CHADEMA wako tayari kumpokea Lowassa

Kama CHADEMA inataka kuwa sawa na CUF na ijaribu kumkaribisha EL ambaye amejaa tuhuma kila kona ya vyombo vya habari na midomoni mwa watz, CHADEMA itajiua yenyewe na kama mpango ndo hou wa kuanza kubeep tension ya wapenzi wa CDM hapa sio.

mbona hamtujuzi makosa yake? Au ni siasa za chuki? Dr. Slaa alimuhusisha na RICHMOND lakini EL alishatolea ufafanuzi ndani ya kikao halali cha chama. Naamin muda utaamua!
 
Hapa ndipo Chadema wataanza kukoroga RASMI, hafai hata kugombea ubalozi wa Nyumba kumi kumi chadema, anaweza waibia wananchi Mahindi yao, mwizi ni mwizi tu.

Bila shaka una hoja lakini umesahau kuwa katiba ya nchi inatoa ruhusa ya mtu kuwa chama chochote. Lowassa kuhamia CDM haina maana kuwa atapewa uongozi wa juu na hata kufikiri kuwa makosa aliyonayo yatasafishwa. Bali ni haki yake kikatiba kuwa chama chochote na bila shaka akaribishwe tu CDM. Akitangaza kuwa sasa anahama CCM kuja CDM, je utapiga yowe kupinga?
 
Kwanza kabisa naomba niwarejeshe kwenye kaulimbiu ya JF, inasema, "The Home of Great Thinkers". Ukweli niliougundua ni kwamba tuna wana JF wengi sana humu ambao si great thinkers. Naomba nizungumzie mambo mawili tu:

Kwanza tunachofanya humu ndani ni kisa tulichosimuliwa zamani kwamba baba mmoja alikutwa na mkewe akinoa panga. Mke akamuuliza unanoa panga la nini, yeye akajibu hivi: "Ninanoa hili panga ili nikafyeke shamba halafu nilime pamba nikivuna na kuiuza nitanunua ng'ombe wawili: mweusi na mweupe. Yule mweusi hata wewe unaweza kumkamua lakini mweupe nitakuwa namkamua mimi tu". Mke akasema haiwezekani mweuupe umkamue peke yako. Hata mimi nitakuwa namkamua. Mme akasema haiwezekani umkamue ng'ombe wangu. Wakabishana mpaka wakapigana. Ndicho ninachokiona humu ndani. Watu wanatoa macho kiasi kwamba baadhi wangekuwa karibu yule aliyemtukana eti Tuntemeke Mwigamba aondoke atuachie chama, labda angeweza hata kumpiga. Tunatoleana macho utadhani Lowassa katangaza kuingia CDM na sasa tunabishana ama tumpokee ama tuache. Kumbe inawezekana jamaa hana hata mpango huo!

Jambo la pili naomba tusome tena hii nukuu hapa kama Mwandishi wa gazeti alivyomnukuu Mwigamba:

“Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,”

Kama mmesoma hayo maneno ya Mwigamba between lines, hamna sababu ya kumshambulia kiasi hicho. Hajasema kwamba leo hii inaweza kutokea tu EL akaja akaomba kuingia CDM na yeye kama mwenyekiti wa mkoa akampokea. Amesema lazima aeleze sababu za kufanya hivyo na akatumia neno la wingi "na sisi" ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama. Maneno yake yanaonyesha collective responsibility kwamba watakuwa jopo la viongozi. Watamuuliza kwamba unataka kuja CHADEMA lakini una tuhuma hizi na hizi. Wakiridhika na maelezo yake ndo wataamua kama viongozi si yeye kama mwenyekiti wa mkoa. Naomba niwaulize swali mnaotumia msuli mkubwa kupinga EL kuja CDM kwa vyovyote vile. Hivi akija na uthibitisho kwamba madudu yote yamefanywa na Mkapa na Kikwete. Yeye kafanywa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuiokoa serikali isidondoke kama alivyofanyiwa gavana wa zamani wa benki kuu Daudi Ballali, hivi akaja na ushahidi wa kile alichokitamka Mwakyembe kwamba kuna vitu walificha ili serikali isidondoke na vitu hivyo kumbe EL akafanikiwa kuonyesha kwamba ni ushahidi kwamba ufisadi wote wa Richmond ni wa JK na si wa kwake Lowassa. Hivi akija akakiri na kutubu kwa kuonyesha ushahidi wa baadhi ya vitu alivyovifanya kwa kulazimishwa na system kwa ajili ya chama na akavijutia na kuviungama na kuwaomba radhi wananchi, akasema ametoa maisha yake kama serikali itamuua kama ilivyommaliza Ballali yuko tayari ili mradi ukweli wote uwe hadharani, hivi mtakataa kumpokea awe mwanachama wa CHADEMA. Try to use your bongos badala ya kutumia misuli kupinga kila kitu kwa ushabiki.
 
Lowasa naye aje atumike kama ambavyo watatumika wenzake waliokimbia umande baada ya kuona wanapoteza au wameshapoteza umaarufu ndani ya magamba. Karibu EDO uhakikishea majimbo yote ya kaskazini ni chadema then uendelee kanda nyingine na hadi ikifika 2014 utakuwa umemalizia kule kwa mtoto wa mkulima ili ifikika 2015 ushindi kwa CDM tsunami. Again, welcome sir!! Our funeral manager for CCM!!!
 
Suala la msingi ni kwamba Chadema wako tayari kumpokea mtazania yeyote kuwa mwanachama wao. Sasa suala la kwamba kila mwanachama wanayempokea anapewa nafasi ya uongozi ni tofauti kabisa. EL anaruhusiwa kuingia Chadema - kama any next Tanzanian. Period.
 
Kwanza kabisa naomba niwarejeshe kwenye kaulimbiu ya JF, inasema, "The Home of Great Thinkers". Ukweli niliougundua ni kwamba tuna wana JF wengi sana humu ambao si great thinkers. Naomba nizungumzie mambo mawili tu:

Kwanza tunachofanya humu ndani ni kisa tulichosimuliwa zamani kwamba baba mmoja alikutwa na mkewe akinoa panga. Mke akamuuliza unanoa panga la nini, yeye akajibu hivi: "Ninanoa hili panga ili nikafyeke shamba halafu nilime pamba nikivuna na kuiuza nitanunua ng'ombe wawili: mweusi na mweupe. Yule mweusi hata wewe unaweza kumkamua lakini mweupe nitakuwa namkamua mimi tu". Mke akasema haiwezekani mweuupe umkamue peke yako. Hata mimi nitakuwa namkamua. Mme akasema haiwezekani umkamue ng'ombe wangu. Wakabishana mpaka wakapigana. Ndicho ninachokiona humu ndani. Watu wanatoa macho kiasi kwamba baadhi wangekuwa karibu yule aliyemtukana eti Tuntemeke Mwigamba aondoke atuachie chama, labda angeweza hata kumpiga. Tunatoleana macho utadhani Lowassa katangaza kuingia CDM na sasa tunabishana ama tumpokee ama tuache. Kumbe inawezekana jamaa hana hata mpango huo!

Jambo la pili naomba tusome tena hii nukuu hapa kama Mwandishi wa gazeti alivyomnukuu Mwigamba:

"Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,"

Kama mmesoma hayo maneno ya Mwigamba between lines, hamna sababu ya kumshambulia kiasi hicho. Hajasema kwamba leo hii inaweza kutokea tu EL akaja akaomba kuingia CDM na yeye kama mwenyekiti wa mkoa akampokea. Amesema lazima aeleze sababu za kufanya hivyo na akatumia neno la wingi "na sisi" ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama. Maneno yake yanaonyesha collective responsibility kwamba watakuwa jopo la viongozi. Watamuuliza kwamba unataka kuja CHADEMA lakini una tuhuma hizi na hizi. Wakiridhika na maelezo yake ndo wataamua kama viongozi si yeye kama mwenyekiti wa mkoa. Naomba niwaulize swali mnaotumia msuli mkubwa kupinga EL kuja CDM kwa vyovyote vile. Hivi akija na uthibitisho kwamba madudu yote yamefanywa na Mkapa na Kikwete. Yeye kafanywa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuiokoa serikali isidondoke kama alivyofanyiwa gavana wa zamani wa benki kuu Daudi Ballali, hivi akaja na ushahidi wa kile alichokitamka Mwakyembe kwamba kuna vitu walificha ili serikali isidondoke na vitu hivyo kumbe EL akafanikiwa kuonyesha kwamba ni ushahidi kwamba ufisadi wote wa Richmond ni wa JK na si wa kwake Lowassa. Hivi akija akakiri na kutubu kwa kuonyesha ushahidi wa baadhi ya vitu alivyovifanya kwa kulazimishwa na system kwa ajili ya chama na akavijutia na kuviungama na kuwaomba radhi wananchi, akasema ametoa maisha yake kama serikali itamuua kama ilivyommaliza Ballali yuko tayari ili mradi ukweli wote uwe hadharani, hivi mtakataa kumpokea awe mwanachama wa CHADEMA. Try to use your bongos badala ya kutumia misuli kupinga kila kitu kwa ushabiki.

Atapokelewa ili mradi aseme ukweli na evidence basing on your last paragraph!!!
 
Feedback, mda huu tupo kikazi zaidi,kuliondoa GAMBA CCM, na sio KULIVUA, maana lote ni GAMBA! sidhani kama tuna mda kweli wa kulijadili ni jinsi GANI lilikuwa GAMBA KAKA? ila kama walipenda GAMBA nisikukatishe tamaa, endelea nalo
uttoh hivi gamba ni Lowassa? au gamba ni system? kama gamba ni Lowassa then Lowassa akitoka CCM wote mimi na wewe turudi CCM is that Ok? Lowassa katoka madarakani tangu 2008 je ufisadi umeisha serikalini? Je, haya mdudu yanayopigiwa kelele bungeni leo yamesababishwa na Lowassa?

Mimi bado naamini kabisa Lowassa anasafishika.

Kama kuna ulazima wa kuingia chumbani, kuna njia nyingi za kutumia unaweza kupitia mlangoni au dirishani ikishindikana bomoa ukuta uingie, ingawa kuna hasara ambayo itabidi uilipe. Logical?
 
Hivi inawezekana hata tuhuma za rushwa dhidi ya EL ktk uchaguzi wa Arumeru Mashariki pia hazina ukweli?
 
Huu ni wenda wazimu...

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Arusha, Samson Mwigamba, amesema kuwa yeye yuko tayari kumpokea hata Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, endapo ataamua kufanya uamuzi wa kubadilika na kujiunga na CHADEMA.

“Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,” alisema.

Source: Tanzania Daima

My take: Nimeanza kuamini kuwa inawezekana kabisa Lowassa anaandaliwa mazingira ya kusafishwa.
 
Duh!Umesema huyo mwenyekiti anaitwa mwi-GAMBA?
 
swala la utajiri hata mbowe,mtei,ndesa ambao ni mizizi ya cdm ni matajiri wakubwa pia, kwa hiyo utajiri sio kigezo

Tatizo siyo utajiri, ishu kubwa ni njia gani ulitumia kuupata huo utajiri. lowasa ni fisadi mkuu compared to mbowe and others.....
 
Kwanza kabisa naomba niwarejeshe kwenye kaulimbiu ya JF, inasema, "The Home of Great Thinkers". Ukweli niliougundua ni kwamba tuna wana JF wengi sana humu ambao si great thinkers. Naomba nizungumzie mambo mawili tu:

Kwanza tunachofanya humu ndani ni kisa tulichosimuliwa zamani kwamba baba mmoja alikutwa na mkewe akinoa panga. Mke akamuuliza unanoa panga la nini, yeye akajibu hivi: "Ninanoa hili panga ili nikafyeke shamba halafu nilime pamba nikivuna na kuiuza nitanunua ng'ombe wawili: mweusi na mweupe. Yule mweusi hata wewe unaweza kumkamua lakini mweupe nitakuwa namkamua mimi tu". Mke akasema haiwezekani mweuupe umkamue peke yako. Hata mimi nitakuwa namkamua. Mme akasema haiwezekani umkamue ng'ombe wangu. Wakabishana mpaka wakapigana. Ndicho ninachokiona humu ndani. Watu wanatoa macho kiasi kwamba baadhi wangekuwa karibu yule aliyemtukana eti Tuntemeke Mwigamba aondoke atuachie chama, labda angeweza hata kumpiga. Tunatoleana macho utadhani Lowassa katangaza kuingia CDM na sasa tunabishana ama tumpokee ama tuache. Kumbe inawezekana jamaa hana hata mpango huo!

Jambo la pili naomba tusome tena hii nukuu hapa kama Mwandishi wa gazeti alivyomnukuu Mwigamba:

“Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,”

Kama mmesoma hayo maneno ya Mwigamba between lines, hamna sababu ya kumshambulia kiasi hicho. Hajasema kwamba leo hii inaweza kutokea tu EL akaja akaomba kuingia CDM na yeye kama mwenyekiti wa mkoa akampokea. Amesema lazima aeleze sababu za kufanya hivyo na akatumia neno la wingi "na sisi" ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama. Maneno yake yanaonyesha collective responsibility kwamba watakuwa jopo la viongozi. Watamuuliza kwamba unataka kuja CHADEMA lakini una tuhuma hizi na hizi. Wakiridhika na maelezo yake ndo wataamua kama viongozi si yeye kama mwenyekiti wa mkoa. Naomba niwaulize swali mnaotumia msuli mkubwa kupinga EL kuja CDM kwa vyovyote vile. Hivi akija na uthibitisho kwamba madudu yote yamefanywa na Mkapa na Kikwete. Yeye kafanywa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuiokoa serikali isidondoke kama alivyofanyiwa gavana wa zamani wa benki kuu Daudi Ballali, hivi akaja na ushahidi wa kile alichokitamka Mwakyembe kwamba kuna vitu walificha ili serikali isidondoke na vitu hivyo kumbe EL akafanikiwa kuonyesha kwamba ni ushahidi kwamba ufisadi wote wa Richmond ni wa JK na si wa kwake Lowassa. Hivi akija akakiri na kutubu kwa kuonyesha ushahidi wa baadhi ya vitu alivyovifanya kwa kulazimishwa na system kwa ajili ya chama na akavijutia na kuviungama na kuwaomba radhi wananchi, akasema ametoa maisha yake kama serikali itamuua kama ilivyommaliza Ballali yuko tayari ili mradi ukweli wote uwe hadharani, hivi mtakataa kumpokea awe mwanachama wa CHADEMA. Try to use your bongos badala ya kutumia misuli kupinga kila kitu kwa ushabiki.
Thanks Maskini Mkulima
 
Lowassa akitubu madhambi yake tumkaribishe chadema, kwani binadamu hasamehewi?

kutubu dhambi hili limekua kanisa? kutubu dhambi ni kanisani, akisema anatuomba radhi, tunataka na mali zetu alizoiba..kutubu peke yake kwa kiongozi wa umma hakufai, labda kama aliiba wake za watu ila kama ana mali zetu au mali zilizotengenezwa kutokana na ufisadi fulani fulani basi hana budi kutubu na kurudisha fungu.

hii ya kutubu tu halafu sawa kiendelee, hata wezi wengine ili warefushe maisha yao ya kisiasa na kulinda wakichotuibia watatubu na wenyewe na hatutakomesha huu ufisadi wa kijinga hapa tz..kila mtu ataiba akijulikana, atatubu halafu tunaendelea..ujinga...
 
A LIZARD IN AFRICA WILL NEVER BE A CAT IN EUROPE!. WATCH OUT!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

Nilikuwa napita tu nikaona niwajulie hali wana jamvi.
 
Sidhani Lowasa kama ni mchafu sana kiasi hicho kama tunavyotaka kuaminishwa, kwangu mimi kosa kubwa la Lowasa ambalo namhukumu nalo, ni kwakuwa alishiriki kwa kiasi kikubwa katika mipango ya kumweka Kikwete madarakani na huku akichafua wengine kupitia mtandao wao walioubuni enzi hizo, na Sitta akiwemo. Kuhusu suala la Richmond, jamani ifike mahali sasa na EL naye aseme hadharani Richmond alihusika vipi. M/kiti wa kikao cha baraza la Mawaziri ni Rais, sasa kuendelea kukaa kimya kwa EL ndiyo ataendelea kujichimbia kaburi. Ok ametubu kama Mwigamba alivyosema na viongozi wakapima akaja CDM na akawa mwanachama wa kawaida, je akataliwe? na wote mnaomhukumu kiasi hicho kila mtu ajitazame ni msafi kiasi gani. Kwetu sisi wakristo Biblia inatuambia kuwa hata yule mwana mpotevu baada ya kutapanya mali za baba yake, akagundua kosa, akajuta, akarudi kwa baba yake, je baba yake si alimpokea?

waafrika tunapenda sana kuoanisha dini na siasa, tukifanya hivi sasa mageuzi ya nini? si tuwasamehe tu hawa CCM wote kwani katika macho ya mungu na biblia ni watoto wake na hawajui walitendalo...kuwa makini we Noboka kama ni kijana hizi imani za kijinga achana nazo kama wewe ni mzee, sisi vijana hatugeuzi shavu la pili tukichapwa la kwanza..politics is neither spirituality nor faith, ndiyo maana hawa hawa akina Lowassa wanaweza kuua na baadae kutubu kwa mungu
 
Viongozi wa CHADEMA kama mnataka KUZOMEWA NA KUPIGWA MAWE kila mtakapoonekana, mkarisheni Lowasa!! Watanzania wengi tutajua hata nyinyi ni wachumia tumbo!! Na kama mna mpango wa kumkaribisha Lowasa tafadhali tuambieni mapema tujue mbinu mbadala na mturudishie vijimiamia vyetu maana pesa ya Mungu haichangamani na pesa ya shetani kamwe!!!

STIDE,

..Lowassa akabidhiwe kadi ya CDM baada ya kufanya yafuatayo:

1.azunguke nchi nzima na ripoti ya Tume ya Mangula, ile ambayo ilielekeza JK afukuzwe CCM.

2.azunguke nchi nzima na kuwaeleza wananchi na kuwaomba radhi kutokana na fitina na majungu yaliyowezesha wana mtandao kuingia madarakani mwaka 2005.

3.aeleze kile ambacho Dr.Mwakyembe alikificha katika ripoti ya Richmond ili kutokuiabisha serikali. aeleze nani alikuwa akimpa maelekezo na baraka za kukiuka maamuzi ya vikao na kulazimisha Richmond kupewa mkataba.

4.aeleze wahusika wa Dowans ni kina nani.

5.akubali kustaafu rasmi siasa akiwa ametubu madhambi yake kwa wa-Tanzania.
 
Back
Top Bottom