CHADEMA vs Mitandao ya Jamii

viongozi wa CDM wanajaribu kua interactive
Wakuu wa CCM bado wana communicae poorly
Haijulikani what they think about key events
hawatoi maoni yao binafsi, wanasubiri chama kiseme
hiyo inaboa sana, na ndio maana watu wengi mtandaoni
wanakua sympathetic toward CDM: they communicate.
 
Yaliyoandokwa mengi yana ukweli, hata hivyo ikumbukwe kuwa kuna tabia ya unafiki miongoni mwa vijana wa kitanzania. ukikutana na mtu anakuchekea chekea kumbe ukigeuza kisogo tu anaanza kusengenya. Ile ari ya freedom of speech bado haijawaingia watu vizuri, watu wanabaki na madukuduku yao moyoni.

Sehemu kama JF inawapa watu wenye dukuduku walilofuga moyoni nafasi ya kulitoa.
Kuna vijana kadhaa ninaofahamu id zao hapa JF, maisha yao wanayoishi na wanayopotray kwenye JF ni tofauti kabisa. Siwezi kushangaa kusikia kuwa miongoni mwa magwiji wa kuishambulia CCM mitandaoni ni vijana wa Lumumba.

Hata hivyo siwezi kuwalaumu kwa asilimia 100 kwa sababu kwenye siasa ukiwa too straight forward yanakukuta kama yanayomkuta kaka yangu Hamis Kigwangwallah.
 
viongozi wa CDM wanajaribu kua interactive
Wakuu wa CCM bado wana communicae poorly
Haijulikani what they think about key events
hawatoi maoni yao binafsi, wanasubiri chama kiseme
hiyo inaboa sana, na ndio maana watu wengi mtandaoni
wanakua sympathetic toward CDM: they communicate.

Wakitoa maoni binafsi yatawakuta kama yanayomkuta Zitto Chadema kwa kutoa maoni yake binafsi. ukitoa maoni binafsi halafu yakatofautiana na msimamo wa chama kwa siasa za Tanzania unaonekana umehasi.
Tofauti kubwa iliyopo ni kwamba chadema vijana wamefanikiwa kupenetrate katika maamuzi ya chama whereas in CCM vijana wanahesabiwa kama wanaandaliwa, maamuzi bado yanafanywa na wazee ambao hata email address hawana - huo ndio ukweli.
 
Hii inabeba tafsiri nyingi:
1:CHADEMA kimebeba matumaini ya wanyonge wengi wa nchi hii.
2:Wanachama wa CCM ni wavivu wa kufuatilia mitandao ya kijamii.
3:Wana CHADEMA si wepesi wa kuvumilia fikra tofauti dhidi yao.
Hili la tatu si zuri,kwani pale chama kinapo kosea ni vema kusikiliza hoja kinzani dhidi yake ili kujirekebisha.
Otherwise,
ni dalili njema kwa Chadema.
 
sabina ccm ishakufa mie najiandaa kwenda msibani. hao ccm wanaiponda mitandao kwasababu inawapasha ukweli live bila chenga.
 
ccm yetu tunaipenda sana, sema sisi sio watu wa kushoboka ovyo, nyie vaeni magwanda tu, pigeni kwata lkn urasi kwenu ndoto.

hapo kwenye red...nina shaka na elimu yako...hv ni nani mwenye upeo asiyejua madudu ya ccm....i ll never like ccm!
 
Mkuu mleta mada. Kwa uzoefu, kama ukibhatika kuongea na mtu ambaye huko nyuma alikuwa SSM damu leo hii hataki kabisa kusikia habari za chama. Wanachama wanakiponda chama chao wakitumia sababu mbalimbali tena wazi kabisa bila hata kuongopa. Hii imedhihirishwa na chaguzi nyingi siku hizi watu wanasema kabisa sichagui chama bali nachagua mtu ambaye anaweza kutusaidia regardless of SSM. Kwa mantiki hii chaguzi nyingi unaona kabisa vyama vya upinzani vinapata viti kuanzia kwenye mashina hadi Bungeni. Na kwa hakika huu ndiyo mwisho wa SSM. Ni bora tuangalia tena upande mwingine wa shilingi.
 
Nimekuwa nikitafakari kwa muda mrefu sana kuhusu Posts na Comments ninazokutana nazo kwenye mitandao ya jamii, zinahusiana na siasa za Tanzania. Mitandao hiyo ni kama hii Jf, twitter, facebook, blogs nk; wengi wanaotoa comments inaonekana kuwa kama si washabiki basi ni wanachama wa CHADEMA. Hii dalili nzuri kwa chama hiki pendwa kwani watumiaji wengi wa hii mitandao ni wasomi na/au vijana ambao wanao uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko.

Ukweli huu unadhihirika pale anapokuwa anatoa Topic/Thread mwanachama au mshabiki wa CCM; hiyo topic ikiwa imelalia upande wa CCM, wengi wanaochangia wanam-oppose vikali sana. Sasa ambacho najiuliza ni kuwa hizi ni dalili gani kwa Chadema? Kuna mchango gani mitandao hii ilionayo katika kukua kwa Chama cha siasa? Wasomi wengi (ambao ndo wanaitumia sana mitandao hii), wameichoka CCM? Kifo cha ccm? Au humu wengi ni wahuni, kama wanavyojitetea ccm?
Nawasilisha!

Hawa wasomi wa kwenye mitandao hawaipi shida CCM. Taabu iko kwa kile chama cha msimu ambacho kimeamua kwa makusudi kurefusha msimu wake na kuwachochea wananchi wa vijijini ambao ndio haswa mtaji wa CCM kwenye chaguzi zote.
 
Safar ni ndefu lkn fupi sana,katika harakati zote za kuleta mabadiliko wengi watasema hovyo lkn wachache wenye mtazamo chanya watakusifia,jamani cdm wenzangu msiogope wala kukatishwa tamaa na mtu yeyote,tutapambana na watanzania wenzetu si kwa mabaya lkn kwa nia ya kuleta neema itakayofurahiwa na wale tuliopambana nao,najua ni kaz ngumu lkn dalili zote za kufikia mwisho wa safar yetu unanukia,msiogope Mungu yu pamoja nasi,peoples'....
 
Kwenye mitandao ndio wanakimbiaga kabisa!kule fb wengine tume kuwa blocked!
Viva cdm....
 
Watu tumechoka tunaishi km wakimbizi ndani ya nchi yetu,hatutendewi haki,ukidai haki kwa njia ya amani hupewi,mfano madaktari na walimu,tukiandamana tunauawa,watawala bado wanatumia mbinu mfu kuongoza nchi kwa kutisha watu nk,hizi ni baadhi ya sababu ya wasomi,vijana na sasa huko mitaani wananchi wa kawaida wanaichukia ccm
 
Huu ni ukweli usiopingika, CCM haina tena watu kama hawa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Ukweli ndiyo huu kuwa kwa mtu yeyote ambaye kwa neema za Bwana amefanikiwa kufika angalau kidato cha nne akasoma Civics hata kwa uelewa wa chini kabisa, kama si kwa unafiki na tamaa ya kupata cheo kwa upendeleo wa Chama hakuna hata mmoja anayeipenda CCM kwa moyo wa dhati. Huu ni ukweli.
Napenda niwahakikishie kuwa hata Nape Mnauye haipendi CCM bali anapenda madaraka aliyopewa tu. Hivi kwa yule anayejidai kuipenda CCM kwa anaweza kutoa hoja gani kuiuza CCM ikanunulika? Hadi sasa mtaji wa CCM ni ujinga wa watanzania. Kwa sasa ongezeko la uelewa wa watanzania unaendana sawa kabisa na kiwango cha kuporomoka kwa CCM.
 
Back
Top Bottom