Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
WanaJF,
Suala la CDM kumtambua au kutomtambua Raisi wa JMT limezua mijadala mbalimbali.
Kuweka rekodi sawa imebidi niweke hoja mbele yenu. Hoja yangu ni kwamba kama CDM tumeendelea kumtambua Raisi kwa matendo yetu ingawaje kwa vinywa vyetu imekuwa ngumu kutamka.
Nakubali kwamba ilitamkwa kwamba hatumtambui Raisi na haijawahi kutamkwa vinginevyo. Nakubali kwamba hata wakati wa sherehe za kumuapisha tuligoma kwenda na alipolihutubia Bunge tulitoka.
Lakini, muda huo huo tumeendelea kuhudhuria vikao vya Bunge na kuwahoji mawaziri aliowateua. Tunawahoji kwa nafasi zao za uwaziri na kutegemea watafanya yale tunayoyahoji.
Je inawezekana kuwatambua mawaziri na kazi zao kama humtambui aliyewateua?
Tunaishinikiza 'serikali' ifanye yale tunayoyataka, je serikali inaweza kuwepo kama Raisi hayupo? Au kutomtambua Raisikuna maana gani? Ni kutotambua mamlaka yake au ushindi wake?
Ufafanuzi huu haujatolewa na CDM hivyo ni salama kuamini kwamba CDM inatambua mamlaka ya Raisi na kuiheshimu.
Katika hili CDM lazima ibebe lawama za kutotoa ufafanuzi wa kauli au matamko kwamba haimtambui Raisi kwa wananchi waelewe. Kwa kiongozi yeyote kauli yake lazima iwe inayoeleweka na ya wazi kiasi kwamba mpokeaji wake anakuwa kwenye nafasi ya kuielewa ili kufanya uamuzi sahihi. Si salama kuacha matendo yakatumika kutoa tafsiri.
Kama CDM bado haimtambui Raisi ni vyema ikasemwa wazi na kwa lugha nyepesi. Huo ni ukomavu wa kisiasa na uthibitisho wa nia njema na thabiti ya kiuongozi.
Mimi binafsi kama mwanaCDM kwa maneno na kauli yangu namtambua Raisi. Napinga ushindi wake na sikubali daima kwamba alishinda kihalali. Kulikuwa na hila za kila aina ili aweze kushinda. Lakini nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa sheria, sheria zetu zimeruhusu Raisi anayeshinda kwa hila aongoze nchi hivyo namtambua kama Raisi wa JMT aliyeshinda kwa hila.
Nawatambua mawaziri na watendaji wengine walioteuliwa na Raisi aliyeshinda kwa hila.
Siwezi kuthibitisha hila hizo kwa sababu sheria hainiruhusu kuthibitisha baada ya NEC kumtangaza mshindi.
Jana, leo, kesho na keshokutwa Raisi wa JMT aliyeshinda kwa hila ndie Raisi na nimetambua na ninatambua na nitatambua hivyo!