Chadema wamvutia pumzi lowasa,wasema hawababaiki,hana jipya

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,930
1,165
MWENYEKITI wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo,
(Chadema), Freeman Mbowe
amesema chama chake
kinamgonja kwa hamu Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward
Lowassa katika kampeni za
uchaguzi mdogo wa jimbo la
Arumeru Mashariki mkoani
Arusha.

Kauli ya Mbowe
inatokana na habari zilizoenea Arumeru ambazo pia
zimethibitishwa na watu
walio karibu na Lowassa,
zikisema Mbunge huyo wa
Monduli (CCM) wakati wowote
atatua Arumeru Mashariki kumpigia kampeni mgombea
wa chama chake, Sioi Sumari. “Mzee (Lowassa) ni kweli
kwamba ana mpango wa kuja
hapa kumpigia kampeni
mgombea wetu wa CCM,
inaweza kuwa ni wiki ijayo au
wiki ile nyingine, nadhani bado anajipanga.

Ila taarifa za
uhakika ni kwamba
atakuja,”alisema mmoja wa
makada wa CCM jana asubuhi.

Chanzo: mwananchi.
 

Attachments

  • lowassa-ngumi.jpg
    lowassa-ngumi.jpg
    11 KB · Views: 62
Lowasa sisi tunamheshimu sana kama anaona kuwa madonda ya uwaziri mkuu yamepona na makovu yamefutika aende Arumeru, Na sisi tutaenda kuwaambia wananchi kuwa kama ana uchungu sana wanameru aliwafanyia nini kipindi akiwa waziri mkuu.
Na ardhi ya wameru ilihodhiwa na walowezi kipindi akiwa waziri wa ardhi, kama hana mshipa wa soni aende tu asije akakimbilia mahakani kama anavyovifanyia vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom