Chadema Wasitumiwe na Wafadhili wa nje

Jamani, kama 90% ya budget ya tanzania inatoka kwa wafadhili swali linakuja , kwanini chadema wasitumiwe na wafadhil kwani wao wanakosa gani ? Angalao tanzania iweze kujiendesha yenyewe. Au bora kutumia wafadhili wa ndani, hao mafisadi wanaofilisi mali za tanzania na bado wapo ndani ya nchi? Mfano ni mmoja wapo wa mmiliki wa dowans.
 
@Gurudumu na AlbertoMsando.

Mmeongea vyema. Mfumo wetu wa kisiasa ndio CHANZO KIKUU cha umasikini wetu leo hii. Ndio chanzo cha matatizo yote ya kijamii,kisiasa na kiutendaji.

Gurudumu umeongelea juu ya tatizo la public transport katika miji yetu. Alberto ukaongelea juu ya ukosefu wa priority. Kwa pamoja hoja zenu zinabebana. Tatizo la usafiri bora wa umma linatokana na serikali kuona suala ilo kama si la muhimu. Watendaji wa serikali badala ya kuja na mfumo ulio bora wa usafiri wa umma,wao wanafikiri kununua daladala na mabasi yao binafsi ili wajinufaishe. Yaani wanaona kuinufaisha serikali kwa njia ya mapato si priority,ila priority ni kutumia tatizo ilo kujaza mifuko na matumbo yao!

Kuhusu wahadhiri kutokua wabunifu katika kuandaa mambo na mitaala mipya katika kozi mbalimbali vyuoni,tatizo linabaki lile lile. Wahadhiri wanakua wabunifu katika kuandaa miradi na tafiti zitakazojaza mifuko na matumbo yao. Ila kuandaa na kuingiza mambo mapya katika kozi yatakayonufaisha jamii nzima kupitia hao wanafunzi,inakua ngumu kwao.

Kwaiyo hapa tunaona tatizo ni kubwa mno,ukitoa mfumo wenyewe wa siasa ulio mbovu,pia kuna tatizo la ubinafsi miongoni mwetu waTZ. Unaweza kuyabebanisha haya mawili kwa kujiuliza ni namna gani serikali yetu inapokea na kutekeleza mapendekezo na mawazo ya wahadhiri,wataalamu na wananchi wengine. Pengine hili ndio linawafanya wakate tamaa ya kujali jamii na kuanza kujali kujaza mifuko na matumbo yao! Nasema ivyo kwavile mawazo na mapendekezo ya wataalamu na wananchi kwa ujumla ni ya muhimu sana katika kubadili mfumo wa siasa na katika kugundua njia za kuondokana na utegemezi wa misaada ya wafadhili.

Nakaribisha kukosolewa.
 
kimsingi cdm wapo makini sana na kila wanachokifanya.viongozi wa CHADEMA huwa wanasukumwa na dhamira na uzalendo katika taifa ndio maana sii kazi rahisi kupokea ufadhili. hoja yako mzuri sana kamanda
 
Naona kwenye ITV, naibu waziri wa Viwanda ndugu Nyalandu akiwa na Mzungu wanakabidhi mradi wa maji kwa wananchi wake. Pia wakaonesha mashangingi yaliyokwamba kutokana na ubovu wa barabara. Kwenye huo msafara inaonekana hata polisi walikuwepo.

Kwamba jukumu la kuleta maji kwa wananchi wetu ni la wafadhili na kazi ya pesa zetu ni kununua mashanginghi ya bei mbaya ambayo tutayatumia kuwapeleka wafadhili huko wakasaidie wananchi. Na wakati mfadhili akija, kila afisa wa serikali idara zote lazima waongozane naye kwenda kumsikiliza. ikibidi wanakijiji wamchezee ngoma pia?
 
Nyandai, umeanika tatizo lingine; UBINAFSI.

Yaani Nyandai amepiga ikulu!!! Isipokuwa kuna ubinafsi wa aina nyingi na kuna ule mzuri. halafu unatofautiana proportion kwa mfano ule ubinafsi uliopo kwenye serikali ya tz kwa sasa hivi, dowans? labda atufafanulie zaidi
 
Moja katika falsafa za Mwalimu Nyerere ni kwamba..."NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MISAADA TOKA NJE"...
Lakini pia wengi wetu huenda mlipata kuona kwenye habari (kuna picha), Wachina walioita Media na kumwalika waziri, kumbe wanatoa msaada wa kandambili za aina ya YEBOYEBO kwa jamii ya Watanzania...ni jambo la kusikitisha kidogo.

Dhana ya utegemezi na misaada kwa Watanzania ni dhana iliyozama kabisa vichwani mwetu...Sielewi ni kwanini hatuwazi kuwa sisi tutasaidia lini nchi zingine...
Wazo la kusema Tanzania ni Masikini limekuwa kama kichaka cha viongozi kujificha huko na kufuja mali za nchi kwa nia ya ubinafsi...Actually studi iliyofanywa na wataalamu inaonyesha kuwa ni asilimia chini ya 50 ya Msaada huwafikia walengwa...

Miaka ya 70 Tanzania ilikuwa na cha kuonyesha kwenye uchumi na soko la dunia kama brand yake yenyewe katika sekta ya kilimo...kulikuwa na Kahawa, Pamba , Katani alizeti nk, ambavvo viliifanya Tanzania iheshimike na kuaminika...Niambie leo hii Tanzania tunajivunia nini kwenye uchumi wa dunia hii, WAKATI Tanzanite yenyewe tumeporwa na Wakenya na wanachukua awards zote za uuzaji na ubora wa zao hilo!...

Mkuu Gurudumu, nakubaliana na wengi hapo juu kuwa kumetokea na muozo kwenye bongo za wananchi wetu kuhusiana na Uzalendo...kutokana na uongozi wetu unavyo'behave(kujilimbikizia mali) wananchi wanakata tamaa na kuamua kulipiza visasi kwa njia wanazozijua wao, kila mtu kwa idara yake, na matokeo yake hakuna productivity, as a result nchi inakuwa stagnant..

Mimi nadhani kuwa kujikomboa na hili si kazi ya siku moja, maana lina miziz kama ya Mbuyu...Bila Rais mwenye nia na dhamiri, hakuna litakalowezekana...Rwanda rais ndiye aliyesimamia kuung'oa ufisadi....na wanafanikiwa kwa kasi ya ajabu sasa.

CDM ina nafasi kubwa sana ya kutekeleza wazo la kung'oa utegemezi...I highly bank on leadership of Dr Slaa...
Kiongozi anapokuwa msafi na mpinzani wa corruption inamaanisha kuwa amejiandaa na anawaandaa wananchi wake kufanya kazi na kujitegemea, na kuchukia utegemezi... si vinginevyo...
 
mkuu, katika vichwa vya watz wengi, hakuna maendeleo bila wafadhili na hatuwezi kutatua tatizo lolote bila wafadhili. mfano mmoja ni huo ulioutoa, majanga. lakini angalia fikra zilivyokosa uhuru na kujitegemea. Kuanzia rais had afisa yeyote serikali akiulizwa kwa nini jambo fulani halijafanyika jibu ambalo limerekodiwa vichwani mwao na halibadiliki ni hivi;

serikali haina pesa kutokana na umaskini wetu. serikali yenu ya ccm imejitahidi sana na kufanya mazungumzo na wafadhili kadhaa kuomba watusaidie. raundi ya kwanza ya mazungumzo ilikwenda vizuri na ya pili sasa tuko kwenye raundi ya tatu. tulianza mazungumzo mwaka juzi, kulikuwepo na mambo ambayo hatukuweza kukubaliana mara moja lakini baada ya kuyafanyia kazi sasa tunaelekea kukubaliana. upembuzi yakinifu umekweshafanyika, mchakato wa kumpata mkandarasi umekwisha anza. kabla ya mwisho wa mwaka huu huo mradi unaweza kuanza.

mara ngapi umesikia hadithi kama hii?

NDUGU YANGU; Naongeza jambo kwneye mchango wako ambalo ni mfano kwamba; Kwenye Kampeni JK alipokea simu katikati ya hotuba yake ya kampeni pale Manispaa ya Iringa. Kisha akawaambia wananchi kuwa Balozi wa marekani amemhakikishia kuwa serikali ya Marekani itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania. Mwaka 2008 USA walisaini mkataba wa shilingi billion 700 kwa muda wa miaka mitano hiyo ni sawa na shilingi bilioni 140 kwa mwaka. Wakati huo huo Serikali ya Tanzania kwa mwaka 2009/2010 ilitoa misamaha ya kodi ya shilingi bilion 700 nusu ya hiyo misamaha ina-originate kwenye madini. na 70% ya migodi inamilikiwa na wawekezaji wa kimarekani hivyo kufanya misahamaha ya shilingi zipatazo bilioni 350 ktk huo mwaka kutolewa kwa makampuni ya kimarekani huku serikali ya marekani ikirudisha shilingi bilioni 140 [Je huo ni msaada?. Kwa kuangalia mfano huo unaona Tanzania haikuhitaji huo msaada badala yake ingepunguza asilimia 20 ya misamaha ya kodi na kufidia hilo pengo hivyo Rais wetu kutojidhalilisha majukwaani kwa kuomba misaada!
 
Naam, hiyo ndiyo hesabu ya kujumlisha na kutoa ambayo ma-dr na ma-professor katika serikali yetu hawawezi kufanya. Siku moja Jenerali Ulimwengu aliwahi kuhoji kwamab iweje ukabidhi madini yako yote kwa wazungu halafu uanze kuwabembeleza wakupe msaada kidogo kidogo?

misamaa ya kodi ni ugonjwa mkubwa katika nchi yetu. kuna wale wafanyabiashara ambao mizigo yao bandarini haikaguliwe kwa sababu eti ni wafanya biashara wakubwa wanaheshimika wanalipa kodi kubwa serikalini. unaweza kufikiri ni kiasi gani cha pesa tunapoteza kwa kuamini kwamba wafanyabiashara wakubwa watakuwa waaminifu kuhusu mali wanazoingiza nchini na kutoa, including mauzo yao.

kuna hii mashine waliyoweka ya risiti, nadhani ulikuwa ni ufisadi tu wa kumpatia mtu tenda ya kuagiza hizo mashine lakini wafanyabiashara hawazitumii kabisa au wanaandika thamani pungufu ya walichouza.

kuhusu kodi kuna harufu mbaya sana inanuka labda kama kuna mtu anaweza kutujuza zaidi hapa ambaye anajua vema haya mambo yalivyo.

hivyo kama ulivyosema, hatukusanyi kodi kutoka kwa wawekezaji na wengi tunawasamehe kulipa kodi, kisha tunawapa bure rasilimali zetu halafu tunasikitika kwamba sisi ni masikini na tunawaomba misaada! it is pathetic
 
Moja katika falsafa za Mwalimu Nyerere ni kwamba..."NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MISAADA TOKA NJE"...
Lakini pia wengi wetu huenda mlipata kuona kwenye habari (kuna picha), Wachina walioita Media na kumwalika waziri, kumbe wanatoa msaada wa kandambili za aina ya YEBOYEBO kwa jamii ya Watanzania...ni jambo la kusikitisha kidogo.

Dhana ya utegemezi na misaada kwa Watanzania ni dhana iliyozama kabisa vichwani mwetu...Sielewi ni kwanini hatuwazi kuwa sisi tutasaidia lini nchi zingine...
Wazo la kusema Tanzania ni Masikini limekuwa kama kichaka cha viongozi kujificha huko na kufuja mali za nchi kwa nia ya ubinafsi...Actually studi iliyofanywa na wataalamu inaonyesha kuwa ni asilimia chini ya 50 ya Msaada huwafikia walengwa...

Miaka ya 70 Tanzania ilikuwa na cha kuonyesha kwenye uchumi na soko la dunia kama brand yake yenyewe katika sekta ya kilimo...kulikuwa na Kahawa, Pamba , Katani alizeti nk, ambavvo viliifanya Tanzania iheshimike na kuaminika...Niambie leo hii Tanzania tunajivunia nini kwenye uchumi wa dunia hii, WAKATI Tanzanite yenyewe tumeporwa na Wakenya na wanachukua awards zote za uuzaji na ubora wa zao hilo!...

Mkuu Gurudumu, nakubaliana na wengi hapo juu kuwa kumetokea na muozo kwenye bongo za wananchi wetu kuhusiana na Uzalendo...kutokana na uongozi wetu unavyo'behave(kujilimbikizia mali) wananchi wanakata tamaa na kuamua kulipiza visasi kwa njia wanazozijua wao, kila mtu kwa idara yake, na matokeo yake hakuna productivity, as a result nchi inakuwa stagnant..

Mimi nadhani kuwa kujikomboa na hili si kazi ya siku moja, maana lina miziz kama ya Mbuyu...Bila Rais mwenye nia na dhamiri, hakuna litakalowezekana...Rwanda rais ndiye aliyesimamia kuung'oa ufisadi....na wanafanikiwa kwa kasi ya ajabu sasa.

CDM ina nafasi kubwa sana ya kutekeleza wazo la kung'oa utegemezi...I highly bank on leadership of Dr Slaa...
Kiongozi anapokuwa msafi na mpinzani wa corruption inamaanisha kuwa amejiandaa na anawaandaa wananchi wake kufanya kazi na kujitegemea, na kuchukia utegemezi... si vinginevyo...

nashukuru kwa mawazo yako mkuu,

hilo la kuita waziri na vyombo vya habari kutoa msaada wa kandambili? mara nyingi hata sisi tunaiga, utaona mtu anapata coverage ya dakika moja nzima kwenye tv akikabidhi vyerehani vitatu! Swali ni hivi, wakati wanasaini hiyo mikataba ya kifisadi wanaitisha media na kutangaza nini walichosaini?

kisha naona umewagusa viongozi wa chadema, sijui kama wanaona hii thread na natamani kusikia mawazo yao.
 
What can Nigeria do to live up the promise of its postcolonial dream? First, we will have to find a way to do away to do away with the present system of political godfatherism. This archaic practice allows a relative handful of wealthy men - many of them half-baked, poorly educated thugs - to sponsor their chosen candidates and push them right through to the desired political position, bribing, threatening and, on occasion, murdering any opposition in the process.

Source: Chinua Achebe, New York, 15 January 2011
 
Mimi bado siwaelewi Chadema. Baada ya haya yote yanayotokea Tumisia na Misri na matatizo ya tz ambayo ni makubwa kuliko ya hizo nchi, wanasubiri nini kuhamasisha watz kuandamana na kuondoa huu utawala madarakani? Mbona baada ya issue ya Arusha wamekuwa kama wamedhititiwa? Kimya!

Umeme, inflation, foleni, ubora wa elimu umeshuka, ufisadi na rushwa vinaongezeka, serikali imeshindwa kuongoza, watendaji wabovu hawajiuzulu, maji mgogoro, huduma za afya mdororo, madini yaanahamishwa na wageni, ajira tatizo, vyuo vikuu migogoro,...........

Kama kweli wanawakilisha nguvu ya umma, ni umma wa nchi gani? Wanasubiri shida gani zaidi ya hizi ndipo wachukue hatua ya kutuunganisha? Au wamedhibitiwa na wafadhili wao?
 
Kwa kweli nakuonea huruma kwa jazba uliyonayo na kuwataka chadema waongoze harakati za kuwalazimisha watawala kubadilika. Nakubaliana na wewe kwa kuainisha matatizo na changamoto zilizopo Tanzania ambazo ni kubwa kuliko za Tunisia na Misri.

Nakushauri tu uwe "awake"(macho?!) kuona kama ni hao chadema, wewe au wengine wanaelekea wapi na mikakati yao. Usisahau hii nchi yetu ni polisi state, uzuri ni kwamba wanaotoa hizo amri ni waoga, hatari ni kwamba madhara ya watu innocent kupoteza maisha ni makubwa. Kunahitajika balancing ya namna fulani. Pia usisahau tumetoka kwenye uchaguzi. Na mbiu ya mabadiliko ilikuwa kulinda kura. Sehemu kubwa waliona ni kitu cha kawaida hawakulinda kura zao matokeo unayajua. Uzuri wa matokeo hayo ya uchakachuaji hata wachakachuaji hawana raha nayo.

Kwa mfano ukiondoa mkakati wa amani walionao chadema wewe na mimi na wengine tuna mikakati gani? Kinachotokea Tunisia na Misri hakijaasisiwa na chama cho chote cha siasa bali ni upinzani wa wananchi ambao wako tayari kwa lo lote.
 
Umesema jambo la msingi kabisa ingawa ulimwengu wa leo ni wa kutegemezana, ila msingi na mwelekeo wa nguvu zetu zote uwe kujitegemea na wafadhili wakubaliane na matakwa yetu si kutekwa na fikra zao.

Mataifa tajiri yanainvest rasilimali au mapesa yao kwenye nchi maskini kwa danganya toto kwa mtindo wa kutumia polite language, ati misaada wakati tunabebeshwa mzigo mzito wa kurudisha pesa zao na riba kubwa. Unabaki rasilimali zako kuwanufaisha kwani kila unachozalisha kinapekekwa kwao kulipia madeni.

Nchi zilizopiga hatua kubwa kujikwamua kiuchumi zilitumia mbinde ya kutotegemea mikopo bali kutumia rasilimali walizo nazo. Mabank ya nchini na taasisi za fedha za nchini ndizo zinazotakiwa kulikopesha taifa fedha kwa ajili ya kunusuru bajeti ya mwaka na mapato yake pamoja na riba itabaki kwenye mzunguko wa uchumi nchini, ndivyo mataifa mengi yaliyoendelea na yanaliyotupita kimaendeleo yanavyofanya.
 
Kwa kweli nakuonea huruma kwa jazba uliyonayo na kuwataka chadema waongoze harakati za kuwalazimisha watawala kubadilika. Nakubaliana na wewe kwa kuainisha matatizo na changamoto zilizopo Tanzania ambazo ni kubwa kuliko za Tunisia na Misri.

Nakushauri tu uwe "awake"(macho?!) kuona kama ni hao chadema, wewe au wengine wanaelekea wapi na mikakati yao. Usisahau hii nchi yetu ni polisi state, uzuri ni kwamba wanaotoa hizo amri ni waoga, hatari ni kwamba madhara ya watu innocent kupoteza maisha ni makubwa. Kunahitajika balancing ya namna fulani. Pia usisahau tumetoka kwenye uchaguzi. Na mbiu ya mabadiliko ilikuwa kulinda kura. Sehemu kubwa waliona ni kitu cha kawaida hawakulinda kura zao matokeo unayajua. Uzuri wa matokeo hayo ya uchakachuaji hata wachakachuaji hawana raha nayo.

Kwa mfano ukiondoa mkakati wa amani walionao chadema wewe na mimi na wengine tuna mikakati gani? Kinachotokea Tunisia na Misri hakijaasisiwa na chama cho chote cha siasa bali ni upinzani wa wananchi ambao wako tayari kwa lo lote.

Mimibaba nakubaliana na wewe. Sasa tutatokaje kwenye huu umasikini tulionao kama bunge ndo chombo cha kutukomboa na kimeshindwa? Ni kweli kwamba hadi sasa sioni tofauti kati ya chadema na ccm kwa sababu wanachoendeleza bungeni ni mijadala tu hakuna kuwajibishana kwa namna yoyote.

Sana sana chadema nao wanaonekana kama wanagombea nafasi ya kula kama ccm, naomba mtu a prove me wrong please
 
Tujaribu kukumbusha hii kitu bana, isijekuwa uhuru wetu unafadhiliwa na mabepari ambao serikali mpya italazimika kuja kuwatumikia tena kama ilivyo kwa serikali iliyoko madarakani
 
Back
Top Bottom