CHADEMA waelezea kilichotokea siku ya tukio la kuuwawa kwa Daudi Mwangosi

Nilitegemea kusikia jipya,bado maswali yangu hayajapata jibu sahihi kuhusu maelezo kuwa marehemu aliwafuata polisi na nini ilikuwa dhamira yake,ukiondoa askari mmoja je kuna mwananchi mwengine aliyejeruhiwa katika purukushani hiyo?. Inaonekana pande zote zilizohusika(CDM+POLISI) katka tukio hazikuwa na nia njema na sasa hivi nafsi zao zinajuta na kuanza kutupiana mpira.
nimekuwa nikisoma post zako na kugundua huwa hazina mashiko..una uliza maswali ambayo hata mtoto wa darasa la pili hawezi kuuliza..
 
nimekuwa nikisoma post zako na kugundua huwa hazina mashiko..una uliza maswali ambayo hata mtoto wa darasa la pili hawezi kuuliza..

Sasa wewe wa darasa la nne B si ujibu unachofahamu au na wewe ni mzungu wa reli?
 
Damu ya mtu huwa haipotei bure na chozi la yule mama pale juu ya kaburi la mumewe litwatesa wengi,na wamesahau kwamba huwa malipo ni hapa hapa duniani!Walikuwepo wengi na wakafa kwa aibu kama akina Mobutu,Sadam,
 
Hapo kwenye RED, ni swali zito sana na la msingi pia.

Mzee tendwa amefilisika kibusara hana hata uwezo wa kujisikiliza ukiona hivyo ujue tumefika pabaya swali alifikaje hapo kwa sababu kwa maneno yake haya na mengine aliyowahi kuyasema inadhihirisha wazi kwamba he is not of right mental capacity shem on him cant he afford any sense of objectivity? Tunamwitaje mtu kama yeye ni msaliti wa umma wa watanzania au ni mjinga. Tendwa na office yake ni sehemu ya matatizo tulionayo kama jamii
 
Benson Singo Masalamakali Kigaila,mkuu wa oparesheni ya M4C akiongea na waandishi leo Iringa


Ikiwa ni siku tano zimepita toka kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa channel ten na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Iringa Daudi mwangosi katika vurugu baina ya polisi na CHADEMA huko nyororo mafinga.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kupitia viongozi wake Iringa wameongea na waandishi wa habari kuhusu kile kilichotokea.
Akiongea na waandishi wa habari Iringa leo Mkurugenzi wa mafunzo na operesheni ya Movement For Change Taifa Benson kigaila, ameeleza kuwa lengo kubwa la Chadema tarehe 2.09.2012 kule Nyororo walikuwa na lengo la kufungua matawi na kufanya vikao vya ndani na wanachama wao na sio kufanya mikutano ya hadhara kama inavyosemekana.
Aliendelea kuleleza kuwa wakiwa katika ufunguzi wa tawi katika ofis ya kata Nyororo Polisi wafika na kutangaza kuwa watawanyike na wakamueleza RCO kuwa wapo kwaajili ya kufungua tawi na kufanya kikao cha ndani na kwamba polisi wakiingilia ndio watakao kuwa wanachochea vurugu.
Aidha Kigaila ameongeza kuwa wakati huo huo wakifungua Tawi hilo vyama vingine kama CCM nchi nzima walikuwa wakifanya chaguzi katika ngazi za Wilaya lakini hawakuzuiwa kwa kile kinasemwa kuwa ni kuingilia zoezi la sensa.
Baada ya kufanikiwa kufungua tawi walitangaza kuwa wanaelekea ofisi ya kata ili wakafungue tawi lingine lakini alipoingia RPC Kamuhanda ndipo alipoagiza na kusema kuwa hakuna kuzindua tawi ni kutawanisha watu na kufunga mkutano” alisema Kigaila.
Wakati wakielekea katika ofisi ya kata Marehemu mwangosi alimueleza kigaila kuwa anawasiwasi alipokuwa akirekodi wengi wa polisi wanaonekana si wa Iringa jambo ambalo anaeleza kuwa ndicho chanzo kikuu cha kuuwawa kwake. Huku akihoji kuhusu kamera na laptop za marehemu kutoonekana na kutotolewa taarifa mpaka sasa.
Naye katibu mkuu wa Zanzibar Hamadi Yusufu akielezea maneno ya mwisho ya marehemu alisema kuwa marehemu alikuwa akilalamika kuwa wamwachie kwani yeye yuko kazini wasimuue kwani anatekeleza majukumu yake “ Jambo ambalo polisi hao hawakuliktilia maanani nakuendelea kumpiga mpaka umauti ulipomfika.
Aidha Hamadi ameeleza kuwa wao kama viongozi walikuwa katika tukio hilo wako tayari kutoa ushaidi mbele ya tume huru itakayoundwa na si Tume iliyoundwa na Jeshi la polisi au Waziri Nchimbi kwasababu kwa macho yao waliona polisi ambao wanasimamiwa na wizara yake wakitekeleza dhana hiyo.
Katibu wa Baraza la Vijana Chadema(BAVICHA) Deogratias Munishi ameeleza “kuhusu kauli ya Msajili ya Vyama John Tendwa kuwa haina maana kwani alitegemea yeye kama mlezi wa vyama vya siasa angefika katika eneo la tukio ili aweze kuwa na ajionee hali halisi vyama anavyovilea yeye vikinyimwa fursa ya kufanya kazi zao kama vyama vya siasa”


KAMA WEWE NI MSOMAJI MZURI WA FASIHI ZA KIPELELEZI ZA KIINGEZEZA, UKAUNGANISHA MAANDIKO NA MATUKIO MBALIMBALI NA UKAPITIA PITIA KANUNI ZA KIUTAWALA UNAWEZA KUFANYA KITU KINAITWA DEDUCTIONS NA UKAJUA MAUAJI YA MWANGOSI NI YENYE MAAGIZO MAALUMU..... KIVIPI?

MATUKIO MBALIMBALI

1. MAUAJI YA MOROGORO TENA KWA MTU ALIYE PEMBENI YA BARABARA.....

2. MATAMKO MBALI MBALI BUNGENI NA KWENYE DURU ZA KISIASA KUWA MWENYE FUJO NI CHADEMA MKUTANONI....NA AZUIWE

3. KUENDELEA MIKUTANO YA NJE YA ccm ILHAKLI YA NDANI YA CHADEMA IKIPIGWA MARUFUKU......

4. TAMKO LA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTISHIA KUIFUNGA CHADEMA.....

5. UWEPO WA MESSENARIES - ASKARI WA KUAZIMWA , PERHAPS WITH SPECIAL ASSIGNMENT KATIKA ENEO LA TUKIO KUTOKA MAENEO MBALIMBALI........HAWA NI WALE WAWEZAO KUMUUA NYANI BILA KUMTIZAMA USONI........

6. UHAMISHO WA - MZEE WA KAZI - RPC KAMHANDA KUTOKEA SONGEA AMBAKO PIA ALISUPERVISE MAUAJI YA RAIA WENGINE WANNE.

KANUNI ZA KIUTAWALA



SOMA VIPANDE HIVI KISHA TUTAFAKARI WOTE.....

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia askari hao wakimshambulia mwandishi huyo na wananchi wengine, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michale Kamuhanda akiwa eneo la tukio.

Alipofuatwa na kuombwa awazuie askari wake kumshambulia mwandishi huyo, kamanda huyo alifunga vioo vya gari lake, akapiga honi mara kadhaa, na akaondoka. Baada ya RPC kuondoka eneo hilo, ndipo bomu lilirushwa na kumfumua mwandishi utumbo.

.......PICHA NA MAANDIKO YA MASHUHUDA ZINAMTAJA MTU MWENYE NYOTA - mkuu wa kituo yaani (OCS) AKIJARIBU KUWAZUIA WENZAKE WASIMPIGE MAREHEMU.....HATA HIVYO NAYE HAJUI KINACHOENDELEA KWA NYUMA AMBACHO NDICHO KIMEMTOA UHAI MAREHEMU NA KUMWACHA YEYE AKIWA HOI.........

kwa kuwa maagizo ya kutoa uhai wa mtu hayawezi kuandikwa kama ujumbe kiofisi hivyo....

1. hakuna circular ambayo imetolewa hivyo mauaji haya yanafanywa na syndicate.........

2. maagizo haya yangeandikwa kiofisi basi hata mkuu wa kituo asingejaribu kupambana kumsaidia marehemu na kuishia kujeruhiwa

3. kupiga honi mara kadhaa na kuondoka kunaweza kuwa ni communique kati ya mzee wa kazi na mtu fulani ambaye kwa namna maalumu alipewa hiyo kazi ........ ambayo hata OCS hajui kinachoendelea.....


mauaji HAYA ARE THEREOF OF SYNDICATE!

hizi ni deductions zangu tu.... i stand chance to be corrected!
 
Nilitegemea kusikia jipya,bado maswali yangu hayajapata jibu sahihi kuhusu maelezo kuwa marehemu aliwafuata polisi na nini ilikuwa dhamira yake,ukiondoa askari mmoja je kuna mwananchi mwengine aliyejeruhiwa katika purukushani hiyo?. Inaonekana pande zote zilizohusika(CDM+POLISI) katka tukio hazikuwa na nia njema na sasa hivi nafsi zao zinajuta na kuanza kutupiana mpira.

Dhamira ya mwandishi wa habari inakuwa suala hapa? Kazi yake si inajulikana? Aidha, kuna taarifa zilizotolewa awali kuwa alikuwa anaenda kuwaomba polisi wamuachie mwandishi mwenzake wa gazeti la Nipashe waliyekuwa wamemkamata -akidai kwa makosa kwani hakuwa mfuasi wa CHADEMA. Mwananchi mwingine angejeruhiwa vipi wakati bomu lililengwa point blank kwa marehemu aliyekuwa amezingirwa na mapolisi?
 
MZEE TENDWA AOMBE SANA MUNGU AMJALIE HEKIMA NA UJASIRI WA KUWEZA KUJITENGA NA U-KADA WAKE KULE CCM PINDI ANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA U-REFARII KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI ILI OFISI YAKE IWEZE KUENDELEA KUHESHIMIKA NA WALA SI KULE KUTAFUT KUOGOPEKA KITU
QUOTE]

Unataka kusema mkaa uombe ili uwe na rangi ya chokaa! IMPOSSIBLE rafiki!
 
Dhamira ya mwandishi wa habari inakuwa suala hapa? Kazi yake si inajulikana? Aidha, kuna taarifa zilizotolewa awali kuwa alikuwa anaenda kuwaomba polisi wamuachie mwandishi mwenzake wa gazeti la Nipashe waliyekuwa wamemkamata -akidai kwa makosa kwani hakuwa mfuasi wa CHADEMA. Mwananchi mwingine angejeruhiwa vipi wakati bomu lililengwa point blank kwa marehemu aliyekuwa amezingirwa na mapolisi?
Yale yale! sasa jiulize na wewe, Daudi Mwangosi alienda kabla au baada polisi kuamrisha wafuasi wa CDM watawanyike? usilete maelezo ya picha za JF na story za kwenye daladala.
 
Sina shaka yoyote juu ya wahusika wa mauaji ya Mwangosi na wananchi wengine wasio na hatia. Ni askari Polisi ndio wahusika. Sisi tutawabana wao halafu wao ndio watatuajia nani wako nyuma yao ktk ukatili huu.

Ni vema tukiweka bayana kuwa katika vyama vyote vya siasa ni CCM pekee ndio chenye influence kwa mihimili ya dola, na ndicho pekee chenye uwezo wa kuliamrisha jeshi la Polisi na likatii. Lakini lazima polisi waje clean mbele ya umma, vinginevyo wao na CCM wasubiri nchi hii irudi mikononi mwetu 2015.
 
MZEE TENDWA AOMBE SANA MUNGU AMJALIE HEKIMA NA UJASIRI WA KUWEZA KUJITENGA NA U-KADA WAKE KULE CCM PINDI ANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA U-REFARII KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI ILI OFISI YAKE IWEZE KUENDELEA KUHESHIMIKA NA WALA SI KULE KUTAFUT KUOGOPEKA KITU

Mpaka hivi sasa mlezi wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa, wala hajua hata kule kulikotokea mauaji na hata akapata taarifa za moja kwa moja toka kwa mashuhuda watukio lenyewe, yeye akiwa amekaa kwenye kiyoyozi ofisini Dar es Salaam tayari keshakimbilia kufunua ukurasa katika vitabu vya sheria na kutoa tamko la kukihuku CHADEMA.

Taswira inayojengeka kwa umma hadi hapo tu ni kwamba yeye alikua anaendelea tu kuigiliza katika eneo ambalo alikabidhiwa na CCM atekeleze bila hata kujua kama kweli mwanamaigizo wa kwanza ambaye ni jeshi la polisi kama walikamilisha eneo lao murua bila kuondoka na masizi usoni kama ambavyo ilivyo hivi sasa kwa kashfa nzito huko mkoani Iringa, pengine tofauti na matarajio kwao.

Hadi hapa ni vema ikafahamika kwa hii taasisi ya usajili wa vyama vya siasa nchini akiwemo mtendaji wake mmojawapo Mzee John Tendwa kwamba CHADEMA HAKITEKELEZI MAJUKUMU YAKE YA KICHAMA NCHINI KUTOKANA NA HISANI YA KUKARIBISHWA NA MTU YEYOTE WALA TAASISI.

Ukweli waa mambo ni kwamba chama hiki (CHADEMA), sawa tu na vyama vingine vy siasa nchini, kina HAKI SAWA NA CCM PAMOJA NA VYAMA VINGINE nchini hivyo kuendelea kuundiwa mizengwe na kuzidi kutikisiwa kiberiti ni jambo ambalo kamwe halikubaliki hata kidogo kisheria.

Kama Tendwa anaona kuna jambo CHADEMA kimekosea aidha wakijadili kwa uwazi au akipeleke mahakamani na wala si kubembelezana.

Kama hoja ni kufanya shughuli ya kisisa (Mkutano wa ndani) siku za ziada za sensa basi hata CCM kilikua na jambo kama hilo hilo tena mkutano wa nje Bububu; kwanini hili la CHADEMA ndio ilete nongwa mezani kwake?????????

Mzee John Tendwa ni mwajiriwa wa CCM perce. Nitaeleza.

Rais Jakaya Kikwete ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa.Huyu huyu ndiye aliyemteua Msajili wa Vyama Mzee John Tendwa. Hapa ndipo penye matatizo! Ndiyo maana kwenye Katiba mpya ijayo tunataka Rais anyang'anywe au apunguziwa madaraka ya kuteua watu kwenye Taasisi nyingi na nyeti ndani ya serikali. Kwa sasa Rais wa CCM ndiye anateua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi-Taifa,ndiye anayeteua Msajili wa Vyama,IGP,Mkurugenzi wa PCCB(TAKUKURU),Mkurugenzi Makosa ya Jinai(DCI),Wakuu wa MikoaRCs) na Wilaya(DCs). Wote hawa wanawajibika kwa Rais ambaye wakti huohuo ndiye Mwenyekiti wa Chama tawala!

Kwa akili ya kawaida tu,hakuna ambaye atakuwa tayari kusaliti Chama Tawala ambacho Mwenyekiti wake ndiye Rais aliyemteua kukalia kiti alichonacho. Yuko tayari kutekeleza amri yoyote toka kwa Rais hata kama ni ya kuua ingawa kuna viongozi wachache sana wanaoweza kutenda kinyume na maelekezo ya Bwana mkubwa,1 in 1000!. Na hivi ndicho tunachokishuhudia kwa sasa kwenye siasa zetu hizi za Tanzania.

Kwa mfumo huu tulio nao wa Katiba hii hata kama CDM wakipewa nchi watatumia udhaifu huhuu wa Katiba kujiimarisha na kutotaka kuachia ngazi hata pale ambapo watakuwa wameshindwa. Wanadamu tumeumbwa hivyo kuwa na tamaa ya kutotosheka,ving'ang'anizi na wasiopenda kukosolewa. That's a human nature.

Lakini ukishaweka sheria na Katiba nzuri hiyo haitaangalia chama ingawa tunajua kuna viongozi duniani hasa kwa nchi za Kiafrika wanaongoza kwa kubadilisha Katiba na Sheria za nchi ili kuwafaa kwa vipindi wanapokuwa madarakani! Kwa sasa Tanzania tulipofikia inaelekea CCM wako tayari kubadilisha Katiba ili iendelee kuwalinda. Bado nina mashaka sana na Tume ya warioba kama itakuja na Katiba tunayoitaka Watanzania. Yumkini wanaweza kuja na Katiba ambayo it'll favour CCM to rule this Nation forever kama ambavyo Makada wake wamekuwa wakitanabaisha mara kwa mara. Let's wait and see, it's just a matter of time!
 
Yale yale! sasa jiulize na wewe, Daudi Mwangosi alienda kabla au baada polisi kuamrisha wafuasi wa CDM watawanyike? usilete maelezo ya picha za JF na story za kwenye daladala.

Have a nice day.
 
TAIFA LETU TULIPENDALO SAAANA LA TANZANIA HIVI SASA LIKO NJIANI KUANGAMIA SHAURI YA KUKOSA UONGOZI SIKIVU, ADILIFU NA WENYE HEKIMA

"Taifaa la Tanzania linaumwa tena linaugua ugonjwa wa hatari sana tangu uchaguzi wa Oktoba 2010, kufanyike juhudi za haraka kulitibu taifaa," alisikika miezi michahe akitoa hii kauli yenye hekima tele yule Mhe Mbuye wa Arusha alie likizoni Godless Lema.

Hata hivyo, ni wangapi ndani ya nchi hii walau waliweza kumuazima sikio na kutafakari ki-undani zaidi hii kauli???????????

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na maswahiba wake wanaoendelea kufilisi nchi hii kupitia Dowans, EPA na rundo la fedha za ki-shetani kwenye Benki Uswisi, wataendeleaa kuishi kwa matumaini ya ulinzi wa FFU mpaka lini?????????

Ama kweli Tanzania taifa langu linaangamia kwa kukosa uongozi wenye hekima na uadilifu.

Kaskazini, mashariki na kusini kuzunguka nje ya uzio wa Ikulu kuna idadi kubwa ya Askari FFU na vifaa vya kazi. Ni idadi kubwa kuliko siku zingine.

Upande wa baharini mahali ambapo ni eneo la kuegesha magari kukiwa na sherehe kubwa ikulu, kuna gari ya maji ya washawasha, defender nne na FFU wamebeba bunduki na mabomu ya machozi.
 
Huyo Mwandishi wa habari alikuwa kikazi kama mwandishi au kiongozi wa chadema? eti yupo kazini. Haya sasa afanye vizuri hiyo kazi.
 
Ben ndugu yangu, hakuna asiyejuwa kuwa polisi walitumwa kuua, na ni mpango wa SSM ili kuwafadhaisha wananchi. But hata iweje, ngoja M4C ianze tena mambo yake, utaona itajaa kama maji ya bahari na hakuna wa kuogopa!!! Jiulizeni maswali!!! Na mjijibu wenyewe SSM!!! Ritz how are you my friend? Naona leo unaulizi ahabari za watu na picha ya marehemu!!! Angalia vizuri utaona marehemu alikuwa anachukua picha kwenye gari unayosema!!! Ni kazi yao waandishi wa habari na kwa taarifa huwa wana kinga (immune).
 
Huyo Mwandishi wa habari alikuwa kikazi kama mwandishi au kiongozi wa chadema? eti yupo kazini. Haya sasa afanye vizuri hiyo kazi.

How are you my friend Zomba? Katika vifo hatusemi hivyo!!! Alikuwa kazini na kamera, laptop na vifaa vingine vya habari na polisi walitoweka navyo na havijapatikana hadi leo!!! Polisi mliowatuma wanajua walichofanya kwa matakwa yenu. Pole sana!! Yamkini tusipate hata ajali ugongwe uwe kama chapati!!! Tusinange kifo hata kama uko mrengo wa kulia!!
 
Back
Top Bottom