CHADEMA yaandaa mapokezi ya kifalme kwa Millya

Arusha Leo

Senior Member
Mar 12, 2012
122
72
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kumwandalia sherehe kubwa ya kumpokea mwanachama wake mpya, James Ole Millya aliyekihama chama cha mapinduzi CCM na kujiunga na chadema akidai ccm ni gari lenye pancha kibaooooooooooooo.



Millya mbaye alikuwa mwenyekiti cha UVCCM mkoa wa Arusha,anatarajia kukabidhiwa kadi kifalme sanjari na sherehe kubwa ya kihistoria ambapo wananchi wamejitolea kuchangia sherehe hiyo kijijini kwake wilayani Simanjiro,ikiwemo kujitolea ngómbe wa nyama.



Akizungumza leo kwa njia ya simu , Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema kuwa kwa sasa chama hicho , wanafanya mawasiliano na Viongozi wa Chama hicho kutoka Mkoa wa Manyara na Wilayani Simanjiro, juu ya kuweka mazingira ya kumkabidhi kadi ya uwanachama wa chadema ndani ya wiki hii.


 
mgeni rasmi?

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kumwandalia sherehe kubwa ya kumpokea mwanachama wake mpya, James Ole Millya aliyekihama chama cha mapinduzi CCM na kujiunga na chadema akidai ccm ni gari lenye pancha kibaooooooooooooo. Millya mbaye alikuwa mwenyekiti cha UVCCM mkoa wa Arusha,anatarajia kukabidhiwa kadi kifalme sanjari na sherehe kubwa ya kihistoria ambapo wananchi wamejitolea kuchangia sherehe hiyo kijijini kwake wilayani Simanjiro,ikiwemo kujitolea ngómbe wa nyama. Akizungumza leo kwa njia ya simu , Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema kuwa kwa sasa chama hicho , wanafanya mawasiliano na Viongozi wa Chama hicho kutoka Mkoa wa Manyara na Wilayani Simanjiro, juu ya kuweka mazingira ya kumkabidhi kadi ya uwanachama wa chadema ndani ya wiki hii.
 
Mpokeeni lakini angalieni asijekuwa katumwa. Kunanini mpaka amuache fisadi papa ambaye alikuwa nae kwa muda mrefu (EL) mpaka ahamie CHADEMA?
 
nategemea hii habari siyo ya kweli...kama ni ya kweli basi kuna maswali mengi ya kujiuliza...
 
Tunamkaribisha sana,karibu milya ,vua magome/magamba na uchukue kombati.karibu katika harakati za kulikomboa taifa letu toka kwa mafisadi na kuingia kwa vijana wapenda maendeleo.Ila angalizo kwa CDM kamati ya wazee imchunguze vizuri huyu mtu asije kuwa mzigo na matatizo kwa chama,pls msije mkaingia kichwa kichwa yakatukuta ya Shibuda.
 
Nilishasema jamani huyu mpelekeni akaungane na Lema kwenye M4C. Then M4C ipewe watu wa kuisimamia yaani Lema, Milya na mwengine aliye Idle na support kutoka kwa Management ya CDM.

Tanzania amka sasa.
 
ufalme wa ole millya unatokana na nini hasa?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
ufalme wa ole millya unatokana na nini hasa?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

hata mimi nashangaa kama ni mtego basi cdm imeuingia kichwa kichwa ni ajabu kwa cdm kumfurahia mtu huku wakiwa hawana uhakika kama kweli mtu huyu ni mpigananji wa kweli au spy tu?
 
ufalme wa ole millya unatokana na nini hasa?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

tumeamua kumpa Millya mapokezi ya kifalme kwa sababu ni moja ya watu ambao walikuwa na nguvu kubwa ndani ya Magamba na nina imani Millya ataleta wanachama sio zaidi ya 5000, na katika hao wanachama na amani kila mwanachama ataleta angalau wanachama watano, hiyo nfo faida, KWA KUA WEWE NI JINGA LAO HUWEZI KUELEWA
 
Mpokeeni lakini angalieni asijekuwa katumwa. Kunanini mpaka amuache fisadi papa ambaye alikuwa nae kwa muda mrefu (EL) mpaka ahamie CHADEMA?
Huwa hata masista duu hujificha hadi kwa masela wahidhani kuwa watamaliza kisirisiri,ila baadaye wanajikuta wamebeba, baadaye wanajikuwa mapromise na matozi sijui ya kuishi km Jay Z na Beyonce hayana dili tena.

SIJUI KWANINI AKAVUNJE CDM WAKATI HANA HAKIKA KM AKIMALIZA VUNJA CDM ATAIKUTA CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom