CHADEMA wadaiwa kupiga na kujeruhi viongozi wawili CCM

Wakati jana imeripotiwa kwamba CCM waliwashambulia kwa mawe wafuasi wa CDM huko Dodoma na kujeruhi vibaya mwandishi wa habari,leo gazeti la serikali Habari Leo limeripoti tofauti na kusema CDM ndiyo walivamia mkutano wa CCM na kujeruhi viongozi wawili kwa mawe.Kama gazeti la Habari Leo litakuwa limepotosha basi Taifa litaangamia kwa aina hii ya uandishi wa kishabiki!


Waongo hao, mimi niliongea na wananchi waliohudhuria mkutano walisema CCM ndo walioingilia msafara wa chadema na mgombea wao na kuanza kuwarushia mawe kitendo kilichosababisha vurugu na kuanza kurushiana mawe!
 
Kumbe kiwanda alicho kuwa ana kisema Mh jk ndio hichi na kina milikuwa na sisimweli.

Kuna watu wana miliki viwanda vya uongo-jk

kumbe alikuwa hajui kama chama chake na cho kina kiwanda kikubwa tu na kingine bado akijajitokeza ila kina julikana.
 
Wakati jana imeripotiwa kwamba CCM waliwashambulia kwa mawe wafuasi wa CDM huko Dodoma na kujeruhi vibaya mwandishi wa habari,leo gazeti la serikali Habari Leo limeripoti tofauti na kusema CDM ndiyo walivamia mkutano wa CCM na kujeruhi viongozi wawili kwa mawe.Kama gazeti la Habari Leo litakuwa limepotosha basi Taifa litaangamia kwa aina hii ya uandishi wa kishabiki!


unashangaa ya leo? umesahauya mke wa mwangosi/
 
Ninacho furahi mimi ni hiki, narudia tena, kwa mtu yeyote makini (sorry, hapa na maana hasa ya watu makini. sio kila mtu) hawezi kuvifanya vyombo vifuatavyo kama ndio source yake of infor:- TBC radio na TV, gazeti la Habari Leo, uhuru, Mzalendo, hivi vyombo labda kama unashida na matangazo ya kazi au habari za kimataifa or michezo, lakini za uchumi, Siasa, Maendeleao! Aah wapi, sio rahisi!
 
Kwa nini unahukumu wakati hukuwepo kwenye eneo la tukio?,unajua tatizo lenu ninyi ushabiki wa mambo umeshawaingia hadi kwenye damu na maji

Bila shaka hatawewe mkuu ume-''think twice'. Hoja inayojadiliwa hapa ni report mbili zinazokinzana. vyanzo vya taarifa ya jana ni mwana jf aliye kuwepo live ktk maeneo ya tukio. Tulifuatilia kwa karibu kilichokuwa kinaendelea, (hii ni pamoja na wewe kama kweli ulifuatilia mjadala huo)
kinyume na taarifa hiyo ya jana ktk gazeti la habari leo inatia mashaka na mkanganyo wa taarifa. sitaki kulaumu upande wowote kwa sababu sikuwepo lakini kama mwendo ndo huo matokeo yake kila upande utatanganza 'liwalo na liwe' hivyo kuwa kama wenzetu Burundi na Rwanda miaka hiyo.

Rai yangu kwa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari ni kwamba wasikubali kuingizwa ktk propaganda chafu zinazowezakuliingiza taifa ktk maafa makubwa. Lakini pia ni waombe watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao waanze kuwabaini mapema waandishi kama hawa kabla taifa halijafika huko. Tuwajue mapema na ndo watatangulia the Hague in case hayo tunayoofia yakitokea.
 
huo ni uzushi mimi jana nilikuwepo kwenye mkutano lililotokea ni kwamba cdm walikuwa wanafanyia mkutano ktk eneo la shule ya msalato ya vipaj na ccm walikuwa wamafanyia eneo la mnadan katiaka kata ya msalato na iliku mgeni rasmi john mnyika aende akasain kitabu cha wagen eneo ambalo na nibarabaran karb na ofis za cdm sasa walipokuwa wanapita ccm wakaanza kuwalushia mawe wafuas wa cdm ambao walikuwa wanapita brbrn wakiongozana na mh john mnyika.cdm wakajib mashambuliz walio anzisha fujo ni ccm.
 
Pengine mfumo ungebadilishwa serikali isiwe na chombo rasmi cha habari bali iwe inatoa taarifa zake kwa vyombo vya habari kunapokuwa na umuhimu wa kufanya hivyo maana wameshindwa kutofautisha vyombo vya serikali na chama tawala. Wengine haturidhiki na makato ya kodi zetu kuhudumia vyombo hivyo
 
bado mnasoma hili gazeti uchwara lenye waandishi wasiozingatia weleledi bali uchama?
ukiandika maoni yako kama yanakosoa serikali au chama chao hawachapishi
wanafiki sana hawa liogopeni hilo gazeti kama ukoma litakufa kifo cha mende

Kumbe inawauma eeh!? Huu mtandao wenu jf-chadema tukiweka maoni mbadala faster wame delete, mbona hamsemi, habari leo for truth and wisdom
 
Mkuu hizo picha umeshindwa ku-down load. Labda zingetumika kamaushahidi, hii ndo dawa ya propaganda chafu.
 
Kwa nini unahukumu wakati hukuwepo kwenye eneo la tukio?,unajua tatizo lenu ninyi ushabiki wa mambo umeshawaingia hadi kwenye damu na maji mwilini mwenu,ThinkTwice.



Kimesababisha lini na wapi,acha uchonganishi,halafu wewe POMPO mbona huwa unakurupuka sana,nimekuwa nikifuatilia sana comment zako hapa JF ni za kukurupuka sana,jaribu kubadilika,weka pembeni ushabiki tuijenge nchi hii,usije ukadhani kwamba wewe unajua zaidi ya wengine kuna watu wanajua zaidi yako lakini so cool.



Mashahiri hya pumba kwa faida ya nani?!weka mambo ya msingi na yenye kujenge hapa sio mahali pa kufikisha fikra zako potofu.



Mwanahalisi halipo tena hata kama ungelilia,halafu kumbuka dua za kuku hazimpati mwewe Wile Gamba,wewe unadhani hivyo lakini wenzako wanafikiri tofauti saana,mwisho wa siku unajikuta umebaki peke yako unang'ang'aa mimacho yako.



Kwa mtanzania yupi mwenye msimamo kama huo wako?!wewe mwenyewe unasema tu humu JF lakini wkati ukifika ninyi ndio mnaowakimbilia hao wakuda wenzenu.
mhariri wa habari leo wape vidonge vyao wakimeza wakitema shauri yao...watu wanataka kukuharibia kazi tu
 
Makajanja wana mwisho wao, mkweli anafungiwa (Mwana Halisi) ili muongo aendelee kutamba mtaani, anyway waache wajifurahishe, randomly ni watu wachache sana wanunuao magezeti sampuli ya hili zaidi ya kulazimishia yanunuliwe kwenye ofisi za serikali, km akili zao ni timamu (kitu ambacho sidhani) wanapaswa wajichunguze na kuchukua hatua.
 
Kwa kweli mungu tusaidie watanzania tuwe ufahamu wa kuchambua vitu, mana hizi siasa za tanzania zinatumia watu kuwadanganya wenzao, hili gazeti linajaribu kupotosho ukweli. Ila mungu ataja lipa kwa huu uongo wote mnao ufanya.
 
Hawa ni wafuasi tu wa serikali, hawajui kuwa wao wanao andika haya maneno ni wanatumiwa tu, wenzao wanakula wao wanateseka, Jaman waandishi wa hir gazeti tufuate miiko ya uandishi yani kama hatujasoma bwana. Kuna msemo husema ukiambiwa kitu changanya na akili zako si kukubar tu.
 
Kumbe kiwanda alicho kuwa ana kisema Mh jk ndio hichi na kina milikuwa na sisimweli.

Kuna watu wana miliki viwanda vya uongo-jk

kumbe alikuwa hajui kama chama chake na cho kina kiwanda kikubwa tu na kingine bado akijajitokeza ila kina julikana.
Kwanza mngejua picha ya kata hiyo ya Msalato iliyoongozwa na Marehemu George Hoya imekaa ktk brbr ya Dodoma Kondoa hadi Arusha
CHADEMA walipewa kijiji cha Msalato Bible (Sekondari ya wasichana) upande wa kutokea Mjini kufungua Kampeni zao na CCM wakapewa Msalato A (mnadani) upande wa kutokea Kondoa kufungua Kampeni zao na hapo ni zaidi ya km 2 kati ya vijiji hivyo
Kilichotokea ni CDM kutoka eneo lao Kampeni Msalato Bible kwenda Msalato A (ambako nako. CCM walikuwa ktk kituo chao cha Kampeni) CHADEMA walienda kufungua Tawi jipya na kupokea viongozi wao waliotokea Arusha
Nani mgomvi?
Kwa vile kuna vijana wa CCM waliolazwa na viongozi wa CDM walioumizwa na magari kuharibiwa tuwaachie Polisi maana hata leo Kampeni zinaendelea kwa hivyo tusilaumu Gazeti au Jk ukweli upo subirini wataupata
 
Baada ya kuona uhuru haliuziki wala kusomeka na watu, wameamua kulitumia gazeti la serikali kufikisha propaganda zao za udhalimu.
 
Nijuavyo mimi karibu na mahali CCM ilipokuwa inafanyia mkutano japo pana umbali kama wa mita hamsini kuna Ofisi ya CDM, na Mwanyika alikuwa naenda kutembelea ofisi hiyo kabla ya kuripoti katika mkutano wa Kampeni ndipo vijana wa CCM wakaanza kuvurumisha mawe kuwaelekea wa CDM, Inapaswa siasa zetu ziendeshwe kwa utilivu bila uvunjifu wa amani wowote! inasikitisha sana!
 
Mtoto: Eti dadi hili gazeti linamilikiwa nani?

Baba: Hili gazeti la Chama

Mtoto:Linafanya kazi gani dadi?

Baba: Kazi yake ni kubadilisha ukweli kuwa uwongo,na uwongo kuwa ukweli!!!!

Mtoto:Sasa kama ni hivyo dadi,tutafika?

Baba : Ndizo sera zetu,tutatfika tuu,MUNGU mkubwa.

Like. . .
 
Back
Top Bottom