CHADEMA wamlima Rais Kikwete Barua juu ya mauwaji katika mikutano yao

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamemwandikia barua rasmi rais Jakaya Kikwete juu ya mwenendo wake wa kukaa kimya na kutochukua hatua yoyote kwa baadhi ya matukio yanayoonuesha kupangwa na wahusika kutowajibika hivyo wanamtaka rais awawajibishe.

Baadhi ya hao wanaotakiwa kuwajibishwa ni kamanda wa polisi wa Iringa, Morogoro, Arusha, Tabora na waziri wa mambo ya Ndani bwana Nchimbi
 
Changa la macho hilo ili kujikosha na kashfa ya kutoa kafara watoto wa watu. Kuna ulazima gani wa rais kutoa kauli wakati ambapo hatua zimeshachukuliwa? Mbayuwayu in action.
 
Ni hatua sahihi na yenye mantiki kwa hatua nyinginezo baada ya hapo endapo mawasiliano hayo yataonekana kupuuzwa kwa namna yoyote ile.
 
Inaeleweka wazi, watendaji wake wanapokea maagizo toka kwake ili kuhakikisha CDM inachafuka mbele ya umma. Wauaji wote wanajulikana, lakini wapumbavu wanasema cdm ndiyo inahamasisha mauaji. Shame on ccm and his Government.
 
Sheria ni msumeno, Ningekuwa Rais ningeanza na kuchukua hatua dhidi ya CHADEMA kwa sababu, chanzo cha vifo vya watanzania wasiyo na hatia ni maandamano na mikutano yao isiyo rasmi.
 
Hawa CHADEMA naona wanataka adhabu kutoka kwa Rais, vifo wasababishe wao halafu wanaomba hatua zichukuliwe? kaz kweli kweli.

Nadhania Rais akiamua na sheria zikapitiwa vizuri, ni wazi CDM wataingia matatani, ngoja tusubiri reaction ya Rais.
 
Mbona asubuhi sana matusi ya nini? hujifunzi tu kuwa mstaarabu humu JF?, mwanzoni tulifikiri ni ugeni kumbe ndivyo ulivyolelewa.

Hata wauaji wakifahamika, lakini ukumbuke kuna kuua bila kukusudia, lakini kitu kibaya ni chanzo cha mauaji, na kwa hili CDM watajiwekaje pembeni?
 
Hujui unachoandika, hebu nikumbushe sheria itayowatia hatiani Chadema kwa kosa la mauaji.Ushabiki usio ma mantiki acha.
 
Wamuandikia na barua nyingine kuwa akishindwa kuwawajibisha basi atakuwa amejiondoa madarakani na tutaitisha uchagyzu mpya Lema akiwa ndie mgombea uraisi
 
Kwa jinsi ambavyo ccm sasa hv walivyowekwa kati, JK hawezichukua hatua yoyote kwa cdm. Washauri wake wamefika mwisho wa mbinu.
 
teh teh teh, kweli hii nchi sasa itakuja kuongozwa na ma-teja, kama wamiliki wa madanguro wamejaribu, Wazinzi wamethubutu kugombea japo walikosa, na sasa tunawasema majambazi, hakika si teja tu watakaojitokeza kugombea bali hata mashoga manake naona hawa nao wanakuja kwa kasi kweli.
 
Hata kama ni ushabiki wa chama, huu wa kwako umezidi. Hutaki kuitumia akiri yako na kujua aliyekufa kule Bububu naye pia alikuwa kwenye maandamano au mkutano wa CDM?
 
Chanzo sio maandamano na mikutano ya chadema. Kama chadema wanakosea au kuvunja sheria yoyote polisi hawatakiwi kuua watu ila wawachukulie hatua za kisheria. Polisi kuua wananchi ni kosa la jinai ambalo wanatakiwa washtakiwe. Polisi haruhusiwi hata kumpiga mtuhumiwa. Haki ya kutoa uhai wa mtu polisi wanaitoa wapi??? Kuishi ni haki ya mtu. Hakuna mtu nwenye haki ya kutoa uhai wa mtu. Nawashangaa mnashabikia polisi wakati wanaua ndugu yako. Sisi watanzania ni ndugu moja na tunatakiwa tuteteane. Vyama vya siasa visitufanye tushindwe kuona kweli. Kama kuna chama kinakosea sheria zipo kishtakiwe sio kuua watu!!!
Sheria ni msumeno, Ningekuwa Rais ningeanza na kuchukua hatua dhidi ya CHADEMA kwa sababu, chanzo cha vifo vya watanzania wasiyo na hatia ni maandamano na mikutano yao isiyo rasmi.
 
Nimefarijika na hatua waliyoachukua CHADEMA,na ndivyo chama makini kinavyotakiwa kuwa,maana inaonekana wazi serikali ilitaka kufunika issue hii.
Mungu azidi kuwahekimisha viongozi wa CHADEMA.
 
Kwa jinsi ambavyo ccm sasa hv walivyowekwa kati, JK hawezichukua hatua yoyote kwa cdm. Washauri wake wamefika mwisho wa mbinu.

Rais yeyote aliyepewa ridhaa kupitia chama chake, lazima afanye maamuzi kwa kufuata ushauri wa mlezi wake ambaye ni chama chake na siyo wanasiasa, itachekesha sana eti rais anawawajibisha watendaji wake kwa shinikizo la wanasiasa, ni kitu ambacho hakiwezekani. Haiwezekani watu kwa chuki zao binafsi na watendaji wa Serikali wamshinikize Mkuu wa nchi kuwachukulia hatua. Wapi watanzania mlishasikia chama kimoja cha siasa kinashinikiza Kiongozi mkuu wa nchi kufanya hivyo, nchi zingekuwa zinatawalika kweli? CDM pitieni sheria zinazoongoza nchi mjiridhishe kama mmeiva
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamemwandikia barua rasmi rais Jakaya Kikwete juu ya mwenendo wake wa kukaa kimya na kutochukua hatua yoyote kwa baadhi ya matukio yanayoonuesha kupangwa na wahusika kutowajibika hivyo wanamtaka rais awawajibishe.

Baadhi ya hao wanaotakiwa kuwajibishwa ni kamanda wa polisi wa Iringa, Morogoro, Arusha, Tabora na waziri wa mambo ya Ndani bwana Nchimbi

Kujipendekeza na kujikombakomba kwa mkuu wa kaya tu hawana lolote wachumia tumbo tu hao.

Huwezi kabisa katika mazingira ya kawaida kumpelekea barua mtu ambae hutambui nafasi yake katika nchi. Tena viongozi wa chama kwa kauli zao wao wenyewe walilisema hili.

Katika watu ambao wamekuwa wakiaminiwa kuwa na msimamo na wanayoamini ni huyu babu wa chadema.

Kwa hili la kujikomba kwa mheshiwa rais ni kujivunjia heshima yake binafsi kwa kuonekana kuwa kigeugeu, kujivunjia heshima kwa wanachama walioiusudu ile kauli yake ya kutomtambua rais na wao kujiona kama mayatima maana kiongozi wao kasaliti kauli yake na mwisho kuvunja heshima ya chama chake.
 
cdm kweli hawana akili nyie ndio mnaochochea vijana wafanye vurugu ili nchi isitawalike nyie hao hao mnamtaka rais achukue hatua? mantiki ipo wapi hapo?
 
Hata waandike utenzi haitowasaidia ikiwa wenyewe ndio chanzo cha migogoro.
 
Back
Top Bottom