CHADEMA wana tabia ya mtu mbinafsi

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
sitakubaliana kwamba kutulia kwa vurugu Mbeya ni kutokana na juhudi za mbunge wa mbeya mjini (CHADEMA) Mr Sugu peke yake ni juhudi za pamoja za viongozi wa mkoa wa mbeya bila kujali vyama wanavyotoka. Sugu au Mr II ni mbunge makini na kwa nafasi yake alikuwa na wajibu wa kibunge kukutana na wananchi haukuwa wajibu wa kichadema.

habari za kuaminika zinaeleza wazi kwamba baada ya Sugu kukutana na uongozi wa mkoa wa mbeya na kukubaliana kwa pamoja kuhusu mambo kadhaa kwa ajili ya utatuzi ikiwemo kuwaacha wafanyabishara hadi suluhu ipatikane ndipo alikwenda kuzungumza na wafanyabiashara ndogo kwa kutumia kauli ya mkoa lakini kila mtu anataka kutuaminisha kwamba zile ni juhudi za chadema na Sugu peke yake.

Tuache kutumia matukio kujijenga kisiasa.
 
ikubalike tu kuwa zilikuwa juhudi na ushirikiano wa pamoja kwa mfano, kama jeshi la polisi lisingesitisha mapambano hata Sugu angeshindwa kupata jukwaa la kuzungumza na machinga. Baada ya polisi wa mbeya kutumia busara na kusitisha kutumia nguvu kubwa kama kule Arusha kulisaidia sana kuepusha maafa zaidi kule mbeya.
 
kama mkoa ungeendelea kushikilia msimamo wa kuwaruhusu polisi kusonga mbele Sugu angekuta risasi kila mahala angetokea wapi? mambo mengine yanakuzwa kisiasa ili ionekane CCM hawakuwa sehemu ya muafaka kati ya pande mbili zinazosigana
 
wakati wote vita havina mshindi. Ukienda Rwanda, Burundi na kwingineko ambako vita na ghasia imetulia huwezi ukakuta kuna kundi linasema limeshinda au limeleta amani. Huwezi kuleta amani peke yako kama mwenzako bado anapigana, anakushambulia au anaendeleza mapigano itapidi na wewe uendelee kupigana. Kama Sugu aliweza kuwakusanya wananchi kwa amani kwenye eneo la vita na kuongea nao ina maana upande wa pili uliamua kusitisha vita. Tuwapongeze wote walioshiriki kuleta amani.
 
sitakubaliana kwamba kutulia kwa vurugu Mbeya ni kutokana na juhudi za mbunge wa mbeya mjini (CHADEMA) Mr Sugu peke yake ni juhudi za pamoja za viongozi wa mkoa wa mbeya bila kujali vyama wanavyotoka. Sugu au Mr II ni mbunge makini na kwa nafasi yake alikuwa na wajibu wa kibunge kukutana na wananchi haukuwa wajibu wa kichadema.

habari za kuaminika zinaeleza wazi kwamba baada ya Sugu kukutana na uongozi wa mkoa wa mbeya na kukubaliana kwa pamoja kuhusu mambo kadhaa kwa ajili ya utatuzi ikiwemo kuwaacha wafanyabishara hadi suluhu ipatikane ndipo alikwenda kuzungumza na wafanyabiashara ndogo kwa kutumia kauli ya mkoa lakini kila mtu anataka kutuaminisha kwamba zile ni juhudi za chadema na Sugu peke yake.

Tuache kutumia matukio kujijenga kisiasa.

Matukio ndio yanajenga kisiasa maana ndipo wananchi wanapojieleza pale watawala wanapokuwa viziwi...
 
katika hali ya kawaida Sugu sio mtendaji ni mwakilishi wa wananchi. watendaji walishakosana na wananchi katika shughuli zao za kiutendaji ni busara na hekima kubwa kumtumia mwakilishi wao kupeleka ujumbe wa amani kwao kuliko wangekwenda watendaji. Ni kazi ya pamoja haikuwa ya Sugu lakini Sugu ninampongeza kwa kujitolea kwake na naamni ni mwakilishi anayewajibika kwa wapiga kura wake. kwa kukaa kwake kiti kimoja na wanaCCM ni jambo jema kwa maslahi ya wana Mbeya
 
Wana mbeya walikataa kuongea na kiongozi yoyote zaidi ya sugu na wakatangaza kuu sugu ndiye rais wa mbeya. Nakushangaa wewe unayesema eti sugu angepitia wapi? Kweli wewe umelala fofofo kama jina lako lilivyo, na pia umelalia hengover za uccm.
 
Matatizo ya wananchi hayasuluhishwi na mtu mmoja.They had to come out as a team to harmonize the situation
 
Kila mtu CDM huwa anasimama kivyake na kila mtu ana maamuzi yake. Hawafanyi kazi kwa umoja na kwa matakwa ya chama kwa ujumla. Mifano dhahiri tunaiona, mfano ishu ya Lema kujipeleka magereza.
Hapa jamvini tumewaona kila mtu akija kwa staili yake. Leo Zitto atasema hiki, kesho Regia ataongea hili na Slaa atakuja kivyake.
Huwa siku zote nafananisha CDM na gari bovu...halina mwenyewe! Inabidi kama CDM wanataka kufika mbali, wajifunze kuwork collectively. Waige kwa CUF, kama mmeshaona ishu zote zinazohusu chama cha CUF Julius mtatiro
 
Wana mbeya walikataa kuongea na kiongozi yoyote zaidi ya sugu na wakatangaza kuu sugu ndiye rais wa mbeya. Nakushangaa wewe unayesema eti sugu angepitia wapi? Kweli wewe umelala fofofo kama jina lako lilivyo, na pia umelalia hengover za uccm.
SUGU ndio Rais wao? waziri mkuu balozi, mambo ya ndani afande sele.

Sasa ndio naamini kuwa Tanzania tumerogwa.
 
Matukio ndio yanajenga kisiasa maana ndipo wananchi wanapojieleza pale watawala wanapokuwa viziwi...

ukiziwi usingeleta amani mbeya labda kama hujui maana ya kiziwi. Ukiziwi ni kitendo cha kutosikia kabisa kama walisikia na kusitisha mapambano
ni ishara kwamba walisikia.
 
Arusha na Mwanza hakuna wakuu wa mikoa na RPC's ndio maana tunataka mwelewe kuwa mbeya kulitumika busara zaidi
 
Wana mbeya walikataa kuongea na kiongozi yoyote zaidi ya sugu na wakatangaza kuu sugu ndiye rais wa mbeya. Nakushangaa wewe unayesema eti sugu angepitia wapi? Kweli wewe umelala fofofo kama jina lako lilivyo, na pia umelalia hengover za uccm.

Usilete siasa mbona kule Arusha Mbowe na Slaa walikamatwa na kufunguliwa mashitaka na polisi hao hao lakini polisi wa mbeya walikuwa na umoja na sugu kuepusha ghasia zaidi. wewe unacheza na dola ikiamua. tukiacha siasa hapa tuwapongeze sana polisi wa mbeya kwa kusitisha mashambulizi dhidi ya machinga na kuingia kwenye meza ya mazungumzo.
 
kumbuka moja ya kauli za Sugu alipozungumza na wananchi ni kwamba warudi sehemu yao ya biashara hadi pale watakapoambiwa utaratibu mwingine lakini pia akasema wamekubaliana kuondoa majeshi mtaani. hii ina maana alikuwa anafikisha ujumbe aliokubaliana na viongozi wenzake wa mkoa. Sugu hana mamlaka ya kuondoa majeshi mtaani au polisi kwa maana nyingine
 
sitakubaliana kwamba kutulia kwa vurugu Mbeya ni kutokana na juhudi za mbunge wa mbeya mjini (CHADEMA) Mr Sugu peke yake ni juhudi za pamoja za viongozi wa mkoa wa mbeya bila kujali vyama wanavyotoka. Sugu au Mr II ni mbunge makini na kwa nafasi yake alikuwa na wajibu wa kibunge kukutana na wananchi haukuwa wajibu wa kichadema.

habari za kuaminika zinaeleza wazi kwamba baada ya Sugu kukutana na uongozi wa mkoa wa mbeya na kukubaliana kwa pamoja kuhusu mambo kadhaa kwa ajili ya utatuzi ikiwemo kuwaacha wafanyabishara hadi suluhu ipatikane ndipo alikwenda kuzungumza na wafanyabiashara ndogo kwa kutumia kauli ya mkoa lakini kila mtu anataka kutuaminisha kwamba zile ni juhudi za chadema na Sugu peke yake.

Tuache kutumia matukio kujijenga kisiasa.
Kwa nini hao viongozi wa mkoa walikuwa kuwepo kwa amani wakati wa kikao chao na Sugu? Mbiona hawakuliona hilo tangu mwanzoni? Wao ndio waliosababisha vurugu hizo, kwa nini walishindwa kuzinyamazisha nmpaka Sugu alipokuja? Ina maana Sugu anabeba akili zao?
 
SUGU ndio Rais wao? waziri mkuu balozi, mambo ya ndani afande sele.

Sasa ndio naamini kuwa Tanzania tumerogwa.

tena mchawi jk na team yake wanaotawala pasipo ridhaa ya watawaliwa! Hebu ona mambo yanavyo mwendea vibaya, arusha, mbeya dsm! Duu! eti zenji nao wameanza kudai uhuru wao mamaweeeee!!! Karume na nyerere kama wangefufuka leo fumbi lingetimka ikulu kama siyo slaa kupewa haki yake.
 
Back
Top Bottom