CHADEMA walikoroga tena uchaguzi Wanawake

Engineer

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
265
0
Mheshimiwa Slaa,

Inakuwaje chaguzi zote zinavurugika? Je hankujiandaa kwa hii mikutano?

Uchaguzi wanawake Chadema nao balaa

Imeandikwa na Lucy Lyatuu;

Uchanguzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) umepata dosari baada ya ushindi wa mgombea kukataliwa na wajumbe huku wakitaka kukata rufaa dhidi yake. Wagombea wa nafasi hiyo ya uenyekiti na kura walizopata ni Leticia Musore (81), Chiku Abwao (75) na Recho Mashishanga (42), na jumla ya wajumbe ilikuwa 198.

K
atibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, alisema jana kwamba akiwa msimamizi wa uchaguzi huo aliagiza urudiwe kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Katiba ya chama.

Alisema alipokea rufaa ya mgombea Chiku akipinga ushindi huo, na akaagiza urudiwe kwa mujibu wa Ibara ya 6.3.1(c) ya Katiba ya Chadema, ambapo mshindi anatakiwa apate si chini ya asilimia 50. Hata hivyo alisema agizo hilo halikutekelezwa, kwa kuwa wajumbe wengi walitoka na hivyo rufaa kuamuliwa kwa utaratibu wa kawaida.


"Hadi rufaa hiyo itakapoamuliwa, mhusika ataendelea kuwa Mwenyekiti," alisema Dk. Slaa. Hii ni mara ya pili kwa Chadema kubatilisha matokeo baada ya kufanyika hivyo katika uchaguzi wa vijana, ambapo matokeo yalisitishwa na uchaguzi kuahirishwa kwa miezi sita kutokana na kile kilichoelezwa na Slaa kuwa ni ukiukwaji wa kanuni na harufu ya rushwa.


Washindani katika kinyang'anyiro hicho alikuwa ni John Hecha na David Kafulila, ambaye anadai alishinda lakini kilichofanyika ni ‘zengwe'.


Wakati Hecha ni Diwani wa Tarime Mjini, Kafulila ni Ofisa Habari wa Chadema. Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto, amesema yeye na Mwenyekiti, Freeman Mbowe wataendelea kuwa kitu kimoja na kuwataka wanachama wasiwe na hofu juu yao.


Zitto alisema hayo mara alipotakiwa kutoa msimamo mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Chama hicho, kwamba yeye na Mbowe wanatofautiana katika mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kuanza leo.


"Wajumbe wa Baraza Kuu ninawatoa hofu yangu na Mbowe, tuko kitu kimoja, tuna kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unakwenda salama tena wote tukiwa imara," alisema Zitto. Aliongeza kuwa chama kimetoka mbali hasa katika mazingira magumu ya kisiasa ikiwemo tangu wakati wa uchaguzi wa kitaifa mwaka 1995 hadi sasa.


Aliongeza kuwa ataendelea kuifanya kazi ya chama hicho huku wakiwa kitu kimoja na aliwapongeza wabunge wenzake wa chama hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya wakiwa bungeni. "Chama kimekua, tuwashukuru wabunge 11 wa chama hicho walioko bungeni kwa kazi nzuri wanayoifanya na kwamba lengo kuu walilonalo ni kukamata Dola mwaka 2010," alisema Zitto.


Awali Mbowe akizungumza, alisema hana uhasama na Zitto na watafanya kazi pamoja bila kutengana na kuwa malengo ya chama ni kuchukua Dola mwakani. Hata hivyo alisema anavishangaa vyama ambavyo vinataka kukifundisha demokrasia chama hicho na kuvitaka kuacha na badala yake vitumie muda uliopo kujiimarisha.


"Ninawaambia vyama vingine kuwa watumie muda mwingi kutibu ‘kansa' waliyonayo katika vyama vyao, kuliko kuyaona ‘mafua' ndani ya Chadema," alisema Mbowe. Hata hivyo, aliomba radhi kwa waliokwazana kwa njia moja au nyingine katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na kwamba hakuna binadamu asiyesamehe.


Alisema kila mmoja anapata mzigo kwa uzito wa kazi yake na kwamba chama kilikabiliwa na changamoto za utendaji kazi ambazo zinaweza kuwa na lawama kubwa. Kabla ya mkutano huo wa Baraza Kuu kuanza, mama yake Zitto, Shida Salum, alikuwa na mazungumzo na muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, huku akimsisitiza kutokukubali chama kufa kwa ajili ya wachache.


Alimtaka Muasisi huyo, kutumia mamlaka aliyo nayo kuwaondoa wasiotaka kuwa kitu kimoja ndani ya chama kauli ambayo ilikubaliwa na Mtei akikiri kuwa hataruhusu mpasuko ndani ya chama.


Wakati huohuo, wajumbe wawili wa chama hicho kutoka Tarime na Kigoma, walizungumza na gazeti hili na kudai kuwa zipo njama za kuhakikisha kuwa Mbowe anapigiwa kura ya hapana na wajumbe wa mikoa 16 kutokana na uamuzi wa kumsimamisha peke yake.


Wajumbe hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini, walisema wazee waliomwita Zitto na kumtaka ajitoe hawatambuliwi kikatiba na hivyo hasira zao zitaoneshwa kwenye sanduku la kura.

 
Kama kweli Chadema inataka mshikamano, basi ni vema itumie katiba yake katika kufikia maamuzi na sio njia za chini ya meza.

Pili, kwa hali jinsi ilivyofikia sasa, kwa wazee kumwomba Zitto ajitoe na kumwacha Mbowe kama mgombea pekee, basi Mbowe alitakiwa atumie busara zake kwa kujitoa katika kinyang'anyiro hicho. Kuendelea na uchaguzi bila kujali tatizo hili Mbowe atakuwa ameonesha udhaifu mkubwa sana wa kuwa kiongozi anayeaminika na kuwajibika mbele ya jamii.

Kosa ambalo wazee wa Chadema wamelifanya litakigharimu chama kwa muda mrefu sana ujao. Sijapenda kuona Chama hiki kinaendelea kuonesha hadharani makovu yaliyotokana na tuhuma za kiukabila na ukanda zilizoelekezwa na kulalamikiwa kwa muda mrefu na hata na baadhi ya viongozi wandamizi wa chama hicho.

Kujikwaa si kanguka, rekebisheni makosa kungali kweupe.
 
Back
Top Bottom