mkuu, usinizungushe tafadhali, naomba uniambie fedha haramu ni nini? ili hatua ya pili ndo tuweze kutathmini kama hizo za sabodo ni haramu
Fedha haramu ni kama za EPA, Sabodo na RA,etc
nafikri umeelewa.
mkuu, usinizungushe tafadhali, naomba uniambie fedha haramu ni nini? ili hatua ya pili ndo tuweze kutathmini kama hizo za sabodo ni haramu
asante michelle, lakini, kwa nini watusaidie? wao wananufaika na nini kutusaidia? halafu kwa nini tusaidiwe? rasilimali zetu hazitoshi kupiga hatua kidogo kidogo kwa uaminifu na dira ya pamoja?
Unajua sioni kama rasilimali za nchi zitagawanywa kwa ajili ya katiba na zaidi kuwapa nguvu CHADEMA ambao umesema wasitumiwe.So,kwa kujua mchakato wa Katiba ni mkubwa na pengine utachukua muda na kuhitaji hela nyingi ndo nikasema kama watajitokeza wenye nia njema na wasio tupa masharti yatakayofanya maslahi ya watanzania yasipewe kipaumbele then tunaweza pokea.....Mchakato uendelee vizuri japokuwa nina amini watanzania watachanga vizuri kama wakihamasika.
Haramu ni pesa za ccm zilizokuwa zikitumiwa kununulia kofia, maji,nepi za watoto, vitambaa vya kichwani, tshirt, kanga, opener, na ushenzi wote ule, wakati wananchi hawawezi hata kulipa michango ya shule na wengine hawaendi tena hospital badala yake wanawatumia sangoma kufanya operation kwa kukata viungo vya albino.Fedha haramu ni kama za EPA, Sabodo na RA,etc
nafikri umeelewa.
Haramu ni pesa za ccm zilizokuwa zikitumiwa kununulia kofia, maji,nepi za watoto, vitambaa vya kichwani, tshirt, kanga, opener, na ushenzi wote ule, wakati wananchi hawawezi hata kulipa michango ya shule na wengine hawaendi tena hospital badala yake wanawatumia sangoma kufanya operation kwa kukata viungo vya albino.
Mawazo ya kitumwa yamejaa vichwani mwa jamii kwa kuwaza wafadhili kila mara wanapojadili maendeleo.
Msingi mkuu wa utumwa ni imani iliyojengeka kwa watumwa kwamba hawawezi kufanya chochote bila msaada wa mabwana au watawala wao.
Umasikini wa jamii utaondoka tu pale ambapo mawazo ya utegemezi yataondoka kuanzia kwa mtu mmoja mmoja hadi jamii yote ibadilike, hivyo siyo kutegemea chadema tu.
Jamii ikiwa na mawazo mazuri.then watapatikana viongozi wazuri kwa kuwa viongozi wanatokana na jamii yenyewe.
Dah, kweli tumefika pabaya sana. Inabidi watanzania wote walazimishwe kusoma kitabu cha Paulo Friere "Pedagogy of the Oppressed" ili kujikwamua kutoka kwenye mawazo ya kitumwa.Hapa tulipofikia, kwamba kuanzia mkuu wa nchi hadi mfagiaji katika ofisi ya serikali anaabudu mzungu, bila kuja kama ni mfadhili au la, ni hatari kabisa. kwa wale ambao wanatembelea ofisi za serikali, unaweza kuwa unaongea na ofisa fulani wa ngazi ya juu, akiingia mzungu yule afisa anaruka kutoka kwenye kiti chake na kuanza kumtetemekea, anasaha kabisa kwamba kuna binadamu mwingine hapo yaani mwenye nchi. wafagizi watasafisha ofisi vizuri zaidi kama wanajua kuna ugeni, wazungu. wakikusikia unampinga mfadhili kila mtu anakaa kimya na kukukwepa asije akaonekana ana uhusiano na wewe, asijedhaniwa alikutuma.
Nimefarijika sana ulipoongelea nchi maskini na Misaada!
Africa is making a huuge mistake to depend on external AID! Kuna wakati namkumbuka mkapa. Mkapa kafanya blunder nyingi lakini kwenye jambo moja ninamuunga mkono kwamba, alisisitiza watanzania wafanye kazi kwa bidii badala ya kufikiria misaada at the same time pressurizing big nation to help Afria. Ninamkumbuka alivyomhamasisha yule jamaa aliyeandika "mtaji wa maskini ni nguvu zake"
Misaada ina hasara na matatizo mengi kuliko faidi!!!! moja ambalo ni kubwa saaana misaada inajenga kifra kwa mpokeaji kuwa bila mtoa misaada kuchangia mpokeaji hawezi kufanikisha azma yake. fikiria mfano rahisi wa mafuriko ya kilosa tathmini ilionyesha kunahitajika shilingi bilioni tatu. Mkuu wa maafa akasema anaomba wafadhili wa ndani na nje watoe misaada ilhali kodi ya ndani kwa wakati huo ilikuwa ni shilingi billioni mia nne kwa mwezi. THINK ABOUT THIS IN WIDELY!
Gurudumu, salaam!
Kwanza nakushukuru kwa hoja yako. Mwanzoni nilishtuka nikidhani unaamini kwamba CDM inatumiwa na wafadhili katika mapambano yake ya kuleta mabadiliko. Baada ya kuisoma nimekuelewa. Umetoa tahadhari.
Najiuliza swali, tunahitaji misaada ili nini? Maendeleo ni nini kwa mtazamo wetu? Tumeshindwa kudefine maendeleo yetu badala yake tunatumia a comparative approach kudefine maendeleo. Tunaangalia maisha ya wazungu tunayatamani na kutaka kuwa kama wao! Tamaa zetu zinatufanya tuwasujudie na kuwaomba misaada ili tuwe kama wao!
Tamaa zetu zinatuponza na kutusabisha kujirahisisha kwao. Ujinga wetu ndio anguko letu!
Miaka 49 bado tunapigana na maradhi, umasikini na ujinga! Miaka 49 kata yangu kina mama wanajifungulia majumbani, watoto wanasomea nje, kipindupindu na kichocho, minyoo ni tatizo! Tunahitaji misaada kupambana na kipindupindu! Tunahitaji misaada kuondoa dampo la taka!
Misaada ikifika tunaitumia vibaya. Tunanua magari ya bei kubwa, tunajenga nyumba za gharama, tunabadili fashion ya kila kitu! Kila toleo jipya la kitu tunataka! Gharama za uendeshaji tunazikuza wenyewe bila sababu za msingi. Mahitaji yetu yanaongezeka wakati uwezo wetu uko palepale!
Naunga hoja mkono! Oops naunga mkono hoja. Suala la kutegemea wafadhili kwakweli nalipinga,na nitalipinga pale kaburini.
Ivi hao wafadhili wakati walipoanza kuendelea walifadhiliwa na nani? Walikua wanatembeza bakuli kwa nani?
Ukisoma historia ya industrial revolution kwa Amerika na Ulaya,utaona kwamba jamaa walitumia rasilimali zao na zile walizoiba toka Afrika na Amerika ya Kusini kwa maendeleo yao. Walitumia wataalamu wao katika kukabiliana na changamoto ambazo ziliwafanya wawe wadadisi na wagunduzi. Pia walitumia pesa zao kutoka kwenye kilimo kuwekeza katika mabenki na kuweza kupata nafasi ya kukopeshana na kuendesha vyema shughuli za viwanda.
Tanzania yetu tuna rasilimali zote,ila bado tunawaza kupeleka bakuli kuomba. Tunapokabiliwa na changamoto,tunawaza mfadhili gani wa kumtafuta ili atusaidie kutatua changamoto hiyo. Tunakopa benki na kununua magari ya kutembelea!
Kwa namna hii hakika maendeleo kwetu yatakua ndoto!
Nini tufanye: tunahitaji viongozi jasiri wanaoweza kusimama bila ya kua na mawazo ya omba omba. Viongozi wanaoweza kumkoromea na kumpinga Obama,Cameroon,Sarkozy,IMF,WB na mashirika yote ya nje yanayoleta na kushinikiza utekelezaji wa sera zenye mlengo wa kutimiza matakwa yao. Pili tunahitaji raia walio na mitazamo chanya ya kupata maendeleo ya taifa kwanza,jamii na kisha binafsi. Pia raia wajue njia bora za kutumia mikopo ya benki,na si kununua gari ya kutembelea ambayo inakua haizalishi chochote,bali inakula tu. La msingi zaidi ni KATIBA MPYA ambayo itaweka misingi imara ya uongozi bora (na si utawala bora),ushirikishwaji wa wananchi wa kada zote na demokrasia halisi.
Huu ni mtazamo wangu. Kukosolewa kunakaribishwa.
Naunga hoja mkono! Oops naunga mkono hoja.
Nini tufanye: Pia raia wajue njia bora za kutumia mikopo ya benki,na si kununua gari ya kutembelea ambayo inakua haizalishi chochote,bali inakula tu.
Huu ni mtazamo wangu. Kukosolewa kunakaribishwa.
Gurudumu, fikra! Ukombozi wa fikra. Jaribu kujiuliza mtanzania wa kawaida anafikiria nini kuanzia anapoamka mpaka anapolala? Fikra hizo zinamsaidiaje kimaendeleo? Anajua maendeleo yake binafsi ni nini? Kwa mfano, wengi wa graduates ukiwauliza wanataka nini jibu ni 'gari zuri, nyumba na kazi nzuri'. Kabla sijaendelea, ni nini mawazo yako kwa jibu hilo la msomi?