CHADEMA waweka mkazo Serikali za majimbo

Hongera Mbunge wangu Wenje, Hilo la vyuo vikuu huwa linanikera sana, sijawahi kusikia mbunge yeyote toka kanda ya ziwa akilalamika kuhusu kukosekana kwa Chuo cha Serikali Kanda ya Ziwa. Wakatoliki wamesaidia sana mikoa ya kanda ya Ziwa mimi nadhani hao ndo serikali yetu kwa watu amabao idadi yao inayokadiriwa kuwa 15 million. Serikali ya majimbo ni suluhisho. Siyo viserikali vya mitaa visivyokuwa na lolote.
 
Wabongo wakisikia majimbo akili zao zinaenda US na Nigeria na kuanza kutoa mapovu juu ya wote wanaozungumzia suala hlo.
Mi nadhani ni mfumo mzuri sana kama tuki-uhariri kulingana na asili ya taifa letu na utamaduni wetu.
Tuchukue mazuri toka kwa nchi zenye mfumo kama huo, tuyapitie mabaya yake tutapata changamoto mpya.
 
Na ukishakuwa gwanda kila jambo litalosemwa na mitume wenu mnaona ndiyo suluhisho.Hivi unafikiri kanda ya ziwa ina rasilimali nyingi kuliko kanda ya kusini?
hovyoooo!!!

Mkuu wangu Kobello, mbona kama unazungumzia hoja hyo hyo tu.
Kweli kanda ya kusini ni tajiri zaidi nakubaliana na wewe, ila kwa mpaka sasa tuna uhakika mmoja kuwa pamoja madhaifu mengine ila mpangilio wa kiutawala wa nchi yetu ni una mkanganyiko zaidi hvyo kupelekea kanda zote kutokuvuna kinachostahili,
katika kuleta muafaka kwa maendeleo yetu kuna watu tunadhani labda pamoja na kurekebisha madhaifu hayo ila pia tubadili mfumo tutumie majimbo!
Je wewe unasemaje?
Kiukweli kanda zote za hii nchi ni tajiri sana na kila moja inamzidi mwenzie kitu fulani hvyo kulazimisha kutegemeana hata tutakapokuwa kwenye hayo majimbo- tunaweza kupata namna ya kuliandika hlo kwenye katiba yetu.
Pia ikumbukwe rasilimali mama ni Ardhi na Watu ambavyo vipo vya kutosha nchi nzima,
na kama tutazingatia kilio cha Prof Shivji juu ya suala la ardhi kuwa ni suala la kikatiba mi sioni ugomvi wetu utokee wapi!
 
.....bado naamini..tatizo letu si mfumo wa kiutawala uliopo...hasha! .. ni rushwa..( ambayo kimsingi ndio baba na ndio mama wa mabalaa yote tunayoyajua... upendeleo wa kikabila/ kidini, majungu, fitina, unafiki,mapungufu ktk uzalendo wetu, umasikini, mapungufu ya kidemokrasia ndani ya vyama vya siasa..nk nk)......nahofia hata mfumo wa majimbo, hautakuwa na matokeo tunayoyafikiria kama kwanza hatutakuwa tumepambana na kuishinda rushwa...comrades...lets get above our parties politics, and fight this "joka kuu of our tym"...
 
Back
Top Bottom