Chadema wasusie uchaguzi

Wakurogwa

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
216
39
Kutokana na hali ninayoiona hadi sasa kuna suala zima la kuboresha daftari la wapiga kura ambapo kila mtu hasa wa CDM wanalalamika kuhusu daftari la wapiga kura halijaboreshwa.Ni vema CDM wakasusia uchaguzi huu mdogo wa Arumeru kwani daftari la wapiga kura halijaboreshwa nina chelea kusema kuwa isije siku matokeo yanatangazwa magamba wameshinda halafu tuone sababu ya kushindwa CDM ikatolewa kuwa daftari la wapiga kura halikuboreshwa.Nisingependa sababu hii ikawepo hapo baadaye baada ya kushindwa.
 
Ni sawa mkuu but mayb chadema waangalie utaratibu mwingine wa kusolve hili tatizo lakin sio kusususia.
 
Hivi uanze kukimbia uwanja wa vita kabla hata mapambano hayajaisha?
Uoga wa aina gani? Kususa na kununa tabia za kike.(rejea mada ya kususa na kununa MMU)

Acha CDM wapambane bwana, hata kama CCM watacheza rafu, msg sent kwamba CDM inakua kwa kasi. So 2015 hapatatosha!
 
Mkuu isijekuwa umetumwa! usiwatafutie CCM njia rahisi ya kushinda uchaguzi kwa ushauri wako huo!. Najua uwanja wa mapambano hauko level lakini wacha CHADEMA wapambane hivyo hivyo kuliko kususa. Kwani mpaka hapo tulipo CCM wako hoi.
 
Mkuu ninachojaribu kukisema hapa kinaweza kuwa kweli katika malalamiko yatakayotolewa hili la Daftari lisiwepo kwani tayari imeshaonekana mapungufu.Mimi sijatumwa haya ni mawazo yangu na siwatafutii Magamba unafuu wowote ule ila ukweli ndiyo huo
 
Unajua ukishajua mbinu za adui yako ni nusu ya ushindi. Sasa hivi CHADEMA wanajua hayo yote, ninaimani kubwa kuwa wanapanga mikakati mizuri tu ya kulinda ushindi wao. Siamini sana kuwa wale ambao wamo kwenye daftari kwa sasa ni wafuasi wa CCM na kikubwa ni kwamba nchi ilipo kwa sasa karibia kila mmoja anafahamu kuwa adui yake mkubwa ni CCM. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa wana wa Arumeru bila kujali umri wao, kikubwa kulinda kura, kwani magamba hayana njia nyingine zaidi ya kutumia mbinu chafu kulazimisha ushindi.
 
Hatugomi wala nn,umetumwa na Kengemaji ee,ivo ivo gozi la ng'ombe litapigwa,cdm wataibuka kidedea
 
Back
Top Bottom