili tofauti.Alisema hati hiyo inaonesha mdaiwa alitia saini Agosti 14, mwaka 2010 na ya pili inaonesha hakimu alitia saini Agosti 18, mwaka 2010 mahakama inashindwa kuelewa kama kweli mdaiwa alitia saini mbele ya hakimu au la.
Aidha Hakimu huyo alisema wananchi wananyimwa haki yao kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria hawakuweza kujua vigezo vya mgombea kutokana na kwenda kinyume cha Sheria ya Uchaguzi mahakama hiyo inaona uchaguzi wa udiwani wa kata ni batili.Kutokana na hayo, alisema maombi ya mdai yamefanikiwa kwamba matokeo ya uchaguzi yaliyomtangaza mdaiwa ni mshindi ni batili.
Hata hivyo alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kumtangaza Bulembo kuwa ni mshindi na kusema uchaguzi urudiwe kwani mamlaka hayo yapo kwenye mamlaka nyingine.Bulembo alifungua kesi hiyo, akidai kutoridhishwa na matokeo hayo ya uchaguzi huku akiwa amewasilisha sababu sita.
Katika sababu hizo aliiomba mahakama itamke matokeo batili, atangazwe yeye ndiyo diwani au kufanyike kwa uchaguzi wawazi na huru.Hata hivyo mahakama ilisema pande zote mbili kama kuna ambaye hajaridhika na uamuzi huo anayo haki ya kukata rufani.