CHADEMA wajiondoa kugombea ubunge - EALA

Status
Not open for further replies.
article no 50 imeweka wazi taratibu za kuchagua wawakilishi wa bunge la afrika mashariki safari hii anna makinda ataumbuka kuwa haongozi kwa kufata kanuni bali kulinda maslahi ya chama chake
 
kWANI UWIANO WA WABUNGE SASA HIVI UKOJE? Na kama watafuata uwiano huo, je CCM itapata wabunge wangapi na Upinzania watakapata wabunge wangapi. Na hao wabunge wa Upinzani je ni lazima watoke CDM au watatoka upinzani wowote kama ambavyo Bunge lilivyowahi kugeuza utaratibu wa kuwachagua wajumbe wa upinzani kwenye kamati zake ili kufurahisha chama tawala.

mkuu wabunge wa upinzani hawafiki 60 na ili waform 20% ya wabunge wote lazima wafike 70. Kwa sasa wanaform only 1% ya wabunge. Huo ndio ukweli mkuu.
 
[SIZE=31. Any question that may arise whether any person is an elected member of the Assembly or whether any seat on the Assembly is vacant [U]shall be determined by the institution of the Partner State that determines questions of the election of members of the National Assembly[/U] responsible for the election in question
[/B][/COLOR]Kwenye undeline hiyo institution ni High Court of Tanzania

Nawasilisha.

[/SIZE]

Suala hapa ni kupata ufafanuzi juu ya interpretation ya Article 50 na sio kiti cha ubunge kuwa wazi au Kama Mtu amechaguliwa kihalali. Chadema wakienda watasikilizwa tu. Article 52 is inapplicable.
 
Kama mwongozo wa EAC unasema hivyo ni dhahiri Mahakma ya Jumuia itatengua maamuzi ya Bunge letu. Hivi kwa nini tunapenda kupata aibu hivi kila wakati? CCM hakuna aliyebaki mwenye ufahamu timamu akasimama na kuelekeza wenzake?
Kweli kumbe kifo kikifika hakuna wa kukizuia. CCM iliyokuwa moja ya vyama mahiri Africa iko ICU inapumulia gas na na mtungi wa gas umebaki robo na hakuna ziada.


kina January Makamba wansojifanya MaLiberals hara hili dogo kiasi hiki wameshindwa kukishauri chama chao na hayo nahafidhina yanayoendelea kuishi ktk karne ya 3.

Asiyeona husubiri kuonyeshwa. sidhani kama hii ilihitaji msomi wa PhD kuishauri ccm. Tabia ya namna hii ya defensive and protective politics ndiyo iloua vyama vingi vya kihafidhina barani Afrika.

tambueni kwamba kama nchi hatuwezi kuendelea kamwe kama hatutaruhusu mawazo tofauti kutupa changamoto za dhati. kumbukeni ni vigumu kukaa kwenye confortable zone alafu ukategemea kuendelea. Sasa subitini muone aibu itakayowakuta

Najua mnajidanya kwa kufanya reference kwenye hukumu ya tarehe 31 Machi 2007 iliyotengua ubunge ea wabunge 9 wa Kenya kwenye bunge la EaC lililopita na Kenya kulazimika kuchagua tena. katk hukumu Tz ilisifiwa kwa kuwa na utaratibu wa kuchagua wabunge wa bunge la EAC, lakini tambueni mazingira yamebadilika sana. lkn muhm kuwa na kanuni ni jambo moja na kanun hizo kuwa za haki kadri ya maelekezo ya mkataba wa EAC ni jambo jkngine.

haoa mabishano yapo jambo moja muhimu. Ni kwa kiasi kanuni zilizopo zinatoa nafasi na haki kwa wanostahili kiipata kwa upande mmoja, na kwa kiasi gani kanuni hizi zinatumoka vibaya kutoa haki kwa wasiyostahili na kuminya haki ya eanostahili kwa upande mwingine.nadhani hapa ndipo busara ya sheria itakapojikita.

Aingii akilini kuona chama chenye wabunge 48 na maana hii kinachoongoza official opposition bungeni kikose mwakilishi kwenye bunge la EAC huku chama ambacho hakina Mbunge hata moja ndani mbunge la Ranzania wala zbar ndicho kitoe mwakilishi.

kwa utaratibu uliyopo kana hauvadilishwi hicho nilichokisema hapo juu kinawezekana kutokea bila shaka. kwa nazingira ya kisiasa yaliyopo kati ya ccm na CDM hii ni lazima itokee ( siyo kamali) ni 100% sure.

Naamini watu wengi wamesihi ccm kutumia busara kuamua hili badala ya husia na husuda za kisiasa zisizo na tija kwa taifa, lakini kama walivyoozea hawakusikia. Aibu siku zote umkuta mjinga.

Haya yaliewezekana miaka iliyopita lakini kwa kizazi hiki hayatawezekana. Tujisahihishe
 
kwani idadi ya wabunge wote wa upinzani hawafiki 70 ili kuwawezesha kupata 20% ili wapate wabunge

Hiyo habari ya wabunge wa upinzania hawafiki 70 umeipata wapi? Una uhakika nayo? Umekuwa hata mvivu kwenda tovuti ya bunge kupata idadi kamili.
 
Najua mnajidanya kwa kufanya reference kwenye hukumu ya tarehe 31 Machi 2007 iliyotengua ubunge ea wabunge 9 wa Kenya kwenye bunge la EaC lililopita na Kenya kulazimika kuchagua tena.

Umechemka Mkuu. Hukumu ambayo inaweza kutumika kwenye kesi ya Chadema ni ile iliyotolewa dhidi ya Uganda mwaka jana. Case No. 6 of 2011. Katufute hiyo then isome.
 
Umechemka Mkuu. Hukumu ambayo inaweza kutumika kwenye kesi ya Chadema ni ile iliyotolewa dhidi ya Uganda mwaka jana. Case No. 6 of 2011. Katufute hiyo then isome.
Kesi ya CDM imeshachelewa mkuu, hakutakuwa na injuction kama Uganda, bali kutakuwa (if any) na kutengua matokeo.
Ukweli ni kwamba, kwa Tanzania tuna proportionality based on sex,part of the union na party affilliation.Sasa CDM wamebase kwenye party affiliation as the only category, which is flimsy.
Mbona CUF wana mgombea nafasi ya wanawake?... kwanini CDM hawajamsimamisha mgombea upande wa wanawake?
Upande wa Zanzibar kuna wajumbe watatu pia. Na huko mkitaka mnaweza kusimamisha mgombea.
Halafu kutakuwa na nafasi nne zilizobakia, kwa sababu mgombea mmoja wa wanawake anatakiwa kutokea Zanzibar.
asilimia 75 ya nne ni Tatu, kwahiyo tatu CCM moja UPINZANI.
 
mkuu wabunge wa upinzani hawafiki 60 na ili waform 20% ya wabunge wote lazima wafike 70. Kwa sasa wanaform only 1% ya wabunge. Huo ndio ukweli mkuu.

Usitumie sana nguvu kutetea kitu ambacho hakina ukweli, nenda hapa: Parliament of Tanzania

Utapata takwimu sahihi za wabunge pote. Kwa kukusaidia tu mgawanyo wa wabunge uko ifuatavyo:

Wabunge wote ni 347
CCM - 259
CHADEMA - 48
CUF - 35
NCCR - 4
TLP - 1
UDP - 1
 
Hiyo habari ya wabunge wa upinzania hawafiki 70 umeipata wapi? Una uhakika nayo? Umekuwa hata mvivu kwenda tovuti ya bunge kupata idadi kamili.

sheria ikitafsiriwa kisiasa inakua mbaya sana...... na hii ni changamoto kwa wanasheria kuwa wakali pale wanasiasa wanapowatumia wanasheria kutekeleza adhma zao
 
Kesi ya CDM imeshachelewa mkuu, hakutakuwa na injuction kama Uganda, bali kutakuwa (if any) na kutengua matokeo.
Ukweli ni kwamba, kwa Tanzania tuna proportionality based on sex,part of the union na party affilliation.Sasa CDM wamebase kwenye party affiliation as the only category, which is flimsy.
Mbona CUF wana mgombea nafasi ya wanawake?... kwanini CDM hawajamsimamisha mgombea upande wa wanawake?
Upande wa Zanzibar kuna wajumbe watatu pia. Na huko mkitaka mnaweza kusimamisha mgombea.
Halafu kutakuwa na nafasi nne zilizobakia, kwa sababu mgombea mmoja wa wanawake anatakiwa kutokea Zanzibar.
asilimia 75 ya nne ni Tatu, kwahiyo tatu CCM moja UPINZANI.

Unaposema kesi ya CDM imeshachelewa una maana gani?
Kwani deadline ya ku-submit injunction ilikuwa lini?
Kwani tayari uchaguzi umeshafanyika?
 
CDM kikiwa chama kinachoungwa mkono na idadi kubwa ya vijana ktk Tanzania,kinaweza dharauliwa na watawala wajinga ndani ya CCM lakini siyo viongozi wa serikali za nchi jirani na Tanzania ktk ushirikiano wa EAC. Toka juzi nimetabiri kwamba watawala wapya wa Tanzania baada ya CCM wataikataa mikataba ya kimangungo yote itakayofanywa na watawala wa sasa!
 
Spika makinda ni mbumbumbu na hana ufahamu wa mambo mengi sana.ye anaongoza bunge as if anaongoza kamati ya kitchen party ya binti yake!! Nchi hii bwana,rais bomu,spika bomu ,pm ndo mautumbo ya bata mwanzo mwisho !!
 
wakuu, kama kawaida, spika ana makinda amekataa mapendekezo yote yaliyopelekwa na wapinzani pursuant to EAC charter kuwa wabunge huchaguliwa kwa uwianao toka bunge la nchi husika. ameshilikia msimamo kuwa ni lazima wabunge 8 watoke ccm na wapinzani kiti kimoja. chadema ili kulinda charte ta EAC, na demokrasia katika ukanda huu wameamua rasmi kujitoa kwenye kinyanganyiro hicho. sasa wanakimbilia kwenye mahakama ya afrika mashariki kutafuta haki


Kwa maoni yangu kwa uamuzi huu CHADEMA wamefanya la maana sana. Utaingiaje kwenye uchaguzi ambao hakuna uwezekano wa kushinda kabisa na ambao umejaa usanii mtupu na rushwa ya kutisha. Hongereni CHADEMA kwa maamuzi ya busara.

:peace::peace::peace:


Alutta Continua
 
mkuu wabunge wa upinzani hawafiki 60 na ili waform 20% ya wabunge wote lazima wafike 70. Kwa sasa wanaform only 1% ya wabunge. Huo ndio ukweli mkuu.

Idadi ya wabunge wa upinzani:
CHADEMA 49 + NCCR 4+ UDP 1+ TLP 1+ CUF (wakuchaguliwa 25, wakuteuliwa ...) tiyari hesabu zinafika wabunge 81 + wakuteuliwa wa CUF. Pumbavu zako unamdanganya nani hapa? Kilaza wewe.
 
Kuna watu wana ushabiki wa kijinga kabisa, cjui ni tatizo la kukulia Chai ya rangi na urojo? :yell:. Walichofanya CHADEMA ni sahihi kabisa. Maadam wameona hawatendewi haki, wameamua kuitafuta. Je mnafikiri hizi Mahakama ziliwekwa za nini? Mnapochangia mambo ya msingi muwe mna busara. :nod:

Speaker wote tunaelewa namna alivyochaguliwa, sasa mkiishangaa maamuzi kama hayo basi hamjui historia yake vizuri. Naendelea kuomba duah, wamalize kipindi chao. Katika historia ya nchi hii, tangu bunge la Uingereza huyu spika ninampa maksi za chini kabisa.:disapointed:

Ila matatizo mengi tutayatatua wenyewe 2015. :heh: Hatuwezi kuruhusu watu ambao wameacha wazazi wamekufa kwenye mgomo wa madakatari bila kutoa tamko lolote:shock: Mikopo wanapewa watoto wa vigogo tu:shock: Nchi haina falsafa, hatujui sisi wajamaa, au sisi wabepari?:disapointed: nchi haina sera za kitaifa:disapointed:nchi nusu ya mapato yetu wanatumia vigogo kwa ajili ya matembezi yao:shock:

CHADEMA nawaunga mkono, This is political maturity:)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
CDM Wameona wanapigwa chini!na hilo wanalijua mapema wanapoteza muda kama kawaida yao wasiopenda kushndwa wataleta kigezo kingne wakishndwa mahakama hajatundea haki!mbona MBOWE HAjawatendea haki wabunge 9 kampitisha mchaga mwenzake kimabavu tuambien katumia sheria gan?mbona hatujahoji hii au baada ya waraka wake wakibaguz aliowapeleka wbunge wanaotoka kaskazin wa CCM kuukataa?tujaribu kuhoji sio kila kitu kumeza,KWELI NAKUBALIANA NA KAURI HII VIJANA NA UMBUMBU WA UELEWA!
 
spika anaonyesha waz kuipendelea serikali na ccm, so my decition haina haja CDM ya kuhangaika kwenda mahakamani achaneni nao. achen watape now coz mwisho wao umekaribia....!!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom