Chadema wana nguvu sana, wanatisha

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Katika hotuba yake ya mwaka mpya JK alisema chadema watachochea migomu vyuoni. muda haukupita vyuo vyote nchini vikakumbwa na migomo. Je, migomo imechochewa kweli na cdm? Basi chadema inatisha kama inaweza kuwashawishi wasomi wote wagome
 
Chadema inatisha, kwani we hukusikia Waziri Kigwangala akisema CHADEMA OYEEEE alipokuwa MIST, Mbeya ndio wanafunzi wakaanza kumsikiliza.
 
Hilo la CDM kuwa na nguvu halina ubishi na hali itazidi kuwa mbaya kwa ccm pindi miaka inavyoenda mbele.

Ushuhuda wazi!!!
Hivi karibuni nimechukua kadi ya CDM ili kuwa mwanachama rasmi, hiyo ilihusisha uchukuaji wa kadi kwa wasomi wengine kama kumi na ambao wanalipa kodi. Nilipofika nyumbani niliichomoa kadi yangu kumuonyesha mke wangu, mtoto wangu mdogo aliye Class One aliita kwa sauti kubwa CHADEMA huku akiwa kanyosha vidole viwili juu. Nilishangaa na kumuuliza alijulia wapi ya CDM naye akajibu kuwa shuleni kwao wote ni CDM. Hawana kadi ila roho zao zilishafika huko.
Siku nyingine nikiwa safarini kuna mtoto mdogo wa chekechea naye alishangaza watu kwenye gari pale aliposema CDM iko juu.

Ushahidi!!
Mimi sijamwambia mtoto wangu juu ya siasa na wala sitaki kumuingiza katika siasa katika umri alionao, mke wangu hapendi siasa ingawa huwa ananiunga mkono. Kwa hiyo watoto wamekuwa damu ya CDM..
 
Ndio Chadema wana Nguvu ndio maana utaona kila hotuba ya viongozi wa Chama cha mapinduzi lazima wawatupie madongo watu wa chadema.Wanafanya hivyo sio kwa kupenda bali wanaelewa yafuatayo

Wanaelewa kwamba wanaitaji Nguvu zaidi ya kupambana na Chadema hasa baada ya propaganda mbalimbali kukwama.Na mara ya kwamnza walipambana na Chadema chini kwa chini huku wakisema CDM sio lolote,wakajikuta wanawaponza watendaji wao wa ngazi za chini kwani nao walipokea wibo wa mabosi wao kwamba CDM sio lolote,wakajikuta wanapoteza karibu majiji yote tanzania huku asilimia ya ushawishi wa kikwete kwa wananchi ikipunguzwa kwa kiasi kikubwa na Dr Slaa

Pili waziri mkuu anahofia kasi na uelewa wa hali ya juu walionao makamanda wa CDM ambao wameenda bungeni.Ndio maana katika semina ya wabunge wapya iliyofanyika Dar es salaa pinda aliwaambia wabunge wake wasome vitu mbalimbali ili waweze kuwa wajenga hoja wazuri.Je watweza kufikia viwango vya akina mnyika,zitto,mbowe,said arfi,halima mdee,selasini,na makamanda wengine akina sugu,anna kommu na wambunge wengine wa Chadema..Tusubiri tuone.

Tatu..wanajua chachu hii ya kupinga ufisadi ilianzishwa na yule mwanamme aliesimama pale mwembe yanga akasema Jamani watanzania wezi wenu ndio hawa hapa? akawataja mchana kweupe mbele ya kamera kibao za vyombo vya habari! ujasiri ule unawatisha CCM ,unawafanya watapetape.Lakini mimi nasema kutapatapa kwa CCm ni haki yake kwani watafanyaje na chama kinakata roho?

Nne wanajua jinsi walivyokosa ubunifu na kila kitu chenye dira wanakuwa sio wa kwanza kuona na kuishia kutekeleza sera za CDM kama Chuo kikuu dodoma,katiba mpya n.k

kwa haya ni lazoma wakiri CDM ina kasi ya ajabu
 
Hilo la CDM kuwa na nguvu halina ubishi na hali itazidi kuwa mbaya kwa ccm pindi miaka inavyoenda mbele.

Ushuhuda wazi!!!
Hivi karibuni nimechukua kadi ya CDM ili kuwa mwanachama rasmi, hiyo ilihusisha uchukuaji wa kadi kwa wasomi wengine kama kumi na ambao wanalipa kodi. Nilipofika nyumbani niliichomoa kadi yangu kumuonyesha mke wangu, mtoto wangu mdogo aliye Class One aliita kwa sauti kubwa CHADEMA huku akiwa kanyosha vidole viwili juu. Nilishangaa na kumuuliza alijulia wapi ya CDM naye akajibu kuwa shuleni kwao wote ni CDM. Hawana kadi ila roho zao zilishafika huko.
Siku nyingine nikiwa safarini kuna mtoto mdogo wa chekechea naye alishangaza watu kwenye gari pale aliposema CDM iko juu.

Ushahidi!!
Mimi sijamwambia mtoto wangu juu ya siasa na wala sitaki kumuingiza katika siasa katika umri alionao, mke wangu hapendi siasa ingawa huwa ananiunga mkono. Kwa hiyo watoto wamekuwa damu ya CDM..

Mtoto wangu wa miaka mitatu kila akiona kitambaa kinapepea mahali anasema Baba/Mama CHADEMA JUU CCM ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom