Chadema waonyesha picha za video alivyouawa Mwangosi;Picha zinaonyesha jinsi RPC Iringa alivyoshuhud

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JUMATATU, SEPTEMBA 10, 2012 05:45 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

*Picha zinaonyesha jinsi RPC Iringa alivyoshuhudia tukio
*Zinaonyesha baada ya Mwangosi kuuawa, polisi walilaumiana
*Waandishi wa habari, viongozi wa Chadema waangua vilio
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeonyesha picha za mnato na video zinazoonyesha jinsi Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Television cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, alivyouawa.

Picha hizo zilionyeshwa jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichohudhuriwa pia na waandishi wa habari. Kikao hicho cha Kamati Kuu kilikuwa ni cha dharura na kilifunguliwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Wakati picha hizo zikionyeshwa wazi wazi, viongozi wa CHADEMA na waandishi wa habari, walishindwa kujizuia kwani baadhi yao walijikuta wakiangua vilio wakionyesha kusikitishwa na jinsi Mwangosi alivyouawa.

Katika tukio hilo, Mbowe ni kati ya waliolia na ilifika wakati akanyanyuka kutoka meza kuu na kwenda nje ya ukumbi, ili asiendelee kushuhudia Mwangosi alivyouawa.

Wakati picha hizo zikionyeshwa kwa zaidi ya masaa mawili, askari polisi walioshiriki kumuua Mwangosi walionekana wazi wazi na pia Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, alionekana pia eneo la tukio akishuhudia Mwangosi akiuawa.

Kwa mujibu wa picha hizo, mwandishi wa habari aliyeanza kukamatwa na askari polisi na kupata kipigo ni Godfrey Mushi wa Gazeti la Nipashe.

Picha hizo za video zilionyesha kuwa, baada ya Mushi kukamatwa, Mwangosi alikwenda kumuokoa mwenzake huyo na alipofika eneo la tukio, askari hao walianza kumpiga na hatimaye kumuua mbele ya Kamanda Kamuhanda.

Picha hizo zinaonyesha kuwa, kabla Mwangosi hajauawa, polisi mmoja alipitisha bunduki yake miguuni kwa polisi mwenzake kisha Mwangosi akauawa.

Baada ya tukio hilo, picha hizo zinaonyesha kuwa, baadhi ya askari polisi waliokuwa wakimpa kipigo Marehemu Mwangosi, walikimbia na kuacha mwili wa marehemu ukiwa vipande vipande.

Kwa mujibu wa picha hizo, polisi hao walipokuwa pembeni, wenyewe kwa wenyewe walianza kulaumiana huku baadhi yao wakimlaumu muuaji na kusema umefanya nini hicho?.

Baada ya hapo, mmoja wa polisi hao alisikika akisema twende tukamchukue mwenzetu na walipofika mahali alipokuwa mwenzao ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa bomu lililomuua Mwangosi, gari ya Kamanda Kamuhanda ilisogea karibu na kumpakia askari polisi aliyejeruhiwa.

Picha hizo za video ambazo zinaonekana zilirekodiwa kwa umakini wa hali ya juu, zinaonyesha baada ya mauaji hayo, askari walishikwa na butwaa huku baadhi yao wakionekana kushika pua.

Wakati hayo yakiendelea baadhi ya askari ambao ni wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), walionekana katika mkanda huo wa video, wakifungua kofia zao zilizokuwa zimefunika uso na macho yao, ili waone vizuri maiti ya Mwangosi iliyokuwa vipande vipande.

Wakati wakivua kofia hizo, baadhi yao walikuwa wakinawa nyuso zao kutokana na moshi uliokuwa umesambaa eneo la tukio wakati walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA.

Pia picha hizo, zilionyesha askari polisi mmoja akiwa amevaa kiraia, huku shingoni akiwa na skafu ya CHADEMA lakini baada ya vurugu kuanza, askari huyo alionekana akiivua skafu hiyo na kuiweka mfukoni.

Alipoivua na kuiweka katika mfuko wa nyuma wa kaptula aliyokuwa amevaa, mwenzake mmoja akampa kofia ya kujikinga na moshi kisha askari huyo akachomoa bastola kwa ajili ya mapambano.

Pamoja na picha hizo kuwaonyesha askari polisi walivyotekeleza tukio hilo, Kamanda wa Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) wa CHADEMA, Benson Kigaila, alionekana pia akijibizana na ofisa mmoja wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Iringa kuhusu wafuasi wa CHADEMA kuwepo katika Kijiji cha Nyololo kilichopo Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.

Vile vile, picha hizo za video, awali zilionyesha marehemu Mwangosi alivyokuwa akimuuliza Kamanda Kamuhanda kuhusu sheria ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na maswali hayo yalionyesha jinsi kamanda huyo wa polisi alivyokuwa amechukizwa nayo.

Kutokana na picha hizo, Mbowe alisema huo ni ushahidi wa kutosha kuonyesha jinsi Jeshi la Polisi lilivyokuwa limedhamiria kuua.

Kwa mujibu wa Mbowe, CHADEMA itatoa tamko zito leo kuonyesha ni hatua gani zitachukuliwa baada ya kifo cha Mwangosi.



KABLA YA PICHA
Awali, akifungua kikao hicho, Mbowe alisema ajenda zitakazojadiliwa na kutolewa tamko ni za kitaifa, kijamii na kiusalama kwa manufaa ya wananchi wote.

Mbowe alianza kutoa pole kwa waandishi wa habari nchini kutokana na kifo cha Mwangosi na kuwataka wawe wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kamati imeundwa kuchunguza tukio hilo.

"Kifo cha mwenzenu marehemu Mwangosi kimetugusa sote, ninachoweza kusema ni kwamba, kimesababishwa na Jeshi la Polisi kwa lengo wanalolijua wenyewe, lakini najua wanataka kuwadhoofisha.

"Jambo jingine ambalo napenda kuwaeleza waandishi, ni kwamba sote tunafahamu Rais Jakaya Kikwete alivyo mwepesi kutoa pole na kuhudhuria pale panapotokea msiba, lakini hadi sasa kitu hicho hakijafanyika.

"CHADEMA tunalaani sana kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kutoa pole hata ya kauli, huku akijua tukio hilo limegusa watu wote duniani, tunashangaa kuendelea kutatua migogoro ya nchi nyingine, huku ya kwetu yakitushinda.

"Hakuna asiyefahamu kuna migogoro ya walimu, madaktari, wafanyakazi wa kada mbalimbali, wakulima, wafugaji na wananchi kwa ujumla, lakini hakuna jitihada zozote zinazofanyika kutatua badala yake tunaendelea kuongeza matatizo mengine," alisema Mbowe.


KAULI YA TENDWA
Akizungumzia kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, aliyesema wiki iliyopita, kwamba atakifuta CHADEMA kama mauaji yataendelea kutokea kwenye mikutano yao, Mbowe alisema haitawezekana chama hicho kufutwa vinginevyo ni kuhatarisha amani ya nchi.

Mbowe alisema, mpango wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia vyombo vya dola kama polisi na viongozi kutaka kuzuia mikutano ya M4C inayoendelea nchi nzima, hautafanikiwa.

"Tendwa asijaribu kutoa kauli za kuhatarisha amani ya nchi, kama ni kufuta vyama aanzie CCM, CHADEMA sio chama cha mfukoni, kama amelewa na usajili wa vyama na kuwa kibaraka wa CCM sasa amekanyaga pabaya.

"Napenda kutangaza rasmi kwamba, mikutano ya M4C itaendelea nchi nzima na hakuna mtu anayeweza kuizuia, tunataka kuleta demokrasia na mabadiliko ya kweli.

"Serikali ya CCM isijaribu kuleta machafuko nchini, itambue kwamba, CHADEMA ina mamilioni ya wafuasi na kila siku wanaendelea kuongezeka na kama Serikali hii itaendelea kulea ufisadi, wizi, ubabaishaji, mauaji na kushindwa kuwajibika kwa wananchi, ijue mwisho wake umefika, hakuna cha kulindana," alisema.



TUZO KWA WAANDISHI
Akizungumzia picha zilizopigwa na waandishi wa habari siku ya tukio la mauaji ya marehemu Mwangosi, alisema wanastahili kupatiwa tuzo.

Mbowe alisema kuwa, CHADEMA kinaandaa tuzo kwa waandishi wa habari waliopiga picha za video na mnato katika tukio la mauji ya marehemu Mwangosi.

"Waandishi wa habari wameonyesha uhodari mkubwa sana licha ya kuwa katika msukosuko wa mabomu ya polisi, picha zilizopigwa zimeondoa dhamira chafu ya polisi na Serikali ya CCM, kutaka kutumia mwanya huo kukichafua CHADEMA, picha zote za mnato na video zimeonyesha ukweli wa jambo na wahusika.

"Sisi kama CHADEMA tunathamini mchango wa vyombo vya habari na umuhimu wake na ni mtaji mkubwa sana kwetu, tumesikia waandishi wanatafutwa hatutasita kuwasaidia na mpaka sasa tupo sambamba katika hili," alisema.


AISHUKIA TBC
Katika hali nyingine, Mbowe alionyesha kutoridhishwa na mwenendo wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kwa kusema kuwa limekuwa likifanya kazi ya kuibomoa CHADEMA badala ya kueleza ukweli ulivyo.


DK. SLAA
Naye Katibu Mkuu CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa alikiri kumtumia ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Said Mwema na kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa.

Alisema alituma ujumbe huo baada ya kuzuiwa barabarani na polisi wakati wakiwa katika mikutano ya M4C.

Alisema baada ya kuzuiwa na kushushwa kwenye magari yao wakiwa mkoani Iringa na kulazimishwa kutembea kwa miguu hadi hotelini, aliamua kumpigia simu IGP Mwema na kumuelezea jambo hilo, lakini hakumjibu na ndipo alipoamua kumtumia ujumbe huo mfupi.

Hata hivyo alimtaka IGP Mwema na Tendwa kueleza chanzo cha kutuma ujumbe huo na kuachana na tabia ya kupotosha jamii.

Alisema kama kweli sms hiyo aliituma kwa uchochezi ni vema wamkamate na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

 
Hii inaumiza sana!! Cha kushangaza Kamuhanda bado yupo ofisin na anaendelea na kazi kama kawaida!! These people are very unserious!!
 
Hii inaumiza sana!! Cha kushangaza Kamuhanda bado yupo ofisin na anaendelea na kazi kama kawaida!! These people are very unserious!!
haya yana mwisho ndugu yangu na mwisho hauko mbali. Mungu hawezi kukaa kimya kwa muda mrefu zaidi wakati maovu haya yakiendelea. Jipe Moyo, ukombozi u-karibu!
 

TBC Jana ilikuwepo kwenye MKUTANO wa CUF; Inaiogopa CUF sababu ya UZEMBE wake Ninavyosikia waliweka kipindi ambacho waliweka IDADI ya Waislamu

Sijui wameitoa ONLINE; Wao Ndio wakaiita Sahihi; Hao Watengenezaji wa KIPINDI hicho nadhani bado wako KAZINI? ingekuwa US au EUROPE wamesimamishwa

Au KUFUKUZWA kazi Mara Moja... Serikali ya CCM hawafukuzani wanajazana pamoja na UCHAFU wao halafu Mkurugenzi anasema ndio yeye mwenye

Makosa... F.Y.I Wakurugenzi huwa hata hawajui VIPINDI VYA TELEVISION kadanganya UMMA wote wa Watanzania...
 
Safi tamko la cdm linajitosheleza kazi kwa magamba,Mwigulu na policcm m4c part 2 ndo inaanza
 
TBC ni imejaa mbumbumbu, na ndiyo maana inafanya mambo ya kishamba hata mtoto mdogo anaweza kugundua wanachokifanya ni upuuzi mtupu, naunga mkono kususiwa chombo hicho cha habari.
 
haya yana mwisho ndugu yangu na mwisho hauko mbali. Mungu hawezi kukaa kimya kwa muda mrefu zaidi wakati maovu haya yakiendelea. Jipe Moyo, ukombozi u-karibu!

Ninamtamani yule Mungu aliyesimamisha jua ili ashughulike na watu wenye shingo ngumu! Huyo anatufaa sana Afrika kwa ajili ya hawa viongozi wanaojifanya miungu watu! Wako radhi kutoa uhai wa mtu kwa ajili ya minyoo ya matumboni mwao na matumbo ya watoto wao.
 
Kiukweli inuma tena inakatisha tamaa ya kuendelea kuiona madarakani serikali ambayo imejaa ubatilivu,utepetevu na unyepenyevu ktk utendaji wake wa kazi.jamani vyombo vya usalama iweni makini katika utendaji wenu hasa kipindi hichi cha vugvugucha la mabadiliko.:a s 465::a s 465:hii ni alama ya utayari. Kwa mabadiliko ya kweli.
 
Bado tuendelee kujifariji kwamba tuna kiongozi ambaye yuko kwa ajili ya maslahi ya walio wengi kama Sio kikundi cha wahuni wachache.
 
kati ya watu muhimu wa kuhoji ni mkuu wa mkoa na wilaya husika jinsi walivyoshiriki kuhakikisha mikutano ya chadema haifanyiki na ni maagizo gani walitoa kwa rpc kamuhanda .
 
Hii inaumiza sana!! Cha kushangaza Kamuhanda bado yupo ofisin na anaendelea na kazi kama kawaida!! These people are very unserious!!

watakumbuka kuchukua hatua wakati tayari ni too late! acha panya waendelee kutoboa mtubwi. heri tuzame,watakao pona wataanza kuheshimiana.
 



Asanteni Kamati Kuu CHADEMA walau kwa kuitikia sauti ya na majonzi ya umma wa Tanzania na kutoa dira kwa Taifa, kukemea na kuainisha mambo gani yafanyike ili kutokomesha UKATILI WA JESHI LA POLISI dhidi ya raia na mauaji yasiokwisha kila kona ya nchi.

Hakika bado tunaomba sana mambo yasiishie tu hapo kwenye ma-tamko bali zaidi wananchi tunaasubiri kuona CHADEMA kinavyofwatilia utekelezaji wa kila agizo la Kamati Kuu taifa kwa faida yetu sisi walalahoi huku vijijini.

Elimu ya uraia kwa umma wa Tanzania sasa ndio iongezewe kasi maraduru ili kila kijiji kiweze kufikiwa ki-undani zaidi na zaidi.

KOVU LA UKATILI WA JESHI LA POLISI DHIDI YA RAIA NCHINI:
WATANZANIA TUNAJIBU GANI KWA 'MACHOZI YA LAANA NA KILIO CHA HAKI YA MWANAMAMA WINFRIDA JOHN' WA KIJIJI CHA NYOLOLO MKOANI IRINGA ???


Kamanda Winfrida John, kada wa CHADEMA kijiji cha Nyololo, bila shaka wewe ni mwana mama mtu mdogo tu hapo kijijini Nyololo ambaye pengine hata mbunge wa eneo hilo huenda asikufahamu kitu achilia mbali wakuu wa wilaya na mkoa huko Mufindi na Iringa kwa mpangilio huo, ila kwa wachache sana tena wenye jicho la mwewe angani huenda lako hili la kipekee mno likawa limewagusa nao pia.

Naam, kabla sijaandika mengi juu yako na kile kilichonigusa mno kwako kwanza niombe kwamba tafadhali Mama Winfrida futa machozi yako, yale ya akinamama wengine wengi zaidi hapo Nyololo na kwamba katu usiendelee kutuhuzunisha zaidi sisi WaTanzania wenzako kwa uchungu wote huo; machozi yako hadharani ya KULILIA HAKI na kutuhoji sote kama taifa tukupe jibu UHURU WAKO WA MAONI, NA KUJUMUIKA ulikopotelea;

Ni kweli kwamba siku hiyo 'SIMBA MLA WANYONGE WANAAOLILIA HAAKI' alipomnyakua makuchani Mtanzania wa 22 (Daudi Mwangosi) afiaye mikononi mwa dola kwa visingizio mbalimbali za kisiasa tangu mwaka huu, bila shaka watu wengi tu hapo Nyololo, Itete na hata vijiji vingine vya mbali sana nao walilia ila wewe hapo chozi laako linageuka kuwa chozi la dhahabu si kwa kuwa tu ulikua kwenye eneo la tukio baali zaidi ni kwamba ni mmoja kati ya wenyeji waliotembelewa naa CHAADEMA kwa shughuli ya ufunguzi wa ofisi mahali haapo.

Hakika ni kutokana na udhahabu huo wa chozi lako tena ukiwaa ni mwanamama tu mnaohitajika kuimarishwa zaidi kushiriki katika siasa na uongozi wa taifa, inanifanya nisiamini tu kwamba hivi karibuni huenda ukawa ni mtu wa kutafutwa sana japo sauti na vyombo vingi vya nyumbani hapa na vile vya kimataifa kama vile BBC, VoA, Deuche Welle ...

... bali zaidi najikutaa pia nikiwa sina wasi wasi kwamba Mama Hellen Kijo Bisimba naye amekusikia popote alipo, naamini kwamba msururu wako wa maswali ya msingi sana uliyoyauliza siku hii hata Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani umemuacha hana amani moyoni;

Ndio, kwa mtaji w kilio chako kikiwakilicha KILIO CHA HAKI kwetu sisi WaTanzania kwa ujumla wetu bila shaka ni wazi kwamba tayari umetuma ujumbe mzito kiasi cha kuwalazimisha hata magwiji wa habari nchiki akina Mzee Jenerali Ulimwengu, Fred Masako, Mzee Mwanakijiji, pamoja na Pasco wa JF.

Nasema kwa kilio cha mwanamama 'kiumbe dhaifu' katika jamii yetu hii inayoendekeza ufalme wa akina-baba tu kwamba vile vile utakua umewakuna akina Mama Nkya, Ayub Ryoba, Muhingo Rweyemamu pamoja na wengine kibao, waondoke kwenye viyoyozi maofisini na kuanza kupiga kiguu na njia wao wenyewe bila kumuagiza mwandishi yeyote wa chini, kwenda kukutafutia majibu sahihi na murua zaidi kiasi cha kuweza kukufuta machozi wewe na vizazi vijavyo;

Mama Winifrida, kwa kilio hiki hapo kijijini Nyololo ni wazi kwamba tayari umewakilisha sauti dhaifu za akina mama wote na watoto Tanzania ambao kweli
siku Daudi Mwangosi alipogeuka RUNDO LA NYAMA hapo kijijini kwenu(kwa hisani ya maagizo ya serikali ya CCM) - wenzetu mmeonekana kuteseka mno kukimbia ovyo na vichanga kuokoa maisha huku mkidhalilishwa na mgeni wenu CHADEMA ambaye ndiye kwanza mlikua mnamkaribisha rasmi hapo kijijini kwenu kwa kumpa eneo akafungulie ofisi yake (kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi) lakini ukarimu wenu wote ukahitimishwa na kilio cha historia yote Nyololo kugeuka ghafla kuwa uwanja wa mauji kama Syria.

Naam, nielewavyo mimi ni kwamba mama yetu Winfrida, hadi hapo ni kwamba tayari umewaamrisha wanaharakati kama Kijana mwenzetu Kibodya, Tundu Lissu, Deus Mallya, Prof Shivji, John Tendwa, pamoja na Mhe Augustino Mrema.

Wengine zaidi ambao wapende wasipende machozi yako ya haki bila shaka yako mabegani mwao ni pamoja na Prof Palamagamba Kabudi, Madam Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Mama Makinda, Prof Safari, Prof Maina, Prof Baregu, Dr Kitila Mkumbo, Dr Azaveli.

Ndio, nasema hawa waheshimiwa wote wanao wajibu kwako usiokwepeka kutoa jawabu kamili tena lisilocha maswali, kila mmoja kwa wakati wake, wakwambie kwamba kwenye katiba mpya wao wanategemea kuona Jeshi la Polisi la aina gani ili Winfrida John wa miaka hiyo ijayo wao wasije wakajikuta wakilia kilio kile kile kilichokumuaga machozi hapo Nyololo.

WaTanznia wote bila kujali itikadi za kidini na kisiasa, je tunalo jibu gani kwa mama huyu Winfrida John wa kijiji cha Nyololo ikiwa ni kielelezo cha kilio cha akina mama wengine wengi zaidi wasiokua na majina katika jamii yetu hii wangali nao wanao wachozi yasiokauka kulilia haki kama vile kule Igunga, Arumeru Mashariki, mauji ya Pemba, Arusha, Tarime, Mbeya ...?


 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom