CHADEMA waige taiba ya kinyonga

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Chadema wanapaswa kusoma ishara za nyakati na kubadilika kutokana na hali inavyokwenda kwa kuendesha shughuli na mikutano kwa utaratibu na sheria. Kuna mambo kadhaa ambayo wapinzani wao wanajua udhaifu wa Chadema ikiwa ni pamoja na force pale inapotokea kugonga kisiki. Kwa mwendo huu kama hakuna kubadilika ipo wakati viongozi wote kuanzia taifa watashtukia wako jela. Kwa sasa uangalifu wa hali ya juu lazima uwepo, na kunapotokea kisingizio cha kusitisha mikutano, bora kufuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja vyombo vya sheria kama mahakama kupelele malalamiko yao ya kusitishiwa mikutano dakika za majeruhi wakati maandalizi yamekamilika. They must be flexable.


 
people's power kwa hapa ndio suluhisho... Hakuna njia mbadala zaidi ya hapo..

Kuwa makini ni muhimu sana, vinginevyo kila kukicha watashtukia wanajikwaa visiki, nini tatizo? Wenzao wanajua njia ya kuwadhoofisha, busara pamoja na ustahimilifu ni njia pekee ya kujenga chama, force can work, but some time not.
 
Ushauri mzuri!! Lakini nyakati hizi watu wanaona, na zisiki ndiyo vinawapa nguvu CDM ya kuendelea kupendwa, wakati mwingine visiki hupangwa ili ionekane hivyo, na ndiyo njia mojawapo ya kujenga chama. Ni maoni tu!
 
Ushauri mzuri!! Lakini nyakati hizi watu wanaona, na zisiki ndiyo vinawapa nguvu CDM ya kuendelea kupendwa, wakati mwingine visiki hupangwa ili ionekane hivyo, na ndiyo njia mojawapo ya kujenga chama. Ni maoni tu!

Ni dhahiri visiki hivi huwekwa kwa makusudi, lakini kama una macho na akili yako timamu unaweza kukikwepa kisiki usijikwae, vinginevyo ukijiruhusu kukwaa kisiki unachokiona unayeumea ni wewe, lazama kuwa makini.
 
Yeah..na pia waache kuoa wake za watu. Halafu wale Senior Bachelorz waoe na kuolewa!
 
Yeah..na pia waache kuoa wake za watu. Halafu wale Senior Bachelorz waoe na kuolewa!

Nilifikiri ungesema vigogo wa Serikalini na CCM waache kuchukua wake za watu kama ilivyotokea kule Igunga?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom