CHADEMA waweka bayana msimamo wao juu ya yaliyowasibu ma-Sheikh Ponda na Farid

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekutana na waandisihi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam leo, ambapo wajumbe wa Kamati Kuu, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, wameweka waziwazi msimamo wa chama hicho kuhusiana na mgogoro kati ya waislamu na serikali na kukamatwa kwa Sheikh Farid huko Zanzibar.

Wanasheria hao wa CHADEMA wamesema kuwa kitendo cha serikali kumnyima dhamana Sheikh Ponda ni kinyume cha katiba na kwamba Chadema kama chama kinachojiandaa kuchukua dola, hakiwezi kuvumilia kuona haki za raia zikivunjwa.

"Tunaweza kuwa miongoni mwetu, wapo watu wanaomchukia Sheikh Ponda, lakini hatuwezi kuficha ukweli kwamba Sheikh Ponda kama raia wa Jamhuri ya Muungano au mkazi wa Jamhuri hii, anayo haki ya kusikilizwa na kupewa dhamana. Makosa ambayo Sheikh Ponda ameshitakiwa yanadhaminika kwa mujibu wa sheria, hivyo ni makosa kwa serikali kufanya hila kumnyima dhamana kiongozi huyu wa kidini," ameeleza Marando katika mkutano huo.

Marando alifika mbali zaidi kwa kusema tatizo lililopo sasa kati ya serikali na waislamu, limetokana na hatua ya serikali kuwalazimisha waislamu wote kuwa waumini wa Bakwata, chombo ambacho wengi wanakiona kinatumika kuwakandamiza.

Naye Profesa Safari alionya matumizi ya nguvu za kijeshi yanayotumiwa na serikali kwa kisingizio cha kulinda amani, huku akieleza kuwa matumizi ya kijeshi siyo suluhu ya kutatua matatizo yaliopo.

Kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Faridi na kumzuia kwa siku tatu, wanasheria hao wamesisitiza kuwa kitendo hicho hakikubaliki.

"Kitendo cha kumkamata na kumshikiria Sheikh Faridi, huku serikali na vyombo vyake vikisema havihusiki, wakati ukweli ni kuwa alikuwa anashikiliwa na watu wa USALAMA wa TAIFA, ni uharamia mkubwa unaopaswa kulaaniwa na wote wanaolitakia mema taifa hili," ameeleza Marando.

Kuhusu uvunjwaji wa makanisa, Profesa Safari amesema CHADEMA kimelaani hatua hiyo iliyotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi. Amewataka waislamu kuvuta subira.

Hata hivyo, Profesa Safari amesena matatizo yanayotokea sasa, yameletwa na CCM kutokana na hatua yao ya kuwatumia baadhi ya waislamu kupandikiza mbegu ya udini nchini.

Jamani hawa jamaa wamesema wamesema mengi, lakini kwa sasa yanatosha kueeleza hayo.
 
Kwa hili am not supporting chadema wale majaaa hawafai chadema tulieni mtajiaibisha hakuna atae enda mtaaani tena

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nimependa sana tamko hili la CHADEMA maana lingekuwa ni la kuzidi kumkandamiza yule hayawani Ponda basi wale wote wanaoichukia CHADEMA wangepata nafasi ya kuchonga zaidi....``Unawaona hawa CHADEMA hakuna siku wanaweza kusimama kumtetea Muislamu nchi hii, wanawachukia sana Waislamu angekuwa ni Padri kakamatwa kauli ya CHADEMA isingemkandamiza Mkristo mwenzao``...Hongereni sana CHADEMA....

Sifagilii hata kidogo yaliyofanywa na Ponda kama sheria zinaruhusu apewe dhamana basi Serikali impe dhamana na masharti makali yakiambatana na dhamana hiyo, akivunja masharti hayo basi arudishwe lupango mara moja.

 
Hii ndio CHADEMA nayotaka kuiona, inayokuwa tayari kusema ukweli hata kama ukweli wenyewe unauma. Sheikh Ponda ni gaidi ila kwa kweli nadhani kumnyima dhamana ni makosa. Na inatupasa kukaa meza moja kuona namna tutakavyoyamaliza matatizo yetu kama watanzania. Waislamu+Wakristo ni ndugu tatizo ni CCM.
 
Tamko la kiuoga hili..naona ifike mahali tuweke siasa pembeni tusimamie sheria. Ponda na wenzake ni wa kufunga milele.
 
Hahahah am the great physician!!!

Nilisema hapa kuwa watakaoongea ndio hao na watakachoongea ndio hicho

Sababu

1. CHADEMA maandamano kwao ndio kawaida, hivyo hawawezi kucondemn

2. Vyombo vya dola kama mahakama na polisi haviaminiki kwao siku nyingiiiii so hawawezi kusema sheria ichukue mkondo wake

3.Kwavile hili jambo lina sura ya dini ,na liko mahakamani, na ili kuwe na a balanced statement; inabidi prof Safari na Tundu lissu (naona kaja Marando...sawa tu) ndio walisemee

4.Serikali na CCm zitalaumiwa


Big to the up CDM
 
Siwowi Sijapenda, hata kidogo. huyu mtu kasababisha madhara makubwa kwa mahubiri na kuhamasisha watu. Huyu ilibidi awekwe detention kama sheria ya detention bado inafanya kazi. Naipenda CDM, lakini kwa hili hapana.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja kwanza niwe msomaji wa huu uzi kabla sijachangia chochote.
 
one thing for sure
ndani ya CHADEMA hakuna anaejua kucheza michezo ya kisiasa
zaidi ya Marando....

na hili tamko ni la Marando binafsi na sio CHADEMA ...

this guy Marando is very very interesting.....muulize Mrema akwambie lol...
 
Hahahah am the great physician!!!

Nilisema hapa kuwa watakaoongea ndio hao na watakachoongea ndio hicho

Sababu

1. CHADEMA maandamano kwao ndio kawaida, hivyo hawawezi kucondemn

2. Vyombo vya dola kama mahakama na polisi haviaminiki kwao siku nyingiiiii so hawawezi kusema sheria ichukue mkondo wake

3.Kwavile hili jambo lina sura ya dini ,na liko mahakamani, na ili kuwe na a balanced statement; inabidi prof Safari na Tundu lissu (naona kaja Marando...sawa tu) ndio walisemee

4.Serikali na CCm zitalaumiwa


Big to the up CDM

Tundu Lissu he is mor of a laywer than a politician

Marando ndio game zake hizi......

this is politics,hakuna genuine tamko hapo
 
Halina mvuto!

toa hoja na wala sio kusema haina mvuto kimsingi chadema kama chama cha kikuu cha upinzani wako halali kuyasema hayo walioyasema suala hapa ni ipi haki kwa pande zote mbili yaani serikali pamoja na waislamu na hata ivo huyu ponda hafai ni bora tu afungwe tu
 
Wamepima wakaona mbali sana.kura za zanzibar zinaamua nani anakua rais wa Tanzania.kwa chadema kupata hata asiliamia 30 za kura zao inawapeleka karibu na ndoto zao za kukamata dola.ukichukulia kua wameshakubalika kwa jamii wakristo.
 
Back
Top Bottom