CHADEMA wamlipua Kikwete Bungeni

Technician

JF-Expert Member
Mar 30, 2010
841
222
na Martin Malera, Dodoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimelipua Rais Jakaya Kikwete kwa kusaini na kuidhinisha Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano kabla ya kupitishwa na Bunge.

Hoja hiyo iliibuliwa jana na Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Mchungaji Israel Natse wakati akitoa maoni ya kambi hiyo.

"…Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63 (3) (c) inasema kuwa majukumu ya Bunge ni "kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo."

Wakati ibara ya Katiba ikitamka hivyo, mpango huu tayari ulishasainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania tangu Juni 7, 2011 na kuwasilishwa bungeni siku inayofuata kama hati ya kuwasilisha mezani, bila kuelezwa ndani ya mpango wenyewe kama kilichowasilishwa ni rasimu.

Aidha alisema kwa mujibu wa mpango wenyewe, Rais ameshashukuru wadau kwa maoni yao yaliyowezesha kukamilisha mpango na ameshalishukuru Bunge kwa mchango katika kukamilisha mpango husika.

"Mheshimiwa Spika, wakati Rais akisema hivyo, kambi ya upinzani haijawahi kushirikishwa wala kushiriki kikao chochote cha Bunge kilichojadili na kupitisha mpango huu. Kwa hiyo, kambi ya upinzani inamtaka waziri aeleze ni kikao kipi cha Bunge na ni mkutano wa ngapi wa Bunge hili, uliowahi kujadili na kupitisha mpango huu wa maendeleo hata kumpelekea Rais kulishukuru Bunge kupitia dibaji yake iliyochapwa kwenye kitabu cha mpango huu?" alisema.

Natse ambaye ni Mbunge wa Karatu, alisema kambi ya upinzani inalitaka Bunge lifanye kazi zake kikamilifu na serikali iwe na utamaduni wa kuheshimu hilo.

"Tunaitaka serikali isiwe na utamaduni wa kuamini kuwa kila jambo litakalowasilishwa hapa bungeni basi Bunge litalipitisha tu. Tunaitaka serikali kuhakikisha kuwa maoni ya wabunge yanazingatiwa na kuingizwa kwenye mpango huu kikamilifu," alisema.

Mbunge huyo pia alihoji lugha ya Kiingereza iliyotumika kuandaa mpango huu. Alisema mpango haulengi kufikishwa kwa Watanzania ambao wanapaswa kuutekeleza kwani lugha iliyotumika haifahamiki kwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wote.

"Tunapenda kuikumbusha serikali kuwa hakuna taifa lolote lililowahi kuendelea kwa kutumia lugha ya kukopa hapa ulimwenguni. Baada ya mpango huo kupitishwa, tunaitaka serikali kuuandaa kwa lugha ya Kiswahili," alisema.

Alisema mpango huu wa maendeleo hauna shabaha za ujumla za kuwezesha kujipima kama taifa kuhusu mafanikio yanayotarajiwa.

Alipendekeza baadhi ya shabaha kuu za mpango huo kuwa ziwe kupunguza umaskini vijijini kutoka asilimia 37 ya sasa hadi asilimia 20. Nyingine ni za kumaliza tatizo la umeme kabisa na kuzalisha umeme wa ziada kwa asilimia 20.

"Tuwe taifa linalozalisha gesi kwa wingi barani Afrika, kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanapata maji safi na salama na kuhakikisha kuwa barabara za vijijini zinapitika kwa wakati wote wa mwaka na mwisho kupunguza vifo vya akina mama na watoto," alipendekeza msemaji huyo.

Kuhusu dhana ya utawala bora na na uwajibikaji, Mbunge huyo alisema Kambi ya Upinzani, imebaini kuwepo kwa mapungufu mengi na dosari kadhaa nzito zinazoweza kuathiri utekelezaji wake au kukwama kabisa.

"Mipango ya aina hii si mipya katika nchi yetu. Tumeshakuwa na mipango ya maendeleo ya miaka mitano-mitano tangu mwanzoni mwa miaka ya 60, lakini hatimaye mingi ilisuasua au kukwama kabisa, kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni kutokuwepo kwa uwajibikaji wa kutosha ndani na baina ya taasisi za serikali," alisema.

Aliendelea kuuchambua mpango huo kwa kusema kuwa miongoni mwa mahitaji muhimu ya taifa letu ni Katiba mpya ambayo haimo kwenye mpango huo.

"Kambi ya Upinzani, imeshangazwa na mpango huu wa maendeleo wa miaka mitano (2011/2012 - 2015/2016) kutolipa kipaumbele hata kidogo hitaji la katiba mpya wala kutenga fedha maalum kwa ajili ya mchakato huo nyeti, katika kuamua hatma mpya ya mwelekeo wa taifa letu," alisema.

Alisema hata kama serikali itasema kuna fedha zimetengwa kwa ajili ya tume ya kurekebisha sheria kiasi cha sh milioni 945, bado kambi ya upinzani inataka kuona fedha za kugharimia mchakato wa katiba mpya zikitengwa na kuonyeshwa waziwazi.

Kuhusu ukadiriaji wa gharama Kambi ya Upinzani imebaini kuwapo dosari kadhaa kuhusiana na gharama zilizokadiriwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huu wa miaka mitano.

Ilitaja moja ya dosari hizo kuwa ni gharama za jumla za kutekeleza mpango huu ambazo ni sh trilioni 42.98 kutowiana na uwezo halisi wa serikali kujipatia mapato yake.

"Ili mpango huu utekelezeke serikali itapaswa kuwa na bajeti ya maendeleo inayozidi au isiyopungua sh trilioni 8.6 kila mwaka ndani ya kipindi chote cha miaka mitano cha utekelezaji wa mpango huu," alisema Natse.

Alisema wakati serikali ikipaswa kuwa na sh trilioni 8.6 za maendeleo kila mwaka ili kutekeleza mpango huu, uzoefu unaonyesha kuwa ni vigumu kwa serikali kukusanya fedha za kutosha ili bajeti ya maendeleo iwe kubwa.
 
Hakuna maendelea hapo ni bla bla tu... watu wanafikiria matumbo yao tu na si mtanzania maskini anayejifungulia njiani kwenye toroli la kubebea mchanga akiwa njiani kwenda kwenye zahanati isiyokuwa na dawa wala wauguzi - hii ni baada ya miaka 50 ya uhuru wetu. shame!!

tumeshasikia mipango mingi sana, hebu mtu alete hata mmoja tu ambao ulifanikiwa. .
 
Mlitaka alete bungeni bila kusaini hoja yake? Mnanshangaza!

Hawa watu Nape anawatoa wapi ?? milembe au??

Yaaan watu hajui hata taratibu za kutunga sheria! hata elimu ya urai ya dalasa la tano hawajapata?

Ulishaona wapi mada ikapelekwa bungeni kujadiliwa imsha sihinwa na Rais, hiyo inakuwa sio mada/rasimu tena inakuwa ni sheria.

Kiutaratibu inatakiwa ijadiriwe bungeni, ikishapitishwa na bunge ndio inahisiniwa na rais kuwa sheria/kanuni.

Lkn...Rais na wasaidiz wake ...mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh!

Tutafika kweli..? kwa mwendo huu wa kuvunja vunja kanuni na taratibu??
 
Hawa watu Nape anawatoa wapi ?? milembe au??

Yaaan watu hajui hata taratibu za kutunga sheria! hata elimu ya urai ya dalasa la tano hawajapata?

Ulishaona wapi mada ikapelekwa bungeni kujadiliwa imsha sihinwa na Rais, hiyo inakuwa sio mada/rasimu tena inakuwa ni sheria.

Kiutaratibu inatakiwa ijadiriwe bungeni, ikishapitishwa na bunge ndio inahisiniwa na rais kuwa sheria/kanuni.

Lkn...Rais na wasaidiz wake ...mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh!

Tutafika kweli..? kwa mwendo huu wa kuvunja vunja kanuni na taratibu??

They are paid according to the number of posts they post.
 
Mlitaka alete bungeni bila kusaini hoja yake? Mnanshangaza!

islam12.jpg
 
Mlitaka alete bungeni bila kusaini hoja yake? Mnanshangaza!

Welevu si kusikika au kuonekana unafanya juhudi bali ni kufanikisha na kuepuka kufanya mambo ambayo mchango wako unakutenga na uelevu. Mpango huu bungeni umewasilishwa ili ukafanyiwe nini?

Tunajua anayewasilisha ni serikali ambaye mkuu wake ni Rais. Lakini inapotokea ameshukuru wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bunge kwa mchango wake nini kusudio lake? Kuwaziba midomo ili wapitishe bila kujadili, na kama anawashukuru kwa mchango wao anawapelekea wakafanye kitu gani. Na ikitokea wakarudisha serikalini kwa marekebisho. Mapenzi ya kisiasa yanakuziba jicho moja na uelevu.

Tunakupenda na tunapenda kuendelea kuwa na wewe jamii forums lakini tunakuomba uitendee haki jamii forum.
 
Back
Top Bottom