CHADEMA wanaandamana upinga ushindi wa Makongoro

Hovyo kabisa.. Chadema ikishinda hukumu MAHAKAMA IMETENDA HAKI...... ikishindwa Kelele,,

Sasa nyinyi wanasiasa gani!???? au wapiga makelele tu

Wewe unaongea nini??! yaaani kusoma hujui hata picha tu kuangalia napo huwezi!!! Wewe kama sio GAMBA basi jaribu kufuatilia tu mwenendo mzima wa kesi yenyewe halfu njoo sasa utoe komenti zako! Acha hizo!
 
nyie mjini andamaneni ila mi npo msituni najifua taratibu sitaki kuja kudharauliwa na wajukuu.
 
nipo na makamanda wezangu tunaelekea makaomakuu yc cdm


##pole ndugu hamna kazi za kufanya ndio maana mnaandamana,kama mgekuwa mmeaga nyumbani kuwa mnaenda kazini msingepata muda wa kuandamana (ndio maana vibaka wanaongezeka)
 
Mikoa yote yenye gahawa, kashata, juice ya tende na wazee wa misuli washindao vibarazani iko nyuma kimabadiliko. Shame on you Tanga, Pwani, Lindi, Mtwara, Dsm and others who are in love with Magamba.
Go "do" yourself!!! we're just Tanzanians like everybody else.
 
wakuu msinganganie maandamano wasije kuwapiga mabomu na kuwauwa,hawachelewi kusema walikuwa wana hatarisha amani na kuchochea fujo.Kikubwa ni kujipanga na kwenda kukata rufaa.Bado naamini jimbo la Segerea ni mali ya CDM.Haki haizulumiwi bali inacheleweshwa tuu.
 
wafuasi+wa+Chadema+baada+ya+hukumu.JPG
 
Leo asubuhi katika moja ya posti zangu nilieleza jinsi ilivo vigumu kwa chadema kushinda kesi ya ubunge kwa majimbo ya yaliyo katika majiji. Ni kweli kuwa cdm wameshinda majimbo ya rural, hii imetengenezwa makusudi ili kutekeleza mkakati wa ccm kuchukua majimbo ya majiji waliyo yapoteza kwa upinzani katika uchaguzi.

Kinachofanyika hapa na mahakama ni kiini macho kwa kuwadanganya wananchi ionekane kuwa kila chama kina nafasi ya kupata ushindi kwnye kesi ili hali ni mchezo ambao tayari ccm wamejipenyeza ndani ya mhimili huu dhaifu wa mahakama.

Hii ni sawa na refa dhaifu wa mpira wa miguu anayeamua kuipa timu penati dhidi ya timu pinzani kama fidia ya adhabu ya kadi nyekundu kwa mchezaji wa timu husika kwa nia ya ku-balance mchezo na kuweka sheria kando ili hali akijua kuwa anachofanya ni uonevu.
 
##pole ndugu hamna kazi za kufanya ndio maana mnaandamana,kama mgekuwa mmeaga nyumbani kuwa mnaenda kazini msingepata muda wa kuandamana (ndio maana vibaka wanaongezeka)

kati ya wenye kazi nawe upo,. Ungekuwa nakazi usingepata hata mda wa kutetea maadui wa tz
 
Inakuwaje mtu akamatwe na kidhibiti live halafu ashinde kesi??

Hii hukumu imeivua nguo mahaka kuu kwa mara nyengine.

Hapo mtu unashindwa kuelewa weledi wa jaji kama Pro. Juma uko wapi, umakini wake uko wapi? na katika hali kama hii wananchi wanazidi kupoteza hata ile imani ndogo wanayokuwa nayo juu ya mahakama zetu.
 
We endekeza ushabiki wa siasa ukalazwe ndani, huyo unaemuandamia unadhani hata anajua sura yako?
 
Hawa nao wanachekesha! Hukumu imetolewa mahakamani halafu maandamano yanaenda ccm office hii imekaaje? Wanabip FFU hawa
 
CDM msipojiangalia mtaporomoka sasa hivi.Mjifunze kushinda na kushindwa,Mnao wanasheria lukuki,toka lini tiba ya kutoridhishwa na hukumu ya mahakama ni maandamano.Sasa tutawaona ninyi ni wasumbufu.Mbona CCM hawakuandamana Singida.
 
Wanaiga siasa za kwenye Tv hawa. Maandamano gani yasioratibiwa. Hata mgombea aliyeshindwa amesema atawasiliana na chama kama kunahaja ya kukat rufaa.sasa hawa wapo chama gani
 
Kwa kweli CDM munatuangusha,Mnachoamini ninyi ni kua maana ya haki ni CDM kushinda kesi zote za uchaguzi.Hao wanasheria wenu luluki mlio nao wanakazi gani.Msipojihadhari mtaporomoka sasa hivi kwa kuonenana wasumbufu.MNATUANGUSHA.
 
Hii hukumu imeivua nguo mahaka kuu kwa mara nyengine.

Hapo mtu unashindwa kuelewa weledi wa jaji kama Pro. Juma uko wapi, umakini wake uko wapi? na katika hali kama hii wananchi wanazidi kupoteza hata ile imani ndogo wanayokuwa nayo juu ya mahakama zetu.
Kaka ukistaajabu ya Arusha utayashangaa ya DSM.

Kule arusha jaji kafanya kusikia tu kwa mdomo kwamba Lema alitukana, bila uthibitisho wowote, tena kusikia kwenyewe ni kutoka kwa watu sijui watatu wa kuokoteza akakubaliana nao.

Huyu wa DSM kapelekewa mpaka na video bado haamini kama Mahanga ni mwizi.
 
Back
Top Bottom