Chadema Wafanye Mkutano mkubwa Dar Haraka maana karibia wakamatwe

Sio WA TZ wote ni CHADEMA au CCM!!! hatutaki nhi yetu iingie ktk mahafuko au vita vya wenyewe kwa wenyewe! tunajua hawa vigogo wote vyama vya kisiasa wana makazi yao Ulaya au Amerika! wanataka tuanze kuuwana wenyewe kwa wenyewe halafu wao wakimbilie nchi za nje!!! sijui ni kwa nini wanajenga chuki na uhasama miongoni mwa wqananchi!! na wengine hata aibu hawana juzi tu wameenda kuzuru kaburi la Mwalimu Nyerere na baada ya hapo wanazunguka kona hadi kona kueneza chuki!!!

Sasa tunasema inatosha! hatuwezi kuendelea kutazama baadhi ya Watu wachache wenye uchu wa madaraka wakiendelea kuharibu nchi yetu!!!
 
We, Majimshindo.
Mtu wa ajabu kweli. Unafurahia umeme kukatwa hovyo, bei za umemem kupandishwa 'beyond' uwezo wa walahoi, kuwalipa makampuni hewa hela zetu na maufisadi mengine, asipite mtu wa kujitolea kuwaambia wananchi amkeni kuuliza kulikoni? Weewe ndugu hutaki watu wajue tunapelekeshwa miaka 50 tuna rasilmali kibao lakini bado twabaki mkia wa maskini wa dunia. Aisee futa kauli yako

Huna hoja.

Umeme kukatwa hovyo si makos aliyorithi kikwete toka kwa Nyerere, Mwinyi, Mkapa. Na ni yeye Kikwete ndie anayapatia ufumbuzi wa kudumu au hulijuwi hilo?

Nani mwenye umeme Tanzania ambae hawezi kuulipia?

Huna hoja, unakurupuka.

Wewe una fikiri hii leo akiingia Silaa ndio atatatua matatizo yote?

Leo hii nenda Merekani, kuna wanaolala nje, wasio hata na nyumba za kujisitiri, kuna idadi kubwa ya wasiojuwa kuandika na kusoma. Na Merekani ni nchi Tajiri duniani. Iweje watu wasiwe na pakukaa? Iweje leo wakati wa kikwete na mema yote ayafanyao iwe mwao.

JK ndie wa kwanza mwenye kilomita nyingi za barabara za lami kuliko awamu yeyote ile.

Mwenye mashule ya sekondari mengi kuliko awamu yeyote ile.

Mwenye ma University mengi kuliko awamu yeyote ile.

Mwenye shule za ufundi (veta) nyingi kuliko awamu yeyote ile.

Mwenye kufichua mafisadi na kuwapeleka mahakamani kuliko awamu yeyote ile.

Mwenye kuondoa urasimu maofisi ya serikali kuliko awamu yeyote ile, kumbuka, mpaka mkapa anaondoka ilikuwa inakuchukuwa muda gani kupata pasipoti kama hujahonga? Forever.

Mwenye kuwafunguwa mdomo upinzani wakaweza kusema yote wayasemayo kuliko awamu yoyote ile.

Leo Rais kama huyo amekuwa hafai?

Duhh, mnashangaza sana.
 
Kwa vile dalilizote zinaonesha kuwa serikali ina lengo la kuwakamata Chadema kwa uhaini, ni vizuri wafanye mkutano mkubwa Dar es Salaam, wahamasishe peoples power ili pindi tu akikamatwa kiongozi yeyote wa Chadema, maandamano yaanzie hapohapo, vilevile naona serikali ya ccm inajiyafutia kifo chake yenyewe. Kwani Chadema hawajafanya uhaini wowote, wanachokiongea ni cha kawaida kabisa, sasa uhaini umetoka wapi? Hali ni mbaya kila mtu anaona. kwa hiyo ni dhambi kusema na kuwaeleza watanzania kuwa hali ni mbaya? Kwa nini watu hawataki kukosolewa? Anayesema hivyo nadhani hajaudhuria mkutano hata mmoja wa CDM. Mie sijaona baya lolote.

Sasa peoples powerrr iko hivi, mkijidanganya mkawakamata CDM, tunaanzia hapo kuingia barabarani nchi nzima. Naomba ufanywe nkutano mkubwa Dar fasta maana mambo yote yanaweza kuanzia hapo. Serikali muache vitisho ....... sasa wakamateni CDM muone .................cha .........moto.

Wajaribu kuwakamata....! then itakuwa ndio mwisho wa KJ
 
unayesema wakamatwe jiulize wamevunja katiba? wamesababisha machafuko? wametumia nguvu kuendesha mikutano? wameimba taarabu jukwaani kama wao? au wanajadili maisha ya kila siku ya mtanzania.
Upinzani wa sasa tanzania unaturidishia maisha yetu yaliyoporwa na wachache.hata wasipoingia madarakani Watawala watakuwa katika mstari watanazania tunaotegemea.
 
kuna quote moja kwenye gazeti la mtanzania la leo ni nzuri sana (iko kwenye ukurasa wa mbele)nikilipata nitaanzisha thread. ok by the way kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake,hivyo basi kwa kuwakamata viongozi wa chadema kutachochoa machafuko zaidi na kusababisha vurugu zisizo na maana,kwa kuwa chadema wanaongelea hali halisi ya watanzania kwa nini viongozi wetu wanakwepa hoja na kujaribu kukemea na kukurupuka.

Ile quote inasema "Heri vita inayodai haki na usawa kuliko amani inayopumbaza....." kuna maneno nimeyasahau hapo kwa mbele
 
Sio WA TZ wote ni CHADEMA au CCM!!! hatutaki nhi yetu iingie ktk mahafuko au vita vya wenyewe kwa wenyewe! tunajua hawa vigogo wote vyama vya kisiasa wana makazi yao Ulaya au Amerika! wanataka tuanze kuuwana wenyewe kwa wenyewe halafu wao wakimbilie nchi za nje!!! sijui ni kwa nini wanajenga chuki na uhasama miongoni mwa wqananchi!! na wengine hata aibu hawana juzi tu wameenda kuzuru kaburi la Mwalimu Nyerere na baada ya hapo wanazunguka kona hadi kona kueneza chuki!!!

Sasa tunasema inatosha! hatuwezi kuendelea kutazama baadhi ya Watu wachache wenye uchu wa madaraka wakiendelea kuharibu nchi yetu!!!

Jifunze kwanza kuandika ndo ulete pumba zako hapa. Kwanza nyie mnao shiba ndio hamtaki mabaliko manake mnajua mmekwisha sisi wachimba chumvi tunataka mabaliko, ili tuwe sawa. We na baba yako fisadi subirini mtakiona cha moto
 
Wenye upungufu wa akili wako wengi... Kati ya hayo uliyoyasema lipi lililosaidia kupunguza mfumuko wa bei, ukali wa maisha, ufisadi? Mbona serikali yake inaishi maisha ya kitajiri wakati sisi tunakufa na umaskini?
 
Huyo Majimshindo labda si Mtanzania mwenzetu ndio maana anatoa mawazo yanayotia kinyaa, Atakuwa Murundi tu huyu.
 
Ningekuwa mie ni sisiem ningefuatilia hayo yote yanayodaiwa na chadema na kisha kuanza kuyafanyia kazi maramoja. Hii ingekata munkali wa cdm maana wangekosa cha kuandamana. Ieleweke kuwa nyani haoni kundule kwa hiyo hii ingekuwa golden chance kwa ssm kuona mapungufu yake na kisha kuyafanyia kazi.
Mie nadhani hii ingekuwa ndo njia muafaka kwa sababu yoooote yanayodaiwa na cdm yanatekelezeka japo si kwa wakati mmoja. Hivyo ccm wangeanza na yale ya muhimu (low hanging fruits) na kuyashughulikia haraka iwezekanavyo.
 
Kazi ya chama cha siasa cha upinzani ni ipi? Imeshaelezwa hapo juu, hatuhitaji vyama vya siasa vya msimu. CDM wanatimiza kazi ya chama chochote cha siasa, tatizo tu ni mazoea (ambayo hujenga taratibu na kanuni yasipoangaliwa mapema). Pia amani inayovunjwa ni ya nani? Kama ni ya wananchi mbona ndo wanaandamana bila fujo wala uvunjifu wowote wa amani? Au ni ya viongozi waliopo madarakani? Nadhani si vema kutumia kigezo (kisingizio cha uvunjifu wa amani) kuziba mianya na haki za raia kujua mambo ya msingi yanayowakabili katika maisha yao.
MAANDANO ni nini haswa maana yake kwa tafsiri ya sheria za TZ?
 
Sio WA TZ wote ni CHADEMA au CCM!!! hatutaki nhi yetu iingie ktk mahafuko au vita vya wenyewe kwa wenyewe! tunajua hawa vigogo wote vyama vya kisiasa wana makazi yao Ulaya au Amerika! wanataka tuanze kuuwana wenyewe kwa wenyewe halafu wao wakimbilie nchi za nje!!! sijui ni kwa nini wanajenga chuki na uhasama miongoni mwa wqananchi!! na wengine hata aibu hawana juzi tu wameenda kuzuru kaburi la Mwalimu Nyerere na baada ya hapo wanazunguka kona hadi kona kueneza chuki!!!

Sasa tunasema inatosha! hatuwezi kuendelea kutazama baadhi ya Watu wachache wenye uchu wa madaraka wakiendelea kuharibu nchi yetu!!!

Humdanganyi mtu yeyote na vitisho vyako uchwara hivyo. Mmezoea kuwanyonya wananchi leo wanaamshwa mnaanza kulialia. Na kama machafuko mnayataka wenyewe.

Nchi inatakiwa iongozwe kwa manufaa ya watanzania na si ya familia zenu tu. Na mtatoka tu cos historia inawafunza adabu wote wanaokiuka masharti na matakwa ya uongozi wa nchi.
 
Mbona serikali yake inaishi maisha ya kitajiri wakati sisi tunakufa na umaskini?

Fanya kazi kwa bidii utafanikiwa, mbona akina Mbowe,Mtei na Ndesamburo wanaishi maisha mazuri chini ya CCM? siri ni kujituma na si kukalia politiki tu? mbona hao wanaojifanya wanawapenda sijawahi kusikia wakiawaambia jinsi walivyofikia umilionea, muulizen Mbowe amewezaje? wakati CCM inatawala yeye anapata utajiri mkubwa na kwa nini ninyi hamuhamasishwi kufanya kazi kwenye mikutano yao? Tafakari Chukua Hatua!!!
 
..Muda wa majungu ya siasa umepita sasa tutumie majungu ya kisayansi kuijenga nchi na kuaibisha madhalimu. kwa mfano tufanye liwezalo kumsahuri rais katika kupata wakurugenzi wa idara nyeti kwa kutumia misingi ya kitaalamu na siyo kisiasa kama kiongozi wa TAKUKURU, Usalama wa Taifa (CID), Tume ya mipango, tume ya haki za binadamu, tume ya uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa nk pia kuondoa taasisi zisizokua na sababu ya kuwepo yaani zinazofanya kazi zinazoingiliana kama mkukuta, mkurabita nk. pia kwa maslahi ya nchi katika kupanga muundo wa serikali, muundo wa mahakama. Haya yote ni hujuma kwa madhalimu na mwisho wake ni kuwadhalilisha bila kujali wanatokea chama gani cha kisiasa maana wanasiasa wote lao sawa ila mipango ndiyo tofauti.

Kuna wakati napata matumaini ya ukombozi lakini nikisoma post kama hii naona safari yetu bado sana!
- Chadema imshauri Kikwete kupata wakurugenzi........
- Usalama wa Taifa (CID)...
- Majungu ya kisayansi....
- CCM ishauriwe ili iondoe taasisi zisizokuwa na sababu...
- CCM ishauriwe kupanga muundo wa serikali

Haya wanachadema pokeeni ushauri wa bure mmepewa na Mabulangati!
 
Wewe naona ni wale wale, Chama cha siasa chochote makini kama kilivyo CDM ni kuhuhubiri siasa. Kwa chama cha cha upinzani kazi yake kubwa ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani. Siyo kazi ya upinzani kuisifia serikali iliyoko madarakani.

Ili uongee na wanachama huwezi kuwafuata mmoja mmoja nyumbani, ni lazima uwakusanye, uwahamasishe na uwaeleze madhaifu ya serikali iliyoko madarakani. Taabu chama tawala kilizoea siasa za wakati wa uchaguzi tu, kinaachwa kipindi chote hiki kinafanya kinavyotaka. Uwajibikaji kwa waajiri wao - yaani wananchi unakuwa hakuna.

Siasa ni kuvumiliana, na hasa kwa chama kilichoko madarakani lazima wakubali kukosolewa na yule anayewakosoa asionekane kama mhaini, kwanza anawasaidia kujirekebasha.

Hayati Mwl Nyerere aliwahi kusema enzi za uhai wake kwamba: Vyama vya Upinzani ni VIOO vya ccm. Inajiangalia kupitia ukosoaji na kutumia muda huo kujirekebisha.

Vyama vya upinnzani ni sawa na mcheza mpira aliyeko Benchi. Ukivurunda tu unaona mtu "ana-troti",(anapiga jaramba), ndivyo CDM wanavyofanya, cha msingi ccm wakaze buti kutatua kero za msingi za waTZ, wanaweza wakacheza hadi dk ya 90. Vinginevyo wachezaji wa akiba tunao wengi, na pengine ni wazuri kuliko waliomo uwanjani kwa sasa.

Nilitegemea leo hii CCM wameshaanza kufanyia kazi yale yote wanayoelezwa, tunafedha nyingi sana zinatoka kwenye Madini na Mbuga za Wanyama Ukikaa pale Getini Ukahesabu magari yanayopita kuingia Ngorongoro kwa siku unaweza zimia pale uatakapo sikia mahesabu yanayotolewa, kama kungekuwa na ukusanyaji mzuri wa fedha na fedha hizi zikafika kwenye huduma za jamii leo hii Tanzania usingekuta Mwanafunzi asiye na computer darasani. HOspital isiyo na Kitanda na watumishi wangekuwa wakutosha. Ni hofu yangu kuwa hizi fedha zinachukuliwa na viongozi wachache walioko madarakani kwa kuwatumia watunza fedha wa mahalia na wanazi channel sehemu nyingine. Hii inawapa taabu sana kwani wanajaribu kufikiria ili kutimiza haya mahitaji ya wananchi lazima kusitisha wizi sasa tufanyeje? Chama tunataka kibaki madarakani na pesa tunazitaka, suluhisho wanalolichukua haraka ni kuwatisha wananchi na kujaribu kuwagawa wananchi kwa njia zozote iwe dini na ukabila ilimradi iwe rahisi kutawala. Haya matisho ndo yalisababisha watu wengi hawakupiga kura. CCm mnatakiwa kujua kuwa hivi sasa Watanzania wameshapevuka kwenye Ulingo wa Siasa na kamwe hamtatudanganya na hili vugu vugu halitasimama hadi pale mtakapo wacha kuchumia matumbo yenu na kuwahudumia wananchi. KWA TAARIFA YAKO WATANZANIA HATUANGALII CHAMA ILA WATENDAJI, HILO MJUE! HIvyo mnanafasi ya kubaki madarakani kama mtawajibika tu. Aluta Continuo.............Mapambano yanaendelea!!!!!!!!!!!!!!
 
Majimshindo nakubaliana na ushauri wako in a sataric way. Ni mzuri unaweza kufast track the process ya ukombozi wa Tanzania. Know what... Hivi unafikiri ule umati uliandamana kila CDM walikoandamana ni wajinga? Wajaribu waone. Chiligati karudi, sijui amefikia wapi na lile la kutoa hoja ya kuwafukuza CDM bungeni. Maana alituahidi kuwa wanajipanga kufanya hilo baada ya Wabunge wa CDM kutoka bungeni Jk alipohutubia
 
Mpaka sasa sijaona mtu wa Dar anayeweza kuandamana kisa kiongozi fulani kakamatwa Arusha sawa sababu mnazijua. Kingine sioni chadema inachofanya katika maandamano kama kafulila alivyosema serikali inaifagilia chadema bure. chadema wanachojua ni lawama, dowans, epa na kutafuta kuonewa huruma, nasema hivi kwa kuwa sijawahisikia wakihamasisha watu kufanya kazi, wakihamasisha vijana kupambana na uhalifu hasa wanapokua wameajiriwa sehemu yoyote bila kujali itikadi zao, vijana kuungana kuikomboa nchi kutoka utumwani.

CHADEMA wajipange upya waje na new strategies za kupambana na malaghai yanayoiangamiza nchi yetu. Strategy ya kucheza na hisia za watanzania zinaanza kuwachosha watu na kuwafanya ccm wawe sugu. Waje na mbinu nyingine kuaibisha madhalimu. Mfano mzuri ni kutumia fedha wazotumia kwa maandamano kutunisha mifuko ya maendeleo katika majimbo yao kama walivyoanza Mh. Lema na baadhi ya wabunge wengine.

Muda wa majungu ya siasa umepita sasa tutumie majungu ya kisayansi kuijenga nchi na kuaibisha madhalimu. kwa mfano tufanye liwezalo kumsahuri rais katika kupata wakurugenzi wa idara nyeti kwa kutumia misingi ya kitaalamu na siyo kisiasa kama kiongozi wa TAKUKURU, Usalama wa Taifa (CID), Tume ya mipango, tume ya haki za binadamu, tume ya uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa nk pia kuondoa taasisi zisizokua na sababu ya kuwepo yaani zinazofanya kazi zinazoingiliana kama mkukuta, mkurabita nk. pia kwa maslahi ya nchi katika kupanga muundo wa serikali, muundo wa mahakama. Haya yote ni hujuma kwa madhalimu na mwisho wake ni kuwadhalilisha bila kujali wanatokea chama gani cha kisiasa maana wanasiasa wote lao sawa ila mipango ndiyo tofauti.

Wewe sasa si uhamasishe kazi kwa vijana! kwani ni kazi ya cdm pekee. mbona ww hupiga ufisadi! idiot
 
Dar ni sehemu yenye siasa za kinafiki sana, siwatukani wakazi wa Dar ila ukweli ni kwamba ni vigeugeu hata ndani ya sanduku la kura,
Kuna jirani aliwahi kuniambia ukitaka kupigwa kubali kuwa wakala wa CUF kwenye uchaguzi lazma utaambiwa umeuza kura kumbe wana CUF wenyewe (Mbagala na Temeke) wakiingia ndani hawawapigii kura watu wao.

Hamshangai CUF hawajai kuwa na mbunge Dar, Dar is all about CCM VOTERS hasa kwa wanaojiita wazawa, ubungo na Kawe kuna upinzani kwa kuwa kuna wahamiaji wengi wa miaka ya karibuni.

STATERGICALLY DAR SIO MAHALI PA CDM wala CUF kuwekeza nguvu nyingi.
kwa taarifa yako ndugu kura za urais na ubunge kwa dar byingi zilienda upinzani (zaidi ya 50%) ila tatizo zilikuwa ni mgawanyo kati ya cdm na kafu
 
Dar ni sehemu yenye siasa za kinafiki sana, siwatukani wakazi wa Dar ila ukweli ni kwamba ni vigeugeu hata ndani ya sanduku la kura,
Kuna jirani aliwahi kuniambia ukitaka kupigwa kubali kuwa wakala wa CUF kwenye uchaguzi lazma utaambiwa umeuza kura kumbe wana CUF wenyewe (Mbagala na Temeke) wakiingia ndani hawawapigii kura watu wao.

Hamshangai CUF hawajai kuwa na mbunge Dar, Dar is all about CCM VOTERS hasa kwa wanaojiita wazawa, ubungo na Kawe kuna upinzani kwa kuwa kuna wahamiaji wengi wa miaka ya karibuni.

STATERGICALLY DAR SIO MAHALI PA CDM wala CUF kuwekeza nguvu nyingi.

Mkuu umemsahau mbunge Frank Magoba wa Kigamboni kupitia CUF? Na analysis yako sio ya kweli, mwaka jana Mpendazoe asingechakachuliwe kura zake na msimamizi wa uchaguzi Fwime angekuwa mbunge kupitia CHADEMA! Wafuasi hususani wa CHADEMA na CUF wako wengi sana DAR!
 
Back
Top Bottom