Chadema wachukue mawakala kutoka nje ya Arumeru

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Ndugu wanachama wa CDM ili tujihakikishie UShindi Wazo langu ni kwamba ni vizuri kama tukipata mawakala wenye mioyo migumu, wasiotishika kirahisi wasiohongeka na elfu kumi naamini tukifanya hivi tutashinda. Yale tuliyoyafanya Igunga kupata mawakala waminifu na baadhi ya maeneo machache tulikosa mawakala waadirifu leo hii Igunga lilikuwa jimbo la CDM.

Pamoja tunasonga.
 
mkuu ni vyema kupata mawakala wanaofahamika,na iwapo watauza mechi waadhibiwe.
 
Naunga mkono hoja hii.

Ndugu wanachama wa CDM ili tujihakikishie UShindi Wazo langu ni kwamba ni vizuri kama tukipata mawakala wenye mioyo migumu, wasiotishika kirahisi wasiohongeka na elfu kumi naamini tukifanya hivi tutashinda.

Yale tuliyoyafanya Igunga kupata mawakala waminifu na baadhi ya maeneo machache tulikosa mawakala waadirifu leo hii Igunga lilikuwa jimbo la CDM.

Pamoja tunasonga.
 
Mkurugenzi wetu wa Kamati ya Ulinzi n Usalama. Mhe Lwakatare,

kwa kushirikiana na BAVICHA pamoja na Machalii wote wa Arumeru Mashariki, tunategemea kwamba mtatangulia kukagwa vituo vya kupigia kura walau siku 2 kabla ya uchaguzi na vile vile kila mmoja awe anafahamu fika kituo atakapopangiwa na Mkurugenzi wetu huyo mapema iwezekanavyo.

Ulinzi imara wa kura ni ushindi mwanana wa chama kote nchini.
 
Arusha mjini 2likuwa wazalendo,2likuwa na wakala 2liowachuja japo kiuchumi yupo hoi ila ukimpa laki hapokei,Lwakatare suala la mawakala mhusisheni G lema,ana sumu kali kwani pia tuliwapiga darasa.ukisema unachukua nje ya arumeru ccm watafanya political issue kama igunga.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
wizi wa ccm unatumia tume ya uchaguzi na mawakala wanaishia vituoni je?huko tume mnamwachia nani?
 
wachukuliwe hukohuko arumeru, wakichukua mawakala toka nje, watawapa ccm cha kusema. Kama igunga. Humohumo kitafahamika tu!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wasichukue nje labda watu wachache sana toka Arusha kuwapa maujanja. Wameru wana roho ngumu kuliko kawaida!
 
Wazo zuri sana wachukue mawakala kutoka Arusha, wakishindwa lawana zisiwepo...
 
Ndugu wanachama wa CDM ili tujihakikishie UShindi Wazo langu ni kwamba ni vizuri kama tukipata mawakala wenye mioyo migumu, wasiotishika kirahisi wasiohongeka na elfu kumi naamini tukifanya hivi tutashinda. Yale tuliyoyafanya Igunga kupata mawakala waminifu na baadhi ya maeneo machache tulikosa mawakala waadirifu leo hii Igunga lilikuwa jimbo la CDM.

Pamoja tunasonga.
Unajua mkiwachukuwa kutoka musoma maana ndiyo kikosi kazi chenu kinachoaminika
Wameru si mnawaona hawana uaminifu? Wanahongeka kirahisirahisi
 
Back
Top Bottom