CHADEMA waweka bayana msimamo wao juu ya yaliyowasibu ma-Sheikh Ponda na Farid

Sijapenda, hata kidogo. huyu mtu kasababisha madhara makubwa kwa mahubiri na kuhamasisha watu. Huyu ilibidi awekwe detention kama sheria ya detention bado inafanya kazi. Naipenda CDM, lakini kwa hili hapana.

Kamanda POMPO alisema nadhani siku tatu zilizopita kwamba kosa ililofanya serikali ni kuwaacha hao watu kwa muda mrefu bila kuwachukulia hatua. Imekuja kushtuka mtu ameshapata wafuasi na popularity. Unadhani ni kazi rahisi kudhibiti kazi za kina Ponda na Sheh Farid kwa sasa?. Hapana! Serikali imekosea Tyming.
 
Last edited by a moderator:
wazenji kama wanataka nchi yao, basi waipigie kura chadema

muungano utavunjika au utasukwa upya

safiiiiiiiiiiiiii
 
Wanataka kutumia nafasi hii ya dhahabu kupata kuumgwa mkono na waislamu.
Good move strategicaly
Hivi ungekuwa wewe ungetoa tamko gani? Hebu liandike hapa tuone! Kusema Sheikh Ponda kama raia wa nchi hii anastahili dhamana ni kutafuta umaarufu? Wakati mwingine kukaa kimya ni busara zaidi kuliko kuropoka.
 
leo tutashuhudia wafuasi wa chadema wakipingana na chama chao kwa mara ya kwanza.
Kisa, ni ishu ya waislam.

Kama ulikuwepo sasa ndio utajua kuwa wafuasi wa CDM ni watu wa aina gani.Nilishauri CDM watoe tamko naona wametoa, nimefarijika. Lakini wafuasi wengi wa CDM ni wadini. Na kwao wanaamini kuwa CDM ni chama cha Kikristo kama sio cha Kichagga.
 
Kama ulikuwepo sasa ndio utajua kuwa wafuasi wa CDM ni watu wa aina gani.Nilishauri CDM watoe tamko naona wametoa, nimefarijika. Lakini wafuasi wengi wa CDM ni wadini. Na kwao wanaamini kuwa CDM ni chama cha Kikristo kama sio cha Kichagga.


Hilo tamko lisingetolewa na SLAA
ndo maana amekwenda Marando lol
 
politics in a verything, everywhere.
huyu ponda ni mtu wa hatari sana.
sidhan kama anastahili huruma
 
....
........hatuwezi kuficha ukweli kwamba Sheikh Ponda kama raia wa Jamhuri ya Muungano au mkazi wa Jamhuri hii, anayo haki ya kusikilizwa na kupewa dhamana. Makosa ambayo Sheikh Ponda ameshitakiwa yanadhaminika kwa mujibu wa sheria, hivyo ni makosa kwa serikali kufanya hila kumnyima dhamana kiongozi huyu wa kidini,” .... matatizo yanayotokea sasa, yameletwa na CCM kutokana na hatua yao ya kuwatumia baadhi ya waislamu kupandikiza mbegu ya udini nchini.

Jamani hawa jamaa wamesema wamesema mengi, lakini kwa sasa yanatosha kueeleza hayo.

Wamejitahidi kuwapenda ndugu zetu na kiongozi wao Ponda BUT je ni kweli hata wanazuoni hawa hawana uhakika na uraia wa huyu sheikh Ponda? Kwanini waseme "raia au mkazi"
Nawapongeza pia kuwa wamemalizia vyema kuwa kile kilichokuwa chama cha wananchi tangu miaka 35 na zaidi iliyopita ndio "mzizi wenyewe wa fitna". Chama kikongwe na kijitokeze kitoe tamko, mbona mko kimya na nchi iko mikononi mwako?
 
Kama ulikuwepo sasa ndio utajua kuwa wafuasi wa CDM ni watu wa aina gani.Nilishauri CDM watoe tamko naona wametoa, nimefarijika. Lakini wafuasi wengi wa CDM ni wadini. Na kwao wanaamini kuwa CDM ni chama cha Kikristo kama sio cha Kichagga.

hongera kwa kuendeleza propaganda za udini na ukabila ulizopandikizwa na chama cha magmba
 
Ukweli unabaki kuwa ukweli tu! Pamoja na makosa ya sheikh Ponda lakini hakuna sababu ya msingi ya kumnyima dhamana na ni kukiuka haki za msingi za kibinadamu kwenye nchi inayojita ya kidemokrasia. Na hata swala la sheikh farid pia serikali haiwezi kuzikwepa lawama na hatawakisema hawakumteka pia bado hawaaminiki kuwa hawakumteka kweli maana hata Dr ully pia serikali imekana kuwa haikumteka lakini ukweli kila aliyefuatilia swala lile anajua ukweli.

Kuna wanaohoji tamko la chadema jinsi lilivyo au jinsi lilivyotoka, hao niwakupuuzwa maana chadema wanahaki ya kumtetea na kumsemea kila mtanzania anaye nyimwa haki zake za msingi kama jjinsi ilivyo kwa taasisi yoyote inayoitakia mema Tanzania yetu, kila mwana chadema mwenye kadi asome nyuma ya kadi yake wajibu wa kila mwanachadema kwenye kutetea haki. Wale wa ccm pigeni kimya washaurini wazee wenu wawaombe radhi watanzania kwa kueneza na kupandikiza mbegu ya udini huku wao wakitoreshea fedha uswis.
 
Back
Top Bottom