Chadema wamepata wapi haki ya kutengeneza CD mauaji ya Mwangosi (R.I.P) na kuiuza

Asante kwa taarifa mkuu Tumaini Makene,hii issue imeshatolewa ufafanuzi na kamanda JJ Mnyika mkururgenzi wa habari na uenezi Taifa,kama unaendelea kuwa king'ang'anizi bwana Ritz una lako jambo....full stop.

I would have said FOOL'S TOP
 
Mkuu Ritz
Kumbe tupo na madalali ndio sababu wamekuwa wakali hata ubinadamu wamesahau

Chama
Gongo la mboto DSM

mnapenda sana kuimba taarabu nyie na hicho kitu kitawacost
 
Mkuu Uwezo Tunao,
Sijui kama una ufahamu wowote wa neno hati miliki...ukinunua DVD yeyote lazima utaona maneno hairuhusiwi kunakili haki zote zimeifadhiwa...DVD za Marekani kuna onyo kabisa kutoka FBI.

Naomba unipe jibu sahihi mauzo ya hizo CD pesa zake ni mali ya nani?

Mimi nilikuwepo daraja mbili jibu haziuzwi ila unakubaliwa changia hata shs 100.
 
kama hili nin la kweli basi haya ndo matunda ya ninyi Magamba kuzuia watu kufanya mikutano,sasa kila tunakichokifanya nyie mnaoana tunawagusa pasipopaswa kushikwa, na bado mtatukoma!
 
Cd hiyo haisambazwi kwa lengo la kuongeza pato la cdm, au kusaidia familia ya marehemu Mwangosi, lengo kuu la usambazaji wa hizo cd ni kueneza/kupandikiza chuki miongoni mwa watanzania.
Serikali ambayo mimi naiona dhaifu kwa kushindwa kuwachukulia hatua kali watu wanaohatarisha kupotea kwa amani ya nchi yetu, itakaa kimya kama kawaida yake.
Mungu tunusuru na majanga ya serikali dhaifu. Amen.
 
Mkuu Uwezo Tunao,
Sijui kama una ufahamu wowote wa neno hati miliki...ukinunua DVD yeyote lazima utaona maneno hairuhusiwi kunakili haki zote zimeifadhiwa...DVD za Marekani kuna onyo kabisa kutoka FBI.

Naomba unipe jibu sahihi mauzo ya hizo CD pesa zake ni mali ya nani?

Ni mali ya mtengenezaji.Je, nawe unataka mgao maana baba kakugawia hadi haki za wazee na yatima na albino. Zoote umechukua.
 
Hakuna sehemu niliotetea Jeshi la Polisi kwa unyama waliofanya, mie naulizia mapato ya CD ya mauji ya Mwangosi mjane anapata kiasi gani?

Ritz umeshahongwa kiasi gani na magamba?.Hakika wewe ni gamba jingine,CD imetengenezwa ikulu na imefadhiliwa na taasisi hiyo.Thus familia ya mwangosi iende huko ikapate haki yake kama fedha zinathamani kuliko ndg yao aliyepoteza maisha akiwa ktk harakati za kupata habari ,kuwahabarisha watanzania.
 
Huyo aliyeamua kusambaza kile kilichotokea huko Nyololo kwa uhalisia wake ili kuwapa haki watz kujua uhalisia wa suala ndo anahojiwa, ili hali aliyetoa amri ya kubomoa haki ya watu kuishi hastahili kuhojiwa.
Anyway, si-shabikii mtu kutengeneza fedha kwa mwendo huu, lakini pia si-ungi mkono watu kudhurumu watu wenzio haki ya kuishi kwa mwendo huu.
 
still naham sana ya kuiona hiyo CD mana ile ya mauaji ya Arusha ilinisaidia kuondoa sintofaham ktk kichwa chng. Ingawa naunga mkono mambo yote muhimu ktk haki ya kuiuza
 
Wanabodi.

Imepita mwezi na siku kadhaa toka yafanyike mauji ya Mwandisi wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, Daudi Mwangosi, baada ya kuuliwa na polisi kwa kuripuliwa na bomu.

Chama Cha Demokrasia na Maendeo Chadema wamezindua CD ya mauaji ya Davidi Mwangosi (R.I.P) na kuisambaza mitaani na kuanza kuiuza. Chadema wamepata wapi haki ya kutengeneza hiyo CD na kuiingiza sokoni kwa mauzo.

Familia ya Mwangosi (R.I.P) pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania wanapata mgao wowote wa mauzo ya hiyo CD kama hawapati jambo ili kisheria linakuaje.

Watoto wa Marehemu ambao ni wadogo kiumri wanajua chochote kuhusu mauzo ya CD ya baba yao kipenzi.

MAJIBU YA CHADEMA:
Niliisha wahi kupigwa ban kwa ku-question CD za mauji ya kijana wa kule A town, na maswali yangu yalikua hayo hayo! be careful kuuliza such questions!
 
Back
Top Bottom