CHADEMA yaanza mikakati mizito ya ushindi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
Dk. Slaa: Tutachukua madaraka 2015
• Mikakati mizito ya ushindi yaanza

na Tamali Vullu
Tanzania Daima




CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitachukua hatamu za uongozi wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa madiwani, ubunge na urais wa mwaka 2015.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, katika mkutano maalumu wa viongozi wa Kanda ya Dar es Salaam wa chama hicho, ambapo Dk. Willibrod Slaa alikuwa mgeni rasmi.

Dk. Slaa alisema kwa sasa chama hicho kimeanza kuandaa mikakati mizito yenye mbinu za kisasa na za uhakika ili kiweze kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambayo hata hivyo, hakuweza kuitaja.
Hata hivyo, aligusia kuwa hivi sasa chama hicho kimefanya marekebisho ya ratiba ya uchaguzi wake wa ndani, ili kuweza kujipanga vizuri kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

“Nimetoa waraka wa kufanya marekebisho ya ratiba ya uchaguzi ndani ya chama. Badala ya kufanyika kila baada ya miaka mitano ambayo huwa karibu na mwaka wa Uchaguzi Mkuu tumerudisha nyuma, hivyo chaguzi ndani ya chama zitaanza mwakani katika ngazi mbalimbali na kukamilika mwaka 2013.
“Tunaamini tukifanya uchaguzi mapema tutaweza kumaliza makovu ya uchaguzi huo, hivyo kuingia katika Uchaguzi Mkuu tukiwa kitu kimoja,” alisema Dk. Slaa.

Alisema sasa CHADEMA kimepokewa vema na kukubalika kuwa chama cha Watanzania wengi, hivyo ni muhimu viongozi kuanza kufikiri tofauti, ili waendane na matakwa ya wananchi.
“CHADEMA ni tumaini jipya, hivyo haiwezi kuwa na mbinu zilezile zilizotumika mwaka 2010, hivyo viongozi hamtakiwi kuacha fikra kwa ngazi moja. Fikra za mbinu mbalimbali zinatakiwa zitoke kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na hata taifa, kwani tunahitaji mabadiliko ya kifikra,” alisema.

Aiwataka viongozi hao kusambaza waraka huo kwa wanachama na kufanya kazi ya kuwaelimisha. Aliongeza kuwa kiongozi atakayeshindwa kufanya hivyo atakuwa ameshindwa kwenda na kasi ya chama hicho.

“Muda wa kubebana sasa umekwisha, atakayeshindwa kutekeleza haya itafika mahala tutachapana, ni lazima waraka huo ufike chini kwa wananchi. Nitapita eneo kwa eneo kuhakikisha kama hilo limefanyika na kwa watakaoshindwa kufanya hivyo nitatumia katiba kuwaondoa na kuwaweka viongozi wa muda. Hatuwezi kuendelea na viongozi wa aina hii,” alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa na viongozi hao.

Dk. Slaa aliwataka viongozi hao kukutana naye Januari 5, mwakani ambapo watatoa taarifa ya utekelezaji wa waraka huo pamoja na ushahidi.
“Chama si kitu cha mchezo. Watu tunahangaika nchi nzima na tumeweka rehani maisha yetu, wengine mnakaa tu, nawaambieni sasa tutachukua maamuzi magumu,” alisema.

Alisema chama hicho kitaweza kufanikiwa zaidi iwapo watainua sauti za wanyonge, hivyo viongozi wabadilike katika utendaji kazi.

Dk. Slaa alisema CHADEMA kinatarajia kutumia njia ya ‘database’ kuwasiliana na wanachama wake kama walivyofanya viongozi wa chama hicho mkoani Arusha.
“Kwa kutumia mfumo huo, ukituma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) moja inaweza kufika kwa wanachama zaidi ya 5,000, hivyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa viongozi kusanyeni namba za wanachama wetu ili tuingize kwenye utaratibu wa aina hiyo,”alisema.

Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alionesha kukerwa kwake na mgogoro unaotaka kuibuka katika Jimbo la Segerea, huku ikijulikana kuwa aliyekuwa mgombea wao, Fred Mpendazoe, amefungua kesi ya kupinga matokeo ambayo inaendelea vizuri mahakamani.

“Segerea nianze na ninyi, nimewapa maelekezo hamjayafanyia kazi. Chama kimetumia sh milioni 12 katika kesi ya kupinga matokeo ya jimbo hilo na inaendelea vizuri, sasa viongozi mmeanza migogoro.
“Mmeanza kueleza mabaya ya Mpendazoe. Mpendazoe si mtu wa kawaida. Nawapa wiki mbili mgogoro huo uwe umeisha, kwani ni mgogoro wa kipuuzi,” alisema.

Aliwashauri viongozi hao kuanzisha matawi na kusimika mabalozi wa nyumba tano, kwani huo ni mtaji wa kisiasa na kuongeza kuwa ni lazima chama kifanye kazi kisayansi.

Akizungumzia mchakato wa Katiba mpya, Dk. Slaa alisema ni lazima mchakato huo urudi kwa wananchi ili waweze kutoa maoni yao na kuongeza kuwa CCM inahofia suala hilo kwa kuwa hawakubaliki kwa wananchi.

“Tukiruhusu Rais Kikwete aunde tume hakuna cha maana kitakachofanyika. Mimi nina uzoefu, nilikuwa mbunge na najua uovu wote na pia nilikuwapo kwenye Tume ya Jaji Kisanga. Wakati ule tume inakusanya maoni, CCM ilituma mawaziri wake waende kwa wananchi na kuwafundisha jinsi ya kujibu hata kabla tume haijaenda, hivyo tume ile iliyoundwa ilikuwa ni geresha tu,” alisema.

Alisema rais akishaunda tume wananchi hawana mamlaka, ndiyo maana wanaipinga na kwamba ikiwapo hata maoni yatakayotolewa na wananchi hayatafanyiwa kazi.
Kwa upande wake, Mbunge wa Ubungo John Mnyika, alisema kinachofanyika sasa ni kuwaelimisha viongozi wao kuhusu sheria ya mabadiliko ya Katiba na baada ya hatua hiyo watakwenda kwa wanachama wa kawaida.

Alimshauri Rais Kikwete asiunde tume ya kukusanya maoni kuhusu Katiba mpya, kwani akifanya hivyo atasababisha mgogoro.
“Pamoja na rais kusaini muswada huo tunamshauri sheria hiyo isianze kutumika mpaka yatakapofanyika marekebisho ya msingi. Akiunda tume, hatutashiriki, bali sisi tutakwenda kwa wananchi na kuwaeleza kuhusu jambo hilo, njia tutakazotumia tutazieleza baadaye iwapo jambo hilo litatokea,” alisema.


 
"Nimetoa waraka wa kufanya marekebisho ya ratiba ya uchaguzi ndani ya chama. Badala ya kufanyika kila baada ya miaka mitano ambayo huwa karibu na mwaka wa Uchaguzi Mkuu tumerudisha nyuma, hivyo chaguzi ndani ya chama zitaanza mwakani katika ngazi mbalimbali na kukamilika mwaka 2013.
"Tunaamini tukifanya uchaguzi mapema tutaweza kumaliza makovu ya uchaguzi huo, hivyo kuingia katika Uchaguzi Mkuu tukiwa kitu kimoja," alisema Dk. Slaa.

Nakukumbuka tulijadili hili sana hapa JF wakati Dr alipoteuliwa kuwa mgombea Urais. It was too late na hakupata muda wa kijinadi. Hata kufanya uchaguzi 2013 halafu uchaguzi mkuu ni 2015, bado naona atakayechaguliwa atakuwa na muda mfupi sana wa kutandaza zege. Kwa nini wasifanye kama wanavyofanya in the West? Kwamba baada ya Uchaguzi mkuu, kama mgombea urais hakufanikiwa kushinda, then chama kinafanya uchaguzi immediately after the general election. Hapo atakuwa na at least miaka minne ya kujijenga na kuzunguka nchi kunadi sera za chama.

Having said that sidhani kama ni sahihi kwa Chadema kusema kuwa kitachukua hatamu ya uongozi katika uchaguzi ujao. The ultimate decision itakuwa kwa Watanzania kama kweli wanataka mabadiliko. Are Tanzanians ready for a change? Few but not all.
 
Nakukumbuka tulijadili hili sana hapa JF wakati Dr alipoteuliwa kuwa mgombea Urais. It was too late na hakupata muda wa kijinadi. Hata kufanya uchaguzi 2013 halafu uchaguzi mkuu ni 2015, bado naona atakayechaguliwa atakuwa na muda mfupi sana wa kutandaza zege. Kwa nini wasifanye kama wanavyofanya in the West? Kwamba baada ya Uchaguzi mkuu, kama mgombea urais hakufanikiwa kushinda, then chama kinafanya uchaguzi immediately after the general election. Hapo atakuwa na at least miaka minne ya kujijenga na kuzunguka nchi kunadi sera za chama.

Having said that sidhani kama ni sahihi kwa Chadema kusema kuwa kitachukua hatamu ya uongozi katika uchaguzi ujao. The ultimate decision itakuwa kwa Watanzania kama kweli wanataka mabadiliko. Are Tanzanians ready for a change? Few but not all.
Nafikiri alikuwa na maana ya kujiandaa kichama sio kumtangaza mgombea.
 
Wenye madharau na mzaha kwa maoni ya CHADEMA nchini, miguu itawaota tende bila kujijua tungali bado hatujafikia hata 0.025 ya mchakato mzima wa kurejesha HESHMA, HAKI NA UTU wa Mtanzania kwa njia zote halali na za demokrasia isioacha hata kijiji kimoja ndani ya mipaka yetu.

Vijana twendeni kazini kujivunjia minyororo yote hii ya MKOLONI MWEUSI mabegani mwetu.
 

Dk. Slaa alisema CHADEMA kinatarajia kutumia njia ya ‘database' kuwasiliana na wanachama wake kama walivyofanya viongozi wa chama hicho mkoani Arusha.
"Kwa kutumia mfumo huo, ukituma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) moja inaweza kufika kwa wanachama zaidi ya 5,000, hivyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa viongozi kusanyeni namba za wanachama wetu ili tuingize kwenye utaratibu wa aina hiyo,"alisema.





Tukimaliza hilo, tunataka kukamilishwa mipango ya cdm tv!
 
Dr. Asifikiri mgogoro wa kipuuzi upo Segerea tu!hata huku Bariadi uongozi wilaya unamgogoro mkubwa sana mpaka viongozi washafikishana mahakamani!na kuna ofisi mbili za wilaya,wenyeviti wilaya wawili!huku mimi naona ni kubomoa na si kujenga!iweje wilaya moja iwe na ofisi 2 za wilaya,wenyeviti 2 wa wilaya huku kila ofisi ikijinadi kuwa yenyewe ndiyo inatambulika!huu ni upuuzi mwingine,hususani kipindi hiki cha chama kujiimarisha katika ngazi zote.Wito wangu kwa Dr. Ninamuomba afuatilie pia mgogoro wa Bariadi hii ni kwa sababu hata viongozi ngazi ya mkoa wamepandikiza watu wao kwenye mgogoro huu!
 
Kwenye msafara wa Bundi lazima hawepo Bundi wa kuwaongoza wenzake!
 
Hiyo ni mipango ya kwenye makaratasi,, utekelezaji wake ni sehemu ingine tena, ina changamoto nyingi na mapito mengi, je? Ukomavu na uvumilivu wenu utawafikisha 2015 bila kupigana vikumbo ninyi kwa ninyi?.. mna lengo zuri lakini jipangeni kitaifa acheni siasa za kulipua mabomu waelezeni wananchi niya na madhumuni ya kutaka kuwaongoza kujenga kuheshimiana na kuaminiana ndani ya chama chenu na vyama vingine , serikari na vyombo vyake.
 
Hii ndio mipango niliyokuwa naifikiria,kweli CDM ni makini...safi Dr na makamanda wengine.....
 
Hiyo ni mipango ya kwenye makaratasi,, utekelezaji wake ni sehemu ingine tena, ina changamoto nyingi na mapito mengi, je? Ukomavu na uvumilivu wenu utawafikisha 2015 bila kupigana vikumbo ninyi kwa ninyi?.. mna lengo zuri lakini jipangeni kitaifa acheni siasa za kulipua mabomu waelezeni wananchi niya na madhumuni ya kutaka kuwaongoza kujenga kuheshimiana na kuaminiana ndani ya chama chenu na vyama vingine , serikari na vyombo vyake.


Nimependa ushauri wako
 
Back
Top Bottom