Scolari Ndenga
JF-Expert Member
- Aug 4, 2008
- 271
- 43
Wadau,
Katika kile kinchoonekana ni kuwaweka wananchama wake na wananchi kwa ujumla mguu pande mguu sawa, Chadema imeamua kusambaza viongozi na wabunge wake Tanzania nzima ili kuweka kinagaubaga msimamo wake na mchakato wake wa kuelekea kupata katiba mpya.
Katika kufanikisha hilo, Chadema kimeagiza kuitishwa kwa mikutano mikuu ya majimbo na mjadala wa katiba kwa maana ya kuweka wazi kwa nini wabunge wake walitoka bungeni, waraka wa chama kwa Rais kikwete, na msimamo wake wa kutoshiriki mchakato wa katiba iwapo hakutakuwapo na mabadiliko makubwa na ya msingi kama wanavyodai.
Ninachokioona hapo, Chadema wana mikakati mingi ambayo hawajataka kuioweka wazi kwa public kwa kua wanasubiri mabadiliko ya sheria kama walivyokubaliana na rais huku wakiendelea na michakato ya kuwaweka wanachama wao mkao wa kijeshi.