Chadema wanamtambua rais: Jana, leo, kesho na keshokutwa

Msekwa alisema kwenye mdahalo kwamba anaunga mkono madai ya katiba mpya wakati mwenyekiti wake alikwishasema watarekebisha katiba. Mbona huyo hamkumuuliza kwa nini aliongea hivyo?

Hata hivyo Alberto ameshasema hayo ni maoni na msimamo wake binafsi na tunajua kwamba yeye siyo msemaji mkuu wa chama chake ngazi ya taifa. Tujadili tu msimamo wake, ambao ni haki yake.
 
AM,

Hapa kuna kitu kinachanganyikana mkuu! Hivi CDM walishatoa tamko rasmi kuwa hawamtambui raisi? au tunafikiri walitamko hayo ''impliedly'' kwa kugomea mfumo na utaratibu mzima uliompa JK ushindi? Na, je ile walk out ya MPs wa CDM bungeni, ni ili kuwa na maana gani? kwamba hawamtambui rais?

Mimi kama nimewanukuu vizuri m/kiti Mbowe na Katibu Dr. W.Slaa sijamsikia hata mmoja wao aliyesema kuwa hamtambui raisi, nafikiri tena walikiri kumtambua raisi bali wakasema wanagomea utaratibu mzima uliomweka madarakani JK, ile kutohudhuria sherehe za kutangazwa mshindi, kuapishwa raisi na ile walk out ya wabunge, haikuwa na maana ya kutomtambua raisi bali kuonyesha watanzania, wafadhili, na dunia nzima kwamba mfumo na taratibu ziliopo ambazo zilimweka madaraka raisi kipindi hiki, zinakinzana na misingi ya kidemokrasia.....! na si vinginevyo! Kwa uelewa wangu, ile migomo yote ilikuwa na lengo la kutoa massage, kwamba hali si shwari kwenye mifumo yetu ya uchaguzi na ofcourse message ilikuwa sent na was delivered and read! matokeo yake sasa hivi unaona kila kona ya nchi hii, kila taasisi inazungumzia mchakato wa kuandaa katiba mpya ikiwa ni pamoja na Mh. Raisi, hii kwa kiasi kikubwa imetokana na legacy za uchaguzi mkuu wa October 2010, ambayo kwangu mimi ni kitu kizuri sana!

So mkuu Albert, sorry sijaona sana concern yako kubwa hapa as far as I know mambo yalivyokuwa, yalivyofanyika na yanavyoendelea kufanyika sasa!
 
Bos Kuna mtu kasema hivi mimi nashangaa hata wewe chamani unaonekana hujaelewa.

Mh. Mbowe alisema kwa mujibu wa katiba JK ndio Rais na hawawez kupinga popote kutoka na katiba ya sasa, na wao wanAchopinga ni mfumo mzima uliompa ushind JK na sio urais wa JK. hiki ndicho walichotokea bungeni..KUPINGA MFUMO MZIMA ULIOMPA URASI JK NA SIO KUPINGA URASI WA JK. Hili Mh. Mbowe alishalirudia kulisema mara kwa mara, hata kwenye mdahalo na Mh. Hamad alilisema hili. Pia Dr. Slaa alilisema hivyo hivyo. Hii ina maana kwamba shinikizo la kutoka bungeni ni kushinikiza mabadiriko ya mfumo wa uchaguzi,uundwaji wa tume na kubadirishwa kwa katiba, ..KUTOKA KULE BUNGENI HAKUKUWA KUSHINIKIZA JK AJIUZULU..Pasco naomba ULEWE VIZURI HAPO.
 
Hivi so long as Chadema na Wabunge wake wataleta maendeleo majimboni kwao..., na kuwabana mafisadi wa CCM..., does anyone cares about this SEMANTICS..??
 
Hivi so long as Chadema na Wabunge wake wataleta maendeleo majimboni kwao..., na kuwabana mafisadi wa CCM..., does anyone cares about this SEMANTICS..??

VoR,

Chadema ikifanya kazi yake ya siasa vizuri na wabunge wakawa chachu ya maendeleo (am having reservations kuhusu concept ya mbunge na chadema kupeleka maendeleo bungeni) then the semantics wont matter. But for now I think it matters ukiangalia propaganda ya CCM kutudiscredit kwamba hatuna msimamo.

As the discussion continues ukweli unaonekana na umuhimu wa suala kwamba CDM inamtambua Raisi au la unaonekana kwamba haupo.

Hii inasaidia kuonyesha ni jinsi gani a non issue can be propagated to be an issue!
 
VoR,

Hii inasaidia kuonyesha ni jinsi gani a non issue can be propagated to be an issue!

True Mkuu, and thats why nchi yetu ipo in a reverse gear and we are going backwards instead of forward.... always using a lot of energy in non issues..., ndio maana hata leo Bungeni Speaker amekataa wazo la Myika la kuzungumzia Tanesco na akaona bora waendelee kufanya uchaguzi ambao wangeweza kuufanya kwenye their own spare time hata usiku .....

Hii nchi kwa haya madudu am feeling ashamed na sijui nitawaambia nini wajukuu zangu kwa upuuzi which has been done by this generation, na kwa mtaji huu am sure nitakuwa ninamuonyesha mjuu ma craters where our madini used to be
 
Katika hili linalojadiliwa hapa mimi naungana na muanzisha mada CHADEMA itabidi igharimike kulitolea ufafanuzi. Sina ushahidi wa moja kwa moja wa kiongozi yeyote wa CHADEMA kwamba alitoa kauli ya kwamba hamtambui Rais, lakini uelewa wa walio wengi ni kwamba CHADEMA walitoka nje ya Bunge kwa sababu hawamtambui Rais.

Kabla ya kuanza kuandika maoni haya nilijaribu kuchukua randomly simu tano kwenye orodha ya simu nilizozi-save kwenye simu yangu ya watu ambao si washabiki wa chama chochote na kuwapigia na kuwauliza swali rahisi tu wao wanaelewa nini kuhusu sababu zilizowafanya CHADEMA watoke nje ya ukumbi wa bunge kabla ya raisi kuanza kuhutubia, wote walisema kwamba sababu ni kwamba hawamtambui Rais. Pili nikajaribu ku-google kwenye mtandao articles sinazohusiana na CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa bunge kabla ya rais kuhutubia, baadhi zilitaja sababu hiyo hiyo. Jaribio kama hili mwana JF yoyote akalifanya.

Kwa kifupi anachokisema mtoa mada mimi naungana nae, uongozi wa juu wa CHADEMA uhahitaji kulitotea ufafanuzi na kama walinukuriwa vibaya na vyombo vya habari wawaeleze wananchi. Kinachoonekana sasa hivi kwa walio wengi ni kwamba viongozi wa CHADEMA hawana msimamo. Leo wanazungumza hili, kesho wanazungumza lile. Wengine wanadiriki hata kusema njaa yao ndio iliyowafanya walegeze msimamo, kwa maneno mengine priority ni matumbo yao baada ya hapo umma uliowachagua. Mtetezi wa kweli ni yule anayejitoa mhanga kwa maslahi ya umma. Hisia hizi si vizuri kuziacha ziendelee vichwani mwa watu, na hasa zinapohusu chama madhubuti kama CHADEMA.

Kimsingi naungana kabisa na MsandoAlbeto kwamba ufafanuzi unahitajika, na kama tulinukuliwa vibaya kwenye TV na magazeti, tuseme tusikae kimya. Binafsi sioni tatizo la ushauri wa MsandoAlbeto.
 
They are very good at pretending

Wanamtambua vema amiri jeshi mkuu wa nchi

Wanatambua vizuri ameshinda kihalali kwa asilimia 61

Wanatambua vema kuwa wamepigwa chini na wananchi pamoja na kuleta siasa za kikanisa nchini

na 2015 tutawapiga chini vibaya ..cdm wanafaa sana kuwa kwenye "complain corner" that is where they are good at ok!
 
Katika hili linalojadiliwa hapa mimi naungana na muanzisha mada CHADEMA itabidi igharimike kulitolea ufafanuzi. Sina ushahidi wa moja kwa moja wa kiongozi yeyote wa CHADEMA kwamba alitoa kauli ya kwamba hamtambui Rais, lakini uelewa wa walio wengi ni kwamba CHADEMA walitoka nje ya Bunge kwa sababu hawamtambui Rais.

Kabla ya kuanza kuandika maoni haya nilijaribu kuchukua randomly simu tano kwenye orodha ya simu nilizozi-save kwenye simu yangu ya watu ambao si washabiki wa chama chochote na kuwapigia na kuwauliza swali rahisi tu wao wanaelewa nini kuhusu sababu zilizowafanya CHADEMA watoke nje ya ukumbi wa bunge kabla ya raisi kuanza kuhutubia, wote walisema kwamba sababu ni kwamba hawamtambui Rais. Pili nikajaribu ku-google kwenye mtandao articles sinazohusiana na CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa bunge kabla ya rais kuhutubia, baadhi zilitaja sababu hiyo hiyo. Jaribio kama hili mwana JF yoyote akalifanya.

Kwa kifupi anachokisema mtoa mada mimi naungana nae, uongozi wa juu wa CHADEMA uhahitaji kulitotea ufafanuzi na kama walinukuriwa vibaya na vyombo vya habari wawaeleze wananchi. Kinachoonekana sasa hivi kwa walio wengi ni kwamba viongozi wa CHADEMA hawana msimamo. Leo wanazungumza hili, kesho wanazungumza lile. Wengine wanadiriki hata kusema njaa yao ndio iliyowafanya walegeze msimamo, kwa maneno mengine priority ni matumbo yao baada ya hapo umma uliowachagua. Mtetezi wa kweli ni yule anayejitoa mhanga kwa maslahi ya umma. Hisia hizi si vizuri kuziacha ziendelee vichwani mwa watu, na hasa zinapohusu chama madhubuti kama CHADEMA.

Kimsingi naungana kabisa na MsandoAlbeto kwamba ufafanuzi unahitajika, na kama tulinukuliwa vibaya kwenye TV na magazeti, tuseme tusikae kimya. Binafsi sioni tatizo la ushauri wa MsandoAlbeto.

Very well said and I totally agree with you. Dr. WS and Hon. FM the ball is in your court, please say something. It is very important for the people who listen to you. Please!
 
Very well said and I totally agree with you. Dr. WS and Hon. FM the ball is in your court, please say something. It is very important for the people who listen to you. Please!

I slaa have nothing to say sir! (absolutely nothing)

I Mbowe just pretending to please Slaa (ameumia sana mzee yule anapenda u-rais)
 
Iramusm,

Hata na mimi nimeelewa hivyo,isipokuwa hawa wananchi walioko huko kijiji cha chemchem tutawabadilishaje waweze kuelewa kama tunavyoelewa?
ALBERTOMSANDO wewe na wengine ndio mko karibu na wananchi mtusaidie ili tujue namna ya kuwaelimisha wananchi lengo likiwa ni kuimarisha chama.
 
Siwezi kutia neno kutokana na kutofahamu cheo chako CDM kwa sababu umetumia jina bandia lakini nadhani wewe utakuwa mtu mzito sana kwenye chama tunashukuru kwa kutoa msimamo wa Chama.
 
pia inaleta shida kuelewa CDM Wanapochangia hotuma ya raisi bungeni ambayo wameisusia nayo imekaaje?huku wanakataa kusikiliza huku wanaomba nafasi kuchangia.kaaazi kweli kweli ndumilakuwili.
 
pia inaleta shida kuelewa CDM Wanapochangia hotuma ya raisi bungeni ambayo wameisusia nayo imekaaje?huku wanakataa kusikiliza huku wanaomba nafasi kuchangia.kaaazi kweli kweli ndumilakuwili.

Wanasema huo ni upopo mie simoooo
 
Siwezi kutia neno kutokana na kutofahamu cheo chako CDM kwa sababu umetumia jina bandia lakini nadhani wewe utakuwa mtu mzito sana kwenye chama tunashukuru kwa kutoa msimamo wa Chama.

Mohamed, naheshimu mawazo yako mara zote. Kama Albert Msando ni jina bandia ni sawa. Uhuru wa mawazo.

Wakati unatumia uhuru wako, just google the name and see. Sina sababu ya kuficha mimi ni nani. Soma post yangu 'wanaJF nisaidieni kufikiri'.

Sikuwa nategemea ungeweza kuweka mbele ushabiki. Napata faraja kwa kujikumbusha kwamba wanadamu hatufanani.
 
Iramusm,

Hata na mimi nimeelewa hivyo,isipokuwa hawa wananchi walioko huko kijiji cha chemchem tutawabadilishaje waweze kuelewa kama tunavyoelewa?
ALBERTOMSANDO wewe na wengine ndio mko karibu na wananchi mtusaidie ili tujue namna ya kuwaelimisha wananchi lengo likiwa ni kuimarisha chama.

Ni lazima kila mwanachama na kiongozi wa CDM kwanza aelewe msimamo wa chama vizuri. Aulewe kwa kiasi ambacho hakuna shaka. Akielewa yeye then atawaelewesha wananchi. Naamini viongozi husika wanayasoma na kusikia yote.
 
Nidhahiri wakati mwingine tunatafuta aibu sisizo namaana! pamoja nakuwa huru katiaka kutoa maoni na hata misimamo binafsi isipokuwa isivunjwe sheria tuna hitaji kujiandaa ili tueleweke mahitaji yetu na michango yetu katika jami.Kama malengo nikuchekesha/kufurahisha wanajamvi kwakuongea mambo ambayo yako wazi na kuyafanya kama yamegunduliwa na mtoa mada kwa mtindo huu basi taifa limekosa wadadisi wakuleta hoja mpya na zenye changamoto katika jamii

Alberto kama kweli wewe ni mwanasheria wa CDM basi kuna hatari chama kuingia kwenye migogoro ya kisheria kwa sababu kama wakili huta weza kusikiliza vizuri hutaweza kusoma maandiko vizuri na hutakuwa na uwezo wa kuchambua mantiki ya matendo/matukio hakika hutaweza kujenga hoja nzuri ya utetezi kwa mteja wako ambaye ni CDM atakapo kabiliwa na maswala ya kisheria mahakamani.

Kauli yaviongozi wa juu wa CDM haijawahi kuyumba au kuteteleka hata kidogo kuhusu mtazamo wao kwa raisi wa jamhuri hii hawajawahi kusema au kuandika mahalipopote kuwa hawa mtambui raisi kama taasisi au kikwete kama yeye binafsi. Kama hili hujawahi kulisikia nina mashaka makubwa sana na taaluma yako, kwani liko wazi nalimekuwa wazi siku zote tangu Dr. Slaa akiwa mgombea uraisi alipo itaka tume ya uchaguzi isitishe utangazaji wa matokeo ya uchaguzi kwa sababu taratibu zime kiukwa.Dr. Slaa alisema wana kataa ila hawapingi matokeo ya raisi baada ya kutangazwa na tume kwa sababu katiba haiwaruhusu kupinga matokeo ya raisi mahalipopote pale yakisha tangazwa na tume.

Dr. Slaa alisema pamoja na uchaguzi wote kuchezewa matokeo ya wabunge na madiwani hawatayakataa ila watayapinga kwasababu sheria za nchi zinaruhusu kupinga matokeo ya wa bunge na madiwa mahakamani.Sasa Alberto kama mwanasheria raisi hapingwi na CDM tafsiri yake ni nini? na kukataa matokeo ya liyo muweka raisi madarakani kwako kuna maanisha nini?nakugomea shuhuri zilizo ongozwa na raisi moja kwa moja aliye wekwa madarakani kwahila inatoa tafsiri gani kwako kama mwanasheria? Je huoni kama CDM haimtambui raisi kwa ushindi wake na sio kama taasisi?

Nimiezi minne sasa toka uchaguzi umalizike je tunahitaji mda kiasi gani kuweza kuchanganua hoja nyepesi kama hii ya kuto mtambua raisi kwa ushindi wake? Mbona Alberto unataka kupotosha watu kwa namna hii ya kutoa hoja iliyo wazi na kuifanya imejificha hivyo nivigumu kwa wengine kutambua.........Usipotoshe umma hakuna chakuuliza hapa kwani kila kitu kina eleweka kuwa raisi hatambuliki kwa ushindi wake lakini sio kama taasisi kwasababu taasisi imewekwa kisheria na lazima iheshimike.Ninani alikufundisha sheria pale mlimani ulipenyaje kwa mtindo huu wa kuto kuwa makini ulipita kwenye mikono ya Fimbo kweli wewe........
 
Kereng'ende, kutomtambua Raisi kwa ushindi wake na sio kama taasisi unamaanisha nini?

Nakubaliana na hoja zako za kutaka kujua taaluma yangu inanisaidiaje. Uelewa wangu mdogo wa msimamo wa chadema ndio ulionisukuma kuleta hoja. Sikuwa na nia ya kuchekesha wala kufurahisha mtu. Wote waliochangia kabla yako wametoa mawazo/ufafanuzi wao. Wengi tumeelewa. Umerudia maneno yao kwamba, Chadema haijawahi kusema haimtambui Raisi. Sasa inaeleweka kati yetu.
 
Back
Top Bottom