CHADEMA wamfungulia kesi Nape

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
Kutokana na vyanzo vyangu vilivyopo Mahakama kuu ya Tanzania Leo Nape amefunguliwa kesi ya madai na imepewa namba 186 ya mwaka 2012.

Kesi hii ni kuhusiana na madai ya nnape kuwa CDM wana pokea pesa kutoka nje ya nchi.

Tuendelee kufuatilia


Updates.

Inaitwa civil case no.186 of 2012 ,board of registered trustees of chadema ... Plaintiff versus nnape nnauye defendant .

nape..%281%29.jpg

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemfungulia kesi Mahakama Kuu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, kutokaa na madai yake kwamba Chadema wanapewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willibroad Slaa, alisema hayo jana wakati wa semina ya viongozi wa chama hicho pamoja na wanachama wa Chama cha Christian Demokratic Union (CDU) cha Ujerumani.

Semina hiyo kuhusu Uhuru, Demokrasia na Mshikamano inawashirikisha baadhi ya wabunge na viongozi wa Kamati Kuu ya Chadema ambapo wanajadili masuala ya kukuza uchumi wa soko unaoshirikisha watu wenye kipato cha chini na juu ambao unaleta dhana ya uwajibikaji kwa taifa na serikali.

Dk. Slaa alisema Chadema kimemfungulia kesi namba 186 /2012 Nape ili aweze kuthibitisha madai yake kwamba chama hicho kinapata mabilioni ya fedha toka kwa mataifa tajiri.

Alisema uamuzi huo umechukuliwa kufuatia propaganda ambazo zimekuwa zikielezwa na baadhi ya watu kuwa Chadema wanapata mabilioni ya fedha kutoka nje wakati hakuna ukweli wa suala hilo.

"Ipo propaganda kuwa chadema inapata mabilioni ya fedha toka nje, kimsingi, marafiki zetu kama Konrad Adenauer Stiftung wanatusaidia kwa ajili fedha za kujengea uwezo, lakini siyo kwa ajili ya kuendesha kampeni au shughuli za kiasiasa," alisema Dk. Slaa.

Chadema hivi karibuni walimtaka Nape kukiomba radhi chama hicho pamoja na kutoa Sh. bilioni tatu, baada ya kudai kuwa Chadema kinapata mabilioni ya fedha toka mataifa ya nje ambapo alikataa kuomba radhi kwa kueleza tuhuma alizitoa dhidi ya chama hicho ni za kweli.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema mifumo ya uchumi katika nchi yeyote inategemea itikadi na sera ya nchi. lakini serikali ya CCM inaegemea ujamaa na kujitegemea ilhali sekta za uchumi zipo chini ya soko huria.

Alisema kwa Chadema inafuata mlengo wa katikati ambapo imechukua yale mazuri ya mfumo wa ujamaa na kujitegemea na kuchanganya na sera ambazo zinalenga kumwinua mwananchi kiuchumi.



CHANZO: NIPASHE


 
Aisee hapa ndipo mahala sahihi wa yeye kuwaeleza waTZ ukweli kama alivyosema. Nape uwanja ni wako thibitisha tunakusubiri!!!
 
Tundu A. Lissu, Prof. Safari, Mabere Nyaucho Marandu etc. Je CCM watamlipia hizo Billion 3?
 
Mahakama ni yao, na hivi tena majaji wapya walioteuliwa na mwenyekiti wa ccm taifa na alishawapa maelekezo mpya ya maslahi ya ccm mbele! Uh!
 
Nape imefka wakat muafaka udhbitshe ukwel kama kesi imeshafunguliwa! Ukishndwa ujue wewe n full vuvuzela la nyinyiem
 
Hii kesi inaweza kuwa ngumu sana kwa upande wa Nape kwa sababu kwenye madai yake (yeye Nape) ni kwamba kuna nchi za nje zinazotoa fedha kwa CHADEMA kwa makubaliano ya kuuziwa/kupewa rasilimali za Tanzania. Hapa issue sio kupekea pesa, ila atatakiwa athibitishe beyond reasonable doubt kuwa kuna nchi zimetoa fedha kwa masharti wa kupewa rasilimali za Tanzania. Sasa itakuwaje kama hizo nchi zitakataa?
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom