CHADEMA Walitumia bilioni 1.3 Uchaguzi wa rais 2010

zitto tutakupa ulinzi huyo mbowe na genge lake walimwondoa wangwe shauri ya kupinga mbowe kuchota mapesa. jihadhari kaka hao wakaskazini ni wabinafsi.

wanapeana mshahara 15 milioni na kuuzia chama mitumba
hoja dhaifu sana,CCM wanafanyia ufisadi ruzuku yao kiasi gani pamoja na mapato yatokanayo na vyanzo vyao vya mapato?
 
Magari ya mitumba yaitikisa CHADEMA

Leon Bahati

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekiri kwamba suala la ununuzi wa magari yaliyotumika lilizua mjadala kwenye kikao chake cha Kamati Kuu kilichomalizika Jumatatu wiki hii.

Maelezo ya mvutano huo yalitolewa jana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya gazeti hili toleo la Jumatatu kuandika juu ya suala hilo.

Hata hivyo, Dk Slaa alisisitiza kuwa mvutano huo ulikuwa wa kawaida hasa ikizingatiwa kuwa ni suala ambalo haliepukiki penye mjadala wa watu wengi akisisitiza kwamba demokrasia ndiyo iliyoamua.

Gazeti hili liliripoti kuwa mkutano huo ulitokana na baadhi ya wajumbe kupinga na wengine kuunga mkono suala la ununuzi wa magari yaliyotumika yenye thamani ya Sh480 milioni.

Baadhi ya waliokuwa wanapinga mkakati huo walisema kuwa ulikuwa unalenga kumnufaisha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alikuwa achukue nafasi hiyo kukiuzia chama magari ambayo tayari ameyatumia.

Miongoni mwa wajumbe wa Baraza hilo, Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo walinukuliwa wakisema kwamba isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali.

Akitoa ufafanuzi huo jana, Dk Slaa alisema msuguano huo ulikuwa ni wa kawaida na ulikuwa sehemu ya kuwezesha demokrasia kuchukua mkondo wake. Alikiri kuwa kwenye mchakato huo, Mbowe ana magari matatu ambayo chama kinataka kuyanunua.

Alisema hoja hiyo ilimalizika kwa Baraza kuamua kuwa Mbowe aendelee kushawishiwa ili akubali kukiuzia chama magari hayo. Alielezea kuwa magari hayo aliyanunua na yakaanza kutumiwa na chama kwenye kampeni za uchaguzi uliopita.

"Magari hayo Mheshimiwa Mbowe aliyanunua kwa ajili ya biashara zake lakini kwa kuwa chama kilikuwa katika matatizo ya usafiri, akakubali kuyatoa yakisaidie ili baadaye tumrejeshee," alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa magari mawili yanaendelea kutumiwa na chama hivyo ni vyema wayanunue.

Kuhusu chama hicho kununua vitu vilivyotumika wakati kimekuwa kikiipinga vikali serikali kutumia vitu vilivyotumika, Dk Slaa alisema njia inayotumiwa na Chadema iko wazi zaidi ukilinganisha na ile ya serikali.

Alidai kuwa kwenye michakato ya ununuzi serikalini kuna mazingira mengi yanayoruhusu ufisadi hasa katika kujadili bei lakini suala la kununua magari ya Mbowe, suala kama hilo haliwezi kupata nafasi.

Mshahara wa Dk Slaa

Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kuwa chama hicho kimeamua kumlipa Dk Slaa mshahara na maslahi yanayolingana na anayopata mbunge.

Alisema hiyo ni kwa sababu chama hicho ndicho kilichokuwa kimemshawishi aache kugombea ubunge katika Jimbo la Karatu, Arusha ambako alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda na kumtaka agombee urais ambao mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete alitangazwa kuwa mshindi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alisema uamuzi huo ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na vikao vikuu vya chama hicho, kama vile Kamati Kuu na kisha kuidhinisha malipo hayo.

"Itakumbukwa kuwa Mheshimiwa Dk Slaa hakuomba nafasi ya kugombea uraisi, aliombwa. Tunajua alikuwa mbunge na alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda tena nafasi hiyo, lakini akakubali ombi la chama," alisema Mbowe na kuongeza: "Hii siyo mchezo!

Uamuzi wa namna hiyo ni wa kujitoa. Ndiyo maana Kamati Kuu ikakubali apate mshahara na marupurupu sawa na yale ya mbunge."

Mbunge anakadiriwa kuwa anapata mshahara pamoja na marupurupu yanayokaribia kufikia Sh7 milioni kwa mwezi.
Chadema kilitumia Sh1.3 bilioni kusaka urais 2010

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu uliopita, Mbowe aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama chake kilitumia Sh1.3 bilioni katika kampeni za uras.

Alivitaja vyanzo vya fedha hizo kuwa ni Sh 338.9 milioni za ruzuku, Sh 235.9 milioni kutoka kwa marafiki, Sh32 milioni michango mbalimbali ya wanachama na mali mbalimbali za watu zenye thamani ya Sh719.7 milioni.

Kwa taarifa hii ya chama cha CHADEMA imenifurahisha sana jinsi mambo yalivyowekwa wazi. Kwa kweli Mh Mbowe anafaa kuwa kiongozi hakufanya mambo kiunafiki, au kiubabe, hakusemea pembeni, alipeleka kwa wahusika na wahusika wakajadili na wakaona faida na hasara. Tuwashukuru hawa watu wanaojitolea kipesa, na wale wanaopoteza muda wao kwa ajili ya kukijenga chama nk. Ninafikiri viongozi wa Chadema wako makini wanaangali mbele na nyuma. Tunajua hakuna mtu aliezaliwa na uongozi ila demokrasia ni lazima ijengwe na demokrasia inapotea pale inapofikia kila mtu anakuwa na uchu wa madaraka bila kuvumiliana au kuridhika.

TAHADHARI: Mbowe hapo alipo mtu asimguse mwacheni aendelee na safari aliyoianza pamoja na viongozi wote wa chama sisi tuwaunge mkono na kuwashauri pale wanapokosea. Magamba wanavyotapatapa sasa hivi wakifanikiwa kupenya tu moto mtauona na chama kitakwenda kufia baharini. Vijana tukaze moyo, kitukizuri hakijengwi kwa mdomo ila vitendo.

VIVA CHADEMAAAA.:israel:
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Piganeni,toeni mapovu,singizieni,danganyeni,fanyeni spinning,tukaneni lakini CHADEMA ni Chama chenye mkono wa MUNGU kitasimimama tu.Kila kitu kimewekwa wazi,tumeeleza hali halisi bado hamuelewi.Tulitarajia haya na tunaendelea kuyatarajia,tutaandikwa sana,Makala nyingi zitaandikwa,vipindi redioni vitajadili lakini wenzenu tunasonga mbele.Nyie mkiwa mnayaendeleza hayo wenzenu kesho tunaenda kuwasha moto Nyanda za Juu Kusini,tunatoa elimu ya Uraia,Tunakomba wanachama,tunasimika Viongozi na Tunajiimarisha Kisiasa.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke,Mbowe Kanyaga twende!!!
Mimi natoka wilaya ya Kilombero, na sitokubali jimbo langu liongozwe na bogus kama wewe!
Yaani kwa sababu Mbowe kakufadhili ubunge unaruhusu afanye chochote with impunity?
Ufisadi ni ufisadi tu! Ufanywe na RA, Manji na hata Mbowe na Mkwe wake!
 
Wakuu hapa ndo kuna undumila kuwili.

Sentensi moja ingesomeka hivi kama nilivoibadilisha ungesikia keyboard zikitwangwa:

"Magari hayo Mheshimiwa ROSTAM AZIZ aliyanunua kwa ajili ya biashara zake lakini kwa kuwa chama kilikuwa katika matatizo ya usafiri, akakubali kuyatoa yakisaidie ili baadaye tumrejeshee," alisema MAKAMBA na kuongeza kuwa magari mawili yanaendelea kutumiwa na chama hivyo ni vyema wayanunue."
Hata habari yenyewe ingepakwa rangi ya kijani, lakini CDM hakuna ufisadi bwana , wao kuna kina MR CLEAN

Laiti kama wangekuwa wanaeleza bayana kuwa RACHEL walisaidia kampeni na sasa lazima chama kiwalipe pesa zao na vyanzo vyakuwalipa vikawekwa hadharani tatizo nikuwa wanawatumia kifisadi fisadi na baadaye wanakuja na kauli tata za kuwa wao ni magamba na wengine ni mafuta ya kuyaondoa hayo magamba na hii ndiyo tafauti iliyopo kati ya CCM na CHADEMA as far as financial resources are concerned.
 
Mimi natoka wilaya ya Kilombero, na sitokubali jimbo langu liongozwe na bogus kama wewe!
Yaani kwa sababu Mbowe kakufadhili ubunge unaruhusu afanye chochote with impunity?
Ufisadi ni ufisadi tu! Ufanywe na RA, Manji na hata Mbowe na Mkwe wake!
siyo lazima umpe kura yako atapewa na wengine, na huna ubabe wa kusema hutakubali ina maana wewe ni Mungu je wananchi wakiamua wampe ubunge wewe utapiga...?
 
Mpango wa Kununua magari ya MBOWE yaliochakazwa na CHADEMA yenyewe wakati wa kampeni sio tatizo hata kidogo. Je. nyie mnaopinga mpango huu MNGEPENDA BOWE aanze kukidai chama malipo yote yaliyotokana na chama kutumia magari yake? (kwani hapo ndio tungeona MBOWE anakitumia chama kwa maslahi yake binafsi, na hatimaye mashabiki wa MAGAMBA mngeanza kufurahi)
 
iPiganen,toeni mapovu,singizieni,danganyeni,fanyeni spinning,tukaneni lakini CHADEMA ni Chama chenye mkono wa MUNGU kitasimimama tu.Kila kitu kimewekwa wazi,tumeeleza hali halisi bado hamuelewi.Tulitarajia haya na tunaendelea kuyatarajia,tutaandikwa sana,Makala nyingi zitaandikwa,vipindi redioni vitajadili lakini wenzenu tunasonga mbele.Nyie mkiwa mnayaendeleza hayo wenzenu kesho tunaenda kuwasha moto Nyanda za Juu Kusini,tunatoa elimu ya Uraia,Tunakomba wanachama,tunasimika Viongozi na Tunajiimarisha Kisiasa.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke,Mbowe Kanyaga twende!!!
Ni hatari kuleta mipasho kwenye ufisadi hapo kwenye blue ndio faida ya ubunge wa kupewa hasara tu kwa taifa, hapo kwenye nyekundu usirudie tena kutoa maneno yako hayo, Mungu awezi kuwa upande wa Mafisadi
 
kwenye blue hapo, we hukumbuki CDM walikuwa wanalalamika kuhusu kuchangia kwa huduma ya SMS, CCM,TISS na makampuni ya simu yalikuwa yanaweka kauzibe na watu yulikuwa tunatuma SMS zilikuwa zinafail, we unaongea vitu bila data. shut up your.....@L;;;;l'''', usije ukanisababishia BAN bure

mumeibiwa mchana kweupe. sms zinafail huku pesa zimechukuliwa

watoe taarifa wangapi wamechangia. chadema shamba la bibi la mbowe.
 
mbowe ni fisadi na huu ushahidi tosha. hii ngo yao inamtajirisha.

slaa anapata milioni 15 kwa mwezi wasitudanganye. kalegezwa na mbowe ili asipige kelele ufisadi wa mbowe.

Naona upo kazini sweetie. Safi sana....
 
Kwa taarifa za kiitelijinsia nilizonazo, budget ya CCM kwa uchaguzi wa 2010 ilikuwa:-

Helcopter 3@ tsh 2,0000,000,000/- = 6,000,000,000/=
Kusomba wahudhuriaji 5,000,000 @ 5,000/- =25,000,000,000/=
First Lady ndege na msafara = 4,000,000,000/=
Riz1-------------------------------= 2,000,000,000/=
Miraji -mtunza hazina--------------------------- 1,000,000,000/=
Wachachuaji database na sms za kampeni....... 1,200,000,000/=
Kurubuni wabunge upinzani 12,000,000,000/=

Hii ni sehemu tu ya budget, budget ya CDM inaweza kuwa ni 0.1 ya CCM.
 
Kusema bilioni 1.3 haitoshi watupe mchakato.

Na hii Ruzuku ya serikali naomba ikome kila kunguru aruke kwa urefu wa mbawa zake

Sisi tunakatwa kodi kubwa kwenye mishahara inaenda kwa wanasiasana porojo zao!!!
 
Sasa wale waliokosa Ubunge na walikuwa wanatumia magari na pesa yao kikao kimewatosa?
Au ni Mbowe tu anayefidiwa?
Mgelifanya vema kuwafidia waliokosa ubunge na wamebaki masikini kuliko Mbowe ambaye analipwa kwa kodi zetu.
 
Magari ya mitumba yaitikisa CHADEMA


Mshahara wa Dk Slaa

Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kuwa chama hicho kimeamua kumlipa Dk Slaa mshahara na maslahi yanayolingana na anayopata mbunge.

Alisema hiyo ni kwa sababu chama hicho ndicho kilichokuwa kimemshawishi aache kugombea ubunge katika Jimbo la Karatu, Arusha ambako alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda na kumtaka agombee urais ambao mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete alitangazwa kuwa mshindi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alisema uamuzi huo ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na vikao vikuu vya chama hicho, kama vile Kamati Kuu na kisha kuidhinisha malipo hayo.

"Itakumbukwa kuwa Mheshimiwa Dk Slaa hakuomba nafasi ya kugombea uraisi, aliombwa. Tunajua alikuwa mbunge na alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda tena nafasi hiyo, lakini akakubali ombi la chama," alisema Mbowe na kuongeza: "Hii siyo mchezo!

Uamuzi wa namna hiyo ni wa kujitoa. Ndiyo maana Kamati Kuu ikakubali apate mshahara na marupurupu sawa na yale ya mbunge."

DAAAAAAAAAAAA!!!!
Siasa kweli hatari! Mh Mbowe, ina maana alijua mapema machungu ya kukosa uraisi akamchomekea Dr.Slaa, sasa anampoza. Hata kama tajiri kupata above 7mil tax free + other perks bila jasho si mchezo. Dr. Slaa 2015 ukiona miyeyusho we kagombee Karatu mzee,
Duuuuuuuuuuuuuuuu.
 
Dr.Slaa ni dr.wa ukweli mshahara wake kama inawezekana uongezwe hata mara ishirini zaidi.Kama tunataka kukomboa nchi hii tuache utani.Mimi binafsi sina utani katika mambo mazito.Mtu kama Slaa akiachwa hivi hivi ataishije.Mbona wenzetu wa Rwanda wameamua kumkodi Ton Blair kuwa mshauri wa uchumi kwa gharama kubwa?
Tuwe wakweli Dr.anastahili malipo makubwa.Kama mtoa hoja ni mtanzania au ni mpenzi wa soka asome profile ya wachezaji mpira tu toka Uingereza au Hispania wanalipwa kiasi gani kwa siku.
 
Back
Top Bottom