CHADEMA waomba msaada kwa mataifa ya nje

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Baraza la Vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) wameomba msaada kwa vyama rafiki duniani ili kufanikisha maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Akihutubia katika Mkutano wa Kimataifa wa Vijana kuhusu demokrasia uliofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Bunge la Australia (North Wales), Sydney, Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Deogratias Munish alisema:
“Chadema tumedhamiria kushika dola mwaka 2015, tunaomba msaada wenu wa hali na mali katika harakati zetu hizi.”

Katika hotuba yake, Munishi alisema kutokana na matatizo mengi yanayoikumba Tanzania hasa katika mfumo wa uchaguzi, wameamua kufanya tathmini ya kukiwezesha kuingia Ikulu kwa kuwashirikisha vijana wa nchini nzima.Alisema ili kufanikisha hilo, kinahitaji kupata uzoefu wa nchi mbalimbali kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi.

“Tunahitaji kufanya ‘home work’ yetu vizuri kabla ya hapo. Ndiyo maana kama vijana wa chama, Baraza letu limeamua kwa makusudi kwenda kukijenga chama vizuri kwa kuwaunganisha vijana wote pamoja kwenye maeneo yao,” alisema.
Alisema kabla ya Bavicha kujipanga kuhakikisha Chadema kinashinda katika Uchaguzi Mkuu ujao, Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa alishaiagiza Bavicha kufuatilia kwa karibu migogoro yote inayohusu vyuo vikuu ambako ndiko iliko ngome kuu ya chama hicho.

Munish alisema Dk Slaa alisema vijana hao wanatakiwa kufuatilia na kuweka wazi hatua mwafaka zinazopaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na matatizo ya vijana.

Alisema uwanja wa siasa nchini ni mchafu kutokana na kuwepo kwa katiba mbovu ambayo pamoja na mambo mengine, inakataza kuhoji matokeo ya urais pindi yatakapotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Alisema ndiyo maana baraza hilo la vijana limeamua kukijenga chama kwa kuwaunganisha vijana wote pamoja kwenye maeneo yao ili kuhakikisha muungano wa ushindi 2015 unapatikana.

Alisema kutokana na vijana wengi duniani kuunganishwa na misingi ya vyama vyenye kusimamia na kuamini katika demokrasia, jambo la msingi ni kuhakikisha haki za binadamu na uhuru wa kweli unapatikana.

“Ninaamini na nina uhakika mtatuunga mkono katika harakati zetu sisi vijana wa Tanzania katika kuhakikisha tunashinda 2015,” alisema Munishi na kuongeza: “Kukua kwa Chadema si kwa bahati mbaya, bali ni kutokana na nia na mipango yake thabiti ya kuutumikia umma wa Tanzania.”

Alisema huduma mbovu za kijamii zimekuwa zikififisha ndoto za Watanzania kufikia maendeleo ya kweli hasa katika kipindi hiki cha kudorora kwa uchumi.Alisema kutokana na hali hiyo, Chadema kimeamua kupambana na rushwa bila woga kwa kuwafichua viongozi wala rushwa ambao wamekuwa wakilifilisi taifa kwa vitendo vyao hivyo.

Alisema Chadema na Watanzania hawajakata tamaa na huku akiwataka wajumbe waliohudhuria mkutano huo kuwaunga mkono katika kuendeleza mapambano ya kuongoza umma kueleza maovu yanayotendwa na Serikali.
Nchi wanachama wa umoja huo wenye wanachama 45 inashirikisha vyama vilivyopo madarakani na ambavyo havipo madarakani.

Baadhi ya nchi hizo wanachama ni Albania, Australia, Austria, Colombia, Croatia, Cyprus, Jamhuri ya Czech, Denmark, Ecuador, El Salvador, Finland, Ufaransa, Georgia, Ujerumani na Ghana.Katika orodha hiyo pia vipo vyama kutoka nchi za Ugiriki, Guatemala, Honduras, Hungary, Iceland, Korea Kusini, Macedonia, Maldives, Moldova na Mongolia.
Vingine vinatoka katika nchi za New Zealand, Nicaragua, Norway, Peru, Ureno, Serbia, Slovenia, Hispania, Sri Lanka, Sweden, Uganda, Uingereza, Venezuela, Belarus, Bolivia, Malta, Msumbiji, Namibia, Panama, Russia na Tanzania inayowakilishwa na Chadema.Katika mkutano wa aina hiyo uliofanyika nchini mwishoni mwa mwaka jana, ulihudhuriwa na nchi 24.

SOURCE:MWANANCHI
 
Ciomrade nakuaminia sana, it is a gud speech naamini zile lecture tulizokuwa tukihudhuria pale nkrumah kwa masanja, thietre kwa maghimbi na yombo kwa mwami zimekujenga vema. Chapa kazi nakuunga mkono
 
CDM hongereni kwa kutimiza masharti na kuweza kuelewana na chama cha David Cameroon. Hatahivyo watanzania hatutaki kutimiza matakwa ya Cameroon
 
CDM hongereni kwa kutimiza masharti na kuweza kuelewana na chama cha David Cameroon. Hatahivyo watanzania hatutaki kutimiza matakwa ya Cameroon

Ukiwa mtumwa wa Magamba uwezo wako wa kufikiri ni sawa na mkia wa mbuzi
 
Hivi misaada ya Conservative kutoka kwa kina Cameroon Uingereza mmeona midogo mnatafuta mingine..

Lakini mtambue lazima misaada kuwepo na masharti kutoka kwa anaetoa msaada.

Mfano misaada ya Conservative masharti yake lazima mkubali ushoga. Na nyie ndio wafadhili wenu wakuu..
 
Hivi misaada ya Conservative kutoka kwa kina Cameroon Uingereza mmeona midogo mnatafuta mingine..

Lakini mtambue lazima misaada kuwepo na masharti kutoka kwa anaetoa msaada.

Mfano misaada ya Conservative masharti yake lazima mkubali ushoga. Na nyie ndio wafadhili wenu wakuu..

Mambo vipi.Umekunywa chai leo?
 
Hivi misaada ya Conservative kutoka kwa kina Cameroon Uingereza mmeona midogo mnatafuta mingine..

Lakini mtambue lazima misaada kuwepo na masharti kutoka kwa anaetoa msaada.



Mfano misaada ya Conservative masharti yake lazima mkubali ushoga. Na nyie ndio wafadhili wenu wakuu..

kwani misaada anayoomba jk hadi uarabuni malipo yake nini?si unawajua waarabu sheikh?
 
CDM hongereni kwa kutimiza masharti na kuweza kuelewana na chama cha David Cameroon. Hatahivyo watanzania hatutaki kutimiza matakwa ya Cameroon

Tayari Serikali ya CCM imesharidhia hayo masharti na inavuta mshiko toka huko kwa kwenda mbele.
 
Sasa kuiongoza nchi yenu mnataka msaada kutoka nchi nyingine?mbona kama hapa sijawaelewa Magwanda.Msaada upi huo hasa mnaoutaka?na siku hizi hakuna vya bure mmejionea wenyewe US na UK wanataka tuwe mapunga.
 
CDM hongereni kwa kutimiza masharti na kuweza kuelewana na chama cha David Cameroon. Hatahivyo watanzania hatutaki kutimiza matakwa ya Cameroon

We mwenyewe unategemea msaada wa magamba sasa sijui utailipaje? Kwani ufahamu kwako umekuwa hadimu kama hedhi kwa kikongwe. BRAVO BAVICHA...........
 
Tunacho kifaa cha kufa mtu pale kwa jina la Munish kumbe hivi kumbe!!!!!!!!!!! Hakika CHADEMA chuo cha ma-kada chipukizi si utani.
 
Leo tunataka ukombozi wa Taifa letu hili kuweza kupata uhuru wa kweli! Kama ndo hivi kwa kuomba msaada kutoka nje na hasa kwenye kukuza Demokrasia BASI kamwe haitatokea kamwe kuwa na uhuru wa kweli. BAVICHA kwa hili la kuanza kutapata na kuomba msaada kutoka huko nje badala ya kuiungunisha jamii na kuielimisha jinsi ya kuleta mabadiriko na uhuru wa kweli nyie mwaenda nje! It is a shame sababu hili litatufanya tuendelee kuwa tegemezi hadi kwenye fikra na kufikiri then ukoloni mambo leo. Hapa naweza amini maneno haya "The beautful ones Are not yet Born"
 
Back
Top Bottom