CHADEMA waamua ku-'OCCUPY ARUSHA'; Kushinikiza LEMA aachiwe!

Bakeza

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
348
192


occupyarusha.png




379632_312655355418231_100000213075378_1452646_302647982_n.jpg




Niko katika viwanja vya NHC arusha mvua inanyesha mno. Lissu anatoa ufafanuz wa kisheria ili Dr. Slaa atoe msimamo wa chama ambao ni kuhakikisha Lema lazima atolewe. Naona kuna Libya inanukia...

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza mkusanyiko wa siku saba katika viwanja vya Unga Ltd jijini Arusha, kwa lengo la kuishinikiza serikali kumuachia huru mbunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya chama hicho, Bw. Godbless Lema, ambaye anashikiliwa mahabusu.

Uamuzi huo umetangazwa na katibu mkuu wa chama hicho, Dr. Wilbroad Slaa, wakati alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja hivyo kusikiliza tamko la chama hicho juu ya sakata la mbunge huyo ambaye amegeukwa kuwa gumzo kuu nchini hivi sasa.

Lema, ambaye pamoja na washtakiwa wengine 18 wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali katika mahakama mjini Arusha, ni mshtakiwa pekee miongoni mwao kukosa vigezo vya dhamana hali ambayo inamlazimu kurejeshwa mahabusu kusubiri kesi yake itakapotajwa tena mahakamani Novemba 14 mwaka huu, ikiwa ni siku saba kuanzia leo.

Na maamuzi hayo ndio yaliyowasukuma viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA, kutoa tamko ambalo lilisubiriwa kwa hamu na wananchi wakereketwa wa chama hicho, ambao walijikusanya katika viwanja vya Unga Limited jioni ya leo kwa ajili ya kujua nini hatma ya Lema.

Na ni katika tamko hilo ambapo Dr. Slaa, ametangaza kuwa chama kimeamua kuwa kuanzia leo kitawahamasisha wanachama wao pamoja na wakereketwa wa chama hicho kuweka kambi ya kudumu katika eneo hilo kwa muda wa siku saba kuanzia leo hadi siku ya kesi ya Bw. Lema, ikiwa ni ishara ya kuishinikiza serikali kumuachia mbunge huyo ambaye amekuwa na misukosuko toka akwae kiti hicho.

""Katibu ametangaza kuwa katika siku hizo saba, viongozi wote wa chama watakuwa hapa pamoja na wakereketwa wa chama watakaokuwa wamekusanyika hapa na wameazimia kukaa hapa kwa siku saba kuanzia leo hadi Novemba 14, ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Lema, pamoja na kuishinikiza serikali kumuachia kwa masharti nafuu" Chanzo cha habari cha kuaminika kimeliambia Jukwaa Huru na kuongeza kusema;

"Ni tukio ambalo kwakweli linatarajiwa kuvuta hisia za vyombo vya habari ndani na nje ya nchi hasa ikizingatiwa kuwa kesho taifa lina ugeni mkubwa toka nje. Hofu ya watu kwa sasa ni nini serikali itafanya lakini kwa kifupi CHADEMA wameamua kufanya maamuzi haya magumu" kiliongeza chanzo chetu cha habari.


CHADEMA wafanya maamuzi magumu – Maskani ya uchambuzi yakinifu
 

Attachments

  • occupyarusha.png
    occupyarusha.png
    8.8 KB · Views: 287
Last edited by a moderator:
Mungu ibaraki Arusha, epusha maafa mengine tena! Zuberi aondolewe Arusha ndiyo chanzo cha machafuko
 
Niko katika viwanja vyaNHCarusha mvua inanyesha mno. Lissu anatoa ufafanuz wa kisheria ili Dr. Slaa atoe msimamo wa chama ambao ni kuhakikisha Lema lazima atolewe. Naona kuna Libya inanukia. Aluta kontinua cdm
Cku ingine usiridie ni NMC na sio NHC
 
Endelea kutujuza mkuu

maamuzi magumu tayar cdm wanagoma mpaka kieleweke. Ni mgomo maandaman mpaka kieleweke. Mbowe haendi bungen mpaka Lema atolewe. Slaa katoa tamko rasmi nikaa NMC kwa siku zisizojulikana
 
Wanachadema kukaa uwanjani NMC kwa siku kadha bila kuondoka, kufuatia kitendo cha serikali na mahakama kukataa kumtoa Lema gerezani!
Uamuzi huu mgumu umetolewa na Katibu Mkuu wa CDM, Dr sLAA!
Kitendo hiki kitaendelea hadi Lema atakapofika Kiwanjani hapa, regardless ya lini ataachiliwa!
 
Mtoto wa Malkia anatarajiwa kutembelea huko kesho kutwa. Wana Arusha wampokee na mabango makubwa yanayosema serikali inakiuka haki za binadamu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom