CHADEMA, Vipi Tuuboreshe Muungano?

Lakini mbona inaonekana Watanganyika wanafagilia muundo Huu wa muungano!.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
Mkuu, siafikiani na wewe kwamba watanganyika wanaufagilia huu muundo wa muungano. Bali usahihi ni kwamba ni viongozi wa ccm ndiyo wanaoufagilia.
 
Mkuu, siafikiani na wewe kwamba watanganyika wanaufagilia huu muundo wa muungano. Bali usahihi ni kwamba ni viongozi wa ccm ndiyo wanaoufagilia.
Hajakosea!
...na ni kina nani walioiweka serikali ya ccm madarakani kama si Watanganyika?!
 
Serikali ya CCM,Haijawekwa na Wadanganyika.Kama kweli tunaona watu wanapenda mfumo huu wa Muungano si ifanyike referendum kuona kama kuna ukweli kwamba ni Watanganyika au wanzanzibar wanapenda muungano huu. Huu ni muungano wa Viongozi wa CCM kwa maslahi yao.
 
Lakini mbona inaonekana Watanganyika wanafagilia muundo Huu wa muungano!.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2

Wazenji ndio wana uwezo wa kujitoa.... lakini hawajitoi, badala yake wanabaki kulialia eti "hawautaki muungano"
Pia wanakuja na gear ya muungano wa mkataba... what for? Si watoke tuu jumla ?
 
Hata majibu ya jambo kama hili huna??????????????
  1. Raisi Mstaafu Karume amekwambia ni vema Muungano wa watu wawili ukajadiliwa upya na ukaundwa upya....na hapa ndipo walipoanzia kumuita Uhamsho.
  2. Kila upande hususani Zanzibar wananchi wa kawaida wanaona Muungano hauna faida kwao bora uvunjwe au ujadiliwe upya.
  3. Muungano maana yake ni vingi kuwa kimoja.....Kuna Zanzibar na Tanzania hakuna Tanganyika, na hapa ndio kuna tatizo kubwa.
  4. Angalia Marekani ni Muungano wa Nchi nyingi sana na leo inaitwa USA....yaani United States of America.
  5. Usawa wa umilikaji rasilimali unaonekana kuwa ni tatizo.
  6. Uwakilishi katika bunge pia ni tatizo, wabunge wa visiwani wanaingia bunge la Jamuhuri (Dodoma) wakati wabunge wa bara awaingii bunge la visiwani.

Je hata haya machache hukuyajua?? Huoni kuwa yanatosha kujadili upya Muungano????

Pia tambua Muungano CUF na CCM ni makubaliano ya vyama viwili tu hakuna chama kingine kilishoshirikishwa??? wewe unaamanini kuwa ccm na cuf ndio watakaoendelea kuchaguliwa na wazanzibar? nani aliamini kuwa uchaguzi wa juzi cuf walizidiwa kura na cdm???? :majani7:


Mkuu fafanua hiyo red yasijetokea ya MULUGO
 
zomba, Mkuu wangu nitazungumza kama Mkandara na mwanachama kipenzi wa chama cha Upinzani japokuwa mawazo yangu sii lazima yachukuliwe na uongozi wa Chadema.

Swala la Muungano sii swala la kuzungumzwa na Chadema isipokuwa litazungumzwa na wale wenye kero za Muungano wenyewe. Kwa maana kwamba Kama Wazanzibar wanaona kuna ubaya wa kuungana ni jukumu lao wao Wazanzibar kukaa chini na kulizungumza. Wanao viongozi wao toka vyama bunge na hata rais hivyo kama hawaridhiki na muungano ni swala lao wao kulijadili na kisha kwa kupitia viongozi wao ndipo wanaweza kutukaribisha sisi kujadili maamuzi yao. Chademna kama chama ina viongozi na wanachama wake Wazanzibar ambao kwa kuheshimu katiba ya nchi wamekubali kuulinda Muungano. Kama kuna hila yoyote kwanza tuvunje Baraza la Mapinduzi halafu ndipo tunaweza kuwa na mamlaka ya kujadili nafasi ya Zanzibar ktk muungano na jinsi ya kuuboresha..

Haiwezekani kabisa sisi bara tukae kuzungumzia Muungano wakati viongozi wao ndio viongozi ktk serikali ya Muungano na wanafanya kazi pasipo kuonyesha kero hizo isipokuwa wanazizungumzia vijiweni. Kama Dr.Shein anaona kuna kero na Mapungufu ktk Muungano na akawakilisha hoja ya Wazanzibar bado sisi tunaweza kukaa nao tukaijadili. Kama baraza la Mapinduzi limekaa na kuona haja ya Zanzibar kujitenga basi hapo tunaweza kulijadili lakini sii Jumuiya ya kundi la watu ambao wanashindwa kuwauliza viongozi wao, wanashindwa kukaa na viongozi wao kuwakilisha hoja zao lakini wanataka majibu yatoke Bara au serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hili haliwezekani..


Na haiwezekani kwa sababu Baraza la Mapinduzi halitaki kuuvunja Muungano maana iikumbukwe ni baraza hili lilofanya Mapinduzi na kuunda serikali ya nchi mpya ya Zanzibar wala sii ile ya Uhuru wa Shamte ilomsimamisha Sultan kama mtawala. Bado kuna vijana wanafikria Zanzibar ya Sultan na uhuru wa Zanzibar ya Sultan kama vile Wazungu wa Zimbabwe wanaofikiria Uhuru wa Ian Smith na Rhodesia. Uhuru ule haupo na ulikufa kutokana na Mapinduzi hivyo ni jukumu la baraza la Mapinduzi kutoa maamuzi.

Kama wananchi wa Zanzibar hawakubaliani na maamuzi ya baraza hili basi wafanya nao Arab spring kuliondoa baraza la mapinduzi maana unaanza kwako kusafisha. Pasipo baraza la Mapinduzi hakuna muungano, huyu ndiye mama wa kuwepo kwa Zanzibar ndani ya Muungano. Nimesema sana ya kwamba hata siku moja mtoto hawezi kudai kuvunja ndoa ya baba na mama yake kwa sababu zake yeye. Wala hawezi kudai sheria ktk ndoa ya mzazi wake isipokuwa ni jukumu la mzazi mmoja kuweka madai hayo wala sii mtoto. Na kibaya zaidi ni ujinga ulioje kwa mtoto kudai kuona cheti cha ndoa cha baba na mama yake ili sijui afahamu kitu gani?..Cheti hakikuzaa wewe, kama una mashaka na wazazi wako kafanye DNA wewe mwenyewe pengine kweli wewe sii mtoto wao yaani sii Mzanzibar..

Aliyeolewa ni nani kati ya tanganyika na zanzibar? Umepita mkondo ambao sio. Acha wananchi waamue kwa kupiga kura. Na wengi wape. Msilazimishe punda kunywa maji wakati yeye anayaona au anafikiri yana sumu.
 
Hata Obama alipoingia ikulu alikuta masharti ambayo hawezi kwenda kinyume! Hata CDM ikiingia ikulu haiwezi kuvunja muungano. Huu muungano wa kiserikali ni wananchi wataamua wenyewe sasa sijui watapitia ktk asasi gani. Visiwani inaelekea no huku bara wengine hatuoni tunachongangania ktk muungano kama kipo serikali ituambie. Undugu utaendelea kuwepo tu kuwe au kusiwe na muungano.
 
Ni imani yangu kabisa ya kisiasa, hususan hii tuliyonayo sasa ya vyama vingi, ni kuwa vyama vya upinzani ni chachu ya maendeleo kwa Taifa, upinzani ni wasimamizi wakuu wa madudu yoyote yataefanywa na yeyote awepo katika uongozi wa Serikali. Kwa kuwa CHADEMA kwa kipindi hiki ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania

Naomba maoni ya wana chadema vipi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uboreshwe?

Kwani muungano ni lazima?
 
................. vipi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uboreshwe?

“Tungejua kama hali ya aina hii itajitokeza, basi tungeanza na kura ya maoni, tungewauliza wananchi kama wanautaka muungano na kama ndiyo, basi uwe wa aina gani au serikali ngapi, mtu angesema moja, mbili, tatu na kadhalika,” alisema Pinda jana kwenye Viwanja vya Bunge mjini hapa.
 
Hivi wakuu zomba yuko wapi kwa sasa huyu ndugu yetu.
Ni kitambo kidogo simuoni humu,ukichukulia huu mchakato wa BMK ya CCM halafu hapost,nahis kuna kiti hakijakaa sawa. zomba, where are you ?
 
Last edited by a moderator:
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom