CHADEMA waweka bayana msimamo wao juu ya yaliyowasibu ma-Sheikh Ponda na Farid

Unafiki wake ni kuongelea dhamana?

profesa safari ni mdau mkubwa sana wa radio imani na radio quran, na magazeti ya al nuur....ikama anaongea hivyo ni mnafiki wa ajabu. ni kitu cha ajabu sana kwamba mtu fanatic kama safari yupo chadema, huyu jamaa ni mdini hakuna mfano, kuna mtu asiyemjua prof safari jamani? hata akiwepo chadema ajue tu kwamba anatakiwa kujifunza kutokuwa mdini. atasemaje waislam wavute subira badala ya kusema waislam waache mara moja ujinga huu? kwani na uprof wake wote hajui kama aliyekojolea kuran ni mwislam, na kwamba ponda hajazuiliwa na selikali per se, bali amezuiliwa na ofisi ya dpp. pamoja na kwamba ofisi ya dpp inawakilisha mashitaka ya jamhuri lakini hii sio moja kwa moja kwamba selikali kuu imeamuru uyo al shabab asipewe dhamana, halafu jambo lenyewe liko mahakamani, kama wao wanaona hiyo si haki na kwamba ponda ana haki ya dhamana si wana wakili wake, wakate rufaa mahakama kuu dhidi ya hiyo certificate ya dpp kuzuia dhamana..kwani tatizo liko wapi? yaani hata mahakama zikifanya lolote lile tunataka ziwasikilize waislam? kwani waislam ni juu ya mahakama? halafu, kwanini kuilaumu serikali peke yake, kwani hakimu kama angeona hio sio sababu ya msingi si angeitupilia mbali certificate ya dpp kuzuia dhamana na upande wa mashitaka/jamhuri wangekata rufaa? mbona tunataka kufanya mahakama ziwe zinaamriwa na wanachi badala ya kuiacha mahakama kuwa huru? kwanini hakimu hajaitupilia mbali hiyo pingamiZI, that means kila mtu amemchoka shehe ponda na kila mtu anamuombea mabaya tu. mtu aliyeichafua tz hadi hivi sasa tumefikia hapa.
 
Unafiki wake ni kuongelea dhamana?
unafiki wake ni kwamba namfahamu. huyo prof amenifundisha evidence law pale udism kama hujui, ninamfahamu kuliko unavyofikiri. ni mtu mwenye siasa kali sana za kiislam, wenzio wanamjua, sijui wewe. sasa anavyoongea hivyo ni unafiki tu, haitoki moyoni mwake.
 
Kwa hiyo kila anaye dai kile anacho amini ni haki yake aangamizwe?
tatizo anavyodai utafikiri tz yote ni mali yake peke yake, bila kujua kuwa kuna watu wengine ambao wanaimiliki tz hii ambao hawaamini anachoamini yeye wala hawasapoti anachosapoti yeye sasa cha muhimu hatakiwi kulazimisha kila mtu aishi au aamni vile anavyoamini yeye. ni upungufu wa akili kuishi kama ponda. ni mtu ambaye hahitajiki hapa duniani kwasababu anasababisha maisha ya wanadamu kuwa magumu badala ya kuwa mazuri, na yeye akilini mwake anaamini kuwa anatetea watu. ni gaidi hakuna mfano wake.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekutana na waandisihi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam leo, ambapo wajumbe wa Kamati Kuu, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, wameweka waziwazi msimamo wa chama hicho kuhusiana na mgogoro kati ya waislamu na serikali na kukamatwa kwa Sheikh Farid huko Zanzibar.

Wanasheria hao wa CHADEMA wamesema kuwa kitendo cha serikali kumnyima dhamana Sheikh Ponda ni kinyume cha katiba na kwamba Chadema kama chama kinachojiandaa kuchukua dola, hakiwezi kuvumilia kuona haki za raia zikivunjwa.

“Tunaweza kuwa miongoni mwetu, wapo watu wanaomchukia Sheikh Ponda, lakini hatuwezi kuficha ukweli kwamba Sheikh Ponda kama raia wa Jamhuri ya Muungano au mkazi wa Jamhuri hii, anayo haki ya kusikilizwa na kupewa dhamana. Makosa ambayo Sheikh Ponda ameshitakiwa yanadhaminika kwa mujibu wa sheria, hivyo ni makosa kwa serikali kufanya hila kumnyima dhamana kiongozi huyu wa kidini,” ameeleza Marando katika mkutano huo.

Marando alifika mbali zaidi kwa kusema tatizo lililopo sasa kati ya serikali na waislamu, limetokana na hatua ya serikali kuwalazimisha waislamu wote kuwa waumini wa Bakwata, chombo ambacho wengi wanakiona kinatumika kuwakandamiza.

Naye Profesa Safari alionya matumizi ya nguvu za kijeshi yanayotumiwa na serikali kwa kisingizio cha kulinda amani, huku akieleza kuwa matumizi ya kijeshi siyo suluhu ya kutatua matatizo yaliopo.

Kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Faridi na kumzuia kwa siku tatu, wanasheria hao wamesisitiza kuwa kitendo hicho hakikubaliki.

“Kitendo cha kumkamata na kumshikiria Sheikh Faridi, huku serikali na vyombo vyake vikisema havihusiki, wakati ukweli ni kuwa alikuwa anashikiliwa na watu wa USALAMA wa TAIFA, ni uharamia mkubwa unaopaswa kulaaniwa na wote wanaolitakia mema taifa hili,” ameeleza Marando.

Kuhusu uvunjwaji wa makanisa, Profesa Safari amesema CHADEMA kimelaani hatua hiyo iliyotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi. Amewataka waislamu kuvuta subira.

Hata hivyo, Profesa Safari amesena matatizo yanayotokea sasa, yameletwa na CCM kutokana na hatua yao ya kuwatumia baadhi ya waislamu kupandikiza mbegu ya udini nchini.

Jamani hawa jamaa wamesema wamesema mengi, lakini kwa sasa yanatosha kueeleza hayo.

Sijalipenda hili tamko la CDM.Tusilete siasa kwenye jambo linaloweza kuhatarisha Amani ya Nchi
 
Lakini aliyo yaongelea ni mambo ya msingi kwa haki za binadamu!

Na hata swala la kuchomwa makanisa wame li laani!
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
unafiki wake ni kwamba namfahamu. huyo prof amenifundisha evidence law pale udism kama hujui, ninamfahamu kuliko unavyofikiri. ni mtu mwenye siasa kali sana za kiislam, wenzio wanamjua, sijui wewe. sasa anavyoongea hivyo ni unafiki tu, haitoki moyoni mwake.
 
Ukilisoma vizuri hilo tamko utagundua wamejaribu kuwapa fursa kila upande, kwani kilicho na watu waliochoma makanisa haikubaliki pamoja na makosa aliyo kuwa akiyafanya ponda na walicho jaribu prof safari na Marando ni kuonesha kuwa pamoja na kuwa na makosa yote yale lakini ana haki ya kupata dhamana!

tatizo anavyodai utafikiri tz yote ni mali yake peke yake, bila kujua kuwa kuna watu wengine ambao wanaimiliki tz hii ambao hawaamini anachoamini yeye wala hawasapoti anachosapoti yeye sasa cha muhimu hatakiwi kulazimisha kila mtu aishi au aamni vile anavyoamini yeye. ni upungufu wa akili kuishi kama ponda. ni mtu ambaye hahitajiki hapa duniani kwasababu anasababisha maisha ya wanadamu kuwa magumu badala ya kuwa mazuri, na yeye akilini mwake anaamini kuwa anatetea watu. ni gaidi hakuna mfano wake.
 
sasa wanapiga makelele ya nini , si wakate rufaa kupinga certificate ya dpp kuzuia dhamana ili high court waipige chini, wao kama wanasheria maneno ya nini wakati jambo liko mahakamani?
 
one thing for sure
ndani ya CHADEMA hakuna anaejua kucheza michezo ya kisiasa
zaidi ya Marando....

na hili tamko ni la Marando binafsi na sio CHADEMA ...

this guy Marando is very very interesting.....muulize Mrema akwambie lol...

una haja kubwa, unaingia bafuni hivi inawezekana....???

V
SENGEREMA
 
Hivi ungekuwa wewe ungetoa tamko gani? Hebu liandike hapa tuone! Kusema Sheikh Ponda kama raia wa nchi hii anastahili dhamana ni kutafuta umaarufu? Wakati mwingine kukaa kimya ni busara zaidi kuliko kuropoka.

ndo maana nikasema good move.katika post history yangu huwezi kuta nimewapongeza hao cdm mara kwa mara.ina maana nimeikubali.
 
Ukiliangalia hili Tamko kwa kuvaa hisia za udini hautalifurahia,ukilangalia kwa kuvaa hisia za haki utalifurahia na kukipongeza CHADEMA kwa kutoa msimamo thabiti kabisa.Tuwe sehemu ya mabadililko tuyatakayo hasa tunapokuwa katika jamii inayoongozwa na utawala dhalimu usiojali haki ya raia wake.You can't build a nation on the sacrifice of equity, it just isn't worth it
 
Nyie mnaoikashafu cdm kwa tamko ndo mnaonfnya niamini kuwa mnakipenda kwa kuwa ni chama cha kikristo kama ccm na baadhi ya watu wanavyosema.cdm wametoa tamko la maana tu ila udini ndo unaowasumbua!'
 
Sijalipenda hili tamko la CDM.Tusilete siasa kwenye jambo linaloweza kuhatarisha Amani ya Nchi
Amani ni Tunda la haki,Hebu lisome tamko la CHADEMA.Tulia kwa umakini mkubwa halafu tafakari tena hii post yako.Again,You can't build a nation on the sacrifice of equity, it just isn't worth it
 
Vyama vingi ndio chanzo cha haya matatizo yote tanzania.vinafanya serikali ishindwe kuwashughulikia wahalifu kwa kuogopa kupoteza kura.ingekuwa enzi zile hata jk mnayemsema kila siku asingekuwa hivi.unafiki ndio biashara ya siku..
Challenging and testing times is now.
 
mi naona we ndo hufai unaewatakia waislamu mabaya kamwe hayawafiki dua la kuku halimpati mwewe wewe.
 
Back
Top Bottom