CHADEMA wamejiandaa vipi KUENDESHA NCHI?

Kwanza anzeni na kurekebisha vijiofisi vyenu kwanza. ofisi za chama zimekaa kama bucha.

There is no question we need changes za uongozi nchini hapa maana dah CCM hapana imeshindwa ila CDM bado wananipa wasi2, waanze na hili la ofc kwanza, naamini wanaweza, decent clean offices hata unapoenda kuchukua kadi unapata picha kuwa they can be trusted na uongozi wa nchi hii. Hebu fikiria kaofisi hakaeleweki then unawaza hivi kama ofc nzuri kuimaintain inawashinda nchi wataiweza?

Pia kujiimarisha vijijini hilo nalo waliangalie,
 
Mimi sijawahi kuwa mwanachama wa chadema wala ccm....but nikiwa kama mtanzania huru ambaye nafuatilia japo sio kwa undani saana siasa za nchi hii.....

Sasa niko convinced kabisa kuwa CHADEMA wanaelekea kuchukua uongozi wa nchi... na kwamba kifo cha CCM sasa ni uhakika.....tatizo langu ni hili .....

Je, CHADEMA wanajiandaa kweli kuendesha nchi?

Wasiwasi wangu ni kuwa wanatumia nguvu kuubwa kupambana na kuiondoa CCM na ikitokea kwa mfano huu uchaguzi wa Igunga CCM wametangazwa kushinda.....basi ni rahisi kwa viongozi wa CHADEMA kuamini kuwa KAZI BADO NI KUBWA MBELE... wakati kiukweli mimi naona CCM is done for good....

Tazama mfano wa Igunga....
Baada yaa kupeleka viongozi wa kitaifa na hila zoote wanatangazwa kushuinda kwa chini ya asilimia 50 kwa jimbo moja...

Je, ukifika wakati wa uchaguzi kwa majimbo yote? Wataweza kufanya fitina ya majimbo yoote?

Kama Igunga ilikuwa yao kwa miaka yote, leo hawapati hata asilimia 50, it's time kwa watanzania tukaanza na kujiandaa na LIFE AFTER CCM..... the sand is shifting beneath.....

Je, CHADEMA wataweza kujiepusha na mistakes za vyama vya upinzani vya Africa vinapopata madaraka?

Kaka, thanks kwa mtazamo wako. CDM wanaWEZA KUTAWALA nchi vizuri sana tena kwa vitendo bile kuonea mtu aibu, na mifano pia tumeiona. Lakini ukumbuke kuwa nchi zilizoendelea duniani, kwa mfano USA, kila rais wa chama pinzani aanavyoingia madarakani, kuna kada ya watu kama 1,200, ambao wanakuwa hawana kazi za kisiasa, na kurudi kwenye kazi zao za awali. Pia CDM wakichukua nchi kuna kada ambazo itabidi warudi kwenye kazi zao za awali kupisha wengine wenye kufanya kazi kwa niaba ya CDM, kwa mfano: Makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, kule ikulu, wote walioteuluwa na JK lazima wapige nyama chini, Nchi nyingine hata wakuu wa najeshi pia hubadilishwa. Wala usiwe na shaka na CDM kama watachukua nchi, mfumo wa uongozi upo wazi dunia nzima. Nadhani umeona Hapo Zambia Satta kafanya nini/. Nikutie amani kaka. T-chao
 
Thread ya Mzee Mwanakijiji :Igunga wakisahihisha Makosa yao tutawasamehe.

Maneno yako Mkuu yangekuwa yanaweza kuwafikia vijana wa Igunga wenye umri wa kuanzia miaka 15 mpaka 45 tungeona mabadiliko makubwa sana Igunga ambayo pia ingetoa mwamko mpya kwa zone kubwa na muhimu sana kwa Taifa [Kwa Makabila ya Wasukuma, Wanyamwezi, Wanyiramba na kwa kiasi Wanyaturu].Tatizo tulilonalo kwa makabila hayo ni mfumo wao wa maisha wa kijadi wa kuwa very royal pasipo kupinga kwa mwenye madalaka japo mhusika atendewi haki na mwenye madaraka.

Upole wa kitabia wa makabila hayo na mfumo wa utawala toka ukoloni na mpaka Serikali huru,tatizo limeendelea kuwepo kwa makabila hayo la kufuata maamuzi ya watawwala [order] pasipo kuhoji na ukitokea kuhoji au kupingana na kiongozi basi wewe ni tatizo kijamii,Na kwa kiwango kikubwa wazee wa kijadi au kijamii wakisimama na kusema kwa umoja wao basi sauti yao ni maamuzi ya jamii.

Na tatizo ili kwa upande fulani pia uligharimu sana Serikali husika kwenye mipangao ya maendeleo japo,kwa kipindi kama hiki cha uchaguzi upole ule na vimbwenga vya wenyeji wa makabila hayo basi ni BONGE YA MTAJI KWA CHAMA TAWALA.Japo ni msiba wa kujiundia kwa siku za usoni.

Umbumbu wa kiufahamu wa wenyeji wa vijijini wa makabila hayo imekuwa sumu hata katika maisha ya kawaida ya kusujudia watawala.Imewagalimu sana kwa majimbo mengi umeona hata aina [silika] ya Wabunge wanawaowachagua kama yule mheshimiwa wa Bastora.

Kwa kiwango kikubwa ninavyowajua makabila hayo ambayo kwa kiwango kikubwa wapiga kura wake walio wengi ni Wanawake na kwa tabia ya makabila hayo iliyowazi ni kuwa kiongozi wa familia ni Mwanamke,basi tegemea ushindi mwingine wa CCM wa Kisayansi.Na CCM kwa kulijua hilo kama ni kanuni ya kimasoko na ambayo hiko sahihi kuwa marketing segment yake ni target halisi ya ushindi wa kuuza bidhaa yake ambayo ni Mbunge wake mtarajiwa.

Chadema inategemea sana kundi la vijana ambao kwa kiwango kikubwa kwa mfumo wa kitabia wa makabila hayo vijana kwa umri huo wa miaka 15-30 huwa na unafiki unaozingatia maslahi yao binafsi na sio kijumuhiya.Na pia umefundishwa kuwa na nidhamu ya woga kwa wakuu wao wa kifamilia ambao ukilejea kwenye staili yao ya kuogopa watawala basi kunauwezekano dakika za mwisho vijana wakatenda ndivyo sivyo kwa CDM.

Ndio maana mwanzoni kabisa mwa mada za uchaguzi wa Igunga nilisema CHADEMA waende IGUNGA kuleta Mwamko ambao kwa ASILIMIA kubwa wametimiza hilo na kuibua nafasi mpya kwa chama hicho kujitizama na kuijsahihisha kama si kujifua na si kujivua gamba kwa kuwa kwa kujivua inaweza kuwa imeshindikana.

CCM watachukua jimbo hilo ila haitakuwa kama KAWAIDA,bali kumeshaibuka CHACHU MPYA YA KISIASA kwa WANA IGUNGA hofu na woga woga wa kijinga na usio na msingi wa kuhofia MAMLAKA baada ya KUHESHIMU MAMLAKA UTAPUNGUA kama si KWISHA.

Hakika yangu vijana wenye umri wa miaka 15-45 ndio wafaidika wa chachu hii kwa kuwa kizazi cha kuanzia miaka 45-kuendelea tayari si mageuzi ya kuleta mwamko dhidi ya Watawala dhalimu.Mpaka sasa kwa makabila hao wenye umri mkubwa bado wanaamini kuwa Baba wa Taifa bado ni moja ya CCM ya leo.

Yote kwa yote TUMEJIFUNZA NA TUTAENDELEA KUJIFUNZA, ukiona mpaka MKUU JOHN POMBE MAGUFULI kaingia ULINGONI [Frontline] ujue hali si sawa kwa CCM,ambao kwa taarifa zisizo na vyanzo rasmi Magufuri kwa vigogo walio wengi ndani ya CCM umuogopa sana kwa kuwa wana imani kuwa uwa ni UNDEFINE CHARACTER.Na hakika kwa kuwa ni Mwana wa Nchi [Son of the Land] amefanya kile kile ambacho ni fumbo kwa wasio ipenda Tanzania kwa kusalimia vyama vyote vya UPINZANI.Kwa picha hiyo Magufuli anajipambanua kuwa CCM kwake ni mfumo tu lakini lililo bora kwake ni Tanzania.

Kwa hilo pia hii zama mpya kwa mabadiliko ndani ya vyama vya kisiasa katika mbinu na mikakati ya kuwajenga [wenyeji wanasema kupepembela] kujiunga na vyama vyao na kuongeza idadi ya wanachama.Maarifa yaliyopatikana IGUNGA na Mbinu na Mikakati imeongeza misamiati katika makarabrasha ya vyama husika.Leo hii tuna tindi kali na Bastora viunoni na risasi nje nje,basi kwa wahusika ni mwanzo mpya wa kuangalia sheria zetu za uchaguzi.

Hakika baada ya IGUNGA nafikilia CCM, watatusaidia tena kutuimizia Wazee wa kujivua Gamba mapacha Watatu sasa itakuwa ni zamu ya Monduri au Bariadi Mashariki.Ni vyema wakafanya hivyo wakatumia chaguzi hizo kujiimarisha huku wakijisafisha.Wakiishia hapo du picha itakuwa nyingine na story ya kujivua gamba ilihairishwa kwa muda kulenga uchaguzi wa igunga kufanyika. Kwa uchaguzi huo kupita tunahakika wapiga kelele wa kujivua gamba wataludi jikoni kuendeleza libeneke.

CCM wajipange upya kwa hilo!!!!!!!!!!!!!


Nilichangia Thread ya Mzee Mwanakijiji siku za Mwisho Mwisho za Kampeni.

Chadema fungasheni rudini Makao Makuu fanyeni analysis nini kimetokea, tumieni SWOT theory analysis msitafute mchawi ukweli ni huo hapo juu.Hapo kwenye nyekundu ndio kazi mliyokwenda kufanya na siku kushinda kupata mtu au mbunge wa Igunga, bali kushinda zama kandamizi za michezo gugumizi ya uchaguzi.Hizo hakika mmeshinda Hongera zenu.
 
pana ukweli flani
BAKWATA imeshinda huku ikiwa hoi
Naamin CDM haitaumia roho sana considering kura ilizopata pia ikumbukwe TABORA si ngome ya CDM
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hata na mimi Mkuu si mwanachama wa chama chochote bali mpenzi na mshabiki, ninayesifia chama kinapofanya jema n nisiemeza ulimi wakati kikivurunda, mchanganuzi na mkosoaji wa chama chochote kikikosa kufanya angalau mambo ya msingi katika uongozi na uendeshaji.

Swali lako ni zuri sana na CDM wangepaswa kuliweka hilo katika manifesto zao. Kusubiri mpaka wamepata nchi ndio waje kuamua kuongoza litakuwa kosa. Kuna mengi ya kujifunza toka ubovu na makosa ya CCM. Ya karibuni kama vile:
- Nchi kuigawagawa mikoa na wilaya kwa utashi - CDM watapunguza mikoa, watazidisha, itabaki hiyo hiyo?
- Hilo hilo la Tawala za Mikoa, kwenye CCM kuna uttiri wa viongozi wa kisiasa, kama wenyeviti wa mikoa, wilaya, kata n.k. wakati watendaji ni makatibu, ambao pia wanachaguliwa kisiasa na si kiuwezo - CDM ingefanya nini kupanua utendaji na kupunguza ulaji?
- Kutokuwa na idadi maalumu ya mawaziri, CCM wanapoamua tu wanaunda wizara mpya - CDM ingefanye? Hatuoni ni busara kuwa na idadi maalumu ya mawaziri kikatiba?
- CCM haina kima maalumu cha maingizo, matumizi, matumizi na madeni - wanaweza kutoa pesa za elimu zikaenda kuwashiwa mwenge, za hospitali zikapelekwa katika uchaguzi, za barabara zikaandaliwa sherehe ya miaka 50 n.k. - Si busara pia kuwa kikatiba tukawa na asilimia maalumu kwa kila matumizi?

Ni mengi lakini pia ni vyema kuzingatia na kujiuliza "CDM inajiandaa vipi kuongoza nchi"", tujiulize pia "Wananchi wamejiandaa/wameandaliwa vipi kuongozwa na CDM?". Tumeshaona namna gani CCM inavyowaandaa wananchi wanaowaongoza: wajinga kwa kukosa elimu, wagonjwa kwa kukosa matibabu, masikini kwa kukosa fursa, mbumbumbu kwa kutojua haki zao, waliokosa imani na serikali, waliotayari kuihujumu serikali kwani serikali haiwatendi haki....na lundo la maovu la serikali dhidi ya wanaowaongoza. Jee CDM ikipewa ridhaa ya wananchi, itaibadilishaje hali hii? Kuiwacha kama ilivyo iakuwa kama kutwanga maji katika kinu.
 
Asanteni sana wakuu kwa michango yenu na HOJA zenye taswira enderevu!

Ila jamani nawaombeni kwa dhati mjitahidi kutumia lugha ya taifa, maana ujumbe wenu unatugusa hata sisi wa shule za kata! Sioni umuhimu wakutumia lugha za kigeni zaidi ikiwa mtoa mada katumia yetu ili ujumbe umfikie kila mtu. Ktk kupambana na ufisadi, ubadhilifu, unyonyaji na mfumo mbovu wa utawala hata mimi (wa shule za kata) nahusika, hivyo jamani msinitenge kwa LUGHA!
MUNGU ISAIDIE CHADEMA!!

Wewe acha uvivu, kusoma shule ya kata haina maana huna uwezo wa kusoma kinge kidogo sana kama hili ambacho so far watu wametumi humu!!! Kuna watu kama Kiranga, na wengineo wakitumia lugha zao si ndo utahama kabsa!! Acha uvivu mkuu, jitume. Do not agree to fail, turn it as challenge to boost your leaning capability.
 
hili ni wazo nzuri hata mie mwanaCCM ninakukubali na ka sasa ninajitahidi kukihama chama kwani kila mara ninawaeleza ukweli ila wamekua wagumu kukubali changamoto za wanachama.Ukweli wengi huku tupo kimaslahi lakini hata kura tunapiga kwingine.
CDM ni chama kizuri, na hata wakipokea nchi bado watahitajika kufanya kazi ngumu katika kuuondoa mfumo ulipo na kuweka wengine waliobora.changamoto za kiutendaji pia zitaonekana kwa viongozi wao wanaoona mbele na mbali, katika kubadili fikra kuwafanya watanzania kuwa wawajibikaji na wenye kufuata utaratibu wa kisheria na kikanuni. Ukweli CHADEMA ni wazuri, wanahitaji kuwaelimisha wazee na pia kwa wabunge wao wanahitajika kuwa karibu san na wananchi wao, kupanga na kujadili changamoto mbalimbali ili wazidi kukubalika vyema. CCCMMM kwisha kwa kweli, tutakuja huko walipo chadema.Naomba watu kama Mh. Sitta naye akiona wanaCCM hawaeleweki, basi aje huko CHADEMA
 
We mtoto, acha kabisa kuchafua jina la nyerere, Nyerere hakuwahi kuiba mke wa mtu, hakuhamasisha wavuta bangi kufanya fujo na team yake nzima ilikuwa inaheshimika sana kwenye hii jamii.
We mzee una mtindio wa ubongo nini? kiongozi wenu wa magamba anatembea na wake wangapi wa watu? Huyo aliyefumaniwa Igunga ni Chadema? Hilo chama la vikongwe kama nyie mnaosubiri kufa ndio limejaa malaya mpaka wanafumaniwa kwenye kampeni. Kufeni haraka mtuachie nchi msituharibie nchi yetu.
 
Ni makosa mno kusema na kuamini kuwa kwanza tuitoe tu CCM halafu tukishafika ndo tukae tujadili tuendeshe vipi nchi.....ni makosa.......

Sasa ndo wakati wa kupanga na kujiandaa ni vipi hii nchi itaendeshwa tofauti na invyoendeshwa na CCM sasa

Boss I concur with you!

Kuna wakati nashawishika kwamba hata JK alifanya fitina zote ili apate Urais wa Jamhuri yetu lakini hakujiandaa kuwa Rais.

Mwerevu hujifunza kwa makosa ya wajinga wakati mjinga hujifunza kwa makosa yake mwenyewe, Chadema wana hiari ya kuwa werevu ama la!
 
Nimeipenda hii mkuu!! Kazi iliyopo sasa hata kama CHADEMA wakishindwa kwa kura chache kama inavyoelekea siyo kukata tamaa ila kujenga taasisi ya CDM ni muhimu sana.

Ukweli ni kwamba CCM hata wafanye nini wataondoka 2015. Haiwezekani kije chama kianzie sifuri na kutaka kuchukua jimbo waliloshikilia kwa miaka 18. Tuanze kujadili taasisi ya CHADEMA chama tawala kuanzia 2015. good idea!!
Such overconfidence ndio inafanya watu webngi waache kushurki katika harakati halisi za kuleta mabadiliko kwa kuwapatiwa watanzania wenye eimu ya chni ya chini au kukosa kabisa ufahamua kuhusu elimu ya uraia, na badala yake wakashinda katika mitandao ya kijamii wakisherehekea ushindi feki kama hapo kwenye red. Ijulikane kuwa hata hii migao ya umeme ni sehemu ya njama za ccm kudhibiti mitandao ya kijamii.
 
The Boss sio kwamba ww hauna chama chochote, wote humu ndani JF tunajuana nani yuko upande gani. Boss wewe ni CHADEMA kufa na unajulikana.

Kuchukua nchi hii kwa CHADEMA bado ni jibu tete sana, na uelewe siasa ni kitu cha mabadiliko hata hao ccm nao wakijipanga vizuri na kutekeleza ahadi zao vizuri usije shangaa wakapita kiubwete. Nalo watakiwa kulizingatia, usiwe one sided ww kama GT

Walau leo umeongea kwa busara, ni kweli kama wakibadilika ccm wakatekeleza ahadi wanaweza kuwadanganya wananchi wasio na mtazamo wa madiliko ya ukweli, ila mimi sioni hali hiyo kwa ccm na hivyo hawatakwepa wimbi la mabadiliko.
 
Hata na mimi Mkuu si mwanachama wa chama chochote bali mpenzi na mshabiki, ninayesifia chama kinapofanya jema n nisiemeza ulimi wakati kikivurunda, mchanganuzi na mkosoaji wa chama chochote kikikosa kufanya angalau mambo ya msingi katika uongozi na uendeshaji.

Swali lako ni zuri sana na CDM wangepaswa kuliweka hilo katika manifesto zao. Kusubiri mpaka wamepata nchi ndio waje kuamua kuongoza litakuwa kosa. Kuna mengi ya kujifunza toka ubovu na makosa ya CCM. Ya karibuni kama vile:
- Nchi kuigawagawa mikoa na wilaya kwa utashi - CDM watapunguza mikoa, watazidisha, itabaki hiyo hiyo?
- Hilo hilo la Tawala za Mikoa, kwenye CCM kuna uttiri wa viongozi wa kisiasa, kama wenyeviti wa mikoa, wilaya, kata n.k. wakati watendaji ni makatibu, ambao pia wanachaguliwa kisiasa na si kiuwezo - CDM ingefanya nini kupanua utendaji na kupunguza ulaji?
- Kutokuwa na idadi maalumu ya mawaziri, CCM wanapoamua tu wanaunda wizara mpya - CDM ingefanye? Hatuoni ni busara kuwa na idadi maalumu ya mawaziri kikatiba?
- CCM haina kima maalumu cha maingizo, matumizi, matumizi na madeni - wanaweza kutoa pesa za elimu zikaenda kuwashiwa mwenge, za hospitali zikapelekwa katika uchaguzi, za barabara zikaandaliwa sherehe ya miaka 50 n.k. - Si busara pia kuwa kikatiba tukawa na asilimia maalumu kwa kila matumizi?

Ni mengi lakini pia ni vyema kuzingatia na kujiuliza "CDM inajiandaa vipi kuongoza nchi"", tujiulize pia "Wananchi wamejiandaa/wameandaliwa vipi kuongozwa na CDM?". Tumeshaona namna gani CCM inavyowaandaa wananchi wanaowaongoza: wajinga kwa kukosa elimu, wagonjwa kwa kukosa matibabu, masikini kwa kukosa fursa, mbumbumbu kwa kutojua haki zao, waliokosa imani na serikali, waliotayari kuihujumu serikali kwani serikali haiwatendi haki....na lundo la maovu la serikali dhidi ya wanaowaongoza. Jee CDM ikipewa ridhaa ya wananchi, itaibadilishaje hali hii? Kuiwacha kama ilivyo iakuwa kama kutwanga maji katika kinu.
Tatizo letu wengi huwa hatusomi ilani na machapisho mbali mbali ya vyama ndio maana tunaulizan CDM wataendesha nchi vipi. Mathalkani CDM ina sera moja ya majimbo, ni lazima tukubaliane hapa tulipofika sera ya mikoa na wilaya imeshindwa kufanya kazi kabisa na kuleta maende;lleo na kuondoa umaskini.
 
Ni wajibu wa wanachadema kuanza kuwapa elimu wananchi kuhusu mabadiliko watanzania tunayoyataka, sio mbaya kwa matokeo ya chadema igunga kwani ni sehemu ambayo hatukua na matawi makubwa na wananchi hawajui katiba ya chadema, Tunaomba viongozi pamoja na wanachama wa chadema kuanza kutoa elimu hususani vijijini ili tuweze kufanya mapinduzi kwenye uchaguzi ujao. Nawashukuruni wanachama wote kwa moyo muliouonyesha kwa kupeana moyo katika chaguzi za ubunge na udiwani zilizofanyika jana.
 
mkuu matokeo yametangazwa wapi?

Ni wajibu wa wanachadema kuanza kuwapa elimu wananchi kuhusu mabadiliko watanzania tunayoyataka, sio mbaya kwa matokeo ya chadema igunga kwani ni sehemu ambayo hatukua na matawi makubwa na wananchi hawajui katiba ya chadema, Tunaomba viongozi pamoja na wanachama wa chadema kuanza kutoa elimu hususani vijijini ili tuweze kufanya mapinduzi kwenye uchaguzi ujao. Nawashukuruni wanachama wote kwa moyo muliouonyesha kwa kupeana moyo katika chaguzi za ubunge na udiwani zilizofanyika jana.
 
Naungana na wote waliochangia kwa mapana suala la Chadema kujiandaa kuchukua nchi. Mimi nitoe tu ushauri kwa chadema. Wanaweza kufikiri huu ni mzaha. Ukweli ni kwamba wanatakiwa kufanya tafiti za kina kuhusu fursa na vikwazo vya maendeleo kwa nchi yetu. Wanaweza kufikiri wanajaribu kuongoza kumbe ndio wanapewa uongozi. Ni wahakikishie tu kwamba lazima wajipage sawa sawa kwani njia yao ya kwenda kuongoza inaonekana wazi wazi.

Pili, ni vema wabunge wa chadema wakajua kwamba nchi haiongozwi kwa jazba wala mapigano. Si kwamba wamepigana hapana, lakini kama chama kikubwa cha upinzani lazima kijue hata ni lugha gani za kutumia kwenye majukwaa, uvaaji, na utendaji wao kwa ujumla. Vitendo vya kihuni huni si vya kwao tena. Watengeneze SERA za MAENDELEO ENDELEVU kuanzia sasa na wahakikishe kuwa zinawagusa wananchi wote na wa vipato tofauti.

KUHUSU VIJIJINI
Tatizo kubwa lililopo kwa watanzania walio wengi ni UFAHAMU na UELEWA wa masuala yanayowahusu. Leo hii hata mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kukuambia nipige kura ya nini? Lakini kibaya zaidi watanzania hawajui haki zao na wala hawana ufahamu wa rasilimali zao. Watanzania wamebaki watu wa kudanganywa tu na vimaneno maneno na vitu vidogo vidogo. Chadema LAZIMA ifike mahali itafute fedha IENDE VIJIJINI kuelimisha wananchi au iandae vijana na kuwapa mafunzo ambayo yatawawezesha kwenda kuwezesha vijijini kwenye suala la elimu ya uraia. Haiwezekani leo mtu aibe halafu anakuja kuombewa kura na anashinda. Watanzania tuna shida kwenye akili zetu. Haiwezekani mtu akataliwe na wananchi Rais anamchagua aongoze mkoa. There must be something wrong upstairs.

Chadema, msikate tamaa. Uchaguzi wa Igunga kwangu ni somo tosha kwa CCM kwamba kutoka lazima watoke kwa sababu waingereza wangesema kwa matokeo ya Igunga ni kama "MOVING FROM ZERO TO HERO". CUF ilitegemewa sana kutoa upinzani mkali lakini ndo chama kilichokufa kabisa. Chadema pangeni safu yenu vizuri mambo yanaenda kuwa mazuri muda si mrefu.

Mungu awatie uvumilivu!
 
sIKU UKIVUA HIJAB UTAKUWA NA AKILI ZINAZOFANYA KAZI
jAMANI USHINDI WA MABOMU NAO UNAJIVUNA????
kWELI KWA KURA HIZO UNA HAJA YA KUTAMBA????


Kufikiria kuwa CHADEMA wanaweza kuongoza kupata kuongoza nchi ni alinacha. Igunga kipimo tosha.
 
Back
Top Bottom