Chadema wanapata ruzuku kutoka nje ya nchi?

izo account zingekuwepo si zingetolewa taarifa mkuu?taarifa ya matumizi na mapato ya chama yanaonesha account moja tu...!!hizo nyingine labda ni siri ya baadhi ya viongozi ndani ya chama..wanachama hawapaswi kujuwa..labda huko ndiko zinapokwenda hizo fedha nyingine!!!!
 
Tatizo la msingi matumizi ya fedha ndani ya chama hayafuati taratibu...fedha nyingi zinachangishwa na wanachama na michango ya wahisani lakini hizionekani zilivyotumiwa...huku ni kukihujumu chama...ufisadi upo wa aina nyingi!!

Hapa kwenye red, unatafuta ugomvi na msajili wa vyama vya siasa. Maana yeye msajili anakagua hesabu za vyama vyote vya siasa na kutoa ripoti kila mwaka. Hii ina maana kuwa ama msajili wa vyama ni kipofu (haoni hayo unayoyaona wewe), au msajili wa vyama amaipendelea Chadema !!
 
Taarifa za kibank zinaonesha kuwa mara baada ya uchaguzi mkuu 2010 chadema wametoa shilingi milioni hamsini na sita tu (56,000,000/=) kutoka katika akaunti ya chama kwa ajili ya matumizi ya mikutano na kuendesha chama..!!!

Swali:
Je ni kweli kwamba mikutano yote ya vuguvugu la m4c na operesheni sangara imegharimu kiasi hiki kidogo cha fedha au kuna vyanzo vingine visivyo rasmi?

Nawakilisha...!!
Lazima uzione kidogo sababu wale hawakodishi malori kwa ajili ya kusafirishia wafuasi,hawakodi bendi wala vikundi vya sanaangoma hawatoi ubwabwa,wala posho kwa mabalozi wa nyumba kumi au kuwapa wauhudhuriaji elfu 3000 zile za dezo,wala hawagawi khanga,T-shirt na vitenge.Wale huchangiwa na wahudhuriaji na kile kidogo wanachokopata hutumia katika matumizi ya kawaida.
 
Nape Nauye anawapotosha watanzania kuhusu michango na ruzuku ya chadema kama ni kiongozi msafi kwanini asingekuwa mwadirifu na mkweli ndani ya chama chake.
 
Mkuu Mzalendo sikatai wanachama kuchangia chama chao..ninachohoji mimi ni vipi wanachama wajifunge mkanda na kujinyima ili waweze kuchangia chama chao halafu watu wachache wazifaidi?..matumizi ya fedha ndani ya chadema hayapo wazi haiwezekani takwimu zioneshe mapato mengi ya harambee alafu matumizi ya mikutano mikubwa tena kila kona ya nchi yawe kidogo sana..
 
Pumba......
Inapokuja swala la maslahi ya taifa hakuna siri...kwa ni mkaguzi wa hesabu za serikali huwa anapata wapi taarifa za mapato na matumizi ya taasisi za serikali?...taarifa za akaunti ya taasisi kama chadema haiwezi kuwa siri kwani wanachama wanapaswa kujuwa mapato na matumizi ya chama chao...
 
VATICAN is the top donor, followed by German's Christian Democratic Union and Israel's Likud in the third place

Interesting facts!

And how much has The Chinese Communist Party donated to CCM so far? oops? and the ANC?
Au hiyo siyo issue ya public interest huh....
 
Kimsingi hoja hii haina majibu ya moja kwa moja au imekosa majawabu kabisa kutoka kwa waandamizi wa Chadema.
 
Kama chama,chadema tukitoa data huwa tunatoa na uthibitisho wa kina,kumbuka michango inatolewa na watanzania maskini kukisaidia chama tena miamia tu,kuchangia mafuta na chakula kwa makamanda,pili cdm haina akaunti moja tu,hadi matawi ya chama vijijini yana akaunti,hebu na nyie twambieni pesa za EPA mlizochota BOT kwa ajili ya kampeni kipindi kile cha mvua nyingi zilitumikaje?
 
Interesting facts!

And how much has The Chinese Communist Party donated to CCM so far? oops? and the ANC?
Au hiyo siyo issue ya public interest huh....

Eheeee na pia watueleze na zile hela malari na neti za bush zile kwendea wap.?
 
Ishu hapa sio mapato,,ishu ni matumizi...chadema wanaweza kuwa wanapata kiasi kikubwa cha ruzuku na mapato mengine ya michango ya wanachama na wafadhali kama wanavyodai...ishu inakuja kwenye matumizi ya fdha hizo...taarifa za bank zinaonesha matumizi kidogo sana ya fedha ukilinganisha na kazi zinazofanywa..kama wanapata fedha nyingi za harambee mbona bank statements hazineshi matumizi sahihi ya fedha hizo..?kwa wale wenye taaluma ya kibank waniambie kama ni sahihi mapato ya chama yanaweza kutumika kabla ya kupitia bank!!!!

Unajua kinachotufanya tushindwe kukusaidia ? umeulizwa maswali ya msingi sana hujajibu. 1. Je, umeweza kupitia akaunti zote za CDM na kujiridhisha kuwa matumizi ni hayo tu ? au huyo aliyekupatia taarifa hizo amekupatia nusu nusu ? 2. Je, ni tatizo mtu au taasisi kutumia pesa kidogo ? na unapoita pesa hizo ni kidogo unalinganisha na zipi ? 3. na kwakuwa umesema taarifa hizo siyo siri, ebu tusaidie umezipata kutoka akaunti ipi ? iliyoko benki gani ? ili tuweze kukupatia pia taarifa toka akaunti zingine. kwa ujumla wake utaweza kujua mtiririko mzima wa pesa za hicho chama.Najaribu kufuatilia hoja za watu wengine pia, naona hapo unatakiwa kujaza maneno yenye hoja, haya mkuu, KARIBU !
 
Mkuu hoja hapa ni matumizi ya hicho kinachopatikana hata kama ni kidogo!!!ukweli ni kwamba kunamatumizi mengi yanafanywa na viongozi wa juu wa cdm bila kutuata utaratibu wa kifedha...

hatukatai, tunaomba data za huo unaoita "UKWELI"
 
Taarifa za kibank zinaonesha kuwa mara baada ya uchaguzi mkuu 2010 chadema wametoa shilingi milioni hamsini na sita tu (56,000,000/=) kutoka katika akaunti ya chama kwa ajili ya matumizi ya mikutano na kuendesha chama..!!!

Swali:
Je ni kweli kwamba mikutano yote ya vuguvugu la m4c na operesheni sangara imegharimu kiasi hiki kidogo cha fedha au kuna vyanzo vingine visivyo rasmi?

Nawakilisha...!!

Kwani mamilioni ya Sabodo yanapitia account ipi au ndio kiini macho?
 
Godbless Lema akipitisha kopo kuchangisha fedha juzi kwenye mkutano wa CHADEMA.Chama hicho kimesema kama ilivyokuwa TANU,kitakuwa kikichangiwa fedha na wananchi badala ya kutegemea mafisadi wachache
Na Mdau wa Mjengwablog
 
Taarifa za kibank zinaonesha kuwa mara baada ya uchaguzi mkuu 2010 chadema wametoa shilingi milioni hamsini na sita tu (56,000,000/=) kutoka katika akaunti ya chama kwa ajili ya matumizi ya mikutano na kuendesha chama..!!!

Swali:
Je ni kweli kwamba mikutano yote ya vuguvugu la m4c na operesheni sangara imegharimu kiasi hiki kidogo cha fedha au kuna vyanzo vingine visivyo rasmi?

Nawakilisha...!!

Ruzuku tu ya Chama kutoka serikalini ni zaidi ya TShs millioni 200 kwa mwezi.

Ongeza na People's power.
 
Chadema hahijalishi mnapata hela wapi tunachokitaka watanzania tuachane na CCM cku ikifika so wadau wetu pambaneni,watanzania wenzangu tusichoke ipo siku mambo yatakuwa sawa............
 
hata Nape mropokaji hawezi leta hiyo hoja ya taarifa ya bank! Me nafikiri unatakiwa ujiulize hayo mabillion mnayo sema yanapitia wapi? Kinyume na hapo unaendeleza utoto wa Nape!
 
Mkuu Mzalendo sikatai wanachama kuchangia chama chao..ninachohoji mimi ni vipi wanachama wajifunge mkanda na kujinyima ili waweze kuchangia chama chao halafu watu wachache wazifaidi?..matumizi ya fedha ndani ya chadema hayapo wazi haiwezekani takwimu zioneshe mapato mengi ya harambee alafu matumizi ya mikutano mikubwa tena kila kona ya nchi yawe kidogo sana..

Acha utoto! Umesha wai kusomewa mapato na matumizi ya ccmwabepande? Nimegundua unaumwa ngoja nikuache hii ni kazi ya madaktari bingwa!
 
Back
Top Bottom