CHADEMA waamua ku-'OCCUPY ARUSHA'; Kushinikiza LEMA aachiwe!

Nyie hamna kazi za kufanya? INASIKITISHA. Halafu mlalamike hali ya maisha ni ngumu!!!!Wapuuzi sana.
 
Toeni picha tafadhali yanayojiri Arusha. Shy Town kesho tupo barabari kuwaunga mkono wana Arusha hakuna kulala mpaka kieleweke
 
Now we have our own Tahir Squire?FREEDOM IS COMING TOMORROW FREEDOM IS NOT FOR FREE
 
Niko katika viwanja vya NHC arusha mvua inanyesha mno. Lissu anatoa ufafanuz wa kisheria ili Dr. Slaa atoe msimamo wa chama ambao ni kuhakikisha Lema lazima atolewe. Naona kuna Libya inanukia. Aluta kontinua cdm

Haya kumekuchaaa!!!!
 
Kazi imeanza Arusha,mkesha wa ukombozi nimeshenyeshewa mpaka basi,
 
Ni zamu ya Mwenyekiti Mbowe anasema kuwa CHADEMA wanaanza hatua nyingine ya mapambano. Hakuna mtu kumsukuma, wala kumbugudhi mtu. Hakuna mtu kuondoka hapa, watoto wadogo wapelekwe nyumbani, maana ngoma ya kukseha hapa Uwanja wa NMC, usiku ni ngoma ya wakubwa. Mwenye simu ampigie jirani yake aje hapa, awaambie walioko nyumbani walete chai hapa. Watu watume msgs kwa marafiki zao wote kuwa waje wajiunge na makamanda waliopo hapa kuendeleza mapambano.

Anasema pia kuwa wananchi wengine wote nchini katika maeneo mbalimbali, Mwanza, Mbeya, Moshi na maeneo mengine yote ya miji mikuu wajiandae kuanza kukutana na kukesha. Anasema hatuwezi kuendelea kujenga taifa la watu waoga. Tuko tayari kwa mapambano, pipoooooooooooz power, anasema kamanda Mbowe. Sasa anaagiza wimbo wa Peoples' Power upigwe na watu wasikilize kwa makini mashairi yaliyomo. Wimbo huo ulitungwa kuwakumbuka watu watatu waliouwawa katika maandamano ya Januari 5, Arusha. Here we go brothers.
 
Enzi za Mkapa hakuna mtu angefanya huo ujinga, atakaa ndani na atatoka kwa kufuata sheria na taratibu, mahakama sio shangazi wa cdm wala Lema. Sheria na taratibu ziliwekwa ili zifatwe...hatuwezi kuendesha nchi ktk misingi hiyo...
 
Mi mwenyewe nimechoshwa na maisha na nakaa hapa mpk kieleweke. WanaJF mjue hl ya kwmb nipo hapa sibanduki A to Z!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom