CHADEMA wana tabia ya mtu mbinafsi

Mtuma post anamkosea fadhila Sugu!Hata kama ni kweli kulikuwa na mazungumzo na serikali ya mkoa,lakini wana Mbeya tulishaweka msimamo wa kutomsikiliza yeyote isipokuwa RAISI WETU SUGU!
Hivyo mchango wa SUGU hauwezi kudharaulika hata kidogo!Kama huamini,kulikuwa na haja gani ya kumwita Sugu toka mjengoni?Si serikali yenyewe ingekaa na kukubaliana na wafanyabiashara?
SUGU moto juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!
 
Sugu moto chini tanlalalalaaaaaaaa ni moto chini sugu ni chama kubwa nafika mpaka bamaco sanfransico huko nafika katika kutafuta mshiko na mampromota koko huko mliko sitaki tena aman katika dili feki sugu sasa namiliki bunduki tunaingiza mamilion mnaonga mademu vitara wanga huko mlipo nawapa dole la kati,ni nani? Ni wewe tuuuuu sugu moto chinix3
 
sitakubaliana kwamba kutulia kwa vurugu Mbeya ni kutokana na juhudi za mbunge wa mbeya mjini (CHADEMA) Mr Sugu peke yake ni juhudi za pamoja za viongozi wa mkoa wa mbeya bila kujali vyama wanavyotoka. Sugu au Mr II ni mbunge makini na kwa nafasi yake alikuwa na wajibu wa kibunge kukutana na wananchi haukuwa wajibu wa kichadema.

habari za kuaminika zinaeleza wazi kwamba baada ya Sugu kukutana na uongozi wa mkoa wa mbeya na kukubaliana kwa pamoja kuhusu mambo kadhaa kwa ajili ya utatuzi ikiwemo kuwaacha wafanyabishara hadi suluhu ipatikane ndipo alikwenda kuzungumza na wafanyabiashara ndogo kwa kutumia kauli ya mkoa lakini kila mtu anataka kutuaminisha kwamba zile ni juhudi za chadema na Sugu peke yake.

Tuache kutumia matukio kujijenga kisiasa.

magamba at work!
 
Mkuu, hoja yako ni nini hapa? Kwangu mimi bado hujaeleweka. Kama hao viongozi wa mkoa walikuwa na ubavu wa kutuliza ghasia, walikuwa na haja gani ya kujadiliana na Mhe. Sugu? Na, aidha kwa nini wao wenyewe hawakutoka kwenda katika mkutano wa hadhara na kuongea na wananchi? Utake usitake, ukweli utabaki katika historia kwamba CDM na Mhe. Sugu kama Mbunge wao, wameweza kuzima vurugu za Mbeya zisiendelee.
 
ikubalike tu kuwa zilikuwa juhudi na ushirikiano wa pamoja kwa mfano, kama jeshi la polisi lisingesitisha mapambano hata Sugu angeshindwa kupata jukwaa la kuzungumza na machinga. Baada ya polisi wa mbeya kutumia busara na kusitisha kutumia nguvu kubwa kama kule Arusha kulisaidia sana kuepusha maafa zaidi kule mbeya.

Mkuu, nani kawaletea hiyo busara? Kwa nini hawakuwa nayo tangu awali wakati wanajipanga kwenda kushambulia? Vitendo vya polisi wetu vinafanana nchi nzima. Wao wanachojua ni kuzima ghasia au maandamano kwa kushambulia tu. Umeiona ile picha ya"busara waliyoitumia" kwa yule binti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( angalia gazeti la Mwanachi la Jana 12/11/2011)
 
busara sio lazima ianze mwanzo wa tukio inaweza kujitokeza katikati ya tukio kulingana na ishara (indicators) kutokujua matokea ya operesheni sio kukosa busara bali kuendelea na operesheni yenye madhara ndio kukosa busara. Bado busara ilitumika
 
Mtuma post anamkosea fadhila Sugu!Hata kama ni kweli kulikuwa na mazungumzo na serikali ya mkoa,lakini wana Mbeya tulishaweka msimamo wa kutomsikiliza yeyote isipokuwa RAISI WETU SUGU!
Hivyo mchango wa SUGU hauwezi kudharaulika hata kidogo!Kama huamini,kulikuwa na haja gani ya kumwita Sugu toka mjengoni?Si serikali yenyewe ingekaa na kukubaliana na wafanyabiashara?
SUGU moto juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!

mtuma post hajamkosea fadhila sugu, soma vizuri usikurupuke na ushabiki
 
kwa hiyo utakubaliana na mimi polis ni waleta na wafanya vurugu kwa niaba ya ccm na green guard

polisi wapo kikatiba na majukumu yao. Hata chadema ikatokea wakashika dola polisi watakuwepo sio wa chama chochote cha siasa
 
Back
Top Bottom