Chadema wanahukumiwa kabla ya kusikilizwa

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
Haya wandugu naomba tujibu maswali yafuatayo:-

1.Katika purukushani za kumkamata muhalifu wa kike na ikatokea shanga,zikakatika,hijabu ikadondoka na saa ikapotea,kitendo hicho ni;
(a)shambulio la aibu
(b)utovu wa adabu wa mkamataji
(c)halali kwasababu bila hivyo vielelezo havitapatikana
(d)si halali kwasababu muhalifu mwanamke inabidi akamatwe na mwanamke na hayupo basi aachiwe'asepe'tu.

2.Polisi wa Tanzania ni wabovu kwa sababu;
(a)hawatumii akili bali hutii amri yoyote kutoka juu.
(b)wanapendelea chama tawala waziwazi.
(c)hawawapendi wapinzani.
(d)(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

3.Kwa kuwahukumu chadema kuwa ni wahuni kabla ya kuwasikiliza Rajabu kiravu ni;
(a)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya uchaguzi.
(b)mkurugenzi mzuri wa tume ya taifa ya CCM.
(c)msimamizi mzuri wa maslahi ya chama tawala.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

4.DC asiye jua ratiba za kampeni zinazo fanyika wilayani kwake ni;

(a)mvivu anaye pokea mshahara asio ufanyia kazi.
(b)mbumbumbu tu wa kazi ya ukuu wa wilaya.
(c)mbabaishaji tu ambaye ni kielelezo cha ubaya wa kuteua watu kwasababu tu ya ukereketwa wao.
(d)mtu safi anaye fanikishwa matakwa ya chama tawala.

5.Waandishi na wachambuzi wanaoilaumu chadema kwa kumkamata mtuhumiwa wa uhalifu;

(a)wanafanya kazi yao vizuri
(b)wanajipendekeza kwa ccm na watawala ili wapate safari na posho.
(c)hawajui walifanyaro kwasababu hawajasoma katiba ya nchi .
(d)mamluki wanao tumiwa na ccm kuvuruga upinzani.

6.Jukumu la kumkamata muhalifu ni la;
(a)polisi pekee.
(b)kila mwananchi.
(c)askari yoyote mwenye magwanda na silaha.
(d)vyama vya siasa.

7.Kama anaye paswa kumkamata muhalifu hataki yaani polisi wajibu wa mwananchi wa kawaida ni;

(a)kumwachia muhalifu aendelee kuvunja sheria.
(b)kumwachia muhalifu aende zake.
(c)kulalamika kwa polisi wale wale wasio taka kukamata.
(d)majibu yote a,b,na c ni sahihi.

8.Wanao sababisha amani kuvurugika katika kampeni za uchaguzi hapa tanzania ni;

(a)polisi wasio taka kutenda haki.
(b)wasimamizi wa uchaguzi na wakuu wa wilaya.
(c)viongozi wa ngazi za juu wano amuru polisi kufanya wanavyo taka na siyo polisi walivyo ona inafaaa.
(d)waroho wa madaraka wanaopendelea ccm kwa makusudi kwa matarajio ya kupandishwa vyeo.


Tafadhali jibu maswali kwa ustaarabu bila kejeli na matusi,toa hoja sio vihoja.
 
Back
Top Bottom