CHADEMA wamruhusu Zitto kufanya apendacho

am really thinking whats going to be the outcome of this meeting, itakuwa mbaya zaidi kama mkutano huo umechukua siku zote hizo then wanatoa pure pumba ! halafu zitto anaview hii page, tuletee basi yaliyojiri !
 
Kutoka Gazeti la Mwananchi.

Chadema chatoa baraka kwa Zitto kuendelea katika kamati ya madini
*Wangwe asema Kamati Kuu ikiamua yeye hana nongwa
* Wafurahia Machunde kujitoa Kamati ya Madini

Na Kizitto Noya

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa baraka zake kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Madini, iliyoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika katika hoteli ya Keys jijini Dar es Salaam, zilisema kuwa Kabwe ataendelea kushiriki katika kamati hiyo, ili kuendelea kutekeleza sera ya chama hicho ya kupitia upya mikataba ya madini.

Hata hivyo, taarifa rasmi ya kikao hicho kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Mzee Said Mzee, inatarajiwa kutolewa leo saa 5:00 asubuhi katika Makao Makuu ya chama hicho.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili mara baada ya kikao hicho, Mbunge wa Tarime ambaye alikuwa mstali wa mbele kumpinga Kabwe, alisema ameridhika na maamuzi ya Kamati Kuu ingawa hakutaka kuingia kwa undani kwa madai kuwa taarifa rasmi ingetolewa leo.

Hata hivyo, Kabwe mwenyewe alipopigiwa simu muda mfupi baadaye, hakutaka kulizungumzia na kudai kuwa kikao kilikuwa bado kinaendelea na kingemalizika leo saa 5.00 asubuhi.

Mapema, chama hicho kilitangaza kuweka kiporo tamko la kamati kuu hadi leo, kutokana na kuchelewa kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwaambia waandishi wa habari katika ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Keys jijini Dar es Salaam kuwa taarifa ya kikao hicho isingepatikana jana kutokana na kikao kuchelewa kuanza kwa kumsubiri mwenyekiti wake Freeman Mbowe.

"Kama tungeanza saa 4:00 tuliyokuwa tumepanga tungetoa taarifa hiyo leo (jana) lakini tumechelewa kuanza kwa kumsubiri mwenyekiti ambaye tulipowasiliana naye hivi karibuni alisema amekwama Nairobi, hivyo taarifa tutaitoa kesho (leo)," alisema Dk Slaa saa 5:45 asubuhi jana.

Hata hivyo, Dk Slaa alisema kuwa kikao hicho chenye agenda moja, kimeitishwa kuchambua Kamati ya Madini na siyo kujadili uteuzi wa Kabwe katika kamati ya madini ya Rais Jakaya Kikwete.

Alisema mjadala wa Kabwe umeibuka kama sehemu ya mbinu za baadhi ya wanasiasa kutaka kuhamisha hoja ya msingi iliyoanzishwa na Chadema kuhusu ufisadi kwa kukitengenezea chama hicho mgogoro.

Kwa mujibu wa Dk Slaa Chadema haina mgogoro unaohusiana na uteuzi wa Zitto bali ina mgogoro wa Kamati yenyewe ambayo baadhi ya wajumbe wake wamebainika kuchangia katika mapungufu yanayolalamikiwa kwenye sekta ya madini.

"Watu wamehamisha mjadala wetu kutoka kwenye ufisadi kwenda kwa Zitto lakini Chadema bado tuko kwenye msimamo wetu kwamba agenda sio Zitto ni Kamati" alisema Dk Slaa.

Alisema hata kama kumekuwa na mawazo tofauti baina ya viongozi wa Chadema kuhusu suala la Zitto na Kamati, tofauti hizo sio mgogoro bali ni kukua kwa demokrasia ndani ya chama na mwisho wa tofauti hizo ni kauli itakayotolewa na Kamati Kuu iliyokutana jana.

Alikitaka kikao hicho kuichambua kwa makini kamati hiyo, hasa historia ya wajumbe wake na kutoa msimamo kuhusu suala hilo kwa lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi.

Alibainisha kuwa msimamo wa awali wa watendaji wakuu wa chama kwamba kamati hiyo inatakiwa kuboreshwa, umeanza kuzaa matunda kwa mmoja wa wajumbe waliokuwa wamelalamikiwa, Peter Machunde, kuamua kujitoa mwenyewe.

Alisema Chadema iliona uwepo wa Machunde, Mary Kejo na Salome Makange kunatia doa katika kamati hiyo kwa kuwa wamekuwa na historia inayowaondolea imani katika kamati hiyo.

Dk Slaa alisema kuwa Aprili 7 mwaka jana Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alimtambulisha Peter Machunde bungeni kuwa ni rafiki yake wa karibu na mfanyakazi wa kampuni yake binafsi ya Vatex Financial Services jambo ambalo linatia shaka kwamba ataweza kupitia mikataba iliyowekwa na rafiki yake Karamagi na kuitoa kasoro.

Aliendelea kuwaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa katika kashfa ya IPTL, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Patrick Rutabanzibwa aliwahi kutoa ushahidi wa kiapo mahakamani kuwa mmoja wa wajumbe alitaka kutoa rushwa ili mkataba huo uendelezwe jambo ambalo pia ni shaka juu ya uwepo wake kwenye kamati.

Alisema mjumbe mwingine amewahi kuwa mshauri wa mikataba ya madini hivyo hawezi kubadilisha ushauri wake katika mikataba hiyo na kupendekeza ushauri mwingine.

Dk Slaa aliwataka wajumbe wawili waliobaki kufuata nyayo za Peter Machunde na kujitoa katika kamati ili kulinda hadhi zao kwani madai yanayotolewa na chama hicho ni ya kweli yanayoweza kutolewa ushahidi popote.

"Ingawa nimeanza kupata taarifa kwamba wengine watajitoa kabla ya kuanza kwa vikao vya kamati hii, ni vyema wakatangaza hivyo sasa kwani sisi (Chadema) tumejitosheleza kiushahidi na nyaraka tunazo," alisema.

Machunde alitangaza kujiuzulu ujumbe wa kamati hiyo juzi kwa kile alichodai kuwa ni ubabaishaji na upotoshaji wa taarifa unaofanywa na Chadema.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa, alielezea matatizo anayokumbana nayo katika kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi, kuwa ni makubwa lakini hayawezi kubadili msimamo wake.

Alisema achilia mbali vitisho alivyopewa na baadhi ya watu aliowatuhumu kwa ufisadi kwamba watamfikisha mahakamani, baadhi ya vigogo wa serikali walimweka kitimoto katika bunge lililomalizika Novemba 16 mwaka huu kumtaka atoe sababu za kusambaza mkataba wa siri wa Buzwagi.

Alisema ingawa viongozi hawa na wale aliowatuhumu kwa ufisadi walimtishia kumshtaki, haamini kwamba anaweza kwenda mahakamani kwa kuwa anachosema ni ukweli na wala si kuwachafulia watu majina.
 
hi Mugo 'the great'

tunashukuru sana kwa taarifa hiyo,

kwa ufupi inaonyesha kuwa CHADEMA na upinzani kwa ujumla wanaendelea kuimarika siku hata siku.
 
Posted Date::11/24/2007
Chadema chatoa baraka kwa Zitto kuendelea katika kamati ya madini
*Wangwe asema Kamati Kuu ikiamua yeye hana nongwa
* Wafurahia Machunde kujitoa Kamati ya Madini

Na Kizitto Noya
Mwananchi

hawa jamaa hawana lolote, and that sh*tty mkutano sijui kamati hata sijui ni ya nini, wanapenda tu misifa na exposure kwenye media!

wee injinia unajificha wapi siku hizi ????????? MCHAMBAWIMA au ??

Kada, matusi ya nini bro?
Huwezi kujadili hoja bila jazbana matusi?
Kila mtu ana haki ya kuwa na exposure, kutoa maoni, nk kwa hiyo kama jamaa wanaipata exposure mie binafsi sioni kosa lao.
Hoja kwa hoja, sio hoja kwa tusi.
Nadhani nimeeleweka.
 
- Dk Slaa alisema kuwa kikao hicho chenye agenda moja, kimeitishwa kuchambua Kamati ya Madini na siyo kujadili uteuzi wa Kabwe katika kamati ya madini ya Rais Jakaya Kikwete.
Alisema mjadala wa Kabwe umeibuka kama sehemu ya mbinu za baadhi ya wanasiasa kutaka kuhamisha hoja ya msingi iliyoanzishwa na Chadema kuhusu ufisadi kwa kukitengenezea chama hicho mgogoro.

Haya ndio maneno niliyoyafahamu mimi,hizi habari za wana CCM kuvumisha utengano ndani ya Chadema ni uhuni mwingine ambao hauna maana kabisa. Kuamini kuwa Zitto anapata Upinzani ndani ni mbinu chafu kwani hata ukisikia maelezo ya Zitto mwenyewe anawazungumzia na kuwanyooshea kidole CCM wanaopinga zaidi kuwepo kwake ktk kamati hiyo. Wameshindwa kwenda through President sasa wamechukua mkondo mwingine wa kuwaburuza Chadema kimawazo.
Chadema kama chama chochote kile ni lazima kuwepo na mgongano wa mawazo hasa ktk teuzi kama hizi na kitu cha kushangaza ni kwamba hata ndani ya CCM kwenyewe kumekuwepo na maoni tofauti kuhusu kuchaguliwa kwa Zitto na baadhi ya wajumbe kutokana na imani ya kila mtu.
Haya ya CCM hayazungumzwi kabisa kwa sababu Zitto kesha wafunika wote na yaonyesha wazi Chadema wanazidi kujipatia points... maanake hata huko vijijini nasikia mazungumzo ni Zitto kuchaguliwa kamati ya madini utafikiri yeye ndiye mwenyekiti na hii kamati ni tume maalum yenye mamlaka ya kutoa maamuzi ya mwisho.

Ama kweli kazi ipo!
 
Kitila mbona watutia kiholo? tayali nini?.... fafanua bro.

Soma ile thread ingine; ni jinsi CHADEMA walivyo-handle hii issue kama wanaforum wengi walivyotaka-another demonstration of political competence, maturity and civilisation on the part of CHADEMA.
 
hawa jamaa hawana lolote, and that sh*tty mkutano sijui kamati hata sijui ni ya nini, wanapenda tu misifa na exposure kwenye media!

wee injinia unajificha wapi siku hizi ????????? MCHAMBAWIMA au ??

mmh.. walio na hoja hawatoi wasio na hoja wanaishia kupuuza!
 
CHADEMA wanataka Zitto akatekeleze sera za CHADEMA kwenye Kamati iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Hili linawezekana vipi? Kwani kamati haina hadidu za rejea? Na je hadidu hizo zipo kwa mujibu wa sera ya CHADEMA? Mbona wanashindwa kupima uwezo wa mtu mmoja kwenye kamati ya watu kadhaa wanaopaswa kutoa msimamo na mapendekezo ya kamati na si mapendekezo ya mtu mmoja? Sasa Zitto atafanya kazi ya nani kwenye Kamati hiyo, ya aliyemteua (Rais, ambayo ina hadidu za rejea) au ya chama chake (kwa mujibu wa kikao chao)? Mimi naona wanamchanganya Zitto, wanamtaka atumikie mabwana wawili, sijui atawezaje. Ushauri wangu kwa Zitto maana nafahamu ni memba hapa ni huu: "Chagua yule utakayemtumikia...". Zitto utamtumikia nani?
 
Najua watu wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu. Kwa kifupi ni kuwa Kamati Kuu ya Chadema watakutana na waandishi wa habari kesho (jumapili) saa tano asubuhi ambapo watatoa tamko rasmi la chama na uamuzi uliofikiwa. Maamuzi yaliyofikiwa na mjadala ulivyokwenda umeonesha ukomavu mkubwa kwa Chadema.

Habari za kuwa Mbowe alizuiwa kuendesha kikao si za kweli hata kidogo kwani alichelewa kufika jiji Dar kutoka Uingereza. Hata hivyo, baada ya majadiliano na wakati wa kufikia maamuzi Mbowe alisimamia kikao hicho. Mkutano ulikuwa wa kiungwana licha mjadala mkubwa na hatimaye ulimalizika kwa kufikia maafikiano ya kichama na maamuzi thabiti.

M. M.
 
Kithuku,
Babu naona unataka kutupotosha hapa. haya maswala ya kutumikia mabwana wawili yametoka wapi haswa kwani swala la msingi hapa ni Uvujaji wa pakacha letu la madini. madini sio mali ya JK ama CCM ni mali ya taifa hivyo inamhusu kila Mtanzania bila kujali rangi yake.
Ebu tazama ile kamati iliyoundwa na Bush kuhusu 9/11,mbona hao demokratic hawakusema wanatumikia mabwana wawili?... hivi JK ni rais wa CCM na sio rais wa Tanzania ikiwemo Chadema yaani JK hana uwezo wa kuchagua ama kuingilia uchaguzi wa Chadema katika swala linalohusu maslahi ya taifa zima. Ama ulitaka Chadema wapewe nafasi ya kuchagua watu wanaowataka wao kujiunga na hii kamati.
Kifupi sielewi tunakwenda wapi kumshauri Zitto kutojiunga na kamati hii hali ni sisi wenyewe tunaopiga kelele kila siku kuhusu swala la Madini. Je, kifanyike kitu gani ikiwa Bunge lenyewe halifai.
Wapo waliopendekeza swala hili litazamwe Bungeni, jamani sio sisi tuliokosa matumaini na Bunge hilohilo?..wajumbe wengi Bungeni wamejaa CCM tena wengi wao wananuka rushwa na homa ya Kutawala, leo mnawataka wao tena walishughulikie swala hili wakati ni hao hao tu majuzi wamemtenga Zitto bungeni bila hata sheria. Chama Chadema kimeshindwa kuchukua hatua zozote kwani hawana sheria ktk nchi ya kutawaliwa..
Nani kati yenu kasimama kupinga uamuzi wa Bunge hilo kwa vitendo kuhakikisha Zitto anarudi Bungeni... hakuna na watu tunaanza kusahau kuwa Zitto sii mbunge tena ila ni mkereketwa nje ya Bunge kisha mnataka swala hili lirudishwe bungeni ambako huyo Zitto sii mjumbe.
Yawezekana kuna utata fulani ktk Uchaguzi huu lakini kwanza tufikirie vizuri zaidi tunachokitaka sisi ni kitu gani na isiwe Zitto. Tutaweza vipi kujadili swala la madini bila Upinzani kuwakilishwa?... then nani anayefaa kuwepo ikiwa sio Zitto maanake kama ni kamba za JK then kamba hii itakuwepo achaguliwe Zitto ama Dr.Slaa maanake kila mmoja wao ni mpinzani.
Ebu, tazameni kipande hiki nimekinukuu toka ktk ile kamati ya Bush kuhusu 9/11 iliyokuwaikiongozwa na Henry Kissinger..na lawama zimemrudia nani BUSH! hatusikii hata mtu akimtaja Kissinger ama kamati ile.

THREATS AND RESPONSES: THE INVESTIGATION; PRESIDENT NAMES KISSINGER TO LEAD 9/11 COMMISSION

By RICHARD W. STEVENSON
Published: November 28, 2002
President Bush today named Henry A. Kissinger, a Republican who has been one of the most respected but polarizing figures in foreign policy and Washington for more than three decades, to lead an independent investigation into the Sept. 11 terrorist attacks.
In choosing Mr. Kissinger, 79, the president selected a person whose reputation as a towering intellect in foreign policy is matched by the passions he has aroused among critics of his role in the Vietnam War, relations with the Soviet Union and the exercise of American power in Latin America. Mr. Bush made the appointment as he signed legislation creating the commission, a step he came to support after opposing the bill for much of the year partly on the ground that it could divert attention from the war on terrorism.
Democratic leaders in Congress, who will appoint half of the 10 members of the commission, immediately named George J. Mitchell, the former Senate majority leader and peace envoy to Northern Ireland and the Middle East, as vice chairman.
The commission's mandate is to conduct a wide-ranging inquiry into the causes of the attacks, whether they could have been averted and what changes are needed to prevent a similar occurrence.
The commission is required to complete its work within 18 months -- a timetable that would have it issue its final report in the middle of a presidential election year -- though Mr. Bush said he hoped it would finish sooner. The leaders of the two parties in Congress must appoint the rest of the members by Dec. 15.
The commission will have the power to issue subpoenas by majority vote, and lawmakers have urged that it cast its net widely and interview current and former government officials, including Mr. Bush and his predecessor, Bill Clinton.

Source:- http://query.nytimes.com/gst/fullpage.html?res=9F07E5D71538F93BA15752C1A9649C8B63
 
Nd. Mkandara... Bush alipelekewa muswada wa kuundwa kamati ya kuchunguza 9/11 (kama unavyoona hapo kwenye bolded statement)... hakujiamulia tu kinyemela.. muswada huo ulitaka kwamba kamati iwe bipartisan..nusu-democrats na nusu- republicans!
Sasa sijui hii kamati ya kwetu imeundwa kwa misingi gani.. na matokeo ya uchunguzi wake yatakuwa na nguvu kiasi gani?
Unafikiri hii kamati itakuja na kitu kipya kitakachofamnya HE. J. K. Kikwete amtose Sinclair??
 
Bravo Dr. Slaa

"Ingawa nimeanza kupata taarifa kwamba wengine watajitoa kabla ya kuanza kwa vikao vya kamati hii, ni vyema wakatangaza hivyo sasa kwani sisi (Chadema) tumejitosheleza kiushahidi na nyaraka tunazo," alisema.
 
Hii mada nimeipenda sana kwa kuwa ni mara ya Kwanza Mzee Mwanakijiji kuonekana wazi kabisa kwamba ni MwanaCHADEMA, siku zote alikuwa akificha identity yake kwa kivuli cha "Ni vita ya kubadili fikra"

Sasa Mwanakijiji na KadaMpinzani kwenye mambo ya vyama ni wa moja,,, wanatofautiana tu namna ya kupresent message zao!!!

KadaMpinzani anaweka hisia zake wazi, Mwanakijiji anazifunika funika kidogo,,,well rika nalo linamsaidia but at the end of the day,,, hawa wawili ni watu wenye hisia za vyamba vya CCM na CHADEMA kwa undani sana.
 
Acha ushakunangu!

Mwanakijiji anachotetea ni fikra za kweli, kama fikra hizo zinatoka CHADEMA basi poa na hata kama zimetoka CCM amekuwa akizitetea humu. Maneno yake yanawachoma nini ndio maana mnalialia?

Mnataka atetee uzushi wa CCM ili tu asionekane CHADEMA?

Mwanakijiji songa mbele mpenzi, achana nao mahasidi wenye wivu

Asha
 
Ama kweli nyani huwa haoni kundule!
Yaani Kilitime umekuwa mtu wa kuwasema watu wengine hali mfano wako ungependeza zaidi kama ungejiweka wewe mwenyewe!..
 
Katika mapambano haya ya kifikra tunayoyahamasisha, fikra zenye nguvu lazima zishinde na fikra dhaifu lazima zioneshwe kuwa ni dhaifu. Hatutaficha fikra zetu kwa vile zinashabihiana na zile za wapinzani au zinakubaliana na zile za CCM... ndio maana nilikataa dhana nzima ya kuwa na "wasomi wa Chadema" na "wasomi wa CCM". Ujumbe wangu nilioutuma kwenye kongamano lile uliwahusu wanafunzi wote...
 
Mkandara,
Heshima kwako mkuu wangu maana hekima zako ziko juu sana na naziheshimu sana lakini niweke wazi kwamba hoja yoyote inayohusu vyama au chama fulani alafu ati Mnyika au kadaMpinzani ndiye anatoa nathimini binafsi huwa nazitilia mashaka maana ndiyo hivyo tena hivi Kitila anaweza kusemea mbofu mbofu hadharani . CHADEMA?
 
Hii mada nimeipenda sana kwa kuwa ni mara ya Kwanza Mzee Mwanakijiji kuonekana wazi kabisa kwamba ni MwanaCHADEMA, siku zote alikuwa akificha identity yake kwa kivuli cha "Ni vita ya kubadili fikra"

Sasa Mwanakijiji na KadaMpinzani kwenye mambo ya vyama ni wa moja,,, wanatofautiana tu namna ya kupresent message zao!!!

KadaMpinzani anaweka hisia zake wazi, Mwanakijiji anazifunika funika kidogo,,,well rika nalo linamsaidia but at the end of the day,,, hawa wawili ni watu wenye hisia za vyamba vya CCM na CHADEMA kwa undani sana.

kuna wakati huwa naamini kilitime unanielewa; ila nyakati nyingine (kama hizi) huwa unanishangaza kwa sababu it seems you have no idea what I stand for, na maslahi yangu ni nini. Ila kama na wewe umeamua kujiunga kwa watu wanaonipa uanachama wa Chadema, yote maazuri. Ungejua ni mara ngapi nazungumza na watu wa CCM na kutoa mawazo yangu ungebakia mdomo wazi, but well utasema najitamba...
 
Acha ushakunangu!

Mwanakijiji anachotetea ni fikra za kweli, kama fikra hizo zinatoka CHADEMA basi poa na hata kama zimetoka CCM amekuwa akizitetea humu. Maneno yake yanawachoma nini ndio maana mnalialia?

Mnataka atetee uzushi wa CCM ili tu asionekane CHADEMA?

Mwanakijiji songa mbele mpenzi, achana nao mahasidi wenye wivu
Du nadhani siwezi mipasho

kila la kheri! mimi huko zero.
 
Back
Top Bottom