"CHADEMA Wamechakachua Picha"!




Mimi ni kati ya watu nisiyopenda propaganda za kijinga.Nani anaweza akaamini kuwa CHADEMA walipata watu umati wote huu jana wakati mtu mmoja alikuwa ameshauawa na wengine kujeruhiwa mchana huohuo? tuache kudanganyana hapa,CHADEMA wametengeneza hii picha siyo halisi.kama kweli watu wamejaa hivi baada ya mauwaji basi chama hiki kipo mioyoni mwa watu na hakuna atakaye kizuia.Hata hivyo msimamo wangu mpaka nitakapopata ushahidi mwingine ni kuwa picha hii chadema wameichakachua tu
MasalaKulangwa

source mjengwa



uwe na tabia ya kuangalia habari,ITV wameonyesha zaidi ya mara 3 jana kuhusu swala hili sasa unapokuja na picha badala ya habari ya itv hutaelewaka
 
Mh.Mbowe na wadau wa Houston
Mheshimiwa Mbowe,

tunaomba HUO MWILI UPUNGUE kwa haraka maana bado kuna kazi kubwa mbele. Mhe Dr Slaa, asante sana kwa kutii ombi letu na kufanya juhudi za haraka sana kupunguza uzito wa mwili wako.

Kazi bado ni kubwa mno hivyo kila kiongozi wa CHADEMA asisahau mazoezi ya viungo sawa na wahesimiwa Zitto, Mnyika, Mr II na Mchungaji Msigwa wanavyoonekana kuzingatia.
 



Mimi ni kati ya watu nisiyopenda propaganda za kijinga.Nani anaweza akaamini kuwa CHADEMA walipata watu umati wote huu jana wakati mtu mmoja alikuwa ameshauawa na wengine kujeruhiwa mchana huohuo? tuache kudanganyana hapa,CHADEMA wametengeneza hii picha siyo halisi.kama kweli watu wamejaa hivi baada ya mauwaji basi chama hiki kipo mioyoni mwa watu na hakuna atakaye kizuia.Hata hivyo msimamo wangu mpaka nitakapopata ushahidi mwingine ni kuwa picha hii chadema wameichakachua tu
MasalaKulangwa

source mjengwa



kwa hiyo wanahabari wote ni chadema?
 
Kwako mtoa mada bado una mashaka kwamba hii picha imechakachuliwa hata baada ya kutazama picha zilizo hapa MICHUZI hasa ukizingatia watu wa jukwaa kuu wanaonekana ni wale wale? kiufupi hiyo picha uliyoweka wewe haija cover watu wote waliokuwepo embu angalia picha zote kwenye michuzi link nimekuwekea, na kama bado hautaamini basi wewe ni wale wale na wewe calculator unaumwa nini?
 
chadema ni chama kilicho ndani ya mioyo ya watanzania wengi .Hawahitaji kuchakachua picha wala kuleta watu kwa malori kwenye mikutano yao
 



Mimi ni kati ya watu nisiyopenda propaganda za kijinga.Nani anaweza akaamini kuwa CHADEMA walipata watu umati wote huu jana wakati mtu mmoja alikuwa ameshauawa na wengine kujeruhiwa mchana huohuo? tuache kudanganyana hapa,CHADEMA wametengeneza hii picha siyo halisi.kama kweli watu wamejaa hivi baada ya mauwaji basi chama hiki kipo mioyoni mwa watu na hakuna atakaye kizuia.Hata hivyo msimamo wangu mpaka nitakapopata ushahidi mwingine ni kuwa picha hii chadema wameichakachua tu
MasalaKulangwa

source mjengwa



Hii picha imetokea kwenye frontpage ya gazeti la Tanzania Daima leo.
Naamini kuna watu walikuwepo kwenye mkutano huo wa CDM na wako kwenye mtandao wa JF wanaendelea ku-browse. Nafikiri hao wangelikuwa ni watu wa kwanza kuikataa hii picha. Kama una ushahidi kuwa hii picha imechakachuliwa lete ushahidi. Tunajua kuna watu ni wataalamu wa ku-edit picture kwa kutumia mfumo wa 3D wanaweza kujua kama madai yako yana ukweli.

To me hii picha ni halisi na imebeba uhalisia wote wa tukio.
 
Huu ni ubishi usio na tija. Huoni kama wananchi wengi baada ya kuona nguvu ya serikali inatumika wakapata hamu ya kwenda kujua ni kitu gani kinachowatisha serikali kwenye hiyo mikutano?
 
Mkuu usiwe na fikra mgando siku zote,kwa hiyo vyombo vya habari vyote tv na magazeti navyo vilichakachua picha?tatizo ukiwa magamba hata akili ya kufikiri vitu vidogo tu inakua imefungwa,hiyo ni asilimia ndogo sana ya sehemu ya umati uliokuwepo jana pale uwanjani,c.c.m hawakuamini kua Morogoro nayo inaweza wapa mgongo na kuachana na ujinga!propaganda za ukabila zilishndwa,udini zikashndwa,za kusaidiwa na mataifa ya magharibi zikashndwa sasa mnakuja na propaganda za kitoto kabisa za kuchakachua picha
 
Dk.+Willibrod+Slaa+kutubia..jpg





Angalia vizuri hizo picha zote ni za jana kwenye mkutano wa Chadema Morogoro, picha hizi majukwaa yanafanana, tofauti ipo kwenye bendera picha moja ina bendera ingine aina, halafu angalia nyuma kabisa picha moja inaonyesha nyumba ingine aina nyumba.



JF daima....:clap2:
 
weka basi! ulio ona wewe!.......
inashangaza unapnga ki2 usicho kijua!...............
cha kusikitsha haukuepo!
 
Wachakachue kwa manufaa ya nani? Chama linajiuza lenyewe kwa walala hoi
 
Extraordinary claims require extraordinary evidence.So that sage Sagan said.

Kabla hujasema "wamechakachua" kuwa na uhakika ukiulizwa "wapi?" unaweza kuonyesha "hapa".

Hao ndio vijana wa Nnauye Jr. Akili nyepesi. If the image has been technologically altered you have to provide forensic evidence not assumptions.

Anyway, tutajua 2015
 
Ndo akili ilipoishia kuwaza nyambaaafu....kwa hiyo na itv jana ilichakachua picha walizoonesha??au unataka kuuaminisha umma kuwa itv ni chombo cha chadema??

Kweli mpumbavu atakaa na kuwaza upumbavu
 
Ni hatari mtu mzima akiamua kujidanganya mwenyewe na akajua kuwa anajidanganya,sasa hawa magamba wanajidanganya wenyewe,mnasema wamechakachua wakifanya hivyo ni kwa faida ya nani,wakati sisi tunataka kutambua jinsi gani watu wanasapoti chama,leo tukijidanganya mwisho wa siku itakuaje?magamba ndi zenu hilo halina ubishi,mlazwe pema peponi magamba nyie
 




Angalia vizuri hizo picha zote ni za jana kwenye mkutano wa Chadema Morogoro, picha hizi majukwaa yanafanana, tofauti ipo kwenye bendera picha moja ina bendera ingine aina, halafu angalia nyuma kabisa picha moja inaonyesha nyumba ingine aina nyumba.
JF daima....:clap2:
Kwa hakika wewe ni kilaza wa kutupwa, pole sana! Jaribu angalau mara moja moja kuficha upumbavu wako...unaishusha hadhi JF!
 
Kwanza hiki ni kipande tu cha umati kama 50%, nilikuwepo na ilikuwa vigumu kupiga picha umati wote kwa mara moja. Labda kama ungepata helikopta.

mod hii thread ya kutoa haina mantiki na si siasa bali ujinga.Mtoa mada jitahidi kuangali vyombo mbalimbali vya tv , redio, magazeti.kufanya utafiti kwnye jf kupata ukweli ni ujinga.ila kwa faida yako ni kwamba hata polisi ilishindwa kuwadhibiti waandamanaji kutokea msanvu baada kuua, ndo wakajiunga vikundi vidogovidogo kuelekea mkutanoni na kufanya umati mkubwa ambao ulionyeshwa kwenye tv jinsi makundi yalivyojikusanya upya na kuwa umati mkubwa kwenye mkutano.Hoja si kupendwa hoja nn cdm anahamasisha kwenye M4C ni kwamba serikali ipo usingizini, rasilimali zinahujumiwa, hakuna haki kama jana ulivyooona polisi kutumia ngvu kubwa.mdc na marc kudhibiti chadema kufanya shughuli za kisiasa, ajira kuwa finyu katika jamii.ccm kukumbatia matajiri na kusahau wanyonge, kundeleza matabaka kama nasaba, elimu, utajiri, dini; hayo yote ni kero katika jamii ndo inapata kiu ya kupata mbadala wa vyama vya upinzani vinasemaje kuhusu hayo.ccm imekaa kupiga porojo na propaganda wakati jamii inateketea kama shule za kata, masual ya afya kudorola kwa kukosa madawa, wa wahudumu wa fya, kilimo kukosa mtizamo sahihi, kama masoko endelevu, shule za wanyonge kuwa za hovyo.na ajira kuwa bomu kubwa.
 
Duble Chris

MKUTANO WA CHADEMA MOROGORO



DK+SLAA+PIX+NO+1.jpg

Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akihutubia wananchi wa Manispaa ya Morogoro katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ndege mkoani Morogoro.
DK+SLAA+MAAMBOZI+YA+KIFO+CHA+ALLY+ZONA+PIX+NO+1.jpg

Katibu mkuu wa Chama chama cha Demokrasi na Maendeleo Dkt Wilbrord Slaa akiongoza umati uliohudhuria mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) baada ya mtu mmoja kudaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia wakati wengine wawili nao wakidaiwa kujeruhiwa kwa kupigwa na risasi na askari wa jeshi la polisi.


Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 asubuhi eneo la Msamvu barabara kuu Dar es Salaam-Morogoro wakati askari hao wakiwatawanya umati mkubwa wa wanachama na wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakisubiri viongozi wa juu wa chama hicho ili waandamane kuelekea katika mkutano wa hadhara uwanja wa Ndege mkoani Morogoro leo.
Dk.+Willibrod+Slaa+kutubia..jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na vitongoji vyake, katika mkutano wa hadhara wa operesheni sanga ,kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege
TUNDU+LISI+PIX+NO+1.jpg

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Morogoro waliojitokeza katika mkutano huo.
MAKAMU+MWENYEKITI+ZN+SAID+ISSA+MOHAMED.jpg

Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar Said Issa Mohamed akifafanua jambo kwa wananchi hao.
IGUNGA+PIX+NO+1.jpg

Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Igunda kupitia Chadema, Joseph Kashinde akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
SUZAN+MUNGI+PIX+NO+1.jpg

Mbunge wa viti Maalum Chadema akimwaga sera za chama hicho.
MNYIKA+AKIPANDA+JUKWAANI+PIX+NO+2.jpg

Mbunge wa jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam John Mnyika akipanda jukwaani wakati akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
UMATI+MKUTANO+WA+CHADEMA+PIX+NO+1.jpg

Sehemu ya umati ambao ni wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake katika mkutano huo. Picha Zote na Juma Mtanda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom