CHADEMA wako tayari kumpokea Lowassa

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Arusha, Samson Mwigamba, amesema kuwa yeye yuko tayari kumpokea hata Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, endapo ataamua kufanya uamuzi wa kubadilika na kujiunga na CHADEMA.

“Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,” alisema.

Source: Tanzania Daima

My take: Nimeanza kuamini kuwa inawezekana kabisa Lowassa anaandaliwa mazingira ya kusafishwa.
 
Mwigamba iko chama kina wenyewe iko na nikilitazama jina lako halifanani kabisa na wenyewe ndugu yangu kuwa makini sana...najua hutanielewa leo ila kuna siku utanikumbuka
 
lowassa kuamia cdm itakuwa jambo la maana sana maana ni mchapa kazi ,huwa blaa blaa hapendi na ushahidi upo.na chadema sio mtu ni chama ambapo wana simamia sera.

La pili jamaa mambo mengi anapandikiziwa kutokana na tamaa za uongozi ndani ya ccm.wamemjua kuwa ni threat kwao. Kama swala la utajiri lowassa alikuwa nao hata kabla ya uwaziri mkuu,issue ya richmond ni ya jk ila aliamua kutoa lowassa kafara ndio maana akina mwakyembe hakutaka kueleza yote.

cdm mpokee maana lowassa ni kiongozi anayetamani kuona mabadiliko .nasema hivyo kwasababu serekali ya awamu ya nne tangu jaamaa ajihuzuru hakuna kinachoendelea ni kama vile serekali iko likizo

Tunataka mabadiliko tuweke chama chenye sera za mabadiliko na ndani yake wawepo watu wanaopenda mabadiliko pia.
 
"Kumkaribisha Lowasa CDM ni sawa na kuiangamiza CDM!!"
Hivi wanachama wa kujiunga CDM watakuwa wameisha hadi kumkaribisha Lowasa!!??
Very pathetic!! Poor Mwigamba!!!
 
Hapa ndipo Chadema wataanza kukoroga RASMI, hafai hata kugombea ubalozi wa Nyumba kumi kumi chadema, anaweza waibia wananchi Mahindi yao, mwizi ni mwizi tu.
 
swala la utajiri hata mbowe,mtei,ndesa ambao ni mizizi ya cdm ni matajiri wakubwa pia, kwa hiyo utajiri sio kigezo
 
...Sidhani kama CHADEMA watakuwa tayari kufanya makosa makubwa kiasi hicho ya kumpokea fisadi EL. CCM ndio inakufa taratibu wengi wao wanatafuta pakutokea kabla magamba hakijazikwa rasmi.

Hakuna ubaya kuwapokea watakaotoka magamba lakini mafisadi wote ndani ya magamba na wala/watoa rushwa kamwe wasiruhusiwe ndani ya CHADEMA.
 
Lowasa siyo fisadi bali ccm yenyewe. Kama umesiliza michango ya wabunge jana utaligundua hilo. Kama angekuw fisadi nchi ingekuwa na maendeleo mskubwa baada ya kuondoka kwake madarakani. Kinyume chake ni kama vile kuondoka kwake kwenye u PM kumewapa nafuu akina Mkulo na wenzake.
 
Hii ndo shida ya kudandia gari kwa mbele, "LOWASA sio FISADI, ila CCM yenyewe" what is CCM? People? who is Lowasa? People? ulitakiwa kusema LOWASA sio FISADI peke yake, LOWASA NI FISADI papa, sio tu FISADI, hapana, ni FISADI wa viwango vya juu ....

Lowasa siyo fisadi bali ccm yenyewe. Kama umesiliza michango ya wabunge jana utaligundua hilo. Kama angekuw fisadi nchi ingekuwa na maendeleo mskubwa baada ya kuondoka kwake madarakani. Kinyume chake ni kama vile kuondoka kwake kwenye u PM kumewapa nafuu akina Mkulo na wenzake.
 
List of shame aliyoisoma Slaa ilikuwa na vielelezo na majina ya mafisadi papa but they are still innocent until proven guilty. Kosa kubwa ambalo Lowassa amekuwa akishikiwa bango ni umiliki wa Richmond.

Endapo Lowassa atakuja public na kuikana Richmond na kutuambia wazi ni ya nani basi nafikiri atakuwa amejisafisha kwa kiasi kikubwa, yatayobaki ni mambo madogo madogo sana ambayo binadamu yeyote anaweza kuwa nayo. Suala la yeye kuwa tajiri halina mashiko.
 
Sidhani kama kuna sababu ya kuelewa hata, LOWASA akitajwa mahali inakera hata kusome, kwa hiyo cha maana ni kumhusisha na UFISADI TU, hata kama sio relevant, SIMPLY FISADI

Umeelewa vizuri hiyo statement lakini?
 
YES, kukana kungemsaidia, ANANGOJA NINI SASA HUYU MWIZI MWENZIO?

List of shame aliyoisoma Slaa ilikuwa na vielelezo na majina ya mafisadi papa but they are still innocent until proven guilty. Kosa kubwa ambalo Lowassa amekuwa akishikiwa bango ni umiliki wa Richmond. Endapo Lowassa atakuja public na kuikana Richmond na kutuambia wazi ni ya nani basi nafikiri atakuwa amejisafisha kwa kiasi kikubwa, yatayobaki ni mambo madogo madogo sana ambayo binadamu yeyote anaweza kuwa nayo. Suala la yeye kuwa tajiri halina mashiko.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Arusha, Samson Mwigamba, amesema kuwa yeye yuko tayari kumpokea hata Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, endapo ataamua kufanya uamuzi wa kubadilika na kujiunga na CHADEMA.

“Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,” alisema.

Source: Tanzania Daima

My take: Nimeanza kuamini kuwa inawezekana kabisa Lowassa anaandaliwa mazingira ya kusafishwa. Nakujibu tu hapo kwenye my take. Kama EL ataamua kujisafisha Kwa maana ya kuachana na ufisadi sioni tatizo la yeye kutokaribishwa popote.[]
 
Viongozi wa CHADEMA kama mnataka KUZOMEWA NA KUPIGWA MAWE kila mtakapoonekana, mkarisheni Lowasa!! Watanzania wengi tutajua hata nyinyi ni wachumia tumbo!! Na kama mna mpango wa kumkaribisha Lowasa tafadhali tuambieni mapema tujue mbinu mbadala na mturudishie vijimiamia vyetu maana pesa ya Mungu haichangamani na pesa ya shetani kamwe!!!
 
YES, kukana kungemsaidia, ANANGOJA NINI SASA HUYU MWIZI MWENZIO?
Come down uttoh2002, najua wewe unasema Lowassa ni fisadi kwa vile tu umesikia wakisema, ukiambiwa tuonyeshe kafisadi nini unaweza kushindwa sana sana utasema alitajwa na Slaa, kama tukisema tuwachukie wote wanaotajwa tajwa tutagombana na wengi itamkumba hadi mkuu wa nchi. Kutaja ni kitu kimoja na ku prove ni kitu kingine, kama yeyote atakuja open kukiri na kutuambia black and white mhusika ni fulani kwanini asisamehewe?
 
Feedback, kwa hili naona umepotoka mkuu wangu!! Kama unasema Lowasa alitajwa na Dr. Slaa kwenye list of shame inakuwaje leo hii umshawishi Dr kumkaribisha Lowasa!? Achana na kivuli cha "ktk siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu," fisadi ni fisadi tu!

Feedback mara hii tu umesahau Lowasa alivoshiriki kuuwa watu hapo Arusha? Umesahau mabomu ya juzi tu hapa NMC wakati Lema amewekwa ndani kwamba lilikuwa shinikizo lake? Umesahau kwamba kamanda Lema kuvuliwa ubunge ni mpango wake wa kuibaka demokrasia? Umesahau kwamba haya madudu ya uwizi serikarini yeye ndie muhasisi wake?

Feedback!! Umesahau kwamba CDM imepata credit kubwa kupitia huyu mwizi, na sasa unatetea akaribishwe CDM ili CCM wapate credit kuiangamiza CDM!!? Who is Lowasa by the way, hadi akikosa yeye CDM haiendelei!!? Kwanini CDM? Si aende UDP na TLP huko?

Naomba wote mnaotetea Lowasa kuja CDM mnijibu:
"NIKWANINI MNADHANI LOWASA AHAMIE CDM NA SIO CCK WALA NCCR-MAGEUZI?"
 
Back
Top Bottom